Zitto: Dr Ulimboka kutekwa, kupigwa na kuumizwa; Serikali inawajibika kutueleza

Naona sasa Zitto nae anaipeIeka hii ishu kisiasa! Kama hana uhakika wa serikari kuhusika asiIete mambo ya hisia zake
 
Tanzania!! Zaidi ya tuijuavyo!!! Waliolaaniwa ndio watawala (nashindwa hata kuwaita viongozi) wetu kwani ukichunguza utaona wapo katika laana kwa mambo yao ya kihuni wanayofanya au kusema... Haya sasa ukidai haki yako ndo hivo unafanyiwa, tutafika kweli? Mungu atusaidie!!
 
Hakika Tanzania yetu sasa inangamia kama serikali imefikia kufanya huu unyama basi tumekwisha.

Natamani serikali nchi yangu ingekuwa inaheshimu haki za raia wake lakini ni kinyume chake.

KWERI KIKWETE HUKUSITAHILI KUWA KIONGOZI WA TAIFA HILI
 

Wednesday, June 27, 2012

ThisDay NewsPaper

Zitto Kabwe:'Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous'.

Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.

Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.

Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa 'agente provocateure' kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.

Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.

Nimemuomba Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one, injuries to all'
Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu.

Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.



 
Napata shida sana kuamini au kuelewa.....kuna aja ya kuliangalia hili swala kwa karibu.hisije ikawa kuna kundi fulani linalotafuta opportunity to bring chaos into this country........people who love this country it is about time to be wise and look into this matter closely.kama ni serikali iko nyuma ya hili jambo basi clearly imekosa mwelekeo but kama kuna kundi jingine behind this basi itabidi lifanyiwe kazi ipasavyo. Tumuombeee dr apone haraka
 
Haiingii akilini kwa binaadam yeyote mwenye fikra japo kidogo, eti Serikali wakuchukuwe, wakupige, wakutupe Mabwepande halafu waje haki za binaadam kukuota.

Unaeleweka huwa unasimamia kitu gani,najua haitawasumbua wachangia mada.
 
Haiingii akilini kwa binaadam yeyote mwenye fikra japo kidogo, eti Serikali wakuchukuwe, wakupige, wakutupe Mabwepande halafu waje haki za binaadam kukuota.
Mkuu umesahau Bwana Zombe alifanyaje na vijana wake kwa wale watu wamadini kutoka Morogoro??? Kwani si walifia huko Mabwepande Mkuu na kupelekwa sehemu nyingine kama ushahidi??? Kuna watu hatari saana serikalini ila hatujui wanapewa na nani amri za ajabu ajabu hadi kuuwa watu innocent kabisa simply tu wanatetea wanyonge!!!!

 
Kama Waliitaka kuifuta family ya Nguza babu seya kisa kidosho siwezi shangaa Kwa yaliyotokea Kwa Dr
 
Inauma sana , inaleta hasira, sitaki kuamini kuwa ktk nchi yetu wenyewe , wananchi tunakosa usalama , usalama uliopo ni kwa ajili ya wachache! kodi zetu zinalipia vyombo vya usalama , lakini impact inaturudia walalahoi na wanaodai haki yao kushughulikiwa ipasavyo PENGINE NA HIVIHIVI vyombo. hii haikubaliki hata kidogo kuishi kama wakimbizi katika nchi yetu wenyewe. get well soon DR STEVEN ULIMBOKA
 
Wana JF,
KUNA WADAU WENGI KWENYE HILI LA DR ULIMBOKA: Kuna serikali, kuna wananchi wanaoathirika na mgomo wa madaktari.Katika waathirika, kuna wahalifu, wapenda amani, wapenda fujo na pia wahuni tu wenye ari ya kufanya uhuni na wanachohitaji ni "kisababishi".Kuna "maadui' wa kawaida wa Dr Ulimboka.
Tusikimbilie kuilamu serikali tu maana tutakosa kuona picha pana.
JF Members should be "THINKERS" above all.Hebu fikirieni zaidi.
 
Huu ni wakati mgumu kwa sababu madaktari wote kwa pamoja hospitali zote nchini wameweka vifaa vyao vyote chini. Hakuna dharura wala chochote. Hawaogopi kufukuzwa kazi, vitisho au hata kifo. Kwani kama wamedhamiria kukuua watakuuwa tu. Wananchi tuelewe kwamba sasa daktari hayuko salama yeye mwenyewe,ataokoa vipi uhai? Kura yangu.......mimi na tanzania......................i wish i could turn back the time.
 
Huu ni wakati mgumu kwa sababu madaktari wote kwa pamoja hospitali zote nchini wameweka vifaa vyao vyote chini. Hakuna dharura wala chochote. Hawaogopi kufukuzwa kazi, vitisho au hata kifo. Kwani kama wamedhamiria kukuua watakuuwa tu. Wananchi tuelewe kwamba sasa daktari hayuko salama yeye mwenyewe,ataokoa vipi uhai? Kura yangu.......mimi na tanzania......................i wish i could turn back the time.
 
Pole sana Dr. Ulimboka. Tunakuombea kwa Mungu Akupe nguvu ya uponyaji haraka.

Kwa wale wanaofikiria watazima vuguvugu la kujikomboa kwa mtanzania kwa kumteka na kumuumiza Dr. Ulimboka wajue ya kwamba wameweka petroli kwenye moto. Ole wao, siku zao zimefikia mwisho.

Kwa wanaokumbuka historia ya Ufaransa, binti mfalme Marie-Antoinette hakuelewa kwa nini watu walikuwa wanaandamana, akamuuliza mama yake Malkia kwa nini wanaandamana. Alipojibiwa 'wanaandamana kwa kuwa hawana mikate', Marie-Antoinette alijibu 'si wale keki?'

Hii inadhihirisha viongozi wa Tanzania hawazijui shida za walalahoi wanaolala chini kwenye hospitali zetu, wanaokufa kila siku kwa kuwa hospitali hazina vifaa kama X Ray, hakuna dawa, hakuna hata bandage za kufunga vidonda. Madaktari wanachodai ni mazingira bora ya huduma za afya na vitendea kazi. Kwa kifupi wanataka serikali iwakumbuke watanzania wanaoteseka bila huduma za afya ambazo ni haki yao ya msingi, wakati viongozi na familia zao wanakimbizwa Afrika ya Kusini, India na hata Ulaya kupata matibabu. Badala ya kutafuta ufumbuzi wa madai haya, serikali inawajibu kwa vitisho na hata kufikia kumteka kiongozi wa madaktari.

Familia ya kifalme Ufaransa iliondolewa madarakani na Marie-Antoinette pamoja na wenzake walielewa maana ya nguvu ya umma. Hatuhitaji keki, tunaomba haki yetu tupate huo mkate!

Mpaka Kieleweke!
 
kumbe mabwe pande imeachwa na serikali kuwa sirikali ya mauaji, basi msitu ule upigwe moto kwani hauna faida zaidi ya mauaji. Watu wanakosa viwanja wao wanaujaza damu za watu wasio na hatia.
 
Chunga tamaa mbaya!

Wewe inaelekea una chuki binafsi na serikali.

Mimi natamani wahusika wapatikane na wa confess

Mkuu nakuona ulivyocharuka kwenye comments zako kuitetea serikali katika counterattack.. Ninapata shaka kama uliandaliwa vlee.. Ulishafahamu mapema kabla ya tukio mkuu..?
 
Serikali ya CCM inatakiwa itafakari.. je Baada ya kumuua Sokoine ufisadi/uhujumu uchumi uliwafikisha wapi, je ndo ulikuwa na manufaa au ndo laana inayoitafuna serikali hadi leo,je hali ya uhujumu uchumi imefikisha wapi taifa, je kama Sokoine angebaki hai hali ingekuwa hivi????
Walipomuuwa kolimba, je kupoteza dira kwa ccm kumefikia wapi? je kwa kuumua ndo walipata dira au ndo walipotea njia na kutokea hapa walipo? je ccm iliimarika baada ya kumuuwa au ndo ilizidi kuyumba???
Walitarajia wamwmuua Dr Ulimboka, je wanafikiri kwa kufanya hivyo ndo wataimarisha huduma za afya? je ndo migomo itaisha? maslahi ya madaktari hayatadaiwa?
 
Back
Top Bottom