Zitto Kabwe Na Ajenda Yake Moja

JIMBONI KWAKE KAJENGA SHULE NGAPI?MAJI,VITUO VYA AFYA N.K naomba Mwandishi wa Zitto aende jimbo la MKONO au kwa LUKUVI ISMANI-IRINGA.

usimfananishe Zito na kina Mkono, wana pesa wale hawategemei serikali wanajenga kwa pesa zao mfukoni.
 
Karibu kwa Mchango wako wa kwanza wenye ujumbe mzito kuliko michango elfu moja ya baadhi ya wana JF humu.

Zitto aliingia mkataba wa kuwatumikia watu wake na hajafanya hilo,anasema hivi sasa anamiliki magari matano ndani ya miaka mitatu ya bungeni, chanzo chake ni watu wa Mwandiga waliompa ile fursa ya yeye kuwa Mbunge na kupata marupurupu hayo. sio sisi JF tuliompa nafasi hiyo.bahati mbaya wachangiaji wengine hapa wana roho mbaya na kuwachukia watu wa Mwandiga wasipelekewe maendeleo na mbunge wao.

Basil Mramba amejenga shule 32 jimboni mwake na mbili za ghorofa kwa msaada wa Waarabu, Yona pamoja na nafasi zote hajafanya kitu kwao.Anna Kilango anapiga vita ufisadi lakini hasahau watu wake wa SAME MASHARIKI kuwapelekea maendeleo.


DR.Salim Ahmed Salim analaumiwa na watu wake kwa kutokupeleka maendeleo kwao.wema huanzia nyumbani,Lwakatare kwa nafasi ya ubunge wa bukoba mjini miaka mitano iliyopita amewafanyia mambo mengi watu wake.kwanini Zitto tumdanganye kuwa ni kamanda wa nchi?


Kazi ya mbunge nikusukuma sheria za kutetea na kuwapa wanachi zitungwe au zifanya kazi
kufuatilia utekelezaji wa fedha za maendeleo ya halmashauri yake kama zinawekezwa kwenye miradi inayotarajiwa kama hayo hayafanyi utueleze.
Mramba shule alizojenga kwa hela ya mifuko ya misaada ya wizara ya fedha ndio zilizomfikisha awe na mgogoro kisheria we hujui hata KIKwete alikataa kata kata kufungua hiyo shule ya ghorofa alimuandalia chakula kwenye kasima yake kubwa kuliko Ikulu Dar es Salaam akakataa kula nadhani alikuwa mjinga alijua ni fisadi tuu

Mkono anatuhumiwa kwa kujinufaisha na fedha za malipo ya kusimamia mikataba ya kampuni ya ukaguzi na fedha za EPA amelipwa mabilioni ya fedha hata benk aliyoanzisha sijui kama inafanya kazi ni fisadi lakini hawawezi kumbana anajua siri ya mafisadi wa nchi hii kuliko mtanzania yeyote


mwache zitto atekeleze majukumu yake ya uzalendo
wapinzani wamepambana na mengi haya minayoyatengeneza kwenye mitandao kwao sawa na chai kwa sbabu wananchi wanajua ukweli
Nawewe kama blogger tuuleze umeifanyia nini nchi yako au upo hapa kubwabwaja tuu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom