Zitto Kabwe live on TBC-1 Asubuhi Hii

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,546
Running order ya Kipindi cha Jambo Afrika, Jambo Tanzania ambacho kinarushwa live na Televisheni ya Taifa, TBC-1, kila siku kuanzia saa 12:00-2:00 asubuhi kimeonyesha Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mh. Zitto Zuberi Kabwe atahojiwa live kwenye kipindi hicho akiwa mjini Dodoma.

Mhe. Zitto aliongea kwa dakika kama 5 matangazo yakakatika kwa sababu za kiufundi.
 
Last edited by a moderator:
Mpaka sasa program imeanza, Zitto hajafika na mtangazaji hajasema lolote kuhusu Zitto. Aliyefika ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Benson Mpesya. The truth ni kosa kumualika Mbunge ambaye sio mtaalamu wa uchumi kuwa curtain raiser wa budget speech, namsikiliza Mpesya anazungumza kama mwananchi wa kawaida, hajiamini kupiga data za uchumi, jamaa anapiga siasa tuu. Anamsifu Mkulu na kusisitiza utekelezaji, maneno yawe mafupi vitendo viwe virefu.
 
Zitto ndio ameingia,
Ameanza kwa kuikubali hotuba ya rais ya jana. Mpaka Zitto kukubali, hii ni big plus kwa JK!.
 
Baada ya kusifu, Zitto ameanza kupiga nyundo. Ameikandia stimulus package kuwa haitastimulate chochote bali kufidia madeni na makali ili mambo yawe kama yalivyokuwa kabla ya msukosuko.

Amesema hajaona stimulus ya kustimulate ukuaji wa uchumi ama kuongeza uzalishaji, huu ni ulaji mwingine mnene on the pipeline.

Alipotaka kupiga nyundo kubwa zaidi, matangazo yakakatika ghafla, studio Dar wakaingilia kati na kutangaza ni matatizo ya kiufundi. Sasa wameweka hutuba ya JK ya jana kusubiria kama mitambo itatengamaa, tusubiri....
 
Amesema hajaona stimulus ya kustimulate ukuaji wa uchumi ama kuongeza uzalishaji, huu ni ulaji mwingine mnene on the pipeline.

Thanks Pasco/Zitto, hata mimi ndio naona shida kubwa iko hapa. Infact tukiwa fair kilichosemwa jana wala hatupaswi kukiita stimulus plan tutafute jina jingine litakalo fit zaidi. Hapa hamna kitu nionavyo mimi ni preparations za uchaguzi tu, imagine hiyo plan yooote eti inapitia kwa Noni mtuhumiwa wa EPA kweli sisi tumerogwa si bure jamani.
 
Wameondoka kabisa kwenye mahojiano sasa wameweka vipindi vingine eti matatizo ya kiufundi. Nadhani ni amri toka juu maana hawataki kupigwa nyundo. Zitto alishaanza kumwaga cheche kwa mpangilio mzuri sana wa data tofauti na huyo Mpesya.
 
Baada ya matangazo kukatika ghafla huku Zitto akianza kipiga nyundo, mtangazaji studio za Dar ameomba radhi kwa kutoendelea na mahojiano ya Zitto na kueleza ni matatizo ya kiufundi.

Natoa wito, naomba tuamini ni matatizo ya kiufundi kweli ambayo yanaweza kutokea hata angekuwa ni rais anaongea. Please lets not start insinuate on anythinng else than technical problem. Wenye mawazo mafupi na wale mafanatics wa Zitto.

Wanaweza kufikiri ni hujuma wamekata matangazo hayo kabla Zitto hajaporomosha makombora.
Hadithi imeishia hapo. Tuisubiri hotuba ya Bajeti, Asubuhi njema!.
 
Hadithi imeishia hapo. Tuisubiri hotuba ya Bajeti, Asubuhi njema!

Mazee na wewe upo kwenye jopo la mafundi wa TBC-1?
 
Baada ya matangazo kukatika ghafla huku Zitto akianza kipiga nyundo, mtangazaji studio za Dar ameomba radhi kwa kutoendelea na mahojiano ya Zitto na kueleza ni matatizo ya kiufundi.

Natoa wito, naomba tuamini ni matatizo ya kiufundi kweli ambayo yanaweza kutokea hata angekuwa ni rais anaongea. Please lets not start insinuate on anythinng else than technical problem. Wenye mawazo mafupi na wale mafanatics wa Zitto wa
Wanaweza kufikiri ni hujuma wamekata matangazo hayo kabla Zitto hajaporomosha makombora.
Hadithi imeishia hapo. Tuisubiri hotuba ya Bajeti, Asubuhi njema!.
kukatika hewani,
mbona una kimbilia kutetea? Kwani watu wame fikiria hivyo au wewe ndiyo una jaribu kuweka wazo hilo kwenye akili za watu? Umekua too defensive kwenye kauli yako kana kwamba watu washa sema wana fikiri hivyo. Wacha wenyewe waseme au wewe spokesperson wao?
 
Heshima yako mkuu,

Kama unafuatilia vizuri matangazo ya 'tibisii wani' hususani vipindi vya bunge, wamekuwa na "matatizo ya kiufundi" pale tu viongozi wa kambi ya upinzani wanapokuwa wanaongea hasa wale wanaoshusha nondo. Mara ya mwisho tulishuhudia wakikatisha hotuba ya mwiba wao Dr. Slaa akisoma 'bajeti" mbadala ya upinzani mwaka jana, kwa sababu hizo hizo za "matatizo ya kiufundi"

Wanajua kwamba hiyo stimulus package ya JK ni maandalizi ya EPA ya uchaguzi wa 2010 sasa wamuache Zitto awafumbue macho wadanganyika? Thubutu!! Tido atakuwa amevutiwa waya na wala nchi wakamuagiza yatokee "matatizo ya kiufundi" basi na ikawa hivyo.
 
Mkuu upande Pasco ungecheki upande wa pili ITV Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi (sorry sikuona jina lake) na yeye alikuwa anashusha nondo kuhusu bajeti ya JK.

Amesifu ukombozi wa mkulima ila ametoa angalizo kuwa mkulima wa Tanzania amekuwa akitaabika miaka yote hata kabla ya "mtikisiko wa uchumi" Hivyo anaona inawezekana ukombozi huu kwa mkulima ni njia ya kumhadaa ili asibanie kura yake 2010.

Pia amegusia mpango wa kununua shule za Jumuia ya Wazazi ya CCM kwa bei ya soko. Anasema shule hizi zilijengwa kwa nguvu ya umma enzi za chama kimoja iweje leo ziuzwe na pesa iwe ya CCM peke yao?

Yeye anaona hapo kuna zengwe la kuipatia CCM pesa za kampeni 2010.

Na mimi nikawa najiuliza kama kweli serikali inaelewa umuhimu wa bei za soko iweje walishindwa kuliona hilo katika marupurupu ya wastaafu wa East African Community?
 
Naaminia alichotuambia mtangazaji. Naomba sote tuamini hivyo. Bunge live karibu linaanza kwa mswali ya moja kwa moja ya PM Pinda.

Again unakua defensive on behalf of TBC mkuu, nani kasema watu hawaamini ni tatizo la kiufundi? Kwa nini unataka kila mtu aamini unacho kiamini wewe. You are talking in a way in which you are assuming you know what's on all of our minds.
 
Baada ya matangazo kukatika ghafla huku Zitto akianza kipiga nyundo, mtangazaji studio za Dar ameomba radhi kwa kutoendelea na mahojiano ya Zitto na kueleza ni matatizo ya kiufundi.

Natoa wito, naomba tuamini ni matatizo ya kiufundi kweli ambayo yanaweza kutokea hata angekuwa ni rais anaongea. Please lets not start insinuate on anythinng else than technical problem. Wenye mawazo mafupi na wale mafanatics wa Zitto.

Wanaweza kufikiri ni hujuma wamekata matangazo hayo kabla Zitto hajaporomosha makombora.
Hadithi imeishia hapo. Tuisubiri hotuba ya Bajeti, Asubuhi njema!.

Duh matatizo ya kiufundi yanatokea pale wanapo pigwa nyundo jamaa angekuwa anasifia mbona yangeendelea.
 
Back
Top Bottom