Zitto Kabwe kuwa kiongozi wa Upinzani Bungeni?

Lakini ni vijana wasio na displine. Ni afadhali wakakaa mbali nasi kuliko kuwa nao kama mzigo ndani ya chama. Mi nadhani tutashirikiana nao vizuri wakiwa nje ya chama kuliko walivyokuwa ndani ya chama. Mnamkumbuka Kafulila na battle ya zitto na wenyekiti? Wacha akae na Mbatia huyo watawezana maana ni wale wale tu, undisciplined.
Inategemea kwako wewe tafsiri ya discpline inaanzia wapi na kuishia wapi! Huenzi kuishi ndani ya Udikteta ukakaa kimya kisa utakuwa huwa adabu. Ndio maana leo hii unawasikia wengine wanakataa kukubali matokeo. Hii yote ni hulka ya kushinda au kuamua jambo bila kupingwa.
 
Sio kila mfumo unaweza kufaa kila mahali. Kiukweli hana hata sifa za kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA. Angalau ndani ya CHADEMA anaweza kuvumilika ila si nje ya CHADEMA.

Ndg, tunasikitikia sana negativity yako. Kwani waweza kutudokezea kuwa una title gani ktk jamii, au stability yako ikoje, maana kama una critisize Mbowe ameongoza chama chenye wanachama mamilioni bila kuyumba, ni tofauti kabisa na wa vyama vingine vilivyosambaratika! Political strength ya mtu ni mobilization capacity, focus na clear destination kwa chama na watu wake. Hii imemfanya hata Mzee Mtei - mwanzilishi wa Chadema alitoa uthibitisho wa ninayosema na alimsifu sana Mbowe kwa uwezo wake. Au una chuki binafsi? Mbowe si kama akina Makamba na Al Shahaf - kinana, kwani porojo wanazopiga, zinaboa, afadhali mtendaji mara mia kuliko mpiga porojo! Pole sana Anfaal!
Nawasilisha.
 
Wakuu, Zitto ni mtu ambaye HAFAI kabisa kuwa mkuu wa upinzani bungeni, sababu kama mnakumbuka humu ndani alishasema yeye huwa ana misimamo yake binafsi na ndio hiyo anaitetea. Sawa kabisa ni haki yake, lakini kwenye siasa hakuna misimamo binafsi, ni misimamo ya ailimia kubwa ya chama chako na especially wananchi wanaosupport hicho chama.

Zitto anadhani yeye ni smart sana na alitetea hoja ya Tanesco kununua mitambo feki ya Dowans na kuleta maneno mengi, mbona mitambo haikununuliwa na Tanesco wamejipanga vizuri kuleta magenarator mapya soon na nchi inaendelea???

Anachofanya ZITTO ni kuleta mgawanjiko mapema sana kwa CHADEMA kwa kujitangazia hadharani eti atagombea!!

Nasema Dr. SLaa aliyeleta namba ya wabunge wa chadema kuwa wengi, akae na wabunge wote wa Chadema na wakubaliane ni nani awe mkuu wa kambi ya upinzani.

Mimi Binafsi sitaki awe Mbowe wala Zitto, nataka awe either Halima Mdee kwa kuwa mwanamke pekee wa upinzani aliyechukua jimbo kwenye ngome ya CCM, au Tindu Lissu sababu huyu bwana anauelewa mkubwa sana wa matatizo ya wananchi na anajua kujenga hoja.

ZITTO huyu atatuletea matatizo sana huko mbeleni, nimeshamwona hulka yake ni kupaparika na kujifanya ana msimamo. Ameshindwa kusaidia hata kupata mbunge mwingine wa Chadema KIGOMA, VILE VILE percent yake aliyoshindia ni ndogo sana.
 
Mmh jamani nimeyasoma mawazo yenu yani yananitia wenda wazimu km zito yuko hvyo nn maana yake?2nachotaka ni umoja wa upinzani
 
Jamani naona nirudie hoja yangu kuwa tunahitaji mtu mature sana katika kipindi hiki. Zito apewe nafasi ya kujifunza zaidi, kuwa msema kweli bila experience na hekima ya kutosha kunaweza kudhuru zaidi kuliko kuponya. CCM itakata sana kutumia ile hali ya Zito kuwa outspoken kuwagonganisha CHADEMA na kuifanya ionekane machoni pa wapiga kura wa 2015 kuwa haifai. Let's be careful. Kwanza kitendo cha kutaka kugombea nafasi hiyo akiwapo mwenyekiti wake chenyewe tu ni questionable, unless wamekubaliana. Tusipuuze vitu kama hivi, ni dalili ya kukosa nidhamu. Ndiyo hali iliyokiharibu NCCR na TLP.
 
Ndg, tunasikitikia sana negativity yako. Kwani waweza kutudokezea kuwa una title gani ktk jamii, au stability yako ikoje, maana kama una critisize Mbowe ameongoza chama chenye wanachama mamilioni bila kuyumba, ni tofauti kabisa na wa vyama vingine vilivyosambaratika! Political strength ya mtu ni mobilization capacity, focus na clear destination kwa chama na watu wake. Hii imemfanya hata Mzee Mtei - mwanzilishi wa Chadema alitoa uthibitisho wa ninayosema na alimsifu sana Mbowe kwa uwezo wake. Au una chuki binafsi? Mbowe si kama akina Makamba na Al Shahaf - kinana, kwani porojo wanazopiga, zinaboa, afadhali mtendaji mara mia kuliko mpiga porojo! Pole sana Anfaal!
Nawasilisha.
Ishu hapa si negativity. Kama unakumbukumbu nzuri wengi tu wameshajadiliwa hapa. Na juzi tu hapa tulikuwa tunamzungumzia Anne Kilango. Kwahiyo ya Mbowe kwa kuwa amegusiwa hapa basi lazima na yeye ajadiliwe. Sina sababu ya kutaja ninachofanya kama wewe ulivyoamua kutumia jina la Masaki. Pia si kweli kwamba CHADEMA haijawahi kuyumba kama unavyotaka kutuaminisha. Siwezi kuwa na chuki binafsi na Mbowe, kwa bahati mbaya tu Dr Slaa hatokuwepo Bungeni vinginevyo ningependa nikimuona akiongoza jahazi kuliko hata Mbowe. Kama utakumbuka tena, ni mara ngapi Mbowe huyu ameripotiwa kuwapiga wananchi au kukusanya wananchi kwenda kupigana? Tuseme ukweli, hii si hulka ya kiongozi anayetegemewa katika utawala wa sheria. Ni vigumu kwake kusimamia sheria wakati hata kutekeleza hawezi. Tumuache na CHADEMA kwa kuwa kina mzee Mtei ndio wanaomuamini km ulivyoelezea hapo.
 
Jamani naona nirudie hoja yangu kuwa tunahitaji mtu mature sana katika kipindi hiki. Zito apewe nafasi ya kujifunza zaidi, kuwa msema kweli bila experience na hekima ya kutosha kunaweza kudhuru zaidi kuliko kuponya. CCM itakata sana kutumia ile hali ya Zito kuwa outspoken kuwagonganisha CHADEMA na kuifanya ionekane machoni pa wapiga kura wa 2015 kuwa haifai. Let's be careful. Kwanza kitendo cha kutaka kugombea nafasi hiyo akiwapo mwenyekiti wake chenyewe tu ni questionable, unless wamekubaliana. Tusipuuze vitu kama hivi, ni dalili ya kukosa nidhamu. Ndiyo hali iliyokiharibu NCCR na TLP.
Zitto apewe nafasi kujifunza, anajifunza nini na ataelimika lini? Kuwa mature maana yake nini?
Hapo kwenye nyekundu. Hiyo ndio demokrasia unless kama mnaiga mfumo wa KiCCM. Pia mbona kuna wengine wamegombea Urais wakati Rais bado? Yaani Demokrasia iwe nje ya CHAMA lakini ndani ya CHAMA ni makosa enh!
 
Wakuu, Zitto ni mtu ambaye HAFAI kabisa kuwa mkuu wa upinzani bungeni, sababu kama mnakumbuka humu ndani alishasema yeye huwa ana misimamo yake binafsi na ndio hiyo anaitetea. Sawa kabisa ni haki yake, lakini kwenye siasa hakuna misimamo binafsi, ni misimamo ya ailimia kubwa ya chama chako na especially wananchi wanaosupport hicho chama.

Zitto anadhani yeye ni smart sana na alitetea hoja ya Tanesco kununua mitambo feki ya Dowans na kuleta maneno mengi, mbona mitambo haikununuliwa na Tanesco wamejipanga vizuri kuleta magenarator mapya soon na nchi inaendelea???

Anachofanya ZITTO ni kuleta mgawanjiko mapema sana kwa CHADEMA kwa kujitangazia hadharani eti atagombea!!

