Zitto Kabwe ataka ufafanuzi kuhusu IPTL

Sumasuma

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
342
110
Midraji Ibrahim, Dodoma
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amemwandikia tena Spika wa Bunge, Anna Makinda, akimuomba kuunda kamati teule ya Bunge kuchunguza ununuzi wa mafuta ya mitambo ya IPTL.

Katika barua yake ya Februari 6 mwaka huu kwenda kwa Makinda, Zitto alisema Aprili 11 mwaka jana alimuomba kuunda kamati hiyo lakini hakupewa jibu na Spika hadi leo.

“Gazeti la The East African la Aprili 6-12 mwaka huu limetoa taarifa kwamba zaidi ya dola za Marekani 54 milioni zimeibwa kwenye ununuzi wa mafuta hayo mpaka sasa. Narudia kuomba uchunguzi wa kibunge kuhusu suala hili,” alisema Zitto.

Zitto kwenye hoja yake anamnukuu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akijibu swali lake Aprili 6 mwaka jana kulithibitishia Bunge kwamba Serikali ilitumia zaidi ya Sh46 bilioni kununua mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL tangu Novemba 2010 hadi Februari mwaka jana.

Alisema Waziri Ngeleja alikiri kwamba Serikali ilitumia mfumo wa zabuni ya dharura na hivyo kuzipa kampuni mbili za Oryx na Total, zabuni ya kuagiza mafuta mazito kwa ajili ya kuendesha mitambo ya IPTL na kwamba, fedha hizo ni wastani wa Sh15 bilioni kwa mwezi.

“Kumekuwa na manung’uniko kuhusiana na zabuni hii na hata kuleta hisia za rushwa miongoni mwa maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini na Kabidhi Wasii Mkuu (Rita) ambaye ndiye msimamizi wa IPTL kwa sasa kufuatia amri ya Mahakama,” alisema Zitto na kuongeza:

“Inawezekana kabisa kwamba wapo watumishi wa umma ambao wanafaidika na tatizo la mgawo wa umeme kwa kuhongwa kutokana na zabuni hii ya mafuta mazito kwa ajili ya mitambo ya IPTL. Vilevile kuna mashaka kuhusiana na utaratibu wa zabuni kama ulifuata sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2004,” Zitto alieleza.

Katika barua hiyo anasema amepeleka ombi kwamba Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ifanye uchunguzi maalumu kuhusu zabuni ya uagizaji mafuta ya kuendesha mitambo ya IPTL.

“Uchunguzi huo, pamoja na mambo mengine, uzingatie malipo yote ambayo kampuni za Oryx na Total zinafanya kwa watu mbalimbali kuhusiana na biashara hii. Malipo yote ya kampuni hizi ya ndani na nje ya nchi yachunguzwe na maofisa wa TRA na CAG wakisaidiwa na Takukuru,” alisema.:eyebrows:
 
Back
Top Bottom