Zitto Kabwe aomba bunge liliridhie, serikali itoe taarifa ya mgomo wa madaktri na kisha ijadiliwe

Kama Bunge limepokea ipo haja ya kufanya mjadala mpana kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya Mwaka 2002 badala ya judali tu matamko ya Mhe. Waziri Mkuu na Mawaziri. Sheria hiyo pamoja na Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003, Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma 2009, Nyaraka mbali mbali za utumishi na maagizo yanayotolewa yana kasoro kubwa ambazo leo ndiyo zinachochea migomo ya moja kwa moja watumishi kama huu wa madaktari au ya chini chini ambayo ni ya hatari zaidi inayofanywa na watumishi wengine wa umma. Ni kawaida siku hizi katika ngazi zote kukuta watumishi wanapiga tu soga badala ya kufanya kazi na mahali pengine viongozi wao; Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wamejikuta wakifanya kazi ya kusaini barua za maagizo, ajira, kualika watu kwenye tafrija na maonyo badala ya kuketi na kufikiri ni kwa kiasi gani wanaweza kutumia dhamana zao kutafuta njia za kukuza uchumi (Kama huamini uliza Wizara ya Afya, TAMISEMI na Utumishi utajua). Pamoja na maboresho ya Serikali yanayoendelea bado changamoto ni nyingi mno kiasi kwamba ni vigumu kujua ni wapi hasa tunaelekea. Kimsingi Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeshindwa kujipambanua kama taasisi inayopaswa kuwa na dira ya kuongoza utumishi Tanzania. Kila mtu ana fanya lake ili mradi siku zinakwenda. Wazee wazoefu kama Mhe. William Shelukindo na Mhe. Ntukamazina wanaweza kuona na kusema ni kwa kiwango gani Utumishi imepoteza dira.

Kaka umenena Vyema, nchi kwa hivi sasa haina Dira.
 
CHADEMA kilisema "Chama kimewasiliana na kimeitaka kambi rasmi ya upinzani bungeni inayoongozwa na CHADEMA kufanya uchambuzi wa kina kuhusu maelezo hayo na kutumia njia za kibunge katika kuisimamia serikali kushughulikia migogoro kati yake na madaktari, maslahi ya watumishi wa umma katika sekta ya afya pamoja na uboreshaji wa huduma katika hospitali, zahanati na sekta ya afya nchini."

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...u-mgomo-wa-madaktari-chadema.html#post3235231

Nashukuru Zitto kama naibu kiongozi wa upinzani ameibua suala hilo kwa niaba ya kambi. Zitto, Mbassa, Mnyika, Mdee, Tundu mmeshafanya uchambuzi muibane serikali kisawasawa ikitoa taarifa yake?

serayamajimbo
 
tusubiri tuone, kwani naona hawajaonekana kwenye uzi huu, pengine wako kwenye uchambuzi makini ili leo kama ni kuwaumbua serikali kazi iwe pevu. bravo
 
Back
Top Bottom