Zitto Kabwe aomba Bunge lisimamishe shughuli zote juu ya Jairo!

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,598
3,671
Kufuatia hatua ya IKULU kumsafisha David Jairo, leo Bungeni kwa mujibu wa Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kunategemewa kuwaka moto kwa sababu Bunge limedharauliwa kwa kumsafisha Jairo ambaye aliwatukana wabunge kuwa ni kama komedy.

Aidha wabunge wamepania kuamua either Jairo abaki ila Pinda ajiuzuru au Jairo aondoke Pinda abaki. Uamuzi wa IKULU kumsafisha Jairo ni dharau kubwa kwa Pinda ambaye alisema angekuwa yeye angemfukuza kazi mara moja, inategemewa kuwa Pinda na wabunge wataungana kumshughulikia Luhanjo na Jairo.

Zitto kishatoa hoja bungeni ya kutaka taarifa ya CAG ipelekwe bungeni mara moja... Wabunge wengi wameunga mkono hoja hiyo, Ndugai kaenda faragha, Simbachawene kavaa joho kwa muda.



Tusubiri tuone.

Here we Go

Zitto Kabwe ametoa Hoja binafsi kwa kuzingatia kanuni 51.3 kifungu F ambacho kinampa mbunge nafasi ya kutoa hoja bila kufuata utaratibu wa Taarifa.


Amenukuu Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi ambaye anasema kwa mujibu wa Taarifa ya makaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ludovick Uttoh amethibitisha kuwa Katibu Mkuu Nishati Madini David Jairo hana tuhuma ya kujibu na arudi ofisini kuanza kazi leo huku akiwa huru kuwachukulia hatua waliomchafua kwa kashfa hizo.
Zito anasema kufanya hivyo ni kuingilia shughuli za mhimili mwingine wa Dola huku mtendaji Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni Mh. Pinda alishatamka kuwa kama angekuwa ni uamuzi wake angemchukulia hatua JairoZito anasisitiza kuwa Bunge si mahakama ila kwa taarifa hiyo ya Katibu Mkuu Kiongozi ni kudhihaki shughuli za Bunge.

Kwa mantiki hiyo, namnkuu '' Napenda nitoe hoja kwa Bunge kusitisha kujadili shughuli zote za serikali mpaka hapo Tarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali itakapoletwa hapa Bungeni na kujadiliwa''
Wabunge wote wanasimama kuonyesha kuunga Mkono hoja hiyo.Jambo ambalo linampa wakati mgumu Ndugai ambaye analazimika kumruhusu Lukuvi kuzungumza kama ana ufafanuzi wowote juu ya hilo.

Ngoma ni Nzito na baadhi ya watendaji wakuu wanaitana chemba kujadili suala hili huku kiti sasa kikikabidhiwa kwa Simbachawene ili kuendesha kipindi cha maswali na majibu wakati huo majadiliano yakiendelea chembe.
 
Ombi maalumu kwa mama Beatrice Shelukindo (mbunge)

Tafadhali tunakuomba uombe radhi kwa wabunge na watanzania uliotudanganya kuwa David Jairo aliwahonga wabunge wakati ni mpango mahsusi unaofanyika wakati wote wa kipindi cha kuandaa bajeti ya wizara ya madini na nishati ya umeme
usiopatikana lakini malipo yanafanyika bila wasiwasi wowote.

Bila kutuomba radhi utajiweka kwenye orodha ya wapambanaji mfu kikundi cha CCJ, wakiongozwa na kamanda wao mfu SS.

Bila kutuomba radhi utawekwa kwenye kundi la mavuvuzela wa chama cha majangili wa rasilimali za watanzania kama kule Ngorongoro, wale wanyama wetu.

NATANIA TUU MAMA WALA USIHANGAIKE WATANZANIA NDIVYO TULIVYO.
 
Baada ya Luhanjo kutoa report inayoonyesha Jairo hana hatia Beatrice Shelukindo inabidi afanye yafuatayo.
1.Apinge report hiyo kwakutoa ushahidi mzuri, akijua fika Jairo ni Swahiba wa Kikwete ambaye amesoma naye.
2.Ajiuzuru kwa kumsingizia baba wa watu huku akimtaka radhi, maana wasije wakaanza kuburuzana mahakamani kwa kuchafuana
 
Tanzania kila mtu anapotuhumiwa huwa anasafishwa. Hata Richmond watu wameonekana hawana hatia, hata serikali iliyojitwalia umaarufu feki kuwa imewashitaki watuhumiwa haikuweza kupeleka ushahidi ili kushinda kesi ya Richmond.

Jairo sio safi, wala Shelukindo hakukosea kusema ukweli huo, ila maadamu tunataka tuishi katika Usanii, basi wnaosema ukweli tuwabeze na wanaodanganya ndio tuwaone wanafaa kwa kuwalinda ili waendelee kufilisi Taifa letu. Hizo chache walizokiri zilichangishwa zilikuwa za nini?
 
Beatrice Shelukindo anatakiwa kuomba Mwongozo wa spika, akanushe ripoti ya Luhanjo, ama akanushe tuhuma zake alizotoa hapa bungeni. Inawezekana huyu mama na pinda wake wamekurupuka kutoa kauli bila ushahidi. inawezekana wabunge wa magamba huwa wanatoa tuhuma bila ushahidi.

Ingelilkuwa ni CHADEMA ndiyo wametoa tuhuma kama hizi, tungekuwa na uhakika kwasababu hawa jamaa huwa nawaaminia kwa ushahidi. wangeingia na rundo la ushahidi bila chenga.
 
Baada ya Luhanjo kutoa report inayoonyesha Jairo hana hatia Beatrice Shelukindo inabidi afanye yafuatayo.
1.Apinge report hiyo kwakutoa ushahidi mzuri, akijua fika Jairo ni Swahiba wa Kikwete ambaye amesoma naye.
2.Ajiuzuru kwa kumsingizia baba wa watu huku akimtaka radhi, maana wasije wakaanza kuburuzana mahakamani kwa kuchafuana

Pengine kuna haja ya kufuatilia kwa karibu hili suala kabla kumwomba mama wa watu aombe radhi. Aombe radhi kwa lipi hilo? Ulishamskia jairo akikanusha kwamba barua aliyokuwa nayo mama bungeni hakuiandika yeye?

Barua iliandikwa kwa institutions 20, 4 zikarespond ambalo bado ni kosa kwani huwezi kutumia mil 500 kulobby budget ipite hiyo budget ni ya sh ngapi na wangapi walihusika kwenye hiyo kazi na malipo yao yalikuwaje? Imagine hizo mil 500 zingewekezwa kwa umeme si ingesaidia?

Wa kuomba radhi hapa ni kikwete kwa kuiendesha hii nchi kama mali yake wakati ni ya watanzania wote.
 
Acha ndoto za alinacha wewe ulitegemea nini kwani kanuni za kufukuzana kazi ziko namna hiyo?
 
KWa pesa zile walizochanga kwa nini wasichange kununua mitambo ya kufua Umeme? wezi wale hakuna haja ya kuomba msamaha...Unatoa 246M na zaidi kwa gharama za kutengeneza budget wakati wananchi wako wapo gizani.....wizi mwingine.
 
Beatrice Shellukindo ana options mbili tu: ama asimamie tuhuma zake kwa kutoa more evidence, au a-withdraw na kuliomba radhi bunge pamoja na wananchi kwa kupayuka! But she cannot stay silent. akikaa kimya she will prove she is the ultimate loose cannon politician.
 
Nakumbuka Jairo baada ya Shelukindo kutoa hoja hii alisema "Wabunge wa CCM ni Ze comedy" nao wakaja juu sana katika kikao chao cha ndani.
Jee kunaweza kuwa na ukweli kuwa wabunge wa CCM ni sawa na Ze comedy?
 
Back
Top Bottom