Zitto Kabwe ana maslahi sakata la UDA?

SON OF DAVID

Member
Apr 1, 2011
42
3
Kitendawili- tega.

UDA imekutwa na ufisadi mkubwa uliowahusisha vigogo wa CCM akiwepo Simba, Masaburi, mtenvu and Azan. Wako ambao hawajajitokeza kwenye magazeti ambao uchunguzi unaweza kuwafumua akiwemo Rizwani Kikwete.

Speaker ameikabidhi sakata hilo kwa Kamati ya Zitto Kabwe.

Zitto ambaye Mimi nina uhakika wa 100% kuwa ni swahiba wa karibu sana wa Rizwani Jakaya kikwete. Urafiki huo ulianza toka UDSM ambako tulisoma mimi na wao - Zitto na Rizwani na Son of David. Zitto alikuja kuwa karibu na Baba wa Rizwani JK na marafiki zao wa karibu Lowasa na Rostam urafiki ambao ulikuja kumletea matatizo na chadema. Na mpaka leo kuna watu wameapa kutompa madaraka makubwa kutokana uswahiba huo.

Sasa hapa jf kuna tetesi nyingine kwamba UDA ina vigogo wengine nyuma ya pazia ambao mmojawapo ni Rizwani wa JK. Nimefuatilia data hizo kwa rafiki yangu mmoja kada wa CCM akaniambia huo ndio ukweli.

Nauliza, kuuliza si ujinga wala wala si dhambi;

A) Zitto ana ubavu wa kumumbua rafiki mkubwa sana ikiwa tetesi hizo ( Rizwani =uda) ni kweli?
B) Je, kama si za kweli, kwa kuwa wa vigogo wengi wa CCM wanafahamu uswahiba wa Zitto na Rizwani, je,wahusika wa UDA hawatamwomba Rizwani awaokoe ktk sakata hilo hata kama Rizwani mwenywe hahusiki?
C) Last senario; Je, Rizwani hataona haja ya kumbana rafiki yake ili aiokoe chama kinachoongozwa na baba yake ili kuficha aibu ya UDA?


Naomba kuwasilisha.

Ni mimi son of David
 
Ni matumaini yangu kuwa tutachangia hoja hii objectively
Maoni unayoyatafuta kwa sasa hayapatikani, sorry jaribu tena baadae..tuthibitishie hiyo 100% ya urafiki kati ya zitto na fisadi ridhiwani..story yako imekaa kiudaku zaidi ndio maana unaona inadoda tu hapa kwenye jukwaa la great thinkers mkuu..
 
Zitto amefanya makubwa zaidi ya hili la sasa, na kama unakumbuka vizuri ni juzi tu amewasilisha ushahidi wa uozo uliopo kwenye Baraza la Mawaziri kwenye maamzi ya kiutawala hasa suala la CHC holdings kwa uongozi wa bunge, atashindwa kufanya kazi ndogo kama hiyo tena ambayo kwa kiasi haimtaji JK directly maana issue kama ya Baraza la mawazili linamgusa JK moja kwa moja kama mwenyekiti wa Baraza.

Kwa kuwa yeye katumwa na Bunge kuchunguza kupitia kamati ya POAC hawezi kufanya maamzi yeye kama yeye isipokuwa itatoka taarifa ya kamati na yeye ameshatoa mwongozo wa jinsi atakavo unda kamati ndogo ndani ya POAC ili ndo ifanye kazi hyo halafu atapatiwa taarfia kwa niaba ya POAC then wataijadili na hatimaye waiwakilshe kwa uongozi wa Bunge.

Kwa sasa nionavo mimi hakuna sababu ya kuhofia independence ya Zitto kwenye hili, tumpe muda afanye kazi yake then tutaona kazi yake itakavokuwa.

Huu ndo mtazamo wangu
 
Back
Top Bottom