ZITTO Kumtetea CEO wa Mwananchi - Kuna Siri gani?

Zitto alikuwa sahihi kabisa maana kuna ulazima gani wa kuogopa maana gazeti la mwananchi zinapendwa sana na wanasema ukweli kabisa juu ya kuandika kwao
 
Mzee wa Usafi

Nakubaliana nawe kimsingi, lakini siku zote mimi si muumini wa huu utaratibu wa kupokea kila aina ya mgeni kufanya kazi nchini kwakuwa tu mwekezaji ametoka nje. Hawa wageni wapewe vibali vya kufanya kazi ambazo kweli itathibitika kwamba hakuna mtanzania mwenye sifa na uwezo wa kushika nafasi hiyo ama kufanya kazi hiyo.

Kama serikali imemnyima kibali kwa sababu ya tuhuma mbalimbali ambazo imekuwa ikizielekeza kwa MCL siwezi kuwaunga mkono na hapo nitamsupport zitto lakini kama sivyo vilevile siungi mkono hoja ya zitto na huyo sholei asipewe kibali atafutwe mtanzania naamini atapatikana mtanzania mwenye uwezo sifa na vigezo vya kuwa mkurugenzi mtendaji MCL.
 
Last edited by a moderator:
Wageni wanaofanyakazi nchi wengi hawana sifa ama uwezo kuliko watanzania. Kinachotokea ni watendaji wetu kukosa uadilifu na uzalendo. Watendaji wa wizara ya kazi pamoja na idara ya uhamiaji ndio wamekuwa wakisababisha wageni wengi kuijaa nchini kufanya kazi ambazo hazihitaji kufanywa na wageni.

Kwa mfano east african cables ilikuwa chini ya uongozi wa wakenya na wakaishia kuajiri masalesman wakenya,tigo kulikuwa na meneja utawala mkenya ameajiri wauza simu wakenya! Tanzania oxygen ltd nayo mambo ni hayo hayo, kwa hali kama hiyo mimi nasema hawa wageni inatakiwa wapunguzwe sana kadri inavyowezekana ili watanzania wafaidike na jasho lao.
 
Ben nakubaliana nawe, siasa zetu bado hazikubaliani na mawazo tofauti, ukiwaza tofauti we msaliti. Hata nyie CDM kila mtu naona anataka Shibuda atimuliwe haraka kisa kawaza tofauti na fikra za wakuu wa chama. Nadhani Zitto kwa nje anaweza kuwa sahihi ila msukumo wake hasa ni maslahi yake kisiasa. Bila shaka serikali nao watakuwa wamemnyima kwa sababu za kisiasa.

Nakubaliana nawe kwenye blue lakini sikubaliani nawe kwenye red, kwa sababu fikra za wakuu wetu wa CDM zinareflect fikra na matakwa yetu watanzania wote bila kujali chama. Shibuda anataka wabunge waongezewe posho hadi 500,000Tsh kwa kikao kimoja hana hata aibu wakati madaktari wanalipwa sh 10,000 kwa kukesha usiku kucha kuhudumia wagonjwa. waTZ wote isipokuwa magamba tunatofautiana kifikra na huyo msaliti Shibuda, na wala si wakuu wa CDM tu. kwanza wakuu wa CDM wanalaumiwa kwa kumuacha hadi sasa ankichefua chama.
 
Nilifuatilia bunge mwanzo mwisho, na aliposimama ZK nikasema yeees, na pia Zito hakutetea Mwananchi ispokua

Kila alichokiongea kilikua na maana napia ni mambo aliyofanyia utafiti kwanza, hakukurupuka inatakiwa tufikea,

sehemu kwenye ukweli na hoja za msingi tuzikubali, si kupinga kila kitu bana.
 
Hofu ya serikali ni uwazi wa gazeti hili la Mwananchi kuwa limekuwa mwiba mkuu katika kuripoti habari hasi. Wenyewe MCL manasema wanafuata professionalism.
 
je zitto angeweza kuwatetea mwanahalisi????/
au angejifanya hawajui?????
 
Mimi nilidhani kwa mtu ambaye analalamika nafasi za kazi za wazawa kuchukuliwa na wageni angeunga mkono huu mpango mahususi wa kumnyima kibali huyu mkenya ili nafasi hiyo sasa apewe mzawa. Zitto hapo haangalii maslahi jumla ya taifa bali maslahi yake binafsi ya kisiasa.
UELEWA FINYU! alichohoji zitto ni haki anayotakiwa kupata mtu regardless ni mtz au mkenya au yeyote yule na hasa kulingana na mikataba mliyowekeana. Wabongo badala ya kuelewa concept ya hoja wanakurupuka kutunga illogical criticisms.
 
Jamani tuache unafiki gazeti la mwanainchi limajili watanzania karibu 90% ya wafanyakazi wake ni wabongo waliotapakaa kila kona ya nchii hii kitu ambacho ni tofauti na magazeti mengine kwa hiyo kwa hili zitto yupo sahihi.
 
Back
Top Bottom