Zitto Kabwe, Hashim Rungwe na Kafulila Waanzisha Chama Kipya cha Siasa - CHAUMA

Status
Not open for further replies.
Mjadala mwema wakuu lakini ni vyema tukaepuka siasa za kuchafuana.

Ahsanteni!
 
Sasa mbona thread ya Millya kurudi CCM mmeifuta ya Zitto kuanzisha chama imeachwa Mods bana.
 
Zito Kabwe anatakiwa kujua kuwa kauli zake za mara kwa mara zimempotezea umaarufu wake sana.Asijidanganye kwamba kuna watu watahamana naye,watu wengi wanatamani aondoke yeye na Shibuda,ila namshauri abadilike,aunganishe nguvu na wenzake kukijenga chama badala ya kung'ang'ania kutaka kugombea uraisi.
 
We av so many jembes there,chama c cha zitto wala slaa.tuko fiti kinoma noma.:a s 465:

Mzee usiwaite majembe viongozi wetu, maana kukubali kuitwa jembe lazima uwe tayari kuchomekwa mpini, je viongozi hawa wa CDM wapo tayari kwa hili???
 
Katika hoja yako sijaona ushahidi kuwa ZZK na Kafulila ni wanacha wa hicho chama. Maneno maneno tu bila tangible evidence ni kupoteza muda mkuu!!!!!!
 
Ndugu,

Mtakumbuka kuwa hivi karibuni Msajili wa vyama vya Siasa, John Tendwa, amekipa usajili wa muda chama kipya cha siasa kinachojulikana kwa jina la Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA).

Chama hiki kinasimamiwa na mwanaharakati (utawala bora) maarufu nchini, Ndugu Walace Mayunga ambaye wenye chama wamemkabidhi kazi ya kukisajili hadi kipate usajili wa kudumu.

Makao Makuu ya CHAUMA ni Kijitonyama Mtaa wa Kameruni. Bandera ya CHAUMA ina rangi nne; nyeusi, nyeupe, nyekundu na njano. Kauli mbiu ya CHAUMA ni Nguvu ya Mabadiliko.

CHAUMA kinaonekana kuwa na mkakati mkubwa kwa sababu kinatumia waliokuwa makada wa CHADEMA, NCCR-Mageuzi na TLP kutafuta wanachama 200 kutoka angalao mikoa 10 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa No. 5 ya 1992.

-Chanzo Mdau wa CHAUMA.

My take:
Ni wazi kuwa mwenendo (kujitenga na M4C) na kauli za ZZK ambazo kila mara zinaonekana kuwa na malengo yaliyofichika; kujijenga binafsi (kupata wafuasi wengi) tayari kwa safari ya CHAUMA mara baada ya zoezi la usajili wa kudumu kukamilika.
Mwache aende,tatizo hamumjui zito,huyu jamaa anatumika na wadau fulani wa CCM na wengineo!
 
Hivi ni kwa nini wafuasi wengi wa CHADEMA wana wasiwasi sana na mwenendo wa Zitto kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya Chadema?

Hatuna wasiwasi,ndo maana tume opt ku ignore kila anachofanya,afanye atakavyo
 
huwezi kukataa kuwa hili lipo ama kukubali kuwa halipo ila ile courage ya wapambe wa zitto kwenye mitandao dhidi ya kumchafua mbowe ,slaa, na wabunge wengine wote maarufu wa chadema isipokuwa mashishanga, wakurugenzi wote wa chama isipokuwa mtemelwa!, viongozi wote wa vijana isipokuwa shonza! muungano wao na mahusiano ya karibu sana na msaliti shibuda,kupinga matamko ya chama hadharani ni sifa zinazonionesha kuwa yawezekana kuna mkakati mbadala wa zitto na siasa za ukanda zilizojiegemeza kwa vijana
 
Msije kushangaa jamaa anajijenga kisiasa akiwa chadema, destination = chauma

Hata afanyaje, hana mvuto, kama hutaki mshauri ahamie huko, kwanza hata Ubunge wenyewe next time kwa yeye kupata ni issue, kwa sisi tuliopo KIGOMA
 
