Zitto Kabwe: Nusu ya walimu wanalipwa mishahara ya bure, hawafundishi

Nikiwa kama mpiga kura kwenye jimbo la ZZK na nikiwa kama mwalimu ninayetekeleza majukumu yangu ipasavyo ndani ya nchi yangu nampinga wazi wazi. Maybe kama angezungumzia kipindi cha JMK bt tangu JPM aingie madarakani hakuna tena mwalimu ambae hatimizi majuku yake ipasavyo....



Ninamuomba aje afanye majuku yake uku kama MBUNGE.....Maana nae ni mbunge hewa tangu achaguliwe haonekani jimboni wala hivyo kusababisha kuongezeka kwa mrundikano wa kero za wananchi hasa ktk usafiri, elimu, afya nk.......

HUKU WANAMWITA MBUNGE WA KIMATAIFA.....
njoo uwatendee haki wananchi waliokuchagua.....
 
Daah ninao rafiki zangu ambao ni walimu sijui wanafundisha muda gani maana muda mwingi nawaona vijiweni tu wakipiga soga muda wa kazi...
 
Hata kama hawafundishi, ni watoro lakini wamenidaidia kuposti hapa ujumbe. mnaeaita vilaza sawa ! hawajui hesabu saw a,
mbona mnasahau watoto upungufu wavitabu, makitaba,vyoo, madarasa, walimu (wasayansi), walimu hao kuchapwa viboko na wenye watoto, maafisa wa elimu, madai yasiyolipwa,.
kama kweli vilaza mwenye kuwachagua kusomea ualimu alitumia vigezo gani na kosa ni LA nani aliyechagua au aliyechaguliwa?
kama shule za sirikali je walimu hao wanaandaliwa vyuo gani?
je hao wanaofundisha hizo zenye kutoa elimu bora wanaandaliwa na vyuo gani?
sikatai kuwa si watoro kwa asilimia zote Ila ltujadili kwa kuangalia pande zote kuanzia sirikali, walimu, na wazazi.
 
Haya mambo ya walimu ni ya muda mrefu sana......anachosema Zitto ni ukweli....yani ni kwamba lazima pande mbili zipatanishwe
Mwalim apewe motisha ya kufundisha vile vile awajibishwe kwa hilo..
Conspiracy ni kwamba ukiongeza mshahara wa walimu. Mishahara ngazi zote zitapanda anzia serikalini hadi sekta binafsi na hivyo kufanya maisha kuwa magum kias kwa mwananchi wa kawaida..( jicho la tatu linahitajika kwa hili)
Maana kwa waajiri watongeza cost of production na importer wataongeza WACP,
So ni kama unarud square one...
Otherwise vitu kama nyumba, mazingira bora ya kaz ni vitu muhim sana..walim wa zaman walifundisha kwa weled sana, japo maslaj yao yalikuwa duni zaid


Hapo piga ua ndo nimekubali mwalimu ni mnyonge mno ukiangalia ni wavumilivu na wastahimilivu sana hongera yao
Hao wapiga meza kila siku wanapiga hela zetu mingi tuu fanya utafiti mpiga meza mmoja anakula hela ya walimu wangapi kwa mwaka??

Ukilinganisha mwalimu wa sasa na wazamani unakua umeenda mlama kidoogo.
Tuliosoma zamani ni mashahidi, shule zilikua na wanafunzi wachache mno na madarasa yalibebeka hii ilimuwea rahisi mwalimu kumtembelea kila mwanafunzi na kutatua changamoto zake, jiulize siku hizi wastani wa mwalimu mmoja ni wanafunzi wangapi?? Jibu unalo, darasa linatengenezwa kwa viwango vya wanafunzi 45 mpaka 50 likikamilika tuu wanafunzi 120 mpaka 150 halafu kipindi dakika 40 mpaka 80. Hayo hamuyaoni kazi mna mshambulia tuu
Zamani mwalimu alikua na thamani yake katika jamii, alipewa uthamani na jamii nzima hivyo akajengewa moyo wa kufanya kazi si kwa ajiri ya mshahara bali kulipa fadhira za uthamani anaopewa na jamii husika inayomzunguka, lakini siku hizi kwanza kanyanganywa majukumu yake ya kulea na hasa anapochukua hatua fula fulani wazazi wanakuja wengine wanadiriki mpaka kumwambia namna ya kufundisha na jamii inayomzunguka siku angalia ni namna gani mwalimu anachukuliwa, ishaonekana ualimu ni kazi kama kazi zingine, mtukane na mnyanyasi ila mpe hela nzuri,
Leo katika kazi zoooote za kitaaluma na kitaalamu ualimu ndio wenye pesa ndogo kwa kizingizio eti ni wengi, kwa hiyo hamjipangi kuwahudumia??

