Zitto Kabwe live on TBC-1 Asubuhi Hii

mbona una kimbilia kutetea? Kwani watu wame fikiria hivyo au wewe ndiyo una jaribu kuweka wazo hilo kwenye akili za watu? Umekua too defensive kwenye kauli yako kana kwamba watu washa sema wana fikiri hivyo. Wacha wenyewe waseme au wewe spokesperson wao?
Lengo ni to make the long story short, Bunge limeanza live na matangazo ya TBC-1 yanakatika katika, katu katu na sasa wamesitisha kidogo wanapiga muziki... Yamerudi sauti mbovu sana. Ikumbukwe Pinda ndiye anafuatia na maswali live.
 
Mod ondoa breaking news, sio breaking news tena, Breaking news sasa ni maswali live kwa PM, Mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed ameanza na swali kuhusu sakata la vitambulisho Zanzibar!.
 
Pinda keshaanza kuulizwa maswali .Kaanza Hamadi Rashid kuhusu kunyimwa haki ya kupiga kura Wazanzibar kwa kukosa kipande. Pinda anasema hajui kipande ni nini
 
Baada ya kusifu, Zitto ameanza kupiga nyundo. Ameikandia stimulus package kuwa haitastimulate chochote bali kufidia madeni na makali ili mambo yawe kama yalivyokuwa kabla ya msukosuko.

Amesema hajaona stimulus ya kustimulate ukuaji wa uchumi ama kuongeza uzalishaji, huu ni ulaji mwingine mnene on the pipline.

At least hapa Mh. Zitto tumeenda sawa.....hii the so called Stimulus Package ya JK is meant only to stimulate ushindi wa ''kishindo''cha pesa,mwaka 2010 tu nothing else.......! so wenye macho tazameni na kemeeni hili!

Pili ule mpango wao eti wakuiuzia Serikali shule za jumuiya ya wazazi then eti pesa ziende CCM.....huu ni ufisadi mwingine wa aina yake.....! binafsi nakumbuka kule home tukiwa P/S tulifanyishwa kazi za kusaidia ujenzi wa shule zile, na kwa wananchi wengine ilikuwa ni lazima au kutoa michango au kwenda kutengeneza tofali kwa ajili ya ujenzi ule....sasa iweje leo shule zile eti iuziwe serikali na pesa ziende CCM tu? Hatuoni hatuwatendei haki wanachi ambao itikadi zao ni tofauti na CCM? kwa maana ya kuwa either wanachama wa vyama vingine au ni neutral na walihusika katika ujenzi wa shule zile?

Halafu kwanini shule hizi ziuzwe sasa.....tukielekea 2010?.....Tafadhali wabunge wetu msianyamazie haya mambo baadaye tuanze kutafuta mchawi kama ilivyokuwa kwa EPA!
 
06_09_5fft5j.jpg

Tutegemee nini kutoka serikali ya awamu ya nne wakati watendaji ndo hawa......Mkulo anasikilizia hotuba ya JK
 
At least hapa Mh. Zitto tumeenda sawa.....hii the so called Stimulus Package ya JK is meant only to stimulate ushindi wa ''kishindo''cha pesa,mwaka 2010 tu nothing else.......! so wenye macho tazameni na kemeeni hili!

Pili ule mpango wao eti wakuiuzia Serikali shule za jumuiya ya wazazi then eti pesa ziende CCM.....huu ni ufisadi mwingine wa aina yake.....! binafsi nakumbuka kule home tukiwa P/S tulifanyishwa kazi za kusaidia ujenzi wa shule zile, na kwa wananchi wengine ilikuwa ni lazima au kutoa michango au kwenda kutengeneza tofali kwa ajili ya ujenzi ule....sasa iweje leo shule zile eti iuziwe serikali na pesa ziende CCM tu? Hatuoni hatuwatendei haki wanachi ambao itikadi zao ni tofauti na CCM? kwa maana ya kuwa either wanachama wa vyama vingine au ni neutral na walihusika katika ujenzi wa shule zile?

Halafu kwanini shule hizi ziuzwe sasa.....tukielekea 2010?.....Tafadhali wabunge wetu msianyamazie haya mambo baadaye tuanze kutafuta mchawi kama ilivyokuwa kwa EPA!

Mkuu naomba unihabarishe zaidi, hizi shule za wazazi (CCM) ni zipi? je, ni zile zilizojengwa na wananchi kama ilivyosasa kwenye shule za kata? Nimewahi kuambiwa kuwa shule za wazazi (most of day schools) hakuna mahali iliwekwa wazi juu ya hawa wazazi kumbe ni Jumuiya ya Wazazi ya CCM? Mungu wangu...na sasa zinauzwa kwa Serikali? i can't believe. Kama kunamambo yatakayonitoa pangoni hili ni moja wapo.
 
Pinda keshaanza kuulizwa maswali .Kaanza Hamadi Rashid kuhusu kunyimwa haki ya kupiga kura Wazanzibar kwa kukosa kipande. Pinda anasema hajui kipande ni nini

kwani masuala ya vitambulisho haya si mambo ya wazanzibari na hayamo kwenye muungano sasa kuulizwa bungeni na sio baraza la wakilishi kuna maana gani? au ndio kuanzisha fitna na kutiana majaribuni
 
Baada ya matangazo kukatika ghafla huku Zitto akianza kipiga nyundo, mtangazaji studio za Dar ameomba radhi kwa kutoendelea na mahojiano ya Zitto na kueleza ni matatizo ya kiufundi.

Natoa wito, naomba tuamini ni matatizo ya kiufundi kweli ambayo yanaweza kutokea hata angekuwa ni rais anaongea. Please lets not start insinuate on anythinng else than technical problem. Wenye mawazo mafupi na wale mafanatics wa Zitto.

Wanaweza kufikiri ni hujuma wamekata matangazo hayo kabla Zitto hajaporomosha makombora.
Hadithi imeishia hapo. Tuisubiri hotuba ya Bajeti, Asubuhi njema!.

Pasco,

mambo ya Tanzania wewe yaache tu si vema kuchagua upande mapema hivyo kwani mara nying utakuja umbuka. Unajua kama unafaidi na system iliyopo sasa na khali inavyowatendea maskini sitashangaa ukiendelea na msimamo huo . Ila kama wewe ni miongoni mwa watanzania 40M wanaoangaika tu ninakuomba ufanya aliyoyafanya pilato kwa kunawa maji na kusema damu yangu haina hatia juu ya mateso ya hawa watanzania!
 
Mkuu naomba unihabarishe zaidi, hizi shule za wazazi (CCM) ni zipi? je, ni zile zilizojengwa na wananchi kama ilivyosasa kwenye shule za kata? Nimewahi kuambiwa kuwa shule za wazazi (most of day schools) hakuna mahali iliwekwa wazi juu ya hawa wazazi kumbe ni Jumuiya ya Wazazi ya CCM? Mungu wangu...na sasa zinauzwa kwa Serikali? i can't believe. Kama kunamambo yatakayonitoa pangoni hili ni moja wapo.

Mkuu Nziku,

Yes kuna shule zilijengwa nyingi sana kati ya mwaka 1980 na 1995 nafikiri kila wilaya zipo hizo shule.

Zile shule zilijengwa kwa nguvu ya wananchi wa maeneo husika na zilikuwa zinaitwa shule za wazazi....sasa kwa kuwa kipindi kile tulikuwa na chama kimoja msukumo wa utekelezaji wake ulikuwa chini ya Jumuiya ya wazazi wa CCM...!

Leo wanataka kuwageuka mamilioni ya watanzania walihusika katika ujenzi ule na kutaka kuwapora shule zile na kuwapora fedha pia shule kuzipeleka serikalini na pesa kuzipeleka CCM.......!Hii si haki ni utapeli wa mchana kabisa huu!
 
keshauzwa huyo mkuu!tunajua kila kitu

Punguza kukurupuka, kusoma hujui hata picha nazo huzitambui?? Fair play kawaeleza vizuri sana kwenye thread mliyoikurupukia kuwa ZITTO ANANG'ATUKA..............Grow up boy
 
Pasco,

mambo ya Tanzania wewe yaache tu si vema kuchagua upande mapema hivyo kwani mara nying utakuja umbuka. Unajua kama unafaidi na system iliyopo sasa na khali inavyowatendea maskini sitashangaa ukiendelea na msimamo huo . Ila kama wewe ni miongoni mwa watanzania 40M wanaoangaika tu ninakuomba ufanya aliyoyafanya pilato kwa kunawa maji na kusema damu yangu haina hatia juu ya mateso ya hawa watanzania!
Niliwahi kusema principle yangu ni kusimama kwenye ukweli, 'nothing but the truth'. No compromise no surender. Kwenye ukweli daima uongo hujitenga, ila kunaweza kutokea diferent view ya the same issue na zote zikwa right kutegemea unaangalia kutokea upande gani. Ili plain truth, yaani ukweli halisi usio na mawaa, siku zote ni mmoja tuu haijalisi umeangalia toka upande gani unless ni kuzikubali both sides of the same coin zinaonekana kwa juu na pia kwa chini ya meza ya kioo.

Nimeshauri lile ni tatizo la kiufundi, nikasema limemkuta Zitto, limeendelea mpaka Bungeni hadi Waziri Mkuu lilimkuta, kama una access ya TV hapo ulipo, watch TBC-1 now, compare na Star TV, angalia picture quality, sikiliza sound quality, utapata jibu TBC inakabiliwa na matatizo ya kiufundi.

Siko kwenye system wala sifaidiki na lolote serikalini bali ni raia mtiifu ninayependa amani na utulivu uliopo, nasikitishwa na kuhuzunishwa na umasikini wa kutupwa uliotuzunguka, sina sababu ya kunawa kama Pilato kwa vile mimi si mmoja wao ila ndiye mimi na wewe, sisi na wao, yule na wale tuliompa pilato ridhaa ya kuyafanya hayo aliyoyafanya na 2010 tunamuongezea tena ridhaa
Kwa miaka mitano mingine.
 
Mkuu Nziku,

Yes kuna shule zilijengwa nyingi sana kati ya mwaka 1980 na 1995 nafikiri kila wilaya zipo hizo shule.

Zile shule zilijengwa kwa nguvu ya wananchi wa maeneo husika na zilikuwa zinaitwa shule za wazazi....sasa kwa kuwa kipindi kile tulikuwa na chama kimoja msukumo wa utekelezaji wake ulikuwa chini ya Jumuiya ya wazazi wa CCM...!

Leo wanataka kuwageuka mamilioni ya watanzania walihusika katika ujenzi ule na kutaka kuwapora shule zile na kuwapora fedha pia shule kuzipeleka serikalini na pesa kuzipeleka CCM.......!Hii si haki ni utapeli wa mchana kabisa huu!

Mkuu asante kwa maelezo, inauma sana, huu ni wizi uliopitwa na wakati. Shule hizo zilijengwa kwa nguvu ya wananchi na wafadhili. Haikulengwa kuwa mali bifsi ya mtu au taasisi ya chama. Tena baadhi ya shule zilishachukuliwa na Serikali na hiyo Jumuiya ya Wazazi haikudai chochote iweje leo?

Kwa mfano, nimewahi kufanya kazi Wilaya ya Mfindi (Iringa), katika kila kata kuna shule ya wazazi iliyojengwa chini ya mfuko ulioitwa Mfindi District Development Trust (MDDT). Karibu kila Wilaya ilikuwa na mfuko kama huu, so, ni shule nyingi sana zilijengwa kwa mpango huu. Mifuko hii ilitangazwa na kuchangiwa na wafadhili mbalimbali wakiwa na lengo la kuisaidia Serikali siyo CCM! Pia wananchi walitoa ardhi yao bure na walifanya kazi zote za mikono pamoja na michango ya fedha. Iweje leo uwaambie wanunue tena? I smell fish..., Serikali hii ni ya wananchi kweli? hapana......
 
Baada ya matangazo kukatika ghafla huku Zitto akianza kipiga nyundo, mtangazaji studio za Dar ameomba radhi kwa kutoendelea na mahojiano ya Zitto na kueleza ni matatizo ya kiufundi.

Natoa wito, naomba tuamini ni matatizo ya kiufundi kweli ambayo yanaweza kutokea hata angekuwa ni rais anaongea. Please lets not start insinuate on anythinng else than technical problem. Wenye mawazo mafupi na wale mafanatics wa Zitto.

Wanaweza kufikiri ni hujuma wamekata matangazo hayo kabla Zitto hajaporomosha makombora.
Hadithi imeishia hapo. Tuisubiri hotuba ya Bajeti, Asubuhi njema!.

Matatizo ya kiufundi??? Aaaaaggghhhhrr Gademit!!!
 
Siko kwenye system wala sifaidiki na lolote serikalini bali ni raia mtiifu ninayependa amani na utulivu uliopo, nasikitishwa na kuhuzunishwa na umasikini wa kutupwa uliotuzunguka, sina sababu ya kunawa kama Pilato kwa vile mimi si mmoja wao ila ndiye mimi na wewe, sisi na wao, yule na wale tuliompa pilato ridhaa ya kuyafanya hayo aliyoyafanya na 2010 tunamuongezea tena ridhaa
Kwa miaka mitano mingine.

Pasco, umesomeka barabara... endelea kutujuza yanayojiri mkubwa
 
Punguza kukurupuka, kusoma hujui hata picha nazo huzitambui?? Fair play kawaeleza vizuri sana kwenye thread mliyoikurupukia kuwa ZITTO ANANG'ATUKA..............Grow up boy

Na we mkuu hapa naona umekurupuka, FP kule kny thread nyingine kakurupuka as well....hakusoma posts zote ajue kwanini ile thread ilirudishwa pale......wakuu someni posts zote vizuri kabla ya kuchangia!
 
Wakuu ni kweli hiki kinachotaka kufanyika kuuza shule zetu kwa bei ya soko kwa kutumia pesa zetu lakini mapesa yaende CCM ni wizi mtupu, labda tukune vichwa tufanyeje kuzuia wizi huu?

Wabunge wetu tafadhali uwasheni huko kwenye jumba letu.. vinginevyo ndo hivo kiranja mkuu kaisha toa tamko kitakacho fuatia ni mabilioni kuchotwa.. jitahidi jama!
 
Nyie ngojeni tuingie uwanjani, tutawabana pumzi viongozi wababaishaji mpaka wabadilike au waachie ngazi wenyewe.
 
Back
Top Bottom