Zitto Kabwe aomba Bunge lisimamishe shughuli zote juu ya Jairo!

Maswali ambayo hata auditor hajayajibu ama kwa makusudi au kwa kusahau,
Wizara hiyo ina watumishi wangapi waliokwenda Dodoma ambao wanatafutiwa mabilioni hayo ya fedha?
Je, si kweli kwamba watumishi waliokwenda Dodoma wote walishaomba fedha zao za kujikimu?

Asante kwa maswali ya msingi, mimi nashindwa kuelewa Jairo anatetewa kwa kipi hapa. Labda Luhanjo aniambie kuwa kwa kuwa wizara zote zinafanya sarakasi hii kwa hiyo kiutendaji wao hilo sio kosa!

Naye CAG akaona kuwa posho juu ya posho ni sahihi kabisa!
 
Waziri mkuu pia anapaswa aliombe bunge msamaha kwa kurupuka na kupayuka bungeni.
Aidha waziri mkuu amuombe Jairo msamaha kwa kauli aliyoitoa bungeni zidi yake(kwani alishamtia hatiani).
Pia mh.Godbless Lema aombe muongozo ikiwa mtu mkubwa kama waziri mkuu atakurupuka na kulielezea bunge kwa kujiamini mambo ambayo hayana ukweli na yanayolenga kuvunjiana heshima bunge linapaswa kufanya nini.
Mwisho rais apime mwenyewe uzito wa tatizo ikiwa watendaji wake wakuu wanatofautiana kiasi hiki afanye nini.
Itabidi afanye kama swahiba wake (wa zamani) EL. Ajiuzulu
 
Mbona hawarudi au wanaongea na Vasco kwenye simu, naanza kupata wasiwasi hii inshu wataichinjia baharini.
 
Here we Go

Zitto Kabwe ametoa Hoja binafsi kwa kuzingatia kanuni 51.3 kifungu F ambacho kinampa mbunge nafasi ya kutoa hoja bila kufuata utaratibu wa Taarifa.


Amenukuu Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi ambaye anasema kwa mujibu wa Taarifa ya makaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ludovick Uttoh amethibitisha kuwa Katibu Mkuu Nishati Madini David Jairo hana tuhuma ya kujibu na arudi ofisini kuanza kazi leo huku akiwa huru kuwachukulia hatua waliomchafua kwa kashfa hizo.
Zito anasema kufanya hivyo ni kuingilia shughuli za mhimili mwingine wa Dola huku mtendaji Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni Mh. Pinda alishatamka kuwa kama angekuwa ni uamuzi wake angemchukulia hatua JairoZito anasisitiza kuwa Bunge si mahakama ila kwa taarifa hiyo ya Katibu Mkuu Kiongozi ni kudhihaki shughuli za Bunge.

Kwa mantiki hiyo, namnkuu '' Napenda nitoe hoja kwa Bunge kusitisha kujadili shughuli zote za serikali mpaka hapo Tarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali itakapoletwa hapa Bungeni na kujadiliwa''
Wabunge wote wanasimama kuonyesha kuunga Mkono hoja hiyo.Jambo ambalo linampa wakati mgumu Ndugai ambaye analazimika kumruhusu Lukuvi kuzungumza kama ana ufafanuzi wowote juu ya hilo.

Ngoma ni Nzito na baadhi ya watendaji wakuu wanaitana chemba kujadili suala hili huku kiti sasa kikikabidhiwa kwa Simbachawene ili kuendesha kipindi cha maswali na majibu wakati huo majadiliano yakiendelea chembe.
 
Mh. @zittokabwe anaomba #BungeTz lisimamishe shughuli zote za serikali maana nafasi ya bunge imepokwa!Makofi mengi sana. Kumekuchaaaa #Jairo
 
We, Bunge linanifurahisha vile! Wabunge wengi wameunga hoja binafsi ya Zitto kuhusu kujadili report ya mkaguzi mkuu wa serikali iliyomsafisha Jairo. Naibu Spika hakumumunya maneno, hakuleta siasa yoyote, akakubaliana na wabunge kuunga mkono hoja ya Zitto.

Kuna yule mzee wa miongozo bungeni (jina limenitoka) ndie alikuwa karibu kabisa na kuharibu hoja ya Zitto kwa visheria na vikanuni vyake visivyo na mbele na nyuma.

Ah, nimemkumbuka kwa jina moja tu, Lukuvi. Ukweli upo wazi: kama Jairo ni msafi basi bunge, hasa hasa Beatrice Shelukindo amwombe radhi Jairo.

Na wabunge inaonekana hawapo tayari kusurrender kwa serikali -- mpaka report iletwe bungeni ukaguzi ufanyike ujadiliwe na wajiridhishe. Very fast developments on this public-government-perliament saga.
 
Kwa mujibu wa matangazo ya bunge yanayoendelea na kuoneshwa na TBC 1 wabunge walitaka taarifa ya Jairo iletwe na kujadiliwa bungeni kwani yaonekana kuna uchakachuaji uliofanyika. Bunge letu linaonesha ni la kidemokrasia na uwazi. Hongereni wabunge wenye kuitakia mema Tanzania.
 
Ila Lukuvi nae anatumia masaburi kutoa hoja sasa hoja nzito kama hii anataka kuizima
 
Mh. @zittokabwe anaomba #BungeTz lisimamishe shughuli zote za serikali maana nafasi ya bunge imepokwa!Makofi mengi sana. Kumekuchaaaa #Jairo

mkuu huwa nakuaminiaga sana unapoleta taarifa zako hapa kwa kina ila leo umechemka, em jipange na ufafanue vizuri watu waelewe
 
Tatizo la serikali Yetu kila kitu kinasafishwa haya Luhanjo a2eleze je ni kwanini maliasili wamejaa wabena tuuuuuuuuuuu!au ndo janja ya kuukwepa huo mjadala kwa kushupalia ya Jairo!!?maana anajua wabongo hawataijadili tena ya ukabila watabaki na ya Jairo& Shelukindo.!!Bado ninaamini Jairo Ana Hatia Hata kama sio Ya Juzi Lakini Kuna Mkono Wa Mkuu WA Kaya
 
Hii nchi ni ya wasanii.
Viongozi wote ni wasanii
kiranja mkuu ni msanii
kiongozi wa sirikali gungeni msanii

video zao ukifutilia walahi waweza omba uhamisho ndani ya nchii
inayomilikiwa na ccm {chama cha mafisadi}.wanajiona wana hati miliki.
Shelukindo yuko sahihi kibaya ni kamgusa rafiki yake na kiranja wa watanzagiza.
 
ni upumbavu wa JK kuruhusu JAIRO asafishwe hata kama ni urafiki lazima uwe na kikomo
 
Tatizo sio kumwadabisha Jairo,aliwaona komedi kwa sababu kila kilichotokea hakikuwa sahihi kwake,sasa afanye nini? hana hatia.Pinda alizungumza bila ushahidi wowote,alitumia maneno ya wanasiasa kumhukumu jairo.<br />
<br />
Kama hana kosa hakuna maamuzi magumu Ya nini? kwa manufaa ya Nani?...CCM inabaki chama bora chenye misingi imara na kinachosimamia tararibu na kanuni.

Erick acha kutumia masaburi kufikiri...jairo kachangisha almost nusu bilioni hilo silo kosa?...
 
Back
Top Bottom