Zitto: Magufuli hajabadili kitu, ameboresha aliyoyakuta

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,306
6,514
SERIKALI ya Rais John Magufuli imekosolewa kwamba haijafanya lolote linaloitambulisha kama serikali ya kimageuzi na badala yake imeboresha tu mambo yaliyokuwepo.

Katika mazungumzo na Raia Mwema yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema ingawa kuna mazuri aliyoyaona kwa Magufuli, hajamuona kama kiongozi anayeweza kuleta mageuzi kwa Watanzania.

Alisema alikuwa anataraji kuwa Magufuli angekuwa kiongozi atakayeweza kubadili mfumo wa nchi yetu katika maeneo muhimu lakini hadi sasa alichoona ni kubana matumizi, kufukuza watumishi na kuongeza juhudi za kukusanya mapato, lakini bila ya kufanya mabadiliko ya vyombo husika kimkakati.

Akimnukuu mwandishi Archie Brown kwenye kitabu chake cha Myth of a Strong Leader, Zitto alisema kiongozi anayeweza kuleta mageuzi kwenye nchi ni yule ambaye “atafanya mabadiliko katika mifumo yote ya kisiasa na kiuchumi ili kuboresha maisha ya watu wake”.

“ Watumishi wa umma takribani 150 wamesimamishwa au kufukuzwa kazi katika kipindi cha siku hizi 100 za Magufuli. Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Edward Hosea, ameondolewa, kama ilivyokuwa kwa Kamishina Mkuu wa TRA, Rished Bade. Lakini, nini kimebedilishwa kwenye taasisi hizo? Takukuru imepewa meno gani? Hayo ndiyo mambo ya kujiuliza,” alisema.

Hata hivyo, Zitto alisema siku 100 ni chache kumhukumu kiongozi ambaye amepewa miaka mitano ya kutawala, ingawa zinaweza kuonyesha picha ya aina gani ya kiongozi ambaye taifa linaweza kuwa naye katika kipindi hicho.

Kwa upande wake, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kitila Mkumbo, alisema baada ya siku 100 za Magufuli, bado anasubiri kuona dira, falsafa na mwelekeo wa kiongozi huyo. Alisema kipimo cha siku 100 kinachowekwa kwa marais wapya, kilianza kutumika nchini Marekani kutokana na mafanikio ya Rais Franklin Delano Roosevelt aliyeapishwa Machi 4, mwaka 1933 na ndani ya siku 100 alikuwa amepitisha sheria mpya 15 zilizosaidia kufufua uchumi wa Marekani.

“Katika hali isiyo ya kawaida, Rais Roosevelt alifanikiwa kushawishi Bunge kupitisha miswaada ya sheria 15 katika kipindi cha siku 100. Mwanahistoria mashuhuri James McGregor anaamini kwamba hadi leo hakuna Rais aliyevunja rekodi ya Rais Roosevelt ya kushawishi Bunge la Marekani kupitisha miswaada mingi kiasi hicho katika kipindi cha muda mfupi.

“Kufuatia kupitishwa kwa miswaada hiyo Serikali ya Roosevelt ilileta mageuzi makubwa ya kiuchumi yaliyosababisha ajira nyingi, na huo ndio ukawa mwanzo wa ukuu wa kiuchumi wa Taifa la Marekani tunaouona leo. “Kwa tathmini yangu ya siku 100 madarakani, Rais Magufuli amejipambanua vizuri kama kiongozi atakayepambana na kero za kijamii kama vile rushwa na ufisadi. Hata hivyo, Rais bado hajijipambanua katika maeneo mengine matatu muhimu ya kiuongozi, ambayo ni falsafa, dira, na ulinzi wa tunu za kitaifa.

Najua wapo watakaosema dira na falsafa ya Rais ni ‘Hapa kazi tu na kutumbua majipu’. Hapana. “Hizi sio dira wala falsafa. Hivi ni vibwagizo tu vya kisiasa! Nikimtakia kila la heri katika utawala wake, naendelea kuitafuta dira ya Rais Magufuli,” ameandika Kitila katika andishi lake lililochapwa kwenye gazeti hili.

Chanzo: Raia Mwema

 
Ni kweli maana bado hadi leo UDART haifanyi kazi, bado wakwepa kodi wanapewa siku 14 za kulipa kodi
Bado hajatumbua jipu la Maliasili na Utalii.
Bado hajatumbua na kipanga upya safu ya Air Tanzania maana yake walipo leo wataendelea kula hela zeru bure bure
Bado barabara zinaharibika, barabara alizosimamia yeye zinakufa mapema mfano ni hii ya BRT
 
"Kitisho kikuu cha uhuru ni kukosekana kwa ukosoaji"
Ni kweli tupu mkuu,kweli kabisa ingawa kwa sasa kila mtu anamwona Rais ni nabii na haipasi kumkosoa nadhani hilo ni kosa kubwa maana maisha yetu yanaanza kufikia mwisho pale tu tunapokaa kimya kwenye mambo yanayotuhusu.
 
hawa wanaojifanya wasomi hawana lolote.ETI RAIS HAJAFANYA CHOCHOTE LAKINI AMEBORRSHA YALOPO.HALIFU WANANUKUU WAZUNGU TU.RAIS AFANYE NINI ZAIDI YA KUBORESHA MAMBO!VIVA RAIS
 
Alicho kiona jana Muhimbili ndio kimempa picha halisi kwamba anachofanya ni kutwanga maji kwenye kinu ,Bunge limekaa badala ya kujadili mambo ya maana kama mstakabali wa Zanzibar ,wameishia kufungia bunge lisionekane wazi, wameishia kudhalilishana kwa kupeleka polisi na mbwa na wabunge wengine wakaenda mbali zaidi kwamba wanawake walishikwa sijui kuvuliwa chupi na shanga

Tatizo la Nchi hii ni mfumo na asipo ubadili basi anajipa presha bure anaziba coco beach wenzie wanavulia Bagamoyo
Kama anataka kuisaidia hii nchi aanze na katiba mpya kwani ndio sheria mama ,

Nasijui hawa wabunge wamechukua hatua gani baada ya huu uzalilishaji wa serikali kuingilia mihimili mingine
Juzi kaanza pia kuingilia mahakama na pesa anatoa yeye ,Ikulu ina account gani ?? Pesa zinatoka hazina na ikiwa zimeidhinishwa na bunge ,TATIZO LA NCHI HII NI MFUMO
 
kubadilisha mfumo ni pamoja na kufukiza hao walarushwa waliopewa dhamana , sasa sijui lip zuri kwa mtanzania mara rais hajafanya kitu mara anafukiza watumishi
 
Kwani huyo Mwami Kabwe hajui kuwa serikali ya Magufuli kwa sasa inatekeleza bajeti ya 2015/16 iliyoandaliwa na serikali ya Kikwete. Asubiri bajeti ya JPM haraka ya wapi wakati hata siku 100 hazijaisha. Ila kipya kipo, ameongeza makusanyo
 
Apewe miaka 54 ya kutawala tuone kama tz haitakuwa tofauti na ilivyo sasa. Kusema ameboresha ni kukubali amefanya. Myonge myongeni ila haki yake msiibanie. Ambacho hajakifanya basi kina zito wamsaidie aweze kukifanya.
 
Zitto astafute kiki za kibwege hapa, kila siku na single ya kukosoa tu na kuwa yeye anajua Zaidi!

Ni wazi kuwa Magufuli anajitahidi sana, ila wapo wanaomkwamisha ndani ya chama chake, tena waandamizi kabisa!
 
Siku 100, halafu tunanza kulalamika hakuna kilichofanyika! Jamani Let's be serious. Ingekuwa after one year halafu yanaongelewa hayo at least tungeweza ku-argue.
 
Zitto acha ushabiki na Jk wako. Pamoja na ukweli kuwa simkubali JPM lakini siwezi kusema kuwa ameboresha aliyoyakuta. Cha msingi ni kuwaambia watanzania kuwa NAFASI ya Tanzania. Kuendelea ipo lkn sio mkono mwa ccm.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom