Zitto: Magufuli hajabadili kitu, ameboresha aliyoyakuta

Ni kweli maana bado hadi leo UDART haifanyi kazi, bado wakwepa kodi wanapewa siku 14 za kulipa kodi
Bado hajatumbua jipu la Maliasili na Utalii.
Bado hajatumbua na kipanga upya safu ya Air Tanzania maana yake walipo leo wataendelea kula hela zeru bure bure
Bado barabara zinaharibika, barabara alizosimamia yeye zinakufa mapema mfano ni hii ya BRT
bado tumep muda roosevert wa marekani alibaatisha siku hizi watanzania ni wajanja sana ukitaka kuwaongoza inabidi utumie akili sana
 
Naungana Na zitto kabwe, Tanzania INA tatizo LA mifumo ndo maana watanzania tulihitaji chama kipya, lkn wao hawataki kushindwa wanalazimisha, chini ya chama cha makaburu tuandike maumivu
 
namuunga mkono mh Zitto kabwe. tunataka mabadiriko ya kimageuzi yenye dira na falsafa mpya yakitoa muelekeo wa matumaini na uhakika wa taifa la Tanzania kwa miaka mingi hata vizazi na vizazi ma zaidi ni kutunga sheria ya kulinda na kudhibiti mali asiri na mali za uma kwani viongoz wetu wamekuwa wakifanya wanayo weza kuyafanya kwa kutumia mamlaka zao eti tu kwasababu kuna ulinzi wa kisheria. This is not fair at all
 
Kuna kibwagizo nimekipenda sana hapo juu,nafasi ya Tanzania kuendelea ipo lakini sio mikononi mwa chama pendwa ccm
 
Kama mnaona vibaya kufukuza watumishi, kwa hiyo awaache hata kama hawatendi kazi inavotakiwa?
 
hawa wanaojifanya wasomi hawana lolote.ETI RAIS HAJAFANYA CHOCHOTE LAKINI AMEBORRSHA YALOPO.HALIFU WANANUKUU WAZUNGU TU.RAIS AFANYE NINI ZAIDI YA KUBORESHA MAMBO!VIVA RAIS
usifikirie kwa kutumia unyayo, siyo kila kitu kinachukuliwa kimihemuko
 
Katika situ 100 za utawala wake Rais Magufuli ameonesha nia na uzalendo wake wa kutaka kuwatumikia wananchi ili wapate maisha bora. Hata hivyo kuonesha nia tu ya kutekeleza yale ambayo mtangulizi wake yalimshinda hakuhakikishi kuwa nia yake itafanikiwa kwakuwa mfumo anaoutumia kutaka kuwakomboa wananchi haukutengenezwa kufanya hivyo!!

Ili Magufuli afanikiwe ni lazima kwanza awe na nyenzo za kuweza kubadilisha huu mfumo na nyenzo hiyo ni kufanikisha kuwepo kwa katiba iliyopendekezwa na wengi na hiyo ndio itakuwa nyenzo muhimu ya kufikia malengo yake ama sivyo itakuwa business as usual na huko mbele mambo yatakuja kuwa magumu sana kwake!!
 
hawa wanaojifanya wasomi hawana lolote.ETI RAIS HAJAFANYA CHOCHOTE LAKINI AMEBORRSHA YALOPO.HALIFU WANANUKUU WAZUNGU TU.RAIS AFANYE NINI ZAIDI YA KUBORESHA MAMBO!VIVA RAIS
Watu kama wewe ni maadui wa maendeleo kazi yenu kuu ni kusifia kila kitu,kama hujui kitu kama kimya wajuvi waendelee sio kuleta taarabu hapa
 
Uboreshaji unaofanywa kisayansi unaweza kuleta mambo mengi chanya kwa nchi nzima. Mifumo ya kodi ilikuwepo lakini heshima ya ulipaji ilishatoweka. Vyeo kama ukuu wa wilaya na ukuu wa mikoa vilishapoteza heshima lakini katika awamu hii watu wanajionea ni jinsi gani vyeo hivyo vilivyo na umuhimu kama vikirudishiwa heshima. Usultani wa awamu ya nne ambapo watu walikuwa wanajiendea hovyo, umeondolewa na unaendelea kuondolewa. Heshima imerudi serikalini na kwenye taasisi zake, kila mtu anamuogopa mwenzake akidhani labda ni wale jamaa wa TAKUKURU.

Uboreshaji wenye kurudisha ndani ya vichwa vya watu ile maana ya nidhamu kazini ni muhimu sana. Rais Magufuli hajaanza kazi na mguu mbaya. Pale ambapo amehisi kwamba panahitajika mtu mwenye profession sahihi hajasita kumpatia nafasi. Uboreshaji wa serikali ya awamu ya tano umefanyika vizuri, nadhani kila mtu kwa sasa anataka aanze kuyaona mapya ya serikali ya awamu ya tano. Ingawa ni wale tu wenye dhamana serikalini wanaofahamu ni kwa kiasi gani ule udhaifu walioukuta, umeshafanyiwa kazi kwa kiwango gani.

Nchi itanyooka tu. Tulio wengi tutajifunza nini maana ya kuishi kadri ya kipato chako halali.
 
Kwahiyo umeamua kutusomea gazeti siyo?
Naamini umesoma mwenyewe.....sijakusomea
 
Kwani huyo Mwami Kabwe hajui kuwa serikali ya Magufuli kwa sasa inatekeleza bajeti ya 2015/16 iliyoandaliwa na serikali ya Kikwete. Asubiri bajeti ya JPM haraka ya wapi wakati hata siku 100 hazijaisha. Ila kipya kipo, ameongeza makusanyo

Tungetarajia angepeleka miswaada ya kutosha ya sheria, sheria anbazo zita sapoti na kulinda mageuzi ya kisiasa na kiuchumi na utendaji serikalini anayofanya.

Nadhani Zito Kabwe na Dr Kitila Mkumbo wako right. Kilichofanyika hadi sasa ni kupaka siagi mkate ule ule. Hakuna mageuzi hapa, hakuna matumaini hapa na zaidi sana hakuna sustainability ya kilichofanyika hadi sasa!!

Kwa hiyo kutekeleza bajeti ya 2015/2016 is not an issue here. Ishu ni kuwa, atakapokuja na bajeti yake mpya ya 2016/2017 itasimamama ktk misingi na mifumo gani mipya tofauti na hii iliyopo ili iendani na kile anachotaka yeye??
 
Kama mnaona vibaya kufukuza watumishi, kwa hiyo awaache hata kama hawatendi kazi inavotakiwa?

Alfan Issa,

Tatizo la nchi hii haliko kwa mtumishi mmoja mmoja mkuu bali ni sheria na mifumo ya utendaji!!

Unaweza kufukuza wooote na ukaweka wa kwako lakini still watajikuta wanafanya yale yale yaliyofanywa na uliowafukuza. Kwa hiyo fukuza fukuza au simamisha simamisha kazi watumishi wa umma ni suluhu ya muda tu, siyo solution ya kudumu ya matatizo yetu!!

Mfano mdogo na halisi ni pale muhimbili hospital. Alisimamisha na kufukuza lakini baada ya miezi miwili karudi kakuta kilichokuwa kikifanyika kabla ya kufukuza kinafanyika chini ya hao hao wapya aliowaweka. Unafikiri tatizo ni nini mkubwa?

Mfano mwingine ni kutoka ktk serikali ya awamu ya nne. Unakumbuka JK alifanya mabadiliko ya cabinet yake mara ngapi?

Kwa miaka kumi aliyokaa madarakani ni zaidi ya mara 10!!

Sababu ni hizo hizo. Tuna tatizo ktk sheria na mifumo yetu hasa katiba ya nchi. Hapo ndipo penye mzizi wa fitna!!
 
Huyu naye atuache na rais wetu kwanza muda bado stori kama hizi aje nazo baada ya mwaka mmoja.
 
huwezi kubadilisha tanzania bila kuandika katiba mpya yenye maoni ya wananchi
tatizo kubwa la viongozi wa kiafrika ni kukataa maoni ya wananchi ndio tatizo sugu na mwalimu nyerere alishakemea
Katiba itaandikwa na Magufuli?
Kipindi kile wabunge walilazimisha kuwa sehemu ya bunge la katiba mwisho wa siku uliona kilichotokea.
Kuna watu wengi sana wa kushughulikiwa kwenye serikali na chama tawala kabla ya kuanza na mchakato wa katiba kwasababu watatumia namba vibaya kulinda maslahi yao.

Amini wanasiasa wengi wataathirika na katiba yenye kulinda maslahi ya wananchi, wengine wanaongea tu lakini dhamira hakuna.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom