Zitto Kabwe akamatwa, afikishwa mahakamani

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923






Na Mwandishi wetu



25th December 2010








headline_bullet.jpg
Ni baada ya kuhutubia mkutano jimboni kwake
headline_bullet.jpg
Adaiwa kutorosha mtuhumiwa kituo cha polisi



Zitto%283%29.jpg

Zitto Zuberi Kabwe




Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amekamatwa na askari wa Jeshi laPolisi kisha kupandishwa kizimbani na kusomewa shtaka la jinai.
Zitto alikamatwa juzi jioni majira ya saa 12:00 akiwa njiani kurejea nyumbani kwake Mwandiga muda mfupi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Kawawa katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Baada ya kumkamata askari hao walimpeleka moja kwa mojaKituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Kigoma kwa mahojiano kisha kumwachia kwa kumpa masharti ya kuripoti jana asubuhi kituoni hapo.
Zitto (34) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alitii amri hiyo na kukamatwa na askari baada ya kuwasili kisha kumfikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Kigoma.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Emmanuel Mlangu, ilidaiwa naMwendesha Mashitaka, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Amoni Chale kuwa Oktoba 27, mwaka huu majira ya saa 5:00 asubuhi katika Kituo cha Polisi Mahembe, mshtakiwa huyo alitumia nguvu kumtoa mtuhumiwa huyo Peter Kibwega ambaye alikuwa chini ya ulinzi halali wa polisi na kumtorosha.
Ilidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni mwanachama wa Chadema alikamatwa na polisi kwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Alexander Bagambena na kumtishia kumuua Nicodemus Stephano na kufunguliwa kesi namba IR/130/20010 kabla ya kudaiwa kutoroshwa na mshtakiwa huyo.
Mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo na kuachiwa baada ya baba yake mzazi, Alhaji Menge Bakari kutimiza masharti ya kuwasilisha barua kutoka kwa afisa mtendaji wa kata kwa dhamana ya Sh. 1,000,000.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Febuari 10, mwakani itakapoanza kusikilizwa baada ya upande wa mashtaka kudai upelelezi wake umekamilika.
Baadhi ya wanachama wa Chadema walikusanyika katika mahakama hiyo wakiongozwa na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Kigoma, Msafiri Wamarwa na kutawanyika baada ya Zito kuachiwa kwa dhamana.



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom