Zitto Kabwe, Meles Zenawi Role Model Politician

Status
Not open for further replies.
Mkuu Ritz heshima sana,

Mkuu wangu Zitto hana sifa za kugombea urais wa JMT kwa katiba ya sasa ambayo imebainisha wazi umri wa kugombea ni miaka 40.Katiba mpya inaweza kufanyiwa marekebisho ya kupunguza umri ili kukidhi matakwa ya Zitto kugombea nafasi hiyo kubwa na nyeti hapa nchini Tanzania.

Iwapo katiba mpya itafanyiwa marekebisho ya kupunguza umri Zitto atakuwa na sifa ya kugombea urais wa JMT.Chama chake hakitakuwa na kipingamizi cha kumzuia atashindanishwa na wanachama wengine atakayepata kura nyingi kuliko wenzake atapewa nafasi ya kugombea.

Zitto Kabwe atatakiwa kujiweka karibu na wanachama wa chama chake kwa kushiriki kukijenga na kuhakikisha kinaenea kila pembe ya nchi.Operesheni zinazoendelea kama Sangara na M4C ni jukwaa atakalotakiwa kulitumia vyema ili kujiweka karibu na wanachama na wapenzi wa CDM wakati huo huo akiomba katibu mpya ya mwaka 2014 ipunguze umri wa mgombea urais.

Maoni yangu mpaka sasa sijaona Zitto akishiriki kukijenga chama chake kupitia M4C badala yake ameanzisha kikundi chake nje ya programs za chama chake kwa minajili ya kutengeneza mazingira yatakayomhakikishia anapewa nafasi ya kupeperusha bendera ya chama.Nadhani bado unakumbuka mbunge wa Kigoma Kusini Mheshimiwa David Kafulila alivyokuwa akibwabwaja bungeni kwamba sasa ni zamu ya Kigoma !.

kafulila alikosea sana kwamba sasa ni zamu ya kigoma wakati wenye chama chetu bado hatujatoa rais hata mara moja(kaskazini)
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu gongo za mchana ni mbaya sana,anadhani watanzania wa leo ni wajinga tena.Mkuu vipi maandalizi ya Jumamosi mzambarauni? PoliCCM wametoa kibali?

Msisipokuwa makini na madude ya kwa pele yatawafanya makamanda muwe kama jamaa zetu wanaokaa kwenye vituo vya madaladala, siku zote mkuu chama kawapa ushauri hamtaki kufuata.
 
Last edited by a moderator:
Kuna mpasuko mwingine wa dhahiri ambayo unafukuta ndani ya Bavicha na Bawacha, kuna kambi tatu kubwa inayojumuisha Mbowe na Dr Slaa, na ile ya Zitto inayojumuisha Bavicha pamoja na Bawacha ambapo kuna wafuasi wake wengi.
 
Hiyo thread sina uhakika kama ritz alishawahi kutoa comment yake. Na akama alitoa comment atakuwa hajaipitia muda mrefu sana hata kabla hajaanzisha huu uzi wake wa ramli.

Mwita Maranya,
Punguza Mapuya, huwezi kushinda urais kwa kura 500 za JF wakati watanzania tupo zaidi ya milioni 40.
 
Last edited by a moderator:
Mimi sasa naamini wanaCCM ndiyo wanaomkwamisha Zitto.Niseme maneno machache sana kwamba CDM haitampitisha kibaraka yeyote wa CCM kugombea urais kupitia CDM.Pili hao vijana wanaomuunga Zitto nchi nzima labda ni mizimu na si binadamu mfano mdogo kuna kura ya maoni inayoendelea hapa JF kati ya Zitto na shujaa asiyeyumba Dr Slaa na wapigaji wa kura ni vijana wasomi sasa kura alizo nazo Zitto mbona ni Aibu? Tangu lini CDM ikatishika na vibaraka wa CCM walioko CDM?

hao vijana wasomi wanaompigia kura slaa humu jf sio wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema taifa kwa hio hawana impact yeyote kama huamini muulize mbowe kilicho mkuta 2009 amshukuru mkwe wake mtei kuja kumuokoa.mwakani zitto anaanzisha oparesheni ondoa wachaga chadema utaona mziki wake.
 
Mkuu Mvaa Tai, the motive behind ni nia dhalimu iliyofichika ya mleta mada ili kutengeneza reaction fulani kwa mada yake!.

Hebu msome hapa!.

"Kwa mujibu watu wa karibu wa Zitto Kabwe", yupo tayari kuishi na kufa akiwa kwenye mapambano " Huu ni uzushi tuu, hakuna watu wowote wa karibu na ZZK, bali ameisoma makala ya ZZK kuhusu Zenawi na sasa anaitumia kumjengea chuki ZZK ili kuwatia hofu wana Chadema kuwa ZZK yuko tayari kupambana hadi kufa ili kuwa mgombea wa Chadema!.

"Wafuasi wa Zitto Kabwe wametoa onyo kwa Mbowe" Huu pia ni uzushi, hakuna mfuasi yoyote aliyetoa onyo lolote kwa yeyote!.

"mkakati wowote mchafu wa kutaka kumkwamisha Zitto kugombea urais" - Huu pia ni uzushi ili kuonyesha kuna mkakati wa kutaka kumkwamisha ZZK kugombea!

" ZZK ndiye anayekubalika" Hakuna survey yoyote iliofanyika kuthibitisha kuwa ZZK ndiye anayekubalika!

"wafuasi wa Zitto ambao wengi ni kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Tanga, Mtwara, Lindi, Singida, Pwani, Ruvuma" Huu pia ni uzushi kwa lengo la kuwaaminisha watu kuwa ni kweli Chadema kina ukabila, hivyo kujenga dhana kuwa ukiondoa kanda ya Kaskazini, wafuasi wengine wote wa Chadema wa mikoa yote hiyo ni wafuasi wa ZZK!.

"mkakati wa Mbowe na Dr Slaa kutaka kumzuia ZZK" huu pia ni uzushi, hakuna mkakati wowote wa kiongozi yoyote wa Chadema kumzua mwanachama yoyote kugombea nafasi yoyote!.

"endapo watathubutu kumzuia basi watamuua kuwapigia kura wagombea wa vyama vingine lakini si Chadema" huu pia ni uzushi wa tisha toto ili kujenga hoja kuwa ushindi kwa Chadema 2015 ni kupitia kwa ZZK pekee, bila ZZK hakuna ushindi kwa Chadema!

"Zitto Kabwe inasemekana ndiye ambaye anaungwa mkono na karibu vijana wote wa nchi hii walioko ndani na nje ya Chadema, na hasa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini," huu pia ni uzushi wenye lengo la kumjengea chuki ZZK!.

Itakumbukwa mwaka 2010 wakati wa kampeni za ubunge jimboni kwake Zitto Kabwe aliwaambia wapiga kura wake wampe muhula wa mwisho mwaka 2015 hatagombea tena ubunge" Ni kweli ZZK aliomba mhula wa mwisho ila sio kweli aliaga ili akagombee urais bali alipanga kuingia kwenye a totally diferent venture away from politics!.

Lengo ni "ill motives"!.

Pasco.

NB: Pasco wa jf, sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa Chadema, bali kama mwanahabari, ninayo direct access kwa top leadership ya Chadema, kama ilivyo kwa CCM, CUF na vyama vingine vyote, na nimeiunga mkono presidential bid ya ZZK kupitia Chadema, kwa CCM naiunga mkono presidential bid ya EL, kwa CUF, Prof. Lipumba ndie mgombea urais wa kudumu wa CUF bara na Maalim kule Zanzibar ila naunga mkono bid ya Jussa kumpokea Maalim, 2020!.

Pasco umetumia nguvu nyingi sana za kifikra kwenye hoja mfu, potofu na ya kijinga

Although .... good job
 
Mimi sasa naamini wanaCCM ndiyo wanaomkwamisha Zitto.Niseme maneno machache sana kwamba CDM haitampitisha kibaraka yeyote wa CCM kugombea urais kupitia CDM.Pili hao vijana wanaomuunga Zitto nchi nzima labda ni mizimu na si binadamu mfano mdogo kuna kura ya maoni inayoendelea hapa JF kati ya Zitto na shujaa asiyeyumba Dr Slaa na wapigaji wa kura ni vijana wasomi sasa kura alizo nazo Zitto mbona ni Aibu? Tangu lini CDM ikatishika na vibaraka wa CCM walioko CDM?

Hivi kweli Kura za maoni za JF ndio unataka kufanya reference, kwanza tambua JF kuna Multple ID's zaidi ya 11,000 NtuNTEMEKE peke yake ana ID's 19, inawezekana wewe umempigia kura Dr Slaa hata mara 10...Watanzania tupo zaidi milioni 40 na kura za humu JF ni kura 300 uoni kama kichekesho mkuu.
 
Last edited by a moderator:
hahahaha leo wanagombana wenyewe.wananuka midomooooo kwa kufume.
 
Ignorance causes darkness

Mods JF,
Ebu kuweni makini na hizi Multiple ID's ambazo kazi yao ni kuchafua mijadala, kama huyu mpuuzi anajiita mdizi mnamjua vizuri ana ID's zaidi ya kumi lakini mnamuacha kama mtashindwa kumchukulia hatua mie binafsi tachukuwa sheria mikononi nipambane nae.
 
Hivi katiba ya nchi inaruhusu mgombea Urais mwenye umri wa miaka chini ya 40?
 
Poleni sana wana-JF woote mlionaswa kwenye mtego huu wa Ritz (aka Ritz-One).
Nawapa pole kwa sababu mmenasw kwenye kitu inaitwa political diversion.
Nimeshawahi mara kadhaa kutoa angalizo kama hili hapa JF.
Kuna watu huwa wanatumia sana hii 'political diversion' kuwavuta watu nje au mbali na mjadala muhimu unaoendelea, au kuwachokoza makusudi ili kuwasahaulisha mambo muhimu.
Huyu jamaa Ritz ni mtetezi na muungaji mkono wa udhalimu wa serikali ya ccm. Sasa kwa sasa kazi yake kubwa aliyopewa ni kujaribu kuwavuta watu mbali sana ma tukio kubwa la mauaji yaliyofanywa na polisi.
Atakuja hapa na thread za kuchokoza watu wamjibu, au watu wajibizane wenyewe, na kusahau tukio baya la udhalimu wa serikali ccm uliofanywa na polisi kule Iringa.

Wana JF angalieni sana hizi 'diversions' zinazotumiwa na ccm kwa kupitia vibaraka wao kama Ritz na wengineo.

Nilitoa mfano wa 'diversion' kama hizi huko nyuma:-
Mfano:-
Mwizi akiiba pesa nyingi za umma na kuanza kukimbia mbio, halafu watu wakaanza kumkimbiza ili wamkamate apelekwe kwenya vyombo vya sheria. Fisadi huyo akianza kurusha mabunda ya pesa barabarani kwa watu wanaomkimbiza, Je ? watu wataendelea kumkimbiza, au wataanza kuokota mabunda ya pesa zilizorushwa barabarani??

Hii ndio kazi aliyopewa Ritz na wenzake wapatao elfu mbili ili waje kwenye mitandao ya kijamii kuleta 'diversions' kama hizi.

Ritz na wenzako wote kumbukeni kuwa:
  • Hata mfanye nini, damu ta watanzania wasio na hatia inawalilia, na hakika, mtalipa kila tone la damu mliyoimwaga kwa kutumia polisi.
  • Na hakika atawalaye kwa upanga, atakufa kwa upanga, na amwagaye damu isiyo na hatia, damu yake itamwagwa hakika.
 
Mods JF,
Ebu kuweni makini na hizi Multiple ID's ambazo kazi yao ni kuchafua mijadala, kama huyu mpuuzi anajiita mdizi mnamjua vizuri ana ID's zaidi ya kumi lakini mnamuacha kama mtashindwa kumchukulia hatua mie binafsi tachukuwa sheria mikononi nipambane nae.

Hii mada ya kijinga ... imejaa upuuzi ... na umeonyesha upuuzi kwa kuingiza hoja ya kipuuzi ambayo hata kama inaukweli ungetakiwa kupeleka kwenye jukwaa husika la complaints

Ficha upumbafu wako ... By Invincible
 
Mwita Maranya,
Punguza Mapuya, huwezi kushinda urais kwa kura 500 za JF wakati watanzania tupo zaidi ya milioni 40.

Ritz unaandika nini wewe kichwa cha kuku. Hujui kwamba hao watanzania milioni 40 ndio walimpigia kura Dr. Slaa 2010 na ndio hao mlichakachua kura zao ili kumrejesha kikwete magogoni?
Hao hao watanzania milioni 40 ndio wanaompokea kwa mikono miwili Dr. Slaa kila mahali anapokwenda hadi mmeamua kuwaua vifo vya fedheha?
Punguza kunywa chang'aa asubuhi asubuhi!
 
Last edited by a moderator:
hao vijana wasomi wanaompigia kura slaa humu jf sio wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema taifa kwa hio hawana impact yeyote kama huamini muulize mbowe kilicho mkuta 2009 amshukuru mkwe wake mtei kuja kumuokoa.mwakani zitto anaanzisha oparesheni ondoa wachaga chadema utaona mziki wake.

Unafikiri wapiga kura wa Chadema ni matutusa kama ninyi magamba? Mitandaoni tupo na kwenye vikao vya maamuzi tupo vilevile.
 
Mimi sasa naamini wanaCCM ndiyo wanaomkwamisha Zitto.Niseme maneno machache sana kwamba CDM haitampitisha kibaraka yeyote wa CCM kugombea urais kupitia CDM.Pili hao vijana wanaomuunga Zitto nchi nzima labda ni mizimu na si binadamu mfano mdogo kuna kura ya maoni inayoendelea hapa JF kati ya Zitto na shujaa asiyeyumba Dr Slaa na wapigaji wa kura ni vijana wasomi sasa kura alizo nazo Zitto mbona ni Aibu? Tangu lini CDM ikatishika na vibaraka wa CCM walioko CDM?

Naunga mkono hoja by 100%.
 
Mods JF,
Ebu kuweni makini na hizi Multiple ID's ambazo kazi yao ni kuchafua mijadala, kama huyu mpuuzi anajiita mdizi mnamjua vizuri ana ID's zaidi ya kumi lakini mnamuacha kama mtashindwa kumchukulia hatua mie binafsi tachukuwa sheria mikononi nipambane nae.

www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/298724-kura-ya-maoni-zitto-vs-dr-slaa-29.html
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom