Zitto Kabwe na 'Saini za Wabunge 70' za kumg'oa Pinda - Tafsiri yangu

Ifikie wawakilishi wetu bungeni wasimamie utaifa badala ya kufumbia macho uozo. The country now is rotten. Wasipofanya hivyo watasulubiwa na wananchi.
 
Kwn wabunge wa upinzani tu, pekee yao saini zao si sinaweza kumwondoa mtoto wa mkulima(PINDA) au mpaka na saini za Magamba? Nimependa kujua idadi ya wabunge wa ccm na wale wa vyama vya upinzani?
 
Ingekuwa Kura ya kutokuwa na Imani na Rais ningeona kweli akina Zitto wana hoja ya maana, lakini kutokuwa na imani na Waziri mkuu sioni kama ni hoja yenye mashiko sana maana hata Pinda na wenzie wakitoka mchagua timu bado ni yule yule so what special there?

Wakimtoa Pinda basi Wassira anachukua kiti, mawaziri 90% wanarudishwa walewale hapo Zitto na timu yake watasemaje? watapiga kura ya pili au?
 
Bila ya vitisho au maombi ya kutoka wana-ccm nguli,kabla ya jumapili saini 70 zitapatikana na mkuu atang'olewa faster. Mbwa kala mbwa,mwisho wa ubaya aibu bana. Wao kwa wao wanageukana,subiri tu watasema yoooooote hadi kieleweke. Zitto komaaa,kitaeleweka tu makamanda
 
Wabunge wa CUF na CDM wote wanasaini hivi sasa ifikapo saa tano tutakuwa na sahihi zote zinazotakiwa. CCM wamesaini 10

Zittokabwe 2 hours ago.

Hii nimepata on twitter, hope its genuine.

Analysis ya Maggid naikubali! Na kama wamesign tayari watu 10 wa CCM basi hilo ni zege nene CDM wakisign wote ni 49 na hizo 10 jumla ni 59 hivyo zinakuwa zimesalia saini 11 tu. Na tayari tumeambiwa kuwa kuna wa CUF na NCCR waliosaini. Huo ni ujumbe mkubwa sana kwa PM na aliyemteua hata kama wale mawaziri watuhumiwa wataamua kujiuzulu leo.
 
Zitto ajichunge sana leo, UWT wataingia chumbani kwake leo kumpekua na kuiba list ya waliosaini ili isiwasilishwe bungeni jumatatu.!!
 
Huu ni mtego mkubwa kwa CCM na hata wabunge wote wa upinzani. Afadhali waweke saini alafu wasifikishe 51% ambayo itakuwa ni kura ya siri
 
Kazi kubwa ya Lukuvi akishirikiana na Wassira ni kuwatisha wenzie........!
Mkuu wanatakiwa wachanganye na za kwao, watakaa wanatishwa mpaka lin? mijitu mikubwa ile, ila watabana watabana mwishoe wataachia
 
Nape yuko wapi hapa? Aseme mwenyewe hawa wanaotafuna nchi ni wasafi zaidi ya wale madiwani anaodai wamekosa mvuto. We nape wewe, ungekuwa hauko katika hicho kiti ulichokalia am sure ungekuwa mkali kama pilipili kichaa. Unaona usalama wa kula yako u hatarini then unakumbatia magamba.
Kaka ZITO, tupo pamoja kaka, ukituhitaji wakati wowote tutakuja. Keep it up.
 
Huu ni mtihani mkubwa sana kwa serikali, nimejaribu kupitia kwenye website ya mkaguzi mkuu wa serikali kwa kweli kiwango cha ubadhirifu na wizi kinatisha. Katika mazingira haya nadhani hii ndiyo njia muafaka kabisa
 
Mjengwa CCM ni zaidi ya Ukimwi,hawaelewi chakufanya na badala yake wote wako njia panda,Tusubiri tuone
 
Ifikie wawakilishi wetu bungeni wasimamie utaifa badala ya kufumbia macho uozo. The country now is rotten. Wasipofanya hivyo watasulubiwa na wananchi.

Ni mashindano: UFISADI Vs UADILIFU. Ikiwa 70 hazitatimia ni kwamba ufisadi umeshinda!
waTanzania tuendelee kuteseka.
 
Ndugu zangu,

Leo asubuhi wakati nikifanya ' jogging' kwenye mitaa ya Dar es Salaam niliwasikia watu wa kawaida kabisa wakijiuliza na kujadili; " inakuwaje Serikali iwalipe marehemu mishahara huku sisi tulio hai hatuna hata uhakika wa milo miwili ya siku?" Wanauliza watu wa mitaani.

Naam, nchi yetu imekumbwa na mafuriko ya habari. Kule bungeni Dodoma kuna moto unawaka. Zimeitishwa sanini 70 ili Jumatatu ipigwe kura ya kukosa imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Ndio, kuna wanaotaka Pinda ang'oke, na labda kutolewa kafara, maana, siamini kama tatizo la msingi ni Pinda, bali ni la kimfumo zaidi. Na jana kuna mbunge wa CCM kayasema makali yafuatayo;

“Mheshimiwa Naibu Spika, inashangaza na kusikitisha kuwa nchi inatafunwa. Wanaofanya haya ni mawaziri wetu. Nchi inakufa na tuelewe kuwa Tanzania sio mali ya CCM, ni ya Watanzania wote.
“Mawaziri wetu wamekuwa mchwa, wanaangamiza nchi na leo nitamtaja waziri anayeongoza kwa kutafuta fedha za Watanzania. Ni Waziri wetu wa Fedha, Mustafa Mkulo. Ameuza viwanja, amelidanganya Bunge baada ya kuivunja CHC,”- Deo Filikunjombe ( CCM) Bungeni jana.

Lakini ya jana yalitanguliwa na ya juzi; Mbunge mwanadamizi wa CCM Godfrey Zambi aliyasema makali haya;

" CCM inaweza kung'olewa madarakani katika uchaguzi wa mwaka 2015 endapo kasi ya ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma itaendelea kama ilivyo sasa"- Godfrey Zambi ( CCM, Mbozi Mashariki).

Kauli za wabunge hao wawili wa CCM zinatoa tafsiri ya kilio cha wabunge wa CCM kuomba msaada kwa anayeweza kuwasaidia. Inatoa tafsiri pia kuwa hicho ni kilio cha wabunge wengi wa CCM. Kwamba hayo ndiyo wanayaongea hata chini chini.

Ndio, wananung'unika na wameanza kuiona adhabu wanayokwenda kuipata kutoka kwa wananchi ifikapo 2015. Wanaona pia, kuwa ' kisungura' hiki kidogo kinachopatikana kila mwaka kinavyoliwa na wajanja na wengine kuachiwa mifupa.

Wabunge wa CCM na wengine wanaona jinsi baadhi ya mawaziri wa kutoka chama chao wanavyojiangalia wenyewe kwa kujikatia zaidi kasungura hako kadogo na hata minofu mingine kuikimbizia kwenye majimbo yao badala ya kuangalia majimbo mengine pia. Hakika, Wabunge wa CCM sasa wanatoa kilio cha kuomba msaada na kilichochanganyika na hasira na hofu ya kupoteza mamlaka ya kuongoza dola ifikapo mwaka 2015. Ndio, kuna wanaokiona chama chao kikielekea kwenye kuzama 2015. Kelele wanazopiga bungeni zimegeuka kama kelele za nyikani, hazisikiki. Wameanza sasa kuwa na ujasiri wa kuzomeana wazi wazi kwenye vikao vyao badala ya kusubiri kuzomewa na wananchi hadharani. Naam, CCM ya sasa inapata tabu hata kwenye kujua namna ya kuitumia misamiati mipya ya kisiasa, maana, kuna wanaojivua gamba, wanaovuliwa magamba na sasa kuna ' wanaojinyambua' magamba wakiwa ndani ya chama- 'Political evolution' ya namna fulani.

Na Mtego wa Zitto Kabwe kwa CCM?

Jana Mbunge Zitto Kabwe ameitega CCM. Ni mtego wa hatari. Saini zile 70 zina maana hii;
- Kama wabunge wa CCM hawatachangamkia kutia sahihi zao zikavuka hata mia na hamsini, basi, kuna ujumbe unaopelekwa kwa umma. Kuwa wabunge wa CCM ni maneno tu, hawana dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi. Wabunge wengi wa CCM hawataiepuka adhabu ya umma inaweza kuwa inawasubiri 2015.
- Kwa wabunge wa CCM kutia sahihi zao na hata Pinda kupigiwa kura ya wabunge kukosa imani nae ina maana pia kuwa wabunge hawana imani na bwana mkubwa aliyemteua Pinda. Busara haiwataki wabunge wa CCM kufikia hapo. Hilo halina maslahi kwa taifa.

Nini kitakachotokea?


Kuna matatu;
Mosi, Mawaziri wale watano wanaotuhumiwa kwa ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma wanaweza kuepusha aibu kwa Serikali kwa wao wenyewe kutangaza kujiuzulu. Ingawa hili ni gumu kufanyika katika nchi hii, lakini, wakati mwingine kuna lazima ya kufanyika- maana, hapo watakuwa wamemnusuru Waziri Mkuu na aliyemteua.

Pili- Likishindikana la kwanza, basi, kabla ya Jumatatu, Waziri Mkuu Pinda awe ameshajiandaa kufanya maamuzi magumu. Kujiuzulu na kulinda heshima yake na ya aliyemteua. Au kutolewe ' Tamko la Serikali' litakalobadili upepo unaovuma sasa bungeni.

Tatu: La kwanza na la pili yaweza yasifanyike, na badala yake. Rais anaweza kuyaona yanayotokea sasa bungeni kama fursa ya kufanya mabadiliko makubwa Serikalini mara akitua Dar kutoka ziara ya Brazil.

Naam, yumkini pale Diamond Jubilee, kabla ya Jumatatu, kuna watakaopewa kazi ya kusafisha ukumbi na kupanga viti tayari kwa Mkuu wa Nchi kusema jambo kubwa kwa taifa kupitia kwa ' Wazee wa Darisalama'.

Na tusubiri tuone.

Maggid Mjengwa,
0788 111 765

kaka yetu macho na masikio tupo tayari kwa lolote
 
Back
Top Bottom