Kweli zitto amewashika pabaya maana kila siku mnaibua jipya kumchafua.
Zitto hausiki kabisa na chaumma na wala hana taarifa zake zozote.
Labda david kafulila anaweza kuhusianishwa na chaumma.kutokana na kwamba nccr siyo chama ambacho kinamfanya ajisikie comfortable ukilinganisha kwamba jamaa ana uwezo,sasa pale nccr hawezi kuonyesha uwezo wake maana nako kuna sera za "ndio mzee" zilizomkimbiza chadema!
Ndo mana nasema atleast kafulila anaweza akahusika, (ushahidi wakimazingira)
Halafu jamaa ni mpinzani halisi hawezi kwenda ccm,na hawezi kurudi cdm.
Ila anaweza akaanzisha chama!hili ana uwezo nalo.
Zitto mumuache kabisaaaaaa katika hili hahusiki labda kama mnaendelexa propaganda zenu zakumchafua.
Endeleeni zitto anasubili kuapishwa 2015 kuwa rais.
 
Ndugu,

Mtakumbuka kuwa hivi karibuni Msajili wa vyama vya Siasa, John Tendwa, amekipa usajili wa muda chama kipya cha siasa kinachojulikana kwa jina la Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA).

Chama hiki kinasimamiwa na mwanaharakati (utawala bora) maarufu nchini, Ndugu Walace Mayunga ambaye wenye chama wamemkabidhi kazi ya kukisajili hadi kipate usajili wa kudumu.

Makao Makuu ya CHAUMA ni Kijitonyama Mtaa wa Kameruni. Bandera ya CHAUMA ina rangi nne; nyeusi, nyeupe, nyekundu na njano. Kauli mbiu ya CHAUMA ni Nguvu ya Mabadiliko.

CHAUMA kinaonekana kuwa na mkakati mkubwa kwa sababu kinatumia waliokuwa makada wa CHADEMA, NCCR-Mageuzi na TLP kutafuta wanachama 200 kutoka angalao mikoa 10 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa No. 5 ya 1992.

-Chanzo Mdau wa CHAUMA.

My take:
Ni wazi kuwa mwenendo (kujitenga na M4C) na kauli za ZZK ambazo kila mara zinaonekana kuwa na malengo yaliyofichika; kujijenga binafsi (kupata wafuasi wengi) tayari kwa safari ya CHAUMA mara baada ya zoezi la usajili wa kudumu kukamilika.

Binafsi sina ushahidi wowote wa kuthibitisha madai kuhusu Zitto lakini naweza kuthibitisha pasipo shaka kwamba Kafulila na Rungwe ni waasisi wa CHAUMA na wameshafanya mazungumzo na vijana kadhaa waasi ndani ya CDM kujiunga nao na miongoni mwao ni hawa wanaochafua viongozi wa CDM hapa JF.Ikihitajika majina ya vijana wote nitayaweka hapa jamvini.
 
binafsi sina ushahidi wowote wa kuthibitisha madai kuhusu zitto lakini naweza kuthibitisha pasipo shaka kwamba kafulila na rungwe ni waasisi wa chauma na wameshafanya mazungumzo na vijana kadhaa waasi ndani ya cdm kujiunga nao na miongoni mwao ni hawa wanaochafua viongozi wa cdm hapa jf.ikihitajika majina ya vijana wote nitayaweka hapa jamvini.

mkuu ni vyema kama utatuanikia majina ya hao waaasi ili tuwavue nguo hadharani.
 
Binafsi sina ushahidi wowote wa kuthibitisha madai kuhusu Zitto lakini naweza kuthibitisha pasipo shaka kwamba Kafulila na Rungwe ni waasisi wa CHAUMA na wameshafanya mazungumzo na vijana kadhaa waasi ndani ya CDM kujiunga nao na miongoni mwao ni hawa wanaochafua viongozi wa CDM hapa JF.Ikihitajika majina ya vijana wote nitayaweka hapa jamvini.

Tuwekee haya majina tuyajadili.
 
Status
Not open for further replies.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom