Zitto: Dr Ulimboka kutekwa, kupigwa na kuumizwa; Serikali inawajibika kutueleza

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765
ulimboka1.jpg

Dr. Steven Ulimboka

Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI
‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous'

Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.


Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.

Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa 'agente provocateure' kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.

Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.

Nimemuomba Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one, injuries to all'

Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.

Kiganyi, JF.
Health - Wotepamoja
 
Serikali IELEZE NINI?

TUPATE MAELEZO YA LHRC KWANZA, Wao walijuajejuaje kuwa Majeruhi yuko Mabwepande
 
Siungi mkono kitendo alichofanyiwa Dr. Ulimboka kama ambavyo siungi mkono mgomo wa madaktari.
 
Kama vipi tuandamane kushinikiza kauzu Pinda awajibike
kwa kauli yake aaaaah!
 
Ningeomba Mh. Zitto aende mbali zaidi ya hapo. Of coz kwa jinsi hali ilivyo CHADEMA ni muhimu sana kutoa tamko, kadhalika vikundi vya haki za binadamu na taasisi nyingine.

Najua kina Nape na Dhaifu watainuka kusema hizo ni propaganda na eti madaktari wanatumika kisiasa lakini hatutajali upuuzi wao huo!

Ni watu wenye akili punguani au kitu cha kufanana na hilo (mfano Zomba) ndio wanaoweza wasione (kwa makusudi) ushiriki na mkono wa Serikali ya CCM ktk tukio hili la kinyama.

