Zitto Kabwe, hii ni kweli?

Mi nafikiri zitto alikuwa na dhamira ya kweli ya ukombozi, no matter hiyo idea ni yake au ametumwa.

Wangapi katika lile bunge wangekuwa na uthubutu wa kufanya aliyoyafanya zitto kwa hiari na utashi wao, baada ya kuona uchungu jinsi majizi yanavyoitafuna mchi yetu?

Au ni wangapi wangeweza kufanya hivyo hata kwa kushinikizwa na hao unaowaita wanorway?

Majibu ni hakuna, au wachache sana, so mimi nampongeza sana zito, at least he tried, na changamoto imeonekana kwa serikali.

Bravo Kabwe Zitto Zuberi
 
Hata km ametumwa na norway mbona bado hoja imeonekana ni nzito na kuungwa na wengi?......kwa hiyo kumbe wanorway wana mawazo mazuri sana ambayo sisi hatufikiri hata kidogo kwa sababu tumechoka kufikiri au tumezuiwa tusifikiri sawasawa............km ni hivyo mimi binafsi nichukue hatua ya kuwashukuru wanorway kwa wazo lao zuri na lenye maslahi makubwa kwetu hata km na wao watakuwa na maslahi poa tu....mbona sisiemu na serikali yake wanawauzia wachukuaji wanaowaita wawekezaji nchi kwa bei chee kabisa?
 
Kwenye gazeti la the Guardian on Sunday la tarehe 22 April 2012 kuna habari inayosema kuwa Zitto kusimamia zoezi la petition kwa ajili ya kumng'oa Pinda linatokana na 'pressure' ya wananchi na baadhi ya 'donors' kutoka Norway.

"In a telephone interview with The Guardian on Sunday, Kabwe, who is Kigoma North MP, said, "I acted alone…I asked God to help me after a lot of pressure from Tanzanians and some donors from Norway."

Mimi nilifikiri msukumo ulikuwa ni wa ndani ya Zitto (patriotism, deep thinking, creativity and political will), lakini kumbe kutoka nje. Je, huku ni kukomaa kisiasa au ndio spanner mkononi?

Source: :: IPPMEDIA (search using a keyword Zitto or Kabwe)

Kuna namna tofauti za kuangalia hili.

1. Kudisclose kwamba kuna pressure inatoka nje si kitu kizuri, hata kama pressure hizo zilitokana na genuine interest ya maendeleo ya Watanzania. The Norwegians help us a lot, and frankly I can understand if they are irked to see misuse of funds. Mawaziri wa Tanzania nchi masikini inayopewa misaada na Norway wanatanua kuliko mawaziri wa Norway. So I can understand why the Norwegians could genuinely pressure a Young Turk like Zitto to champion this cause. But it was political immaturity for Zitto to disclose this in public, because now he is giving some people the ammunition of planting a seed of doubt by insinuating that "Zitto anatumiwa na watu wa nje kuvuruga mambo nchini"

2. Habari za kusema nililala nikafikiri nika move peke yangu zinaweza kuwa ndicho kilichotokea, lakini si kauli ambayo inaweza kutolewa na mtu prudent. Kwa nini? Katika siasa zetu ambazo personality zinazidi principles na policies, ni muhimu sana kujitenga na kauli zinazoweza kuhusishwa na "umimi". Kuna watu wanaweza kutafsiri hii kauli kwamba Zitto anafanya mambo kivyake na pengine hata hesabu zake mpaka sasa hazijulikani, kwa hiyo wabunge wengine wanaweza kukataa kumuunga mkono kwa sababu wanaweza kuogopa kutumiwa katika chess wasilolielewa. Pia kwa kusema kafanya move mwenyewe, Zitto anaonyesha kwamba CHADEMA si chama cha consensus, ni chama cha watu kufanya mambo peke yao bila kushirikishana.

Probably mambo yamefanywa kwa nia njema na frankly the Norwegians worry me less than let's say, the Americans or Chinese, lakini still, Zitto anahitaji kutafakari mambo zaidi kabla ya kuongea kwa passion isiyoangalia kila namna maneno yake yanavyoweza kutafsiriwa.

Ama sivyo atawapa wapinzani wake msemo bureeee.
 
Binafsi yangu namwamini zito ni jembe la ukweli na huu ni mkakati tuu wa watu fulani fulani ndani ya chama chetu kutaka kumchafua zito lakini jamii pana sasa inaelewa ni nini kinaendelea chadema hawa watu wanamuona zito ni tishio la kisiasa kwao thus y
 
quote_icon.png
By Kintiku
Ile move ilishindwa kwa vile Zitto alii personalize mno.....alitaka kuitumuia kumfikisha kwenye kilele cha mafanikio. . Kama kweli alikuwa serious mbona leo kimya si angalau angetupa taarifa what is next, maana watu wamekuwa puzzled wanahitaji maelekezo mapya. Nashauri CDM wajenga hoja kuwa kwa vile PM hajaondolewa, na mawaziri hawajajiuzulu basi next move iwe maanadamano hadi kieleweke
Nyie mnaofikiri plan imeshindwa subirini kimbunga kinachovuma kimya kimya, CCM wenye akili wanajua what is going to happen ndio maana wako kimya.
 
Kama ulifuatilia mjadala vizuri, utagundua kuwa Zitto alimwokoa mkuu wa kaya (Baba mkwe wake) maana move ilikuwa ni kuipigia serikali vote ya kutokuwa na imani, kwa ujanja kabisa ambapo ni watu wachache wanaweza wakagundua, Zitto akafanikiwa kupindisha move na kuielekeza kwa Pinda. Halafu kwa faida ya wengine ambao hawamjui Zitto; Ni kweli kuwa Zitto ni kijana shupavu na mwerevu ni nguzo muhimu kwa chama chetu, lakini ni agent wa ccm - magamba. Hata mkibisha ipo siku mtakumbuka maneno yangu. Kwa taarifa yenu kati ya 2012 - 2014 Zitto atatoka CDM na kujiunga na hiki chama kipya. Atatoka na akina Milya na wengineyo wengi CDM na vyama vingine hasa NCCR. Hii move imeandaliwa na usalama wa taifa + Januari Makamba, wakifikiri kuwa chama hiki kipya kitapunguza kura za CDM 2015, kumbe hawajui kuwa kitapunguza kura za ccm. Waache wajichimbie kaburi lao wenyewe. ASOMAYE NA AFAHAMU.
 
Mkuu MGHAMBA karibu JF. Mkuu sijui kama kuna kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali. Kuna kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ama Rais. Lakini ni ngumu sana kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais; mchakato wake ni mrefu ndio maana Zitto akaamua kuchukua mkondo wa kutokuwa na imani.na waziri mkuu!

Hiyo ya kuhamia chama kingine inawezekana kwa.mwanasiasa yeyote hivyo sitaiona kama jambo la ajabu.
 
Last edited by a moderator:
"In a telephone interview with The Guardian on Sunday, Kabwe, who is Kigoma North MP, said, "I acted alone…I asked God to help me after a lot of pressure from Tanzanians and some donors from Norway."

Ni ukweli lakini haipendezi kusema, kusikia na wala kujulikana. Bwana mdogo naona he is immatured.
 
Nimerudia tena kusoma hili gazeti-ninalo, ni kweli Zitto kasema hivyo, I wonder...hiyo phrase ya Norway sidhani kama ilikuwa muhimu!
 
Nimerudia tena kusoma hili gazeti-ninalo, ni kweli Zitto kasema hivyo, I wonder...hiyo phrase ya Norway sidhani kama ilikuwa muhimu!

Ilikuwa muhimu kwa sababu zifuatazo.

1. Inaonyesha kwamba wafadhili wetu wanaona matatizo ya matumizi mabaya ya fedha na matatizo haya yanawakera. Kwa hiyo katika kuwakilisha hili labda Zitto alikuwa na point kutuonyesha kwamba hili si suala ambalo katoka nalo yeye kichwani mwake tu, mpaka hao wanaotufadhili katika miradi mbalimbali wanakerwa na matumizi mabaya ya fedha za umma.

2. Kwa upande wa pili, kama nilivyosema hapo juu, lina umuhimu kwa kuwa linaweza kutumiwa na wapinzani wake kudai kwamba huu mjadala haujaanzia kwa wananchi wa Tanzania, na kwamba chokochoko zinaanzia kwa watu wa nje.Kwa hiyo labda mwanasiasa mwenye kifua zaidi ya Zitto asingeweza kuwataja wa Norway, kwa sababu madikteta wote siku zote hupenda kutumia karata ya "maadui wa nje" ili kuwaaminisha watu kwamba mabadiliko yoyote ya kuwawajibisha si mazuri kwa sababu yana sababu za kisiasa zinazochochewa na wazungu.

Zitto angechill tu kuongelea hao wa Norway, anaweza kuongeza maswali ambayo pengine hata hayana msingi.
 
Hata kama kuna pressure ni sawa

Zitto punguza ubinafsi, there's a lot you can do more than being a dog in a manger!!

Kua mkuu
 
Kwenye gazeti la the Guardian on Sunday la tarehe 22 April 2012 kuna habari inayosema kuwa Zitto kusimamia zoezi la petition kwa ajili ya kumng'oa Pinda linatokana na 'pressure' ya wananchi na baadhi ya 'donors' kutoka Norway.

"In a telephone interview with The Guardian on Sunday, Kabwe, who is Kigoma North MP, said, “I acted alone…I asked God to help me after a lot of pressure from Tanzanians and some donors from Norway.”

Mimi nilifikiri msukumo ulikuwa ni wa ndani ya Zitto (patriotism, deep thinking, creativity and political will), lakini kumbe kutoka nje. Je, huku ni kukomaa kisiasa au ndio spanner mkononi?

Source: :: IPPMEDIA (search using a keyword Zitto or Kabwe)

vyovyote vile na iwe kama zito katumwa sisi haituhusu awe ametumwa ama hakutumwa lakini hoja inamashiko kwa taifa la tanzania kwani mawaziri sio wezi?.wewe umeleta uchawi wako hilo gazeti ulisoma mwenyewe taja gazeti la
 
Kwenye gazeti la the Guardian on Sunday la tarehe 22 April 2012 kuna habari inayosema kuwa Zitto kusimamia zoezi la petition kwa ajili ya kumng'oa Pinda linatokana na 'pressure' ya wananchi na baadhi ya 'donors' kutoka Norway.

"In a telephone interview with The Guardian on Sunday, Kabwe, who is Kigoma North MP, said, "I acted alone…I asked God to help me after a lot of pressure from Tanzanians and some donors from Norway."

Mimi nilifikiri msukumo ulikuwa ni wa ndani ya Zitto (patriotism, deep thinking, creativity and political will), lakini kumbe kutoka nje. Je, huku ni kukomaa kisiasa au ndio spanner mkononi?

Source: :: IPPMEDIA (search using a keyword Zitto or Kabwe)


So far cijaona tatizo liko wapi.. Na hapo kwenye red Mkuu unapaswa uelewe misaada tunayopata toka Norway na nchi nyingine za Ulaya inatokana na kodi za wananchi wao.. Kwa hiyo wanapocikia misaada yao inakuwa misused ni wananchi ndio wanaokuja juu na kuzilazimisha serikali zao kukata misaada.. Na kwa kuwa demokrasia iko kwao basi wananchi wanacilizwa na misaada inakatwa.. Kama unakumbuka katika bajeti ya mwaka jana wahisani walikata misaada na kusababisha deficit kubwa 2.. So kama tunapokea hela zao za kutusaidia basi wana haki ya kuhakikisha inatumika kwa minajili ya ilioombewa..
 
mi namkubali zito hata kama kuna pressure kutoka norway, hiyo si issue cha msingi inahitajika support ili kuhakikisha kuwa mabadiliko yanatokea. cha msingi ni kuwa issue aliyotoa ni genuine na ni kweli jambo hilo ni vema lifanyike hatutafuti source ya pressure hapa haitatusaidia
 
Kwa tatizo nini?.Nini basic meaning ya mbunge?.kwani si muwakilishi wa wananchi?.Kama ni muwakilishi wa wananchi,kuna tatizo gani kuongea yale aliyotumwa na wananchi?.Bado sijakuelewa ndugu yangu mwanamayu,ingawa nukuu ya gazeti nimeelewa.
 
Zitto ebu jitokeze mkuu kuna watu wanataka kuchafua hali ya hewa humu Jamvini.
 
Last edited by a moderator:
Inamaana hao wanorway ndiyo waliowashawishi mawaziri wawe wabadhilifu na kumshawishi mh.Pinda asiwashughulikie ili mh.Zitto aje apate sababu ya kumtoa waziri mkuu. Hii ni janja ya kupotosha hili jambo.
 
Back
Top Bottom