Zitto Kabwe, Meles Zenawi Role Model Politician

Status
Not open for further replies.
Mkuu Ritz,

nyie ndio mnazidi kumharibia Zitto. Kwanini wana CCM ndio mnaoongoza kumtetea? Wewe ni kada wa CCM sasa unataka Zitto awe rais kuliko unavyotaka kwa mgombea wa CCM? Hizi siasa mngewaachia wale wazee na nyie mjikite kusafisha chama chenu kiuzike kwa watanzania 2015 maana at that time hata Jeshi halitaweza kuwasaidia kubaki ktk Dola!!!
 
Funguka Pasco, mimi nipo puzzled
Mkuu Mvaa Tai, the motive behind ni nia dhalimu iliyofichika ya mleta mada ili kutengeneza reaction fulani kwa mada yake!.

Hebu msome hapa!.

"Kwa mujibu watu wa karibu wa Zitto Kabwe", yupo tayari kuishi na kufa akiwa kwenye mapambano " Huu ni uzushi tuu, hakuna watu wowote wa karibu na ZZK, bali ameisoma makala ya ZZK kuhusu Zenawi na sasa anaitumia kumjengea chuki ZZK ili kuwatia hofu wana Chadema kuwa ZZK yuko tayari kupambana hadi kufa ili kuwa mgombea wa Chadema!.

"Wafuasi wa Zitto Kabwe wametoa onyo kwa Mbowe" Huu pia ni uzushi, hakuna mfuasi yoyote aliyetoa onyo lolote kwa yeyote!.

"mkakati wowote mchafu wa kutaka kumkwamisha Zitto kugombea urais" - Huu pia ni uzushi ili kuonyesha kuna mkakati wa kutaka kumkwamisha ZZK kugombea!

" ZZK ndiye anayekubalika" Hakuna survey yoyote iliofanyika kuthibitisha kuwa ZZK ndiye anayekubalika!

"wafuasi wa Zitto ambao wengi ni kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Tanga, Mtwara, Lindi, Singida, Pwani, Ruvuma" Huu pia ni uzushi kwa lengo la kuwaaminisha watu kuwa ni kweli Chadema kina ukabila, hivyo kujenga dhana kuwa ukiondoa kanda ya Kaskazini, wafuasi wengine wote wa Chadema wa mikoa yote hiyo ni wafuasi wa ZZK!.

"mkakati wa Mbowe na Dr Slaa kutaka kumzuia ZZK" huu pia ni uzushi, hakuna mkakati wowote wa kiongozi yoyote wa Chadema kumzua mwanachama yoyote kugombea nafasi yoyote!.

"endapo watathubutu kumzuia basi watamuua kuwapigia kura wagombea wa vyama vingine lakini si Chadema" huu pia ni uzushi wa tisha toto ili kujenga hoja kuwa ushindi kwa Chadema 2015 ni kupitia kwa ZZK pekee, bila ZZK hakuna ushindi kwa Chadema!

"Zitto Kabwe inasemekana ndiye ambaye anaungwa mkono na karibu vijana wote wa nchi hii walioko ndani na nje ya Chadema, na hasa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini," huu pia ni uzushi wenye lengo la kumjengea chuki ZZK!.

Itakumbukwa mwaka 2010 wakati wa kampeni za ubunge jimboni kwake Zitto Kabwe aliwaambia wapiga kura wake wampe muhula wa mwisho mwaka 2015 hatagombea tena ubunge" Ni kweli ZZK aliomba mhula wa mwisho ila sio kweli aliaga ili akagombee urais bali alipanga kuingia kwenye a totally diferent venture away from politics!.

Lengo ni "ill motives"!.

Pasco.

NB: Pasco wa jf, sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa Chadema, bali kama mwanahabari, ninayo direct access kwa top leadership ya Chadema, kama ilivyo kwa CCM, CUF na vyama vingine vyote, na nimeiunga mkono presidential bid ya ZZK kupitia Chadema, kwa CCM naiunga mkono presidential bid ya EL, kwa CUF, Prof. Lipumba ndie mgombea urais wa kudumu wa CUF bara na Maalim kule Zanzibar ila naunga mkono bid ya Jussa kumpokea Maalim, 2020!.
 
Mkuu Ritz heshima sana,

Mkuu wangu Zitto hana sifa za kugombea urais wa JMT kwa katiba ya sasa ambayo imebainisha wazi umri wa kugombea ni miaka 40.Katiba mpya inaweza kufanyiwa marekebisho ya kupunguza umri ili kukidhi matakwa ya Zitto kugombea nafasi hiyo kubwa na nyeti hapa nchini Tanzania.

