Zitto Kabwe aomba bunge liliridhie, serikali itoe taarifa ya mgomo wa madaktri na kisha ijadiliwe

wanaofuatilia haya mambo kwa karibut watupe taarifa kamili. Kwamba bunge limehairishwa kwa sababu gani? Nani aliyetoa hoja ya kuharishwa huko kwa lengo gani? Labda na swali la mbele, tunatarajia nini katika majibu ya bunge?
 
Kwa sasa Zitto analiomba bunge likubaliane na ombi lake la kupokea taarifa ya mgomo wa madaktari toka kwa waziri mkuu kisha ijadiliwe mjengoni.

SOURCE. Bungeni live TBC

nilivomwona mama posho leo kama anataka kuizima hii hoja ya mgomo wa madaktari maana hadi yeye aamue manake kwa utashi wake binafsi na ninavomjua ataipiga chini tu
 
Kwa sasa Zitto analiomba bunge likubaliane na ombi lake la kupokea taarifa ya mgomo wa madaktari toka kwa waziri mkuu kisha ijadiliwe mjengoni.

SOURCE. Bungeni live TBC

Kama Bunge limepokea ipo haja ya kufanya mjadala mpana kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya Mwaka 2002 badala ya judali tu matamko ya Mhe. Waziri Mkuu na Mawaziri. Sheria hiyo pamoja na Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003, Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma 2009, Nyaraka mbali mbali za utumishi na maagizo yanayotolewa yana kasoro kubwa ambazo leo ndiyo zinachochea migomo ya moja kwa moja watumishi kama huu wa madaktari au ya chini chini ambayo ni ya hatari zaidi inayofanywa na watumishi wengine wa umma. Ni kawaida siku hizi katika ngazi zote kukuta watumishi wanapiga tu soga badala ya kufanya kazi na mahali pengine viongozi wao; Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wamejikuta wakifanya kazi ya kusaini barua za maagizo, ajira, kualika watu kwenye tafrija na maonyo badala ya kuketi na kufikiri ni kwa kiasi gani wanaweza kutumia dhamana zao kutafuta njia za kukuza uchumi (Kama huamini uliza Wizara ya Afya, TAMISEMI na Utumishi utajua). Pamoja na maboresho ya Serikali yanayoendelea bado changamoto ni nyingi mno kiasi kwamba ni vigumu kujua ni wapi hasa tunaelekea. Kimsingi Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeshindwa kujipambanua kama taasisi inayopaswa kuwa na dira ya kuongoza utumishi Tanzania. Kila mtu ana fanya lake ili mradi siku zinakwenda. Wazee wazoefu kama Mhe. William Shelukindo na Mhe. Ntukamazina wanaweza kuona na kusema ni kwa kiwango gani Utumishi imepoteza dira.
 
Spika amesema serikali itatoa taarifa yake na kama itajaliwa au lah..ataamua yeye!

UPDATES;
Ni kwamba mkulu ameomba na ameshapelekewa madai ya madaktari kwa hiyo issue iko juu ngazi ya juu zaidi!!

KINGINE, PM ameomba akutane tena na viongozi wa kamati ya mgomo leo ofisini kwake, ila wamemjibu kwamba awaruhusu kwanza wakae kikao (ambacho alipiga marufuku) ili Madaktari watoe mapendekezo nini wamwambie waziri mkuu kwani wao ni wawakilishi tu!!


Pinda kweli amepinda anataka kukutana na kiongozi gani wakati kesha mtukana sana Ulimboka ambaye ana aminiwa sana na wenzake sasa na wao hawana mwingine zaidi yake itakuwaje na Pinda alisema kwanza Ulimboka ni nani sasa yuko tayari kumtambua ?
 
Pinda kweli amepinda anataka kukutana na kiongozi gani wakati kesha mtukana sana Ulimboka ambaye ana aminiwa sana na wenzake sasa na wao hawana mwingine zaidi yake itakuwaje na Pinda alisema kwanza Ulimboka ni nani sasa yuko tayari kumtambua ?
Ndio matatizo ya viongozi wetu, anasema kabla ya kufikiri. Kufikiri kwao ni jambo la ziada lisilo na umuhimu. Mnakumbuka mkulu aliwaambia wafanyakazi sitaki kura zenu? na baada ya siku akakana kauli yake na kuwapigia magoti watumishi ili wampe hizo kura.
Ndio tatizo,kunena kwanza fikra baadae.
 
Emesahau kuingiza wakuu wa mikoa. nao wanapokuwa bungeni hapata same treatment but they don't contribute to the hojas!!
kama ni mpaka kesho hapa pesa ya wananchi inateketea ina maana siku imepotea na si ajabu wakaifidia siku ya j.mosi posho Tshs 330000/= per day x 325 wabunge=107,250,000/=,ok tutafika tu.
 
limeailiswa = limeahirishwa
kwa Kiswahili "classic" limeakhirishwa.

Limeakhirishwa SIYO kiswahili 'classic' bali ni "Arabic" swahili ama kama hutajali ni "Islamic" swahili.
Limeahirishwa ndiyo Swahili "swahili" kama ambavyo kwa English "english" ungesema "postponed"
 
Kwa sasa Zitto analiomba bunge likubaliane na ombi lake la kupokea taarifa ya mgomo wa madaktari toka kwa waziri mkuu kisha ijadiliwe mjengoni.

SOURCE. Bungeni live TBC

Viongozi wanatakiwa wawe hivyo hongera mr zitto
 
kwa hapa serikali inabidi iwe makini sana kwenye maamuzi, Alisema Pinda yataligharimu taifa, ila hakufanya upembuzi yakinifu kuwa yataligharimu kwa kiasi gani.
chanzo wajue pia ni waliwafukuza wanafundi waliokuwa field kwa vitendo? Mechi inaendelea nadhani half time sasa
 
Hakuna posho nusu, lazima wakamate posho kamaili. Maana walikuwepo Bungeni.

du.. Sina nauli niko mwenge nafatilia kazi bonite home mbezi mwisho, aya bwana..,..napiga njia ya msalaba mwendo mdundo
 
Ndio matatizo ya viongozi wetu, anasema kabla ya kufikiri. Kufikiri kwao ni jambo la ziada lisilo na umuhimu. Mnakumbuka mkulu aliwaambia wafanyakazi sitaki kura zenu? na baada ya siku akakana kauli yake na kuwapigia magoti watumishi ili wampe hizo kura.
Ndio tatizo,kunena kwanza fikra baadae.
Hilo tatizo ulilo libold linaitwa KUROPOKA
 
Ninamsikitikia sana Jakaya Mrisho Kikwete. Analipia usual wake wenye "utata". Maamuzi yote anaachiwa mwenyewe. Suala hili lilianza kwa intern Doctors(hawa ni wahitimu wa bachelor of medicine na sio wanafunzi wa fani hii kama waziri na baadhi ya WAKUU humu wanavyofikiri) kunyimwa posho (allowance)yao ya mwezi. Hii inaitwa posho kwa sababu ingawa intern wanafanya kazi za utabibu kama daktari wanakua chini ya uangalizi wa madktari wazoefu/bingwa na wanapewa malazi na chakula.
Kwa kudai haki hii kiduchu kwa kugoma baada ya kukosa kusikilizwa na hasa kulipwa walidhalilishwa kwa maneno Kama serikali aina hela na wanatakiwa wawe na uzalendo, na hatimae wakarudishwa wizarani ili wakapangiwe upya sehemu za kufanyia "intern"
Chama cha madaktari baada ya kuona dharau Kali ya uongozi wa wizara ukaingilia kuwaunga mkono madaktari wenzao kwa kuweka madai ambayo ni pamoja na kuondolewa kwa uongozi ulioboronga pale wizarani.
Mpaka hapo naweza kuona jinsi Kikwete alivyonamzigo wa "watunga" majipu badala ya watatuzi wa matatizo.
Mzigo mzito zaidi alionao ni Mizengo Kayanza Pinda kiongozi asiyependa kulaumiwa na asiye na maamuzi mwenyemaneno ya kisiasa yanayoibua maswali bila kutatua tatizo. Wakuu angalieni tulipo. Ni Hali ya hatari na maisha ya WATU wengi Yanapotea hata ninavyochangia....nimepandwa na hasira naishia hapa
 
Back
Top Bottom