Mdudu halisi
JF-Expert Member
- May 7, 2014
- 2,730
- 4,768
Bila kuboresha maslahi yao, tusitarajie muujiza toka kwa walimu. Wataendelea kutofundisha kwani wengi wao wanatumia muda wa kazi kujiongezea kipato. Wengi wa walimu vijana ni bodaboda huku walimu ambao ni akina mama wa makamo kazi yao kubwa ni kuzungusha vitumbua na visheti mitaani. Suluhisho ja utoro wa walimu shuleni si kuwasema bungeni, bali ni kuwapatia mishahara inayokidhi angalau theluthi ya mahitaji yao pamoja na kuwapatia posho ya kufundisha na hata kuwapandisha vyeo kwa wakati. Hapo watakuwa wanabaki vituoni huku wakijituma kwa 100%