Zitto Kabwe, Kikwete na Rais wa Sudani ya Kusini

Zitto,tatizo ni kwamba taarifa kama hizi huwa unafanya
haraka sana kuziweka kwenye facebook na twitter,sijui kwanini
una chelewa kutuambia watu wa JF (kama sio kui-under value)!

Sidhani kama ungetoa maelezo kama haya siku unaenda yangetokea majungu kama
haya,kama nisingesoma post yako kidogo niandike na mimi maswali juu ya safari hiyo,...
so far nimekuelewa,lakini please jamii forum inastahili taarifa kama hizi pia
Kuna vitu mnatakiwa kuvifikiria kabla hamjakurupuka kupost. Wenje alisafiri na Makamu wa Rais mbona hakutoa taafifa kwenye hizo mnaziita twita na fesibuku? Semeni ukweli tu kuwa Zitto HAAMINIKI
 
Ninyi mna jeuri sana....sijui mnajiamini nini

Mwingine huyu.Kiburi na Jeuri mnaambiwa ukweli.Mnaogopa kwa sababu ya usaliti unaoanikwa hapa?mwenzako picha zake na watoto wa kizungu, kihindi,kithailand na kizambia zilianikwa hapa akiwa chuo kikuu.Akasema ni majungu hadi mleta mada akafungiwa.bado za kwako tu.Huko southern sudan uwezi chakachua na kuharibu.sio viti maalumu

Ni sawa lakini vipaji vyote hivi mnavitumia kujenga mitandao yenu hadi sasa mmeelekeza nje ya nchi?kila kitu usemacho siku hizi mimi huwa nakitafakari sana kwa kina.Tumia basi uwezo wenu kukisaidia chama chenu

Una uhakika sikisaidii chama? Hebu acha kuingia hapa kuchafua majina ya watu.
Duh...Upotoshaji huu! wacha nijisemee,Ni muda mfupi uliopita nimemaliza kazi ya kukisaidia chama changu katika ajenda fulani za bunge hili la bajeti.Naomba uniache na uche kuchafua watu na kufanya upotoshaji kwa maslahi unayoyajua.
 
Nitarudi Juba hivi karibuni. Ninashauri badala ya kupoteza mud a kujadili nani kaenda Juba na nani tujadili jinsi ya kuwazidi Wakenya Huko Jamhuri ya Sudan Kusini na kupata biashara kwa nchi yetu. Delegation ya Kenya ulikuwa na Rais na Waziri Mkuu, Mawaziri kumi na makatibu wakuu. Siku ya pili nikiwa Airport Makamu wa Rais alikuwa anawasili. Sisi tunakalia maneno na majungu tu!
Mkuu Zitto Kabwe hapo umenena, nashangaa sana wanapojadili haya, kama kiongozi nadhani kupata exposure juu ya mambo ya kimataifa ni jambo muhimu. Usikatishwe tamaa na maneno ya watu! Unafanya vizuri katika siasa, upo makini usikate tamaa!
 
Kuna vitu mnatakiwa kuvifikiria kabla hamjakurupuka kupost. Wenje alisafiri na Makamu wa Rais mbona hakutoa taafifa kwenye hizo mnaziita twita na fesibuku? Semeni ukweli tu kuwa Zitto HAAMINIKI
Swala la kutoaminika msililete humu, zitto kachaguliwa na spika kuliwakilisha bunge. Ila itabidi na yeye apunguze huo urafiki wake na jk hata kama ameifanyia kigoma mengi, urafiki/ukaribu ubakie ktk kazi na masuala ya msingi!
 
Nadhani hoja hii inapewa uzito usiostahili hapa jamvini. Kuna masuala mengi ya msingi ya nchi kujadili badala ya anni kasafiri na nani. Mwezi Aprili mhe. Hezekiah Wenje alisafiri na mhe Makamu wa Rais, sikuona maneno. Wabunge mbali mbali wa CHADEMA wamesafiri na viongozi Kama Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais. Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa katika shughuli za Bunge.

Fuatilieni misafara yote ya viongozi wakuu, kuna wabunge wa pande zote mbili. Kule Juba nilikwenda na Waziri kutoka Zanzibar wa CCM ndugu Mwinyihaji Makame.

Ndani ya miaka mitano hii mtaona misafara ya aina hii na Spika ndiye anayeamua. Namshukuru Mungu kuwa nimekuwa mmoja wa Watanzania ambao tumeshuhudia historia hii ya watu wa Sudan Kusini kujiondoa kwenye makucha ya ukandamizaji wa Waarabu wa Kaskazini. Ningependa kuona Umoja wa Afrika, lakini sio kwa gharama ya kuwanyonya, kuwakandamiza na kuwadidimiza Waafrika wa Kusini ama kwa sababu ya rangi Yao au Dini Yao.

Ni rai yang kuwa Tanzania iangalie fursa za kibiashara Huko. Mie ninaelekea kupata kazi ya kuishauri Wizara ya Madini ya Sudan Kusini kuhusu Sera ya Madini na Sheria ya Madini. Natarajia kurudi Juba hivi

Eee Mungu waepushe S. Sudan na hili janga!!
 
Nitarudi Juba hivi karibuni. Ninashauri badala ya kupoteza mud a kujadili nani kaenda Juba na nani tujadili jinsi ya kuwazidi Wakenya Huko Jamhuri ya Sudan Kusini na kupata biashara kwa nchi yetu. Delegation ya Kenya ulikuwa na Rais na Waziri Mkuu, Mawaziri kumi na makatibu wakuu. Siku ya pili nikiwa Airport Makamu wa Rais alikuwa anawasili. Sisi tunakalia maneno na majungu tu!
hapa umenena
ila watanzania hata kama tungepeleka mawaziri wote bado mambo yaleyale.
 
Bado uhuru wa Tanganyika, is coming tomorrow. Na bendara yetu, na wimbo wetu wa taifa, na madini yetu na.....
 
Zitto alikwenda huko mapema sana na pengine kabla ya kujua kuwa Jk atakwenda huko hivyo siyo deal kuwa heading yake hapa na pengine ni kitu cha kawaida kabisa
 
Nadhani hoja hii inapewa uzito usiostahili hapa jamvini. Kuna masuala mengi ya msingi ya nchi kujadili badala ya anni kasafiri na nani. Mwezi Aprili mhe. Hezekiah Wenje alisafiri na mhe Makamu wa Rais, sikuona maneno. Wabunge mbali mbali wa CHADEMA wamesafiri na viongozi Kama Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais. Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa katika shughuli za Bunge.

Fuatilieni misafara yote ya viongozi wakuu, kuna wabunge wa pande zote mbili. Kule Juba nilikwenda na Waziri kutoka Zanzibar wa CCM ndugu Mwinyihaji Makame.

Ndani ya miaka mitano hii mtaona misafara ya aina hii na Spika ndiye anayeamua. Namshukuru Mungu kuwa nimekuwa mmoja wa Watanzania ambao tumeshuhudia historia hii ya watu wa Sudan Kusini kujiondoa kwenye makucha ya ukandamizaji wa Waarabu wa Kaskazini. Ningependa kuona Umoja wa Afrika, lakini sio kwa gharama ya kuwanyonya, kuwakandamiza na kuwadidimiza Waafrika wa Kusini ama kwa sababu ya rangi Yao au Dini Yao.

Ni rai yang kuwa Tanzania iangalie fursa za kibiashara Huko. Mie ninaelekea kupata kazi ya kuishauri Wizara ya Madini ya Sudan Kusini kuhusu Sera ya Madini na Sheria ya Madini. Natarajia kurudi Juba hivi

Mungu wangu South Sudan wamekwisha!! Kama utawapa ushauri kama uliowapa Tanzania then bora watafute mtu mwingine, sijaona lolote zuri kwenye sera Sera na Sheria za Madini hapo Tanzania.
 
Wamekwisha kwa lipi? tanganyika ndio imekwishachukuliwa msukule, hata haijitambui, Mungu okoa tanganyika.
 
Nitarudi Juba hivi karibuni. Ninashauri badala ya kupoteza mud a kujadili nani kaenda Juba na nani tujadili jinsi ya kuwazidi Wakenya Huko Jamhuri ya Sudan Kusini na kupata biashara kwa nchi yetu. Delegation ya Kenya ulikuwa na Rais na Waziri Mkuu, Mawaziri kumi na makatibu wakuu. Siku ya pili nikiwa Airport Makamu wa Rais alikuwa anawasili. Sisi tunakalia maneno na majungu tu!