Nasema Dr. SLaa aliyeleta namba ya wabunge wa chadema kuwa wengi, akae na wabunge wote wa Chadema na wakubaliane ni nani awe mkuu wa kambi ya upinzani.

Mimi Binafsi sitaki awe Mbowe wala Zitto, nataka awe either Halima Mdee kwa kuwa mwanamke pekee wa upinzani aliyechukua jimbo kwenye ngome ya CCM, au Tindu Lissu sababu huyu bwana anauelewa mkubwa sana wa matatizo ya wananchi na anajua kujenga hoja.

ZITTO huyu atatuletea matatizo sana huko mbeleni, nimeshamwona hulka yake ni kupaparika na kujifanya ana msimamo. Ameshindwa kusaidia hata kupata mbunge mwingine wa Chadema KIGOMA, VILE VILE percent yake aliyoshindia ni ndogo sana.
Watu mnachanganya saana issue. Hivi huyo Tundu Lissu anauzoefu gani na siasa za Bungeni? Zitto ni smart na wala issue si kudhani. Kutofautiana kwa hoja hakumfanyi mtu aonekana muasi au mjuaji. Zitto dhana yake ni ukombozi wa nchi au maendeleo kwa watanzania na si maendeleo kwa CHADEMA.
Eti Zitto hajasaidia kupata majimbo! Hivi unafaham unachoandika? Kina Mbowe, makam M/kiti na Mnyika nk wao ndio wamesaidia? Zitto ameonekana mara ngapi akipiga kampeni kwenye majimbo mbalimbali nchini huku akiliacha jimbo lake?
 
Its better akae tu pemebeni pale pagumu sana anaweza akchukiwa na hata wana chadema kusafiri za nje nyingi posho kibao so ni rahisi kutegema bomu la pesa pale akapoteza umaharufu wake na chama chake
 
kusema kweli ZITTO ALIPOTEZA tunu yangu AWEZI KUONGOZA mana siasa zake siku hizi hazieleweke
amedrop from 100% to 10% hapa kuna kitu kinafuata kwa Mh Zitto

Bora Tundu Lissu au Mbowe
 
Kuna vijana wawili walioondoka Chadema wameshinda Kigoma. Wangekuwa CHADEMA ushindi ungeongezeka.

.... Labda kama wangetangazwa cku kabla ccm (kinana+makamba) na dola hawajakaa kuweka cut off ya wabunge wa chadema na kura za rais.
 
Nami pia SINA IMANI na Zitto, mtu ambaye matakwa na maslahi yake yanatangulizwa mbele kuliko Taifa na hata kuimarika kwa umoja na mafanikio ya ukombozi wa wananchi kupitia chama chake.
 
Nami pia SINA IMANI na Zitto, mtu ambaye matakwa na maslahi yake yanatangulizwa mbele kuliko Taifa na hata kuimarika kwa umoja na mafanikio ya ukombozi wa wananchi kupitia chama chake.
Wapi matakwa yake ameyatanguliza? Yaani juzi tu katoka kukampeni katika majimbo ya CHADEMA, leo matakwa yake yako mbele zaidi kuliko maslahi ya Taifa? Alitolewa Bungeni kwa sababu ya kutetea Taifa, leo matakwa yake yako mbeleni? tatizo ni huo Uenyekiti au kuna lingine?
 
Je, Chenge kugombea nafasi ya Spika ni sahihi? Maana ninaanza kupata mashaka kwamba nawe mgombea ubunge kupitia CCM mawazo yako yamekaa kiitikadi zaidi. Angalieni na ninyi, mkienda kwa mwendo huu hata huko vijijini moto wa mabadiliko unakuja, hamtaendelea kuwadanganya wananchi kwa sera za kiungo uongo kwa kutumia ujinga na umasikini wao kama mtaji.

Ndiyo maana nimesema watu kama mgombea ubunge wanaenda kuendeleza CCM status quo huko bungeni. Hana jipya!!!!!
 
yes, Imani yangu kwa zitto ilishapotea, kama anataka kujenga heshima yake akae pembeni arudishe imani yake kwa watanzania
Tafadhali usiwasemee Watanzania, endelea kusisitiza imani yako wewe peke yako. Nadhani huna kumbukumbuku kuwa kuna watu wamemchagua huko Kigoma. Pia unasahau kwamba kutokana na imani ya CHAMA kwake alienda kupiga kampeni majimbo mengine.
 
Mimi bado sijakubaliana na nia ya Zitto.

Hata hviyo, kama atagombea nafasi hio kwa kupitishwa na chama chake mimi nitamuunga mkono. Lakini kama atafanya hivo kwa nia ya kuchuana na Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa chama, mimi sioni kama itakuwa ni busara kwa Zitto kufanya hivyo. Manake itaonekana dhahiri kwamba kuna msuguano wa kugombea madaraka baina ya Zitto na Mbowe. Kama mtakumbuka hawa watu wawili walivutana sana wakati wa kutafuta mwenyekitiwa CHADEMA.

Sasa naona inataka kujirudia tena. Lakini kama hali ndio hii then inamaanisha Zitto ni mtu wenye uchu wa madaraka. Pamoja na kwamba Zitto anauzoefu wa kukaa bungeni kwa kipindi cha miaka 5 iliopita sioni kama ni vyema yeye kuongoza upinzani wakati mwenyekiti wake yupo ndani ya bunge hilo.

Angalia hata UK, mwenyekiti wa chama ambacho kina wabunge wangi bungeni na ambaye ni mbunge ndio huwa kiongozi wa upinzani bungeni na sio vinginevyo...! So kiherehere cha Zitto kugombea au kutaka madaraka kinaweza kumsababishia kuanguka kisiasa kama Mrema...!
 
Ili kukata mzizi wa fitna, mimi nadhani wagombea Urais wote wangeruhusiwa kuingia moja kwa moja Bungeni kama Wabunge wateule na kiongozi wa Upinzani atakuwa yule chama chake kitakuwa na idadi kubwa ya wabunge waliochaguliwa.

Wakuu zangu sioni sababu kabisa ya ubishi huu kwa sababu hakuna mfumo maalum wa kiti hicho hivyo kumlalamikia Zitto wakati nafasi hiyo ni wazi na inataka watu kugombea basi sioni shida hapa. Kama wanachama wa Chadema hawapendi Zitto kuongoza Upinzani bora tupeni sababu zaidi ya ugonvi wake na Mbowe.

Hii ni aibu kubwa sana kuona wanachama tena wa Chadema mkibishana hapa kuhusiana na watu hawa ambao tumewachagua sote kutuwakilisha kisha mnaingiza chuki zenu binafsi ili mradi chama kionekane dhaifu na hakifai. Na wala msifikirie mnajenga hoja isipokuwa mnawaacha uchi watu ambao mmewapa dhamana kubwa ya uwakilishi bungeni..Hivi yule alowamaliza wakati wake alipatikana vipi, na alikuwa na nafasi gani ndani ya CUF, mbona wao hawakufikia matusi kama haya nayoyasoma hapa!

Yes, Zitto anaweza kutokuwa chaguo bora la nafasi hiyo lakini sii kumtukana hapa hali mkimsifia Mbowe au kumtokana Mbowe ili kumsifia Zitto hizi chuki zimetoka wapi?. Na isitoshe kwa nini leo tunalia na Zitto kuhusiana na Kigoma hali uamuzi wa kumfukuza Kafulila ambaye Zitto aliomba sana tumwache kutokana na uwezo wake pamoja na kwamba huyu kijana ana ukorofi wake lakini tunamhitaji na anakubalika sana huko jimboni..tulitegema nini yaani Zitto atuletee Kafulila mwingine au?..Jamani, Demokrasia ina machungu mengi sana na lazima tujifunze kukubali kutokubaliana pasipo kuingiza Uadui ndani yake.

Kweli kabisa Zitto atakuwa anakosea sana kufdikiria kwamba yeye anaweza kuwakilisha mawazo yake binafsi kwa sababu tu anafikiria ndio the right thing to do! Mbunge ni sawa na wakili unamwakilisha mtu wako hata kama ana makosa ili mradi utetezi wako ni kwa manufaa ya yule unaye represent na siku zote kumbuka unafanya kazi under lawfirm ambayo ina uongozi wake unaopanga nani amwakilishe nani na kwa nini....

Sasa kama Zitto anazo sababu au anafikiria kuwa yeye atakuwa mwakilishi bora zaidi wa Upinzani ni muhimu kuomba ridhaa ya chama kwani nguvu ya kupata nafasi hiyo imetokana na chama kushika nafasi ya pili na haikuwezekana hivyo pasipo ushirikiano wa chama kizima.
 
Back
Top Bottom