Iwapo katiba mpya itafanyiwa marekebisho ya kupunguza umri Zitto atakuwa na sifa ya kugombea urais wa JMT.Chama chake hakitakuwa na kipingamizi cha kumzuia atashindanishwa na wanachama wengine atakayepata kura nyingi kuliko wenzake atapewa nafasi ya kugombea.

Zitto Kabwe atatakiwa kujiweka karibu na wanachama wa chama chake kwa kushiriki kukijenga na kuhakikisha kinaenea kila pembe ya nchi.Operesheni zinazoendelea kama Sangara na M4C ni jukwaa atakalotakiwa kulitumia vyema ili kujiweka karibu na wanachama na wapenzi wa CDM wakati huo huo akiomba katibu mpya ya mwaka 2014 ipunguze umri wa mgombea urais.

Maoni yangu mpaka sasa sijaona Zitto akishiriki kukijenga chama chake kupitia M4C badala yake ameanzisha kikundi chake nje ya programs za chama chake kwa minajili ya kutengeneza mazingira yatakayomhakikishia anapewa nafasi ya kupeperusha bendera ya chama.Nadhani bado unakumbuka mbunge wa Kigoma Kusini Mheshimiwa David Kafulila alivyokuwa akibwabwaja bungeni kwamba sasa ni zamu ya Kigoma !.
 
Last edited by a moderator:
Ritz baada ya kuishiwa hoja za kupost sasa umeanza kupiga ramli.
Sisi ni wacha Mungu hatuogopi wala kutishwa na ramli za waganga njaa wa ccm.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Pasco
Ritz ni Mtu ambaye anaeleweka hapa JF na wala hamtishi mti kwa Propaganda zake. Ritz hana tofauti na Martin Shigela. Ritz ni kijana asiyejiamini kwa kila anachokipost hapa ndio maana mara nyingi akipost hapa JF watu wakimjibu anamwita chama aje kumsaidi ila naona siku hizi chama amegundua kutetea Propaganda za Ritz ni kujishushia Thamani

Nilishamwalika katika Mnakasha Ulioanzishwa na Mwana CCM mwenzake Mchambuzi lakini Ritz hakutokea nikathibisha Maneno ya Mchambuzi kwamba CCM inakosa Mvuto kwa sababu ya Vijana kama akina Ritz
 
Last edited by a moderator:
Iwe kweli au si kweli
kitendo cha Zitto kumlilia sana Meles Zenawi
ni kitendo cha kushangaza mno...

Zenawi alikuwa dikteta period...

Zitto amekuwa Zitto kwa sababu ya demokrasia na uhuru ambao wapinzani wa Zenawi
hawana.......

Sasa Zitto ame over look yoote hayo na kujifanya 'analia saana' kwa kifo cha dikteta wa Ethiopia
tena wazi wazi bila kificho.......ni very alarming na very 'ugly ' to see that....

Zitto deep down ni mwana demokrasia?
au deep down ni Dikteta kama Zenawi,Kagame na wengine?

What if akawa Rais na kuwa Dikteta tena bila 'akili za kina Kagame'???

akawa na akili za JK na udikteta juu?????????
 
Thread ya ki-ZUZU kabisa hii! Kwani Meles Zenawi (role model wa ZZK) alipambana na nani? Waliokuwa kwenye chama chake au utawala mbovu wa Mengistu uliokuwa madarakani ukiwakandamiza wanyonge.

Otherwise, kama upuuzi wa thread hii ni sahihi then Meles Zenawi sio role model wa ZZK kwani (Meles) hakupambana na walio wake bali adui na hiyo ina-justify tetesi za muda mrefu kwamba jamaa ni msaliti na ritz ametuthibitishia hilo.

Vinginevyo, komeni kabisa kumchonganisha Zitto na chama chake.

dudus,

Nadhani hujui historia ya Meles Zenawi, na Mfalme Mangistu, ngoja nikupe darsa kidogo.

Mapambano ya Zenawi chini ya mwamvuli wa kikundi chake cha Ethiopia People's Revolutionary Democratic Front (EPRDF) na Mfalme Mangistu yalilenga kutokomeza utawala wa kiimla, wa kikabila, na wa kiuneo kwa faida ya makabila yote ya nchi hiyo, hali hiyo ya Ethiopia ya wakati huo wa utawala wa Mfalme Mangistu, haina tofauti tofauti na hali ilivyo sasa kwa Chadema ambayo inapigania maslahi ya mikoa mitatu ya Kaskazini Kilimanjaro, Arusha, Manyara.
 
Last edited by a moderator:
Mimi sasa naamini wanaCCM ndiyo wanaomkwamisha Zitto.Niseme maneno machache sana kwamba CDM haitampitisha kibaraka yeyote wa CCM kugombea urais kupitia CDM.Pili hao vijana wanaomuunga Zitto nchi nzima labda ni mizimu na si binadamu mfano mdogo kuna kura ya maoni inayoendelea hapa JF kati ya Zitto na shujaa asiyeyumba Dr Slaa na wapigaji wa kura ni vijana wasomi sasa kura alizo nazo Zitto mbona ni Aibu? Tangu lini CDM ikatishika na vibaraka wa CCM walioko CDM?
 
Wanabodi,

Zitto Kabwe mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Chadema na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Naibu Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.

Kwa mujibu watu wa karibu wa Zitto Kabwe, yupo tayari kuishi na kufa akiwa kwenye mapambano kama ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi, ambaye ni kipenzi chake alianza mapambano na aliyekuwa Mfalme wa Ethiopia Haile Mariamu, akiwa na umri wa miaka 19 na hatimaye kufanikisha mapambano yake ya kuingia Ikulu akiwa na umri wa miaka 36.

Wafuasi wa Zitto Kabwe wametoa onyo kwa Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho kuwa mkakati wowote mchafu wa kutaka kumkwamisha Zitto kugombea urais wakati ndiye anayekubalika utakigharimu chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wafuasi wa Zitto ambao wengi ni kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Tanga, Mtwara, Lindi, Singida, Pwani, Ruvuma, wanapinga mkakati wa Mbowe na Dr Slaa kutaka kumzuia endapo watathubutu kumzuia basi wataamua kuwapigia kura wagombea wa vyama vingine lakini si Chadema.

Zitto Kabwe inasemekana ndiye ambaye anaungwa mkono na karibu vijana wote wa nchi hii walioko ndani na nje ya Chadema, na hasa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, Itakumbukwa mwaka 2010 wakati wa kampeni za ubunge jimboni kwake Zitto Kabwe aliwaambia wapiga kura wake wampe muhula wa mwisho mwaka 2015 hatagombea tena ubunge bali atagombea urais ili aweze kuwatumikia Watanzania wote kwa ujumla wao.
Bado kijana mdogo mwacheni kwanza akue angalau afikishe miaka 45 tumwandae labda aje agombee 2020 ili tumwelewe vizuri.Je Zito Kagwe ameoa?
 
Zitto ukiona mpaka unashabiikiwa na huyu mwenye sura chafu ritz ujue umekwisha na cdm tunakuli timing tu.......tamaa,sifa na uroho ndio vimekufikisha hapo..........
 
Wanabodi,

Zitto Kabwe mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Chadema na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Naibu Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.

Kwa mujibu watu wa karibu wa Zitto Kabwe, yupo tayari kuishi na kufa akiwa kwenye mapambano kama ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi, ambaye ni kipenzi chake alianza mapambano na aliyekuwa Mfalme wa Ethiopia Haile Mariamu, akiwa na umri wa miaka 19 na hatimaye kufanikisha mapambano yake ya kuingia Ikulu akiwa na umri wa miaka 36.

Wafuasi wa Zitto Kabwe wametoa onyo kwa Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho kuwa mkakati wowote mchafu wa kutaka kumkwamisha Zitto kugombea urais wakati ndiye anayekubalika utakigharimu chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wafuasi wa Zitto ambao wengi ni kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Tanga, Mtwara, Lindi, Singida, Pwani, Ruvuma, wanapinga mkakati wa Mbowe na Dr Slaa kutaka kumzuia endapo watathubutu kumzuia basi wataamua kuwapigia kura wagombea wa vyama vingine lakini si Chadema.

Zitto Kabwe inasemekana ndiye ambaye anaungwa mkono na karibu vijana wote wa nchi hii walioko ndani na nje ya Chadema, na hasa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, Itakumbukwa mwaka 2010 wakati wa kampeni za ubunge jimboni kwake Zitto Kabwe aliwaambia wapiga kura wake wampe muhula wa mwisho mwaka 2015 hatagombea tena ubunge bali atagombea urais ili aweze kuwatumikia Watanzania wote kwa ujumla wao.

www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/298724-kura-ya-maoni-zitto-vs-dr-slaa-29.html
 
Mimi sasa naamini wanaCCM ndiyo wanaomkwamisha Zitto.Niseme maneno machache sana kwamba CDM haitampitisha kibaraka yeyote wa CCM kugombea urais kupitia CDM.Pili hao vijana wanaomuunga Zitto nchi nzima labda ni mizimu na si binadamu mfano mdogo kuna kura ya maoni inayoendelea hapa JF kati ya Zitto na shujaa asiyeyumba Dr Slaa na wapigaji wa kura ni vijana wasomi sasa kura alizo nazo Zitto mbona ni Aibu? Tangu lini CDM ikatishika na vibaraka wa CCM walioko CDM?

Mkuu Molemo reaction yako ndiyo Akina Ritz wanaitafuta. STUKA Mkuu.
 
Last edited by a moderator:
kabla hajafikia kuwa Meles atakuwa ameshakimbizwa CDM.Washauri wake mmemshauri atafute urais kwenye facebook
na twitter
 
Kamanda zitto ,mpambanaji wa kweli,mwenye uwezo wakulikomboa taifa hili ni wewe,na sisi wazee wa kaskazini tumeamua kukuunga mkono katika harakati zako za ukomboni.jipe moyo mkuu kijana wetu!

We kilaza futa neno mbeya kwenye id yako coz watu wa mbeya hatuko wajinga kias hcho..
 
Ikumbukwe mwaka 2009 Zitto alichukuwa fomu ya kugombea ya uenyekiti wa Chadema, akimpinga Mbowe ambaye tayari alikuwa amechukuwa fomu ya kugombea kipindi kingine cha pili hali iliyoleta kizazaa kikubwa ndani ya chama hicho, kabla ya wazee kuingilia kati na kushauri Zitto aondoe jina lake. Wafuasi wa kambi ya Zitto safari hii wamesema wamejipanga kimkakati kuhakisha kwamba Zitto anagombea uenyekiti.[WENYE UAMUZI NI KAMATI KUU YA CHAMA NA SIYO MBOYOYO KAMA NYIE.
Sidhani kama kuna kura yoyote ya maoni imepigwa kuhalalisha hisia zako. Na pia kukubalika kwa mtu katika nafasi fulani ya uongozi kuna vigezo vingi vya kuzingatia. Urais ni moja ya nafasi nyeti sana katika nchi, si ya kukimbilia wala ya kufanyia majaribio. Kati ya sifa nyingi za urais, uadilifu unazitangulia, si tu kwamba mtu awe muadilifu, bali pasiwe na chembe ya shaka juu ya uadilifu wake.
 
Kamanda zitto ,mpambanaji wa kweli,mwenye uwezo wakulikomboa taifa hili ni wewe,na sisi wazee wa kaskazini tumeamua kukuunga mkono katika harakati zako za ukomboni.jipe moyo mkuu kijana wetu!

www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/298724-kura-ya-maoni-zitto-vs-dr-slaa-29.html
 
Sidhani kama kuna kura yoyote ya maoni imepigwa kuhalalisha hisia zako. Na pia kukubalika kwa mtu katika nafasi fulani ya uongozi kuna vigezo vingi vya kuzingatia. Urais ni moja ya nafasi nyeti sana katika nchi, si ya kukimbilia wala ya kufanyia majaribio. Kati ya sifa nyingi za urais, uadilifu unazitangulia, si tu kwamba mtu awe muadilifu, bali pasiwe na chembe ya shaka juu ya uadilifu wake.

www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/298724-kura-ya-maoni-zitto-vs-dr-slaa-29.html
 
dudus,

Nadhani hujui historia ya Meles Zenawi, na Mfalme Mangistu, ngoja nikupe darsa kidogo.

Mapambano ya Zenawi chini ya mwamvuli wa kikundi chake cha Ethiopia People's Revolutionary Democratic Front (EPRDF) na Mfalme Mangistu yalilenga kutokomeza utawala wa kiimla, wa kikabila, na wa kiuneo kwa faida ya makabila yote ya nchi hiyo, hali hiyo ya Ethiopia ya wakati huo wa utawala wa Mfalme Mangistu, haina tofauti tofauti na hali ilivyo sasa kwa Chadema ambayo inapigania maslahi ya mikoa mitatu ya Kaskazini Kilimanjaro, Arusha, Manyara.

www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/298724-kura-ya-maoni-zitto-vs-dr-slaa-29.html
 
Last edited by a moderator:
Iwe kweli au si kweli
kitendo cha Zitto kumlilia sana Meles Zenawi
ni kitendo cha kushangaza mno...

Zenawi alikuwa dikteta period...

Zitto amekuwa Zitto kwa sababu ya demokrasia na uhuru ambao wapinzani wa Zenawi
hawana.......

Sasa Zitto ame over look yoote hayo na kujifanya 'analia saana' kwa kifo cha dikteta wa Ethiopia
tena wazi wazi bila kificho.......ni very alarming na very 'ugly ' to see that....

Zitto deep down ni mwana demokrasia?
au deep down ni Dikteta kama Zenawi,Kagame na wengine?

What if akawa Rais na kuwa Dikteta tena bila 'akili za kina Kagame'???

akawa na akili za JK na udikteta juu?????????

That is why I love this forums...no stone is left unturned...teh teh teh
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom