Zitto Kabwe Afichua Wizi Wa Silaha

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
MWENYEKITI wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA), jana aligeuka mbogo na kuwafukuza watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Nchini (Tawiri) baada ya kubaini kupotea kwa silaha ambazo hadi sasa hazijulikani ziliko.

Zitto akiungwa mkono na wajumbe wa kamati hiyo, alisema kamati hiyo imepata hofu kubwa juu ya kutoweka kwa bunduki hizo, na zaidi baada ya kubainika kuwa moja ya silaha zinazoaminika kumilikiwa na taasisi hiyo kuhusishwa na tukio la mauaji mjini Mugumu, mkoani Mara.

Mbali na kuwafukuza watendaji wa taasisi hiyo, aliwaagiza kuwasilisha haraka ndani ya wiki mbili, ripoti kamili itakayoeleza kinagaubaga namna silaha hizo aina ya bunduki zilivyotoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu mwaka 1980.

Zitto alisema kuwa suala la upotevu wa silaha hizo, na nyingine kuhusika katika matukio ya kihalifu ni nyeti, na hivyo kamati hiyo ya Bunge inahitaji maelezo ya kina kutoka kwa watendaji hao, hivyo akawatimua, na kuwaagiza wawasilishe kwake ripoti ya kina mjini Dodoma wakati wa mkutano wa bajeti unaotazamiwa kuanza Juni 12, mwaka huu.

"Sisi kama kamati tumeamua kutoendelea kuijadili taarifa hii kutokana na kuwa na hofu na suala hilo kwani hivi sasa kuna taarifa ya silaha yenu namba 00980 ambayo inashikiliwa katika kituo cha polisi Mugumu tangu mwaka 1999 baada ya kudaiwa kutumika kwenye mauaji," alisema Zitto.

Mwenyekiti huyo alishangazwa na kitendo kilichoonyeshwa na taasisi hiyo cha kushindwa kufuatilia zilipo silaha hizo jambo ambalo linatoa taswira kuwa zinaweza kuwa zinatumika katika uhalifu unaojitokeza nchini.

Alisema silaha hizo zinazomilikiwa na tawi la utafiti la Kingupira lililoko mbuga za wanyama za Serous ziligundulika kutokuwepo katika kituo hicho baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa mwaka 2008 na 2009.

Zitto alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida na inayotia mashaka, watendaji wa taasisi hiyo hadi sasa hawajatoa taarifa polisi kuhusu kutoonekana silaha hizo kwa kipindi chote hicho.

"Ninachofahamu ni kuwa kama silaha yako haionekani kitu cha kwanza ni lazima utaarifu vyombo vya dola …lakini ninyi wenzetu mmenyamaza kimya wala hamjawa na hofu na suala hilo," alisema.

Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora (CCM), alitaka kujua kwa nini baada ya mkaguzi kugundua suala hilo limechukua muda mrefu bila kushughulikiwa.

"Hivi mnafahamu unyeti wa suala hili? Mnajua kwa sasa nchi yetu iko katika wakati gani katika suala la uhalifu? Sio katika maeneo ya mijini tu bali hadi katika hifadhi zetu wanyama wengi wanauliwa hovyo. Inawezekana silaha hizo ndizo zinatumika," alisema Lugora.

Akijitetea Kaimu Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori, Paul Sarakikya, alisema kuwa hawajalipeleka suala hilo polisi kutokana na wizara kuanza kufanya uchunguzi.

Alimuomba mwenyekiti wa kamati hiyo kuwapa mwezi mmoja ili kukamilisha uchunguzi huo jambo ambalo halikuafikiwa.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Simon Mduma, alisema kuwa kutokana na uzito wa suala hilo Aprili mwaka huu walilazimika kuiandikia Wizara ya Maliasili na Utalii barua na kuhoji ziliko silaha hizo kwa kuwa hata katika vitabu vyao hakukua na taarifa zozote.


CHANZO: Tanzania Daima
 
MWENYEKITI wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA), jana aligeuka mbogo na kuwafukuza watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Nchini (Tawiri) baada ya kubaini kupotea kwa silaha ambazo hadi sasa hazijulikani ziliko


  • Kawafukuza kazi? (Zitto ana mamlaka ya kufukuza kazi watendaji)?
  • Kawakimbiza (Mbio)?

Ebu nifafanulieni hapo
 
Silaha zenyewe kama hii au?

attachment.php
 
Inawezekana Maige iliiijua hili? naye ashitakiwe na awajibishwe
 
Wakafanye uchunguzi Polisi, Magereza, JWTZ ndiko kwenye silaha nyingi zaidi. Kwi kwi kwi teh teh teh.
 
dah!,mmekula pesa za nchi hamkushiba,mmekula madini,hamkushiba,mmekula wanyama hamkushiba,mali zote na madaraka ya nchi hii mmechuka hamjashia,sasa mmeona ni bora kugawana siraha tena mchana kweupe.sizani kama tutakuta kitu 2015,Mungu ibariki Tanzania.
 
Pana vioja kwa serikali ya awamu hii na inavyoonyesha kabla ya 2015 tutayasikia mengi.
 
Back
Top Bottom