Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndugu,
Mtakumbuka kuwa hivi karibuni Msajili wa vyama vya Siasa, John Tendwa, amekipa usajili wa muda chama kipya cha siasa kinachojulikana kwa jina la Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA).
Chama hiki kinasimamiwa na mwanaharakati (utawala bora) maarufu nchini, Ndugu Walace Mayunga ambaye wenye chama wamemkabidhi kazi ya kukisajili hadi kipate usajili wa kudumu.
Makao Makuu ya CHAUMA ni Kijitonyama Mtaa wa Kameruni. Bandera ya CHAUMA ina rangi nne; nyeusi, nyeupe, nyekundu na njano. Kauli mbiu ya CHAUMA ni Nguvu ya Mabadiliko.
CHAUMA kinaonekana kuwa na mkakati mkubwa kwa sababu kinatumia waliokuwa makada wa CHADEMA, NCCR-Mageuzi na TLP kutafuta wanachama 200 kutoka angalao mikoa 10 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa No. 5 ya 1992.
-Chanzo Mdau wa CHAUMA.
My take:
Ni wazi kuwa mwenendo (kujitenga na M4C) na kauli za ZZK ambazo kila mara zinaonekana kuwa na malengo yaliyofichika; kujijenga binafsi (kupata wafuasi wengi) tayari kwa safari ya CHAUMA mara baada ya zoezi la usajili wa kudumu kukamilika.
Kwenye Ndoto hizo hizo za ki-CCM AMOEBA (sawa na familia ile ile ya CCM UFISADI tunachokifahamu vema zaidi), kinadharia Urais unabakia CCM Orijino, Umakamu kwenda CCM-ADC aka kijana wa Pemba anayeendelea kuegesha matairi zake pale KAFU hadi hivi sasa na CCM-CHAUMA kutoa Uwaziri Mkuu aliye na nguvu na madaraka kamili kwenye katiba.
Lakini vyote vya huko ma-njozini ni swala la kuyaachilia huko huko kitandani na kuendelea kuchapa kazi ya kufa mtu pale CDM kwa kuimarisha zaidi ile SILAHA YAKE YA MAANGAMIZI YA HALAIKI YA MAFISADI; Movement for Change. Mkuu Dr Slaa na Makamanda wote wa M4C taifa hadi vitongojini nadhani sote tuko pamoja hadi hapo.
Mara baada ya M4C na BAVICHA kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kukibomoa CCM kila kona ya nchi, hivi sasa kombora lielekezwe kutwanga CCM-AMOEBA na wanawe wote wa kisiasa kote nchini.
Kipimo chetu cha mafanikio kiwe ni kuwanasa uongozi wa serikali za mtaa kwa asilimia 90 kote nchini. Na hili liwe ni ombi letu wakati wote tunapokutana na wananchi kwamba CHADEMA kinawataka kukichagulia madiwani waadilifu kwa asilimia zaidi ya 90 ili safari yetu ya 2015 iweze kuwa maridhawa zaidi.
Sasa ZITTO KABWE; HASHIM RUNGWE na KAFULILA na Pia kuna KIONGOZI aliyeki-register hicho CHAMA
Sasa Ukiangalia na kuwapa EXAM ya nani awe MWENYEKITI ni nani atabaki CHINI bila kukimbilia JUU ?? SISI tunajua
Wasiofaaa... lakini Mmmm...
View attachment 67131
Nadhani hatumtendei haki zitto na chadema pia, mpaka sasa yeye ni kiongozi mkubwa kwenye chama na bado anafanya kazi za chama kupambana nae kusema kweli ni kupambana na chadema kwa sababu kadhaa..kwanza, ni kutengeneza makundi ndani ya chama maana lazima wapo watu ndani ya chama ambao wanamkubali zitto na wanampenda kama icon waoand he is very right!
Zitto hawezi kuondoka Chadema nyie wote mmemkuta kajiunga Chadema ana umri wa 16 na ndoto zake ni kugombea urais mwaka 2015 kupitia Chadema.
Labda kwa matendo yake kutwa yuko misafari na mwenyekiti wa CCM,halfu matangazo ya kutaka uraisi anayatoa kukiwa na agenda muhimu ya chama kuvuruga ile agenda na kubadilisha attention labda ndio maana wanamuona kirusiHivi ni kwa nini wafuasi wengi wa CHADEMA wana wasiwasi sana na mwenendo wa Zitto kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya Chadema?