sasa hapo wafuasi wake si watu wa kuonewa huruma kwa kweli???
yaani kuna watu wanafikia mpaka kushauri Lema agombee urais mwaka 2015..
hii nchi ina vituko vipya kila siku
Uongozi una asili mbili: WATU & HAKI. Na Walinzi wa HAKI za WATU ni watu wenyewe, si mtu mmoja mmoja kwani hakuna mtu aliyejuu au aliyekuwa muhimu kuliko CHAMA;
Waanzishe tu,watanzania tutawahukumu kwa unafiki wao.Tena napendekeza Bashe ndio awe mgombea wa urais,ili Rost tamu
asikasirike!
Waanzishe tu,watanzania tutawahukumu kwa unafiki wao.Tena napendekeza Bashe ndio awe mgombea wa urais,ili Rost tamu
asikasirike!
mkuu utajivunjia heshima ukija na jazba hapa
sikusema sio haki wala sikusema wamevunja sheria
wewe ukija hapa ukisema Mzee Majuto anafaa kugombea urais mwaka 2015
hatutasema huna haki
lakini tutakuwa na haki ya kuhoji busara zako....
Vituko haviishi kwa kweli. Mimi Lema kwa kweli huwa sielewi nini hasa anakisimamia. Kuna wakati Jenerali Ulimwengu alitushauri kabla hatujachagua Rais angalau tujiridhishe Huyo anayetaka kuwa Rais wetu aliwahi kuandika wapi mawazo yake ili tuyatambue. Lema ni mtu wa kulaumu bila ya kutoa suluhisho.
Kwa mfano watu wengi hawajui kwamba na Lema naye ni sehemu ya mgogoro wa umeya Arusha. Lema aliingilia mamlaka ya uongozi wa CHADEMA Mkoa na Wilaya kwa kutoa maamuzi ya kuonesha kwamba yeye ni "makini" na kwa bahati mbaya CHADEMA inaamini kwamba Lema ni nembo ya CHADEMA Arusha kwa hiyo kati ya kuchagua uongozi wa chama na mbunge CHADEMA kikachagua Mbunge.
ndiyo wewe ni mbaguzi kwa kigezo cha umri dhidi ya wazee
Uwezi kujiita makini ilhali ufuati misingi yoyote ya kukufanya uwe makini, misingi hiyo inaanzia kwenye tabia binafsi na jinsi jamii inavyokuona, matendo yako na ushauri wako juu ya mambo mbalimbali ya kimsingi katika kujenga jamii nzima. Ndio maana umakini hauwezi kutokana na mashabiki wako pekee, zaidi ni jamii nzima inayokuzunguka ambayo ina weza kuona chanya na hasi juu yako.Kibs achana na washabiki,
..... ukijiita makini huo umakini unatoweka? hata kama ni majivuno wewe mwenyewe kujiita makini.
Tatizo liko hapa...wanaotoa maoni na kusema kwa uhuru wanalalamika kwamba demokrasia na uhuru wa mawazo unaminywa kwa maslahi binafsi ya wachache
Wanaoshindwa kuvumilia uhuru wa mawazo na kuona maslahi yao yako hatarini basi husingizia siri za chama,vikao au uhuru bila nidhamu.So uhuru wa mawazo,demokrasia na wigo wa mamlaka ndani ya vyama vya siasa uende sambamaba na dhana ya uwajibikaji na kuzingatia maslahi mapana ya chama.Hii ni kwa viongozi wa vyama vya siasa na wanachama wa chama husika
Wakati mwingine tunaipinga CCM kwamba inaminya uhuru wa mawazo na demokrasia.Pia tunapinga na kulaani matumizi ya maneno kama siri za jeshi au nyaraka za siri.hii imekuwa silaha kubwa kwa madikteta wote kwenye vyama vya siasa na viongozi wa serikali (hasa viongozi dhaifu).Ndiyo maana leo hii unaona south Africa bado Zuma amekaliwa kooni na Archbishop Desmund Tutu(Mshindi wa Tuzo ya amani ya Nobel) pamoja na wanaharakati wengine juu ya mswada kandamizi na utakaofifisha dhana ya uwazi na uwajibikaji (mswada wa kulinda nyaraka za siri)
Niseme tu kwamba kiongozi dhaifu au adui wa Demokrasia hana chama,kabila wala dini.Mathalani watetezi wa haki na uhuru wa maoni au demokrasia hawana kabila,dini,wala chama cha siasa.Madikteta ni madikteta tu
Chama kingine? hawawezi. Ninachokiona ni jitiohada za kutaka kupanua demokrasia ndani ya vyama vya siasa.
Wanatoa ujumbe mahsusi wa kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kujenga tabia ya kuvumiliana na watu wanaopishana nao mitazamo ya masuala mbalimbali hata kama wako ndani ya chama kimoja. Kwamba watu wote lazima wawe na mtazamo mmoja juu ya kila jambo ni kitu hakiwezekani na kwahiyo, haki ya mtu kuwa na mawazo tofauti na kiongozi wake ni lazima ilindwe na iheshimiwe.
Katika hili,niko pamoja na Zitto, Dr. Kitila, Ben Saanane, Kafulila na wengine wote wanaopigania demokrasia halisi ndani ya vyama vya siasa. Lazima tutoke kwenye maigizo ya demokrasia ndani ya vyama na tuwe na demokrasia ya kweli. Hakuna kushabikia nidhamu ya uoga kwa sasa.
Nimegundua kuna mambo yanaendelea huko CDM.Lema anasimama wapi katika kundi hili?
..... halafu very naive, si kama wananchi wa kawaida...
Hivi unajua kwamba Makamu wa Rais wa Marekani Bwana. Joe Biden aliwahi kusema hadharani kwamba Bwana. Baraka Obama hafai kuwa Rais wa Marekani kutokana na kutokuwa na uzowefu wa sera za mambo ya nje? Sasa Biden alivunja nidhamu ya chama chake?