Zitto Kabwe live on TBC-1 Asubuhi Hii

Baada ya kusifu, Zitto ameanza kupiga nyundo. Ameikandia stimulus package kuwa haitastimulate chochote bali kufidia madeni na makali ili mambo yawe kama yalivyokuwa kabla ya msukosuko.

Amesema hajaona stimulus ya kustimulate ukuaji wa uchumi ama kuongeza uzalishaji, huu ni ulaji mwingine mnene on the pipeline.

Alipotaka kupiga nyundo kubwa zaidi, matangazo yakakatika ghafla, studio Dar wakaingilia kati na kutangaza ni matatizo ya kiufundi. Sasa wameweka hutuba ya JK ya jana kusubiria kama mitambo itatengamaa, tusubiri....

Huo ndiyo utaratiu wetu Mkuu Pasco!!! Hiyo ni order ilitoka!!! Unakumbuka siku EL alienda TBC1 na wakarusha kipindi ili ajisafishe kuhusu lile sakata la Rich wa Monduli. Order ilitoka, mitambo puuu!!!! Zitto ni mtaalam na wangempa nafasi angegalagaza the so called Stimus of the 2010 election then ingeonekana zero i.e ange-m-dilute Mkuu kabisa. Kazi kweli kweli!!
 
Running order ya Kipindi cha Jambo Afrika, Jambo Tanzania ambacho kinarushwa live na Televisheni ya Taifa, TBC-1, kila siku kuanzia saa 12:00-2:00 asubuhi kimeonyesha Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mh. Zitto Zuberi Kabwe atahojiwa live kwenye kipindi hicho akiwa mjini Dodoma.

Mhe. Zitto aliongea kwa dakika kama 5 matangazo yakakatika kwa sababu za kiufundi.
Tundu Lissu pia kuna siku ataalikwa
P
 
Back
Top Bottom