Zitto: Dr Ulimboka kutekwa, kupigwa na kuumizwa; Serikali inawajibika kutueleza

Nilifikiria hiki ni kipindi cha Madaktari wote kuonyesha u'serious wao katika kuishinikiza serikali kutekeleza matakwa yao kwa kuendelea kugoma,kumbe wito wa tofauti ndo unaotolewa.

Inamaana Ulimboka ni tofauti na Watanzania wengine?
Narudia tena nalaani kwa nguvu zote kitendo alichofanyiwa Dk Ulimboka,lkn pia napinga kwa nguvu zote kitendo cha Madaktari kugoma
 
Haiingii akilini kwa binaadam yeyote mwenye fikra japo kidogo, eti Serikali wakuchukuwe, wakupige, wakutupe Mabwepande halafu waje haki za binaadam kukuota.

zomba, Kitendo cha watu wa haki za binadamu kupata taarifa za huu mkasa wa Dr Ulimboka ni kielelezo tosha kuwa wananchi hawana imani na serikali pamoja na vyombo vyake. Wananchi wanatembea na number za simu za taasisi za kiraia badala ya polisi! huu ni msiba wa taifa.
 
viongozi dhaifu hawajui namna ya kutatua matatizo ya wananchi! viongozi dhaifu wanachoweza ni kulipa kisasi!

naona yalio tokea libya , na syria sasa yanakuja tanzania ..utabiti wa mrema....

huko libya wakundi ya kutumika walikua wakiua watu then akisingiziwa ghadafi na serikali yake..hatimae tunajua kilichofata...
na huko syria wauaji walio funzwa vyema wanauwa vichanga , watoto na wanawake then wanasingiziwa majeshi ya serikali...propaganda zinapigwa dunia nzima kwamba serikali ya Bashar assad inaua...mbona huko nyuma hajamuua hata sisismizi ?
mbinu hizi zilitumika sehemu nyingi ..lengo kuifanya jamii waichukie serikali yao....
naomba serikali ichuke tahadhari kubwa na kufanya uchunguzi wa kina na pia ushauri wa mrema na kauli yake kwamba aliwahi kuitwa na ubalozi mmoja ili kufanya mambo kama haya lakini mrema alikua shujaa na mzalendo halisi akakataa.

hakuna mantiki kwa serikali au pinda au kikwete kuwa wanahusika...serikali sana sana ingewafukuza hawa madaktari na kuwapiga marufuku kufanya shughuli yoyote ndani ya nchi.basi ingetosha kuwa ni adabu ya kwao kugoma kwa sababu za kisiasa.
tujihadhari...
 
Bogus kabisa wewe subiri siku yako ifike ndio itakuingia akirini.

Nyinyi ndio bogus mnaokuja na habari za uongo kila siku na mnaokubali kila mnachoambiwa bila kungoja kujuwa ukweli.

"akirini" ndio nini?
 
Nasita kusema Zomba ana akili mgando kama sio mmoja wao. Hivi inaingia akilini kujua kama serikale inaweza fanya hivyo. Napata wasiwasi kuamini kwamba na wewe kama si mmoja wao basi ni rafiki wa hao.

Sihitaji kuhusisha hili na elimu yako-kwani hoja yako hii inaonyesha kwamba kama sio darasa la saba basi una shule ya kuungaunga-lasaba-certificate-certificate diploma....

Wote wenye nia njema tumwombee mwenzetu apone-uhakika utafahamika tu siku moja.
 
Mbona ni afadhali wakati wa JK amepigwa na amepatikana, wakati wa Nyerere usinge muona kabisa na angetoweka kwenye historia ya ulimwengu, wewe hata historia hujui kumbe. Nyamaza kama hujui kitu.
well said mkuu!,
ndOmaana nakwambia ile kauli ya kayanza ina utata!, yule jamaa alifundishwa mbinu za kimafia na nyerere pale ikulu alipokua uwt. kakaa pale ikulu zaidi ya 20 years, LIWALO NA LIWE hii sentesi ni tata sana na INAHUSIKA, ichunguzwe
 
Serikali ya wahuni ufanya vitu vyake kihuni, sasa kama Madaktari wamegomea mwajiri wao hiyo ni haki yao na cha kufanya ni kufukuzwa , Sio kuwasaka na kuwafanyia vitu vya kihuni kama hiki. Sio lazima watu wafanye kazi ya udaktari kama wanaona ni manyanyaso , Ndio maana wako wengi wameacha hii taaluma. Jambo la kufanya ni kuwafukuza lakini sio kuwaua
 
Nimeshangazwa sana na kauli ya zitto ya kuiambia serikali itoe kauli kuhusu swala la Dr.Ulimboka wakati tukio
zima lina fingerprrint chungu nzima za serikali. ningetegemea hata angeomba tume huru ambayo inge involve
watu kama shivji au ulimwengu kuchunguza tukio zima. hakuna raia wanaweza kufanya operation ya kijeshi
kama ile kama ukiangalia vizuri operation hii inafanana kabisa na ile iliyoendeshwa na zombe kipindi kile.

utabiri wangu.
Rais Dhaifu kama kawaida yake ili kupiga changa la macho watu atakwenda muhimbili au popote alipo ulimboka
kumsalimia huku akiaidi serikali kuchunguza swala hilo kiundani(yaani muuaji ajichunguze mwenyewe kana kwamba
kweli anahusika na mahuaji.
 
Mkuu nakuona ulivyocharuka kwenye comments zako kuitetea serikali katika counterattack.. Ninapata shaka kama uliandaliwa vlee.. Ulishafahamu mapema kabla ya tukio mkuu..?


KIONGOZI najaribu kuwa balanced. Unajuwa watu wengi wameihukumu serikali kuwa inahusika; siamini mimi kama Kiongozi wa Juu wa Serikali anaweza kuamuru tendo la kinyama kama lile
 
Nimeumizwa sana moyoni kwa taarifa hizi. Yaani ni zaidi ya mshtuko, Taifa limepoteza Dira, Serikali yetu Kipofu,..

Dalili za chama tawala kuanguka ndo hizo, mjipange kuwa chama cha upinzani.Ama kweli dhaifu huzaa dhaifu,baada ya hapo sijui mtaendelea kuua wapi?Damu zao hazitapotea bure siku mtalipa yote mabaya mlotenda hapa hapa duniani.
 
KIONGOZI najaribu kuwa balanced. Unajuwa watu wengi wameihukumu serikali kuwa inahusika; siamini mimi kama Kiongozi wa Juu wa Serikali anaweza kuamuru tendo la kinyama kama lile

Mkuu najua we dnt need to jump into conclusion kwa tukio hili.. Kuna comment ambayo niliandika kwenye thread ya mwanzo kwamba tuwe makini na tuwaachie polisi (japo nilisema credibility ya polisi kwenye matukio kama haya inatia shaka) bt Serikali ina uwezo mkubwa wa kujiondoa kwenye tuhuma kama watakubali kuunda chombo huru kitakachokuwa na watu huru kuchunguza tukio hilo.. Imani yangu findings toka kwa chombo hicho haitaacha shaka miongoni mwa wananchi.. Chini ya hapo nionavyo mie itakuwa shaka kubwa kwa Serikali kujiondoa kwenye tuhuma hizi..
 
Pole sana Dr Ulimboka. Vilio vyetu na salam zetu hakika zitamfikia Muumba na hatakuacha, ila utasimama tena na kuwatia maadui zako chini ya miguu yako.

Nalilaani sana tukio hili pamoja wote waliolipanga na kulitekeleza. Hakika kwa matukio kama haya, Tanzania haitakuwa tena iliyokuwa jana!

Tunakuombea Ulimboka pamoja na familia yako. Hii nchi ni yetu sote na tumehamasika zaidi kuzidai haki za Watanzania.
 
zomba nani mwingine anayeweza kufanya jambo kama hilo halafu akabaki salama? Serikali ina nguvu sana na ina resources za kufuatilia yale inayotaka kufuatilia.Kama ni mambo mema, basi nchi itajaa mema...kama ni ukauzu ndo hivyo tena...watu watakuwa wanaishi kama nchi siyo yao.

Kuna watu wasiyoitakia mema hii nchi na wameshasema kuwa "watahakikisha" hii nchi "haitawaliki".
 
Naona Bunge nalo limefunika KOMBE mwanaharamu apite!

Ifike mahali Serikali iache kuingiza mikono yake katika mihimili mingine vinginevyo hakutakuwa na haja ya kuwa na mihimili hii.

Bi Kiroboto anapokuwa msemaji wa Serikali na kutetea na kukataa kuleta riport ya kamati ya huduma za jamii ni kuongeza ukubwa wa tatizo na si kutafuta suluhu.

Kiganyi, JF.
www.wotepamoja.com
 
Ni jambo la kusikitisha sana kuona Tanzania yetu imefikishwa hapo na watendaji wabovu wa nchi hii. Najaribu kufikiria ni jinsi gani tunaweza kujinasua na huu mtego. Tuko kwenye vicious circle. Angalia tatizo moja linaanzisha tatizo jingine ni jambo la kusikitisha sana.

Hapa si issue ndogo tumeona watu wetu wengi wakiuawa au kudhururiwa katika mazingira ambayo hayawezi kuelezeka na kuzua maswali mengi. Hii inaonesha wazi kuwa serikali na viongozi wetu wameshalewa madaraka na kwa kuwa wanayoyafanya hayakubaliki wanaogopa kuwajibika hivyo kutumia vitisho, kudhuru na pengine kuuwa watu ili kuficha madhambi yao.

Kuna matukio mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu lakini serikali imekuwa ikikaa kimya au kutokushughulikia ipasavyo hasa pale serikali inapokuwa na maslahi. Tunayo mambo mengi yaliyozua maswali na yameishia juu juu tu yaani wameyapotezea.

1. Nani asiyejua Kifo cha Amina Chifupa- Kilizua maswali Kibao
2.Dr. Mwakembe na Prof Mwakyusa wamewekewa sumu nini kinaendelea ni usanii tu.
3.Ditopile kaua adharani mnakumbuka kilichotokea.
4. Kifo cha Kombe nani anaelewa?
5.Mkurugenzi wa zamani wa TFDA. Mnakumbuka?
6.Wale wafanya biashara wa madini Morogoro kesi iliendeshwaje?
Ninachoona tuko kwenye situation ambayo tumempa fisi atulindie bucha tukitegemea ulinzi dhabiti ni kujidanganya.
Vijana na wananchi wote tuamke tufanye mabadialiko vinginevyo nchi yetu imekwisha.
 
Kuna watu wasiyoitakia mema hii nchi na wameshasema kuwa "watahakikisha" hii nchi "haitawaliki".

zomba, kama ni strategist, is the killing or torturing approach provides the last solution? I think tulipofika badala ya kutunisha misuli na kufikiria tuko kwenye holywood movies, watawala waanze kuwatumikia watanzania na kutimiza wajibu zao. Kama madaktari wanamakosa, na wezi wa mali ya umma nao wana makosa. Tutumie platform sawa katika kushugulikia mambo yote yanayotuhusu.
Ukali na ubabe ni strategy wanayotumia watu walio very weak.....heshima ya serikali na vyombo vya dola itashuka sana kama hali ya ubabe itakuwa ndio first approach kwenye kutatua matatizo yanayotuzunguka. Turudi tena kwenye hekima, uadilifu na diplomasia
 
Angalia wasije waka Mkolimba,sababu Kolimba alikuwa mwana ccm kweli kweli lakini baadae alikolimbwa.
 
tusistaajabu ya jk je tunakumbuka ya mkapa pale muembechai na kule zanzibar hiyo ndio ccm ni juu yako kupima
 
Back
Top Bottom