Zitto kabwe: Umejifunza nini na matokeo ya udiwani

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,358
6,422
Zitto umeyaona matokeo ya udiwani. Unadhani urais huo unaokuhangaisha utaupata kwa mtaji huu? Matokeo ya udiwani ni kioo cha kujiangalia CHADEMA mnakubalika/mmeenea vipi vijijini.
 
Last edited by a moderator:
Mbona unamuuliza zzk tu, mbona humuulizi Slaa au mbowe:confused:
Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
 
Mbona unamuuliza zzk tu, mbona humuulizi Slaa au mbowe:confused:
Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
Umeona jinsi watu walivyo na mtazamo hasi dhidi ya baahi ya watu?maana utafikiri Zitto ndiye anawakwaza au yeye ndiye anawajibika katika kila kitu ndani ya CDM,bora wajiweke wazi na waeleze tatizo lao nini dhidi ya huyu mchapakazi!
 
Mbona unamuuliza zzk tu, mbona humuulizi Slaa au mbowe:confused:
Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2

Slaa na Mbowe wanahangaika kukijenga chama, zito anahangaika kukigawa kwa makundi ya urais. Mbowe na slaa hawajatangaza hata mara moja kugombea urais 2015
 
Umeona jinsi watu walivyo na mtazamo hasi dhidi ya baahi ya watu?maana utafikiri Zitto ndiye anawakwaza au yeye ndiye anawajibika katika kila kitu ndani ya CDM,bora wajiweke wazi na waeleze tatizo lao nini dhidi ya huyu mchapakazi!

Ali, Zito anakigawa chama kwa kuleta makundi ya URAIS. Ni hilo tu, wala hafanyi lolote kukijenga
 
Ali, Zito anakigawa chama kwa kuleta makundi ya URAIS. Ni hilo tu, wala hafanyi lolote kukijenga
Ndugu yangu Chuakara, mi sioni tatizo hapo kuwa na camp tofauti katika kuwania urais si tatizo endapo kila mmoja ataitambua dhamira ya pamoja ya chama,sidhani Zitto yuko tayari kukigawa chma kwa mgnitude unayomnasibisha nayo.
kama yuko interest na hilo ni tusubiri awe tested na tutajua kama anafaa,mi siamini kama mashabiki wa zitto kuwa hawatamuunga mkono Dr endapo Kaka Zitto ataenguliwa,Chadema wako smart kuliko hapo.
 
CHUAKACHARA

Ni kweli ZZK amekuwa haraka sana kutaja mambo ya uraisi, lakini kuhusu uchaguzi wa jana Mh. CHUAKACHARA naona hujui masuala ya kukokotoa (Data processing and data analysis. Kuhusu uchaguzi wa jana wakokotoaji wanaona kama CHADEMA imepata ushindi mkubwa kwa sababu,

1. CCM walikuwa wanatetea kata zao 26 kati ya hizo 29 zilizofanya uchaguzi jana, pia CHADEMA walikuwa wanatetea kata 2 . Kati ya hizo CHADEMA imetetea kata zake zote 2 pia imeipoka CCM kata 4 mpaka hapo CHADEMA ni kidedea

2. CHADEMA hikupoteza kata zake ingepoteza hata moja kingekuwa kiashilia kibaya sana kwa CHADEMA

3. CCM iimepoteza kata ingine wilayani Newala kwa CUF hii pia ni kiashilia kibaya kwa CCM
Kimsingi hapa CCM inatakiwa ijifunze kitu na wala siyo CHADEMA,
 
Last edited by a moderator:
Ukiona watu wanang'ang'ania kupata nafasi za uongozi ndani ya ccm usidhani hawana akili nzuri. Ukiona watu wanatishiana hadi kwa bunduki kupata uongozi ndani ya chama kinachochukiwa na wa2 wengi cha ccm,usiwabeze na ukiona vijana bado wanavaa mavavi ya kijani pamoja na kuzomewa mitaani usidhani kwamba hawajui wanachokifanya.

Haya yote nayasema kwa sababu ccm bado inamtaji mkubwa wa wapiga kura ambao unawawezesha kuendelea kuwa madarakani,somo kwa Wana CDM wenye nia ya dhati na nchi yetu ni kwamba tuwaze kujijenga zaidi,mkiwafuata ndumila kuwili kama ZiZuKa tutaendelea kuiacha inchi njia panda
 
Nyie CCM mkitaka kupima kama mtaweza kushinda chaguzi zijazo boresheni daftari la wapiga kura na muache kununua kadi za kupigia kura na pia msitoe rushwa.Uchaguzi uwe huru na haki.Nawaambia nyie ndugu CCM,kuna wakati wananchi hawatawavumilia tena,itabidi wachukue hatua kudai haki zao.
 
Matokeo ya udiwani yana changamoto nyingi za kuzifanyia kazi kwa chama chenye ndoto ya kuchukua dola mwaka 2015. Faraja ni kwamba kiukweli, matokeo yanatia moyo kwa kuwa kata zilizopatikana sehemu kubwa zilikuwa ccm! Pili daftari la wapiga kura halijaboreshwa!
 
Ali, Zito anakigawa chama kwa kuleta makundi ya URAIS. Ni hilo tu, wala hafanyi lolote kukijenga

we sema tu unakundi lako la kuutaka urais ila mnakuwa wanafiki hamtangazi hadharani. kama katangaza mmja tu unawezaja kusema kuna makundi? maana wangekuwa wametangaza wawili na kuendelea ndo tungesema kuna makundi. waambie kundi lako nao waweke hadhara waache unafiki wa kujificha otherwize mpaka sasa tunajua mmoja tu kwahiyo makundi hamna.
 
Ndugu zangu hawa manyang:au wa ccm kuwashinda kwa kura yatupasa tupige na kulinda kura kwa nguvu zote na kama ikishindikana ni kufanya kama misri tu
 
Umeona jinsi watu walivyo na mtazamo hasi dhidi ya baahi ya watu?maana utafikiri Zitto ndiye anawakwaza au yeye ndiye anawajibika katika kila kitu ndani ya CDM,bora wajiweke wazi na waeleze tatizo lao nini dhidi ya huyu mchapakazi!

Halafu cha kufurahisha ni kwamba alipokuwepo Mh.ZZK 2015 tumepata ushindi wa kishindo, lakini alipokuwepo Slaa mmmh!!
 
Sioni kiongozi mwingine wa kupewa ushauri zaidi ya Mh Zitto , kwani kijana ni mkweli, mnyenyekevu,msikivu na mzalendo kwa nchi yake. najua huo ushauri ataufanyia kazi kwa manufaa ya Watanzania wote. nasisitiza watanzania wote si CCM wala CDM.
 
Umizeni vichwa lakini jueni 2015 dola itakwenda ccm huu ni ukweli mchungu but upinzani hawana ajenda watawafanyia nini watz
 
Back
Top Bottom