ZITTO Kumtetea CEO wa Mwananchi - Kuna Siri gani?

MJIMPYA

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
506
272
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amesema ili Tanzania ijiweke katika mazingira mazuri ya ushirikiano na nchi nyingine za Afrika Mashariki, lazima itende haki kwa raia wa nchi hizo wanaofanya kazi mbalimbali nchini.

Akichangia hotuba ya makadirio na mapato na matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika mwaka wa fedha wa 2011/12 bungeni jana mjini Dodoma, Zitto alimtolea mfano Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Sam Shollei ambaye alidai amenyimwa kibali. MCL ni kampuni inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.

Zitto alisema nchi inapoamua kuingia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, haipaaswi kuwa na uwoga.

"Kampuni ya Mwananchi Communications imewekeza kwa kiasi kikubwa nchini, tena uwekezaji wake mkubwa ni kutoka Kenya, wamewekeza hapa na ndiyo vinara katika soko la hisa Dar es Salaam," alisema Zitto.

"Leo hii CEO wa Mwananchi (Shollei) kamaliza muda wake ameomba kuongezewa kibali serikali yetu inamnyima, tunatuma meseji gani kwa wenzetu," alisisitiza.

Alihoji kuwa kama serikali inataka Watanzania wakafanye kazi, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi na wakinyimwa vibali, itamlaumu nani."Wakinyimwa tutasema nini, lazima tuwe makini katika maamuzi tunayoyachukua," alisema Zitto.

Alisema licha ya kuelewa kwamba kuna haja ya kujenga uwezo wa ndani, lakini kabla serikali haijaruhusu uwekezaji wa ndani, lazima iwaruhusu wenye mtaji ili waweze kuendesha shughuli zao.

Je ni kweli Zitto ana maanisha au kuna siri ktk hili? Kuna mtu aliwahi kuandika kuwa Mwananchi ni gazeti ambalo huwa linamwandika vizuri Zitto, je hii ni kurudisha fadhira?

Na je kwanini hakutaja/kufuatilia sababa za huyu kunyimwa kibali? Kuna wa-Kenya wengi sana wanafanya kazi TZ kwa miaka mingi tu, kwa nini huyu mmoja tu Zitto ndo ajudge kuwa TZ haiwatendei haki?

Nikuulize Zitto make najua utasoma hapa, una uhakika Kenya mTZ anaweza kuishi na kufanya kazi kwa uhuru na amani kama wao wanavyoishi TZ? Kwa taarifa yako hata wewe ukienda Kenya likakupata lolote hakuna mbunge anaweza kukusema bungeni kwao, hata magazeti ya udaku yanaweza yasiandike habari yako.

Kuna waTZ wengi sana wametendwa mabaya huko Kenya, hakuna mtetezi na hata habari haziandikwi.

Acheni mambo hayo.
 
Mimi nilidhani kwa mtu ambaye analalamika nafasi za kazi za wazawa kuchukuliwa na wageni angeunga mkono huu mpango mahususi wa kumnyima kibali huyu mkenya ili nafasi hiyo sasa apewe mzawa. Zitto hapo haangalii maslahi jumla ya taifa bali maslahi yake binafsi ya kisiasa.
 
Hakuna ubaya wowote kama huyo CEO alifuata taratibu zote za kazi yaani kutokukandamiza wafanyakazi na kuheshimu utawala wa sheria wa Tanzania na kuheshimu sheria za uhamiaji sioni sababu ya kumnyima mda wa kuendelea kufanya kazi Tanzania
 
Tatizo la wabongo m2 akisema ki2 anamaslai binafsi
Hya huyo mkurugenzi anyimwe kibali 2taona km ht mwanasport mnayoipenda wanamichezo km mtasoma
By ze way Mwananchi wako juu na wanatoa taarifa za uhakika hakuna maslai ya Zitto hapo ye alikuwa anasema swagga za ukwel .
P inakuja serikari wanabifu na gazet hlo eti wakidai inawafagilia cdm.
Leo mnaanza Mwananchi,soon wazawa watafata km Tanzania daima,raia mwema,mwanahalisi ndo ucseme plus nipashe
Sa2 hapo ndo mtajua Zitto alikuwa ana mean wat.
Kip on blamin
 
Wakenya ndo wanaoongoza kwa uwekezaji nchini, sasa kampuni kama hii kunaubaya gani ikiajiri mkenya kama CEO halafu wengine wakawa wabongo???? Kwanza MCL imeongeza ajira, pili kodi mbalimbali zinapatikana kutokana na uwepo wao......Tatizo(kwa magamba) Wakenya hawataki kutumiwa na magamba ndo maana wamekataa kuongeza muda wa kibali chake....mbona kuna mawaiter kibao tu kwenye mahotel na wanavibali???

Tujikumbushe wakati wa uchaguzi mwaka jana serikali nzima na idara ya habari maelezo waliikuwa wanaitishia kulifungia Mwananchi eti kwa uchochezi....Tyso mwaka huu alilalamika kwamba hakulala alikuwa anafikiri na akadai kuwa tena gazeti lenyewe ni la nchi za nje. Serikali ya magamba inaogopa ukweli na kufagilia propaganda basi
 
Tatizo la wabongo m2 akisema ki2 anamaslai binafsi
Hya huyo mkurugenzi anyimwe kibali 2taona km ht mwanasport mnayoipenda wanamichezo km mtasoma
By ze way Mwananchi wako juu na wanatoa taarifa za uhakika hakuna maslai ya Zitto hapo ye alikuwa anasema swagga za ukwel .
P inakuja serikari wanabifu na gazet hlo eti wakidai inawafagilia cdm.
Leo mnaanza Mwananchi,soon wazawa watafata km Tanzania daima,raia mwema,mwanahalisi ndo ucseme plus nipashe
Sa2 hapo ndo mtajua Zitto alikuwa ana mean wat.
Kip on blamin

Kwenye red na blue unajichanganya mwenyewe! Unaonekana unalikubali gazeti kwa sababu CCM hawalikubali.
Lazima tukubali kuna maslai ya kisiasa ndo maana jamaa anapiga kelele. Ingekuwa issue ya gazeti lile la Mbowe angefurahi sana maana huwa alimwandiki vizuri.
 
Zitto yuko sahihi...huwa tunafanya kazi kwa kuangalia maslahi ya kisiasa bila kuangalia socio-economic implications.Yale yale ya Tido mhando ndiyo tunayopeleka sekta binafsi.Very shame!
 
Zitto yuko sahihi...huwa tunafanya kazi kwa kuangalia maslahi ya kisiasa bila kuangalia socio-economic implications.Yale yale ya Tido mhando ndiyo tunayopeleka sekta binafsi.Very shame!

Ben nakubaliana nawe, siasa zetu bado hazikubaliani na mawazo tofauti, ukiwaza tofauti we msaliti. Hata nyie CDM kila mtu naona anataka Shibuda atimuliwe haraka kisa kawaza tofauti na fikra za wakuu wa chama. Nadhani Zitto kwa nje anaweza kuwa sahihi ila msukumo wake hasa ni maslahi yake kisiasa. Bila shaka serikali nao watakuwa wamemnyima kwa sababu za kisiasa.
 
Hata nyie CDM kila mtu naona anataka Shibuda atimuliwe haraka kisa kawaza tofauti na fikra za wakuu wa chama.

Hapa CDM hawawezi kukubaliana na wewe, mabaya huwa mabaya yakifanywa na CCM yakifanywa na CDM ni mazuri.
 
Kenya imefuta work permit requirement kwa raia wote wa EA, kwa hivo sisi watanzania tunaweza kuajiriwa au kufanya biashara Kenya bila vikwazo mradi ufuate taratibu husika. Hatua ya kumnyima kibali cha kazi huyu raia wa Kenya kinatia shaka commitment ya Tz kwa EA
 
Mimi nilidhani kwa mtu ambaye analalamika nafasi za kazi za wazawa kuchukuliwa na wageni angeunga mkono huu mpango mahususi wa kumnyima kibali huyu mkenya ili nafasi hiyo sasa apewe mzawa. Zitto hapo haangalii maslahi jumla ya taifa bali maslahi yake binafsi ya kisiasa.
wange kuwa wanajali maslahi ya taifa vile viwanda vyote vingekuwa viko hai mpaka sasa na ile tipper pale kigamboni ingeendelea kusafisha mafuta kwa hiyo hapa anachofanya zitto ni kama mfanyakazi wa NIC..
 
Kenya imefuta work permit requirement kwa raia wote wa EA, kwa hivo sisi watanzania tunaweza kuajiriwa au kufanya biashara Kenya bila vikwazo mradi ufuate taratibu husika. Hatua ya kumnyima kibali cha kazi huyu raia wa Kenya kinatia shaka commitment ya Tz kwa EA

Kwenye blue ngoja nikupe mfano (Japo sina uhakika kama ni kweli), nilikutana na mtaalam wa sheria m-Italiano, alisema EU wao wanaruhusiwa kufanya kazi nchi yoyote, lakini akasema hayo ni maandishi tu, akatoa mfano kuwa kwa culture ya wa-Jerumani si rahisi kwa yeye kufanya kazi Germany japo wao wakija Italy inawezekana. So tofautisha maandishi na uhalisia wa mambo.
Pamoja na hayo wa-Kenya wako wengi sana TZ wakifanya kazi kuliko wa-TZ walioko kenya.
Wingi wao pia unachangiwa pamoja na mengine mengi na makampuni yaliyoanzia kwao yakaingia TZ
 
Hapa CDM hawawezi kukubaliana na wewe, mabaya huwa mabaya yakifanywa na CCM yakifanywa na CDM ni mazuri.
Sio kweli, nadhani unajichanganya umewezaje kuwajua chadema humu? Au kwako yeyote anayepinga ccm ni chadema!
 
shida ni kutowafagilia magamba! Mmesahau yaliyomkuta baregu? Walisema mkataba wake umekwisha wakati kuna kina magamba kibao ambao mikataba yao inarudiwa
 
Back
Top Bottom