Elections 2010 Zitto kabwe Kukipiga Bukombe kwa siku tatu mfululizo

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,780
3,227
Nimepata taarifa muda si mrefu kuwa baada ya Dr.SLAA kumaliza kampeni kigoma kijana machachari mbunge mtarajiwa Zitto Kabwe leo anaingia jimbo la Bukombe kuongeza nguvu kwa mbunge mtarajiwa Prof. Kahigi wa bukombe.Inasemekana Jimbo hilo ni lulu kwa chadema kwani WAANCHI wako tayari kwa mabadiliko na mbinu zote za CCM kupata ushawishi zimegonga mwamba kuanzia kwa m/kti taifa hadi m/kti wa kitongoji wa CCM.
Wana-bukombe ndiyo waliomzomea JK na kumkatisha tamaa kuwa HAWADANGANYIKI.
 
ni vema zitto akasaidiaa katika kuongeza uwakilishi wa chadema bungeni..wanabukombe hiyoo ni nafasi yenu muhimu kufanyaa mabadilikoo.
 
Safi sana ZITTO,,,

Kafute nyayo za Makamba, nasikia alikwenda huko kubembeleza.
 
zitto ur a hero,chadema is a hero,the only mkombozi wa tanzania aliyebaki ni chadema

jf tafakari chukua hatua

usifanye makosa october 31
 
Good, Ittakuwa vizuri pia kama akitembelea majimbo ya kishapu na shy mjini watu wanahitaji kuelimishwa vizuri huko. angalau kwa siku moja moja. waarabu huko wanataka waingie bungeni ili wakajipimie maeneo ya alimasi!! watu bado hawalijui hilo.
 
Yaani balaa tena hapo kishapu wa mali lukuki watu wanalala sasa, waarabu ndo wenye nazo. Jamani huo wote ni ujambazi wa ccm
 
KWa hili Mkuu Zitto nakupaheshima ya Juu, mimi siku zote nina Amini kauli ya Zitto ina mchango mkubwa sana katika mabadiliko ya hii nchi,
 
mkichagua hovyo,msijesema hovyo watakapo watenda hovyo,tunakaribia kufika safari yetu,
go zitto,msaidie mwl wako kahigi mwana mapinduzi wa kweli
 
Nimepata taarifa sasa hivi kuwa kule Bukombe ZITTO anaendelea na kikao na kwamba watu wamefunga maduka kwenda kumsikiliza.Nyomi si ya kawaida watu wako tayari kwa mabadiliko.
 
Zitto ana mchango mkubwa sana nakumbuka harakati za uchaguzi wa ndani CCM alikuwa akihaha kuwashawishi wanaCCM kuhamia CHADEMA pia nakumbuka aliwahi kukwaruzana na wakubwa zake ndani ya chama kuhusiana na suala la Kafulilah Dr W Slaa alipokwenda Kigoma bila shaka alijionea mwenye kosa walilofanya.

Zitto kaza buti siasa za Tanzania zinahitaji watu madhubuti na hekima.
 
Back
Top Bottom