Mwalimu anapostaafu masikini hana hata ka kibanda zaidi hukaa mda mfupi na kupoteza maisha,
Ikumbukwe mwalimu ni mwanafunzi siku zote husoma yanayoendelea na yaliyopita ili kujiimarisha katika msimamo darasani.
Sasa walishasoma na kuelewa kua wameterekezwa na aliyewaajiri anaona kama kawasaidia si kwamba wanamchango wowote, wameamua na wao angalau wajitahidi kujinasua kwenye hii dunia, siku nne kazini siku tatu mishemishe, na ndio maana wansoishi hivi angalau uhai wa familia zao inaridhisha, waliokaa kutegemea kazi na mshahara huishia kufanyia kazi madeni ya vibandani na kuweka vibati

MWISHO WA SIKU AKINA ZITTO WASIKALIE KUMLAUM MWALIMU WAANGALIE HATA NAMNA KAZI ZA WALIMU ZILIVYOZINGILWA NA CHANGAMOTO NYINGI, WAO CHANGAMOTO YA KUTOKUA LIVE BUNGENI WAMEPIGIA KELELE SANAA LAKINI CHANGAMOTO ZA WALIMU WAPO WANAOSEMA ETI HAZIZUIII KUFUNDISHA,

NACHEKA SANA KUJIFANYA HAWAYAONI HAYA NA KUMLAUMU MWALIMU, YAANI HATA MATANGAZO YA HAKI ELIMU HAMYASIK ???
SIKU ZOTE UKITEGA PANYA KWA SUMU NDANI UJUE HARUFU YA MUOZO HAIEPUKIKI NDANI

LEO UNAMCHEKA MWALIMU MAISHA MAGUMU KESHO UNAMLALAMIKIA HAFUNDISHI SI DHARAU HIZI,

SAWA NA KUMPIGA MTOTI HALAFU UNAMKATALIA KULIA


MWISHO
WALIMU KAZENI MIOYO MALIPO YENU SI DUNIANI TENA PALILIENI SAFARI YENU ACHANENI NA KAULI ZA WANASIASA AMBAO HUJIFANYA WANAJUA KILA KITU HASA HAWA WAGONGA MEZA
 
Unalipwa 500000 kwa mwezi na nchii hihi ya sukari 3500 na una familia inaitaji nguvu za giza kukaa masaa yote kazini bila kutafuta kipato cha ziada mkuendesha maisha. Serikali isipo sikia kilio cha kuongeza mishahara na marupurupu mengine wasitegemee kuona hawa watu wakikaa shule masaaa yote.
Siku zote unaongea pointi ila ya leo umekomesha,
Mtu amekaa miaka mitatu kuitafuta taaluma hii halafunamlipa laki tano
Halafu alishe familia na ajikizi mahitaji yake yote, inahitaji miujiza kama ya yesu kulisha watu elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili

Walimu pigeni dili hao hao ukistafu na kiatu kiloenda upande wa kwanza kukucheka
 
Wewe unajitambua ndio maana unayaona haya, ila wapo mbumbu wengine wanafuata mkumbo tu. Juzi nimefika shule moja Mwalimu anaishi nyumba nyasi na anaikarabati mwenyewe kwa kuweka Saruji chini! Zito anatafuta umaarufu kwa mgongo wa Walala hoi.
Siasa za uchwara tulishazitambua wao kuzimiwa kutokua live wanatamani waifute serikali, ila changamoto rukuki wanalazimisha zivumiliwe,hivi ikitokea m bunge alazwe kwenye nyumba ya nyasi itakuaje??
Hapo sihitaji hata kipeperushi kuelewa lengo la wanasiasa
 
Ndio mana tunasema walimu wengi ni failures na ndio mana hawapo willing kufundisha mathematics. Na sio tuu hawapo willing, wengi wao ni vilaza yani hawajui kabisa mathematics sasa hapo watafundisha nini?

Hivyo system ichekiwe upya yani walimu wawe na good foundation yani performance zao walipokuwa wanasoma zijulikane na hapo ndio kuna umuhimu wa systems kuwa computerised so watu wasiweze ku cheat.
Mishahara iongezwe kwa 70% ili ku attract walio pass vizuri hasa wanafunzi wa universities kufundisha. No way, mwanafunzi aliyesoma hadi university akawe mwalimu wa kulipwa laki mbili kwa mwezi.

At the moment watu wengi hawachukulii kufundisha ni km career, kufundisha ni km kazi ya kuziba gap na ndio mana walio pass wanafanya vitu vingine vya kuwaimgizia kipato bora kuliko mshahara wa ualimu ambao hulipwa kwa mbinde.

Halafu atakuja mtu aseme money is not everything, wakati wenyewe wanafanya better jobs with good salaries then wana expect walimu wakajitolee kufundisha.
Matokeo yake tunazalisha taifa la wakalili madesa
Kwa nini mliofaulu msije kufundisha
Hili swala laiti ningekua mwalimu mi naona kuna haja ya kuburuzana mahakamani ukaueleze umma, sasa napo basi
Sema walimu walipewa kipawa cha upole basi tu
 
Bila kuboresha maslahi yao, tusitarajie muujiza toka kwa walimu. Wataendelea kutofundisha kwani wengi wao wanatumia muda wa kazi kujiongezea kipato. Wengi wa walimu vijana ni bodaboda huku walimu ambao ni akina mama wa makamo kazi yao kubwa ni kuzungusha vitumbua na visheti mitaani. Suluhisho ja utoro wa walimu shuleni si kuwasema bungeni, bali ni kuwapatia mishahara inayokidhi angalau theluthi ya mahitaji yao pamoja na kuwapatia posho ya kufundisha na hata kuwapandisha vyeo kwa wakati. Hapo watakuwa wanabaki vituoni huku wakijituma kwa 100%
Watu mna mawazo mpaka ya ziada asee
Kwa hilo sibishi kabisaaaa nawaonaga sana
 
Wabunge wajibikeni kila kukicha mnashindana kusoma tafiti, njooni na majibu tumechoshwa na maswali yenu yaleyale kila kukicha. suala la elimu yetu mnaongea yaleyale kila siku mbona hamna reaction... Walimu hawafundishi sawa, wana hali ngumu sawa, mazingira/maslahi duni sawa, mitaala mibovu sawa, sera ya elimu sawa, so what now?
 
Ameongea ukweli baafhi ya mambo, hilo la 49% ya walimu hawapo shuleni labda kg.
Ye mwenyewe anayujua mazingira ya kj, kuna sehemu njia za maji ziwa tanganyika nauli yake 30000 mpaka 20000 ili ufike kigoma mjini,, ukifika huko miundo mbinu sahau, hakuna chochote nahisi hata ukipeleka sola zinagoma,, utakuta nwalimu mawasiliano anayafuata kama kilometa kumi mpaka ishirini,, akienda kuwasiliana na familia akirudi siku ineisha, halafu unaropoka tuu upuuzi wake hapa, hakusema sababu ni nini??

Tatizo la zito hua ni rafiki wa wana kigoma kampeni zikikaribia,
 
Basi angeacha kazi, mbona kuna watu kibao wanafanya kazi ngumu kwa malipo kiduchu na bado wanafanya kwa ufanisi? Mfano walinzi. Wamekuwa watu wa kulalamika kila siku wakati hawatimizi wajibu wao!!! Wafanye kazi kwa bidii then wailaumu serikali kwa kutowajali, hapo hata sisi wananchi tutawatetea....siyo kwa mtindo huu wa kuzurula ovyo na kusubiri huo mshahara wanaouita mdogo! Wanaboa.
Bahati nzuro unachokiongea hukijui
Mwalimu ni mtu mwenye akili mno, usitegemee kushindana nae
 
Ni kweli walimu hawafundishi kwa 50% maana yake walimu hawasimamiwi kikamilifu.
Mtu wa kwanza kabisa kusimamia mwalimu afundishe ni mkuu wa shule.
Zitto amesema tatizo ni motisha kwa mwalimu.
pia ni tatizo ni motissha kwa msimaamizi. wakuu wa shule hawana hata posho mara nyingine hulazimika kutumia hele zao za mshahara kwa masuala ya shule mfano nauli na mawasiliano. wakuu hulazimika kwenda kazini hata wakati wa mapumziko kama siku za weekend.
Mara kwa mara wakuu huhitajika kwa afisaelimu na mikutano. kipindi wakuu hawapo walimu wengine hupata fursa ya kutega au kutoroka kazi
ni vizuri wakuu wapewe meno, insentives na posho. mawasiliano na ofisi ya afisa elimu yatumie zaidi tehama na mara chahe sana iwe physical contact probably Jumamossi lakini with posho au overtime.
Unamuweka mkuu kwenye mkutano masaa 10 hata maji ya kunywa hakuna kila wakati leta hiki leta kile humpi nauli wala nini halafu unalaumu walimu hawafundishi.
management is the same thing be in edecation health or factory.
Tujifunze ni kwa nini mameneja kwenye sekta binafsi wanapewa hata magari ...
Mkuu wa shule ana mshahara mdogo kuliko mwalimu anayemsimamia anaomba lift kwa malimu au anamwomba mwalimu mwenye gari akamchukulie mitihahani au ampeleke mtoto mgonjwa hospitali!
Tuanze na wakuu wa shule sio kwa masheria na makanuni tu bali kwa kuwawezesha wasimamie elimu tuone kama walimu hawatafundisha
Siasa inaharibu elimu!
 
Tatizo letu tunapenda kuharalisha uovu kwa uovu!!! Kwanini tusianze kulishughurikia hili la walimu kutotimiza wajibu wao then hayo mengine yafate? Inamaana unaona sawa tu walimu wanavyozurula ovyo mitaani wakati wanetu wako madarasani wakiwasubiri!!!? Huoni kama hili ni hatari zaidi!? Tunajenga kizazi kipi cha kesho!!? Comment za aina yako zinanipa picha kwanini miaka50+ ya uhuru bado tuko palepale.
Huwezi tatua tatizo bila kuanzia kwenye chanzo, uovu wa mwalimu umetengenezwa embu mfanyieni mwalimu yale anayostahili kisha akushindwa hapo tumshambulie kwa kila njia hata kum buruza mahakamani

Mkewe akitoka nje ya ndoa usikurupuke kumfukuza jichunguze kwanza unamapungufu gani halafu chukua hatua

Sikatai katika kundi kubwa la watu kuna wapuuzi tu watatokea, sasa ili kuwachuja embu tatueni hivi vilio vyao vya kuwalaza kwenye nyasi huko vijijini au kuwafanya waishi kwa mikopo ya vibanda vya akina mangi huko mijini
Baadae ndoo tuwachuje wapuuuzi
 
hapa kazi tu katika elimu ni ndoto kama hakuna insetives. Ndio, unaweza ukafanikiwa wakaingia darasanini, wakaandaa na hata kufundisha lakini ualimu ni zaidi ya hapo. yaya anaweza kumlisha mtoto chakula kama ulivoagiza lakini namna anavomlisha matters more than the food itself.
Mwalimu anaweze kuingia darasani lakini moyo wake na namna aqnavyofundisha matters too. there are so many little things that might be overlooked but very important in the process of teaching and learning. Motivation is one! huwezi kupima ufundishaji kama unavyohesabu tripu za mawe yaliyobebwa and the pay according to number of trips. paying teachers basing on attendance doesnt mean efficiency or effectiveness. therefore, denotatevely, teaching is more than teaching!
 
Back
Top Bottom