Zitto,
Baada ya kuona na kujifunza hili kutoka kwa Wakenya, unakusudia kushirikiana nasi vipi kuisaidia Tanzania na vijana wa Kitanzania kunufaika na ziara yako ijayo?
 
Mungu wangu South Sudan wamekwisha!! Kama utawapa ushauri kama uliowapa Tanzania then bora watafute mtu mwingine, sijaona lolote zuri kwenye sera Sera na Sheria za Madini hapo Tanzania.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Katika kamati ya madini mchango wa Zitto wa enzi zile utabaki kuwa alama yake ya mzalendo kwa Taiafa.
 
Nadhani hoja hii inapewa uzito usiostahili hapa jamvini. Kuna masuala mengi ya msingi ya nchi kujadili badala ya anni kasafiri na nani. Mwezi Aprili mhe. Hezekiah Wenje alisafiri na mhe Makamu wa Rais, sikuona maneno. Wabunge mbali mbali wa CHADEMA wamesafiri na viongozi Kama Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais. Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa katika shughuli za Bunge.

Fuatilieni misafara yote ya viongozi wakuu, kuna wabunge wa pande zote mbili. Kule Juba nilikwenda na Waziri kutoka Zanzibar wa CCM ndugu Mwinyihaji Makame.

Ndani ya miaka mitano hii mtaona misafara ya aina hii na Spika ndiye anayeamua. Namshukuru Mungu kuwa nimekuwa mmoja wa Watanzania ambao tumeshuhudia historia hii ya watu wa Sudan Kusini kujiondoa kwenye makucha ya ukandamizaji wa Waarabu wa Kaskazini. Ningependa kuona Umoja wa Afrika, lakini sio kwa gharama ya kuwanyonya, kuwakandamiza na kuwadidimiza Waafrika wa Kusini ama kwa sababu ya rangi Yao au Dini Yao.

Ni rai yang kuwa Tanzania iangalie fursa za kibiashara Huko. Mie ninaelekea kupata kazi ya kuishauri Wizara ya Madini ya Sudan Kusini kuhusu Sera ya Madini na Sheria ya Madini. Natarajia kurudi Juba hivi

Sidhani kama hii hoja inapewa uzito isiyostahili. Tulichotaka kujua ni uamuzi wa kwenda na rais unatoka kwa nani. Sio kosa kuuliza hilo. Ni moja ya njia za kufuta ujinga.
Kama wananchi ni haki yetu kujua haya kwa vile sisi ndio tunalipia kila kitu.
Swali la ziada: Spika anachagua kwa njia gani? Na wanaenda wabunge wangapi?
Hiyo kazi uliyopata ni kama mbunge au ni kutokana na kuwa expert katika hiyo field?

Nitarudi Juba hivi karibuni. Ninashauri badala ya kupoteza mud a kujadili nani kaenda Juba na nani tujadili jinsi ya kuwazidi Wakenya Huko Jamhuri ya Sudan Kusini na kupata biashara kwa nchi yetu. Delegation ya Kenya ulikuwa na Rais na Waziri Mkuu, Mawaziri kumi na makatibu wakuu. Siku ya pili nikiwa Airport Makamu wa Rais alikuwa anawasili. Sisi tunakalia maneno na majungu tu!

Tueleze hizo opportunities zilizopo huko basi. Au na sisi tufunge safari kwenda kuangalia kwanza?
 
ila nimempenda zito, nahisi anataka mkubwa awe sharobaro, kwamba walau akanyoe ndevu aonekane handsome baada ya kazi nzito.
 
Rais wa South Sudani, anazungumza kiswahili - halafu ebu mwambieni aondoe hiyo kofia ya cowboy, hata haifanani.
 
Sasa safari muhimu kama hii yenye fursa kwa watanzania na bidhaa zao hajaenda hapo simuelewi sasa.Hapa ndio alitakiwa 'ajitambulishe' na kumueleza Salva kiir kuna watanzania wanaoweza kusaidia taifa hili changa katika nyanja mbalimbali na aende na wafanya biashara waangalie fursa za kule.

Nini tutawasaidia South Sudan. sie wenyewe tunanjaa na wafanya biashara wetu bado watoto. South Sudan wameisha waambia waarabu waje kuwekeza. Karibuni kutakua na mkutano Dubai juu ya miradi na uwekezaji South Sudan
 
Back
Top Bottom