Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

Kama kawaida mimi napenda kutoa maoni ya kile ninachoona ni sawa bila kufuata ushabiki wowote wa chama pamoja na kwamba mimi ni mfuasia wa chama kimoja tu humu ndani ya Jamhuri.
Zitto ni kiongozi amabaye anaonekana kuwa na kiu kubwa ya mafanikio, huenda anataka ikiwezekana yaje kesho. Tabia na mwenendo wake vinanipa kuamini kuwa Ifikapo mwaka 2020 pengine atakuwa na uzoefu wa kutosha kuongoza nchi hii. Si maanishi umri bali Utulivu wa ki-utu uzima bado hajaufikia. Hata tatizo kuu ninaloliona kwa raisi wetu wa sasa ni hilohilo. yaani kakosa utulivu wa ki-utu uzima. Utulivu huu hauji kwa kuishi miaka mingi, wala kwa kufanya kazi mda mrefu. Sharti uzaliwe nao kisha uendelee kukomaa taratibu kwa kadiri unavyoishi. Zito anao ila nadhani mpaka 2018 utakomaa lakini si 2015
 
Hayo maneno kayasemea wapi na kamsemea nani?

Magic FM akihojiwa na Fina Mango
Hizi habari nyingine bwana hatari tupu. Yaani mtu anajitungia tu maneno yake na kuyarusha JF. Na kwasababu JF imejaa watu wa kuchangia chochote hata kama kimetoka uvunguni, basi ndiyo hivyo tena watu wachangia tu uzi.

Sina historia ya kutengeneza habari angalia record yangu, sina sababu yeyote ya kumtungia au kumzushia mtu, ninaheshimu sana utu wa mtu. Zito kasema kwa akauli yake na kwasababu yuko humu usijali atakuja mwenyewe akiona inafaa.

Kasema wapi na lini? maana humu sasa itaanza habari, chanzo hatukijui, mm huyu jamaa namkubali lkn akitokeza tena TUNTEMEKE mara Shose Genda huelewi nani ni nani ndo maana mm nakimbia hizi story sasa

Aache uropokaji wa kiaina manake anajiona yeye ndiye top.. Ajenge chama chake kwanza urais baadaye

Inawezekana haropoki ila anasema anachokiamini, tuwe na uwezo wa kumwelewa wakati mwingine sio rahisi wote wakawa sawa. Misimamo inatofautiana.
Magic Fm akihijowa na Fina Mango katika kipindi kipya kiitwacho MAKUTANO

Asante sana Mkubwa umenisaidia sana
 
Back
Top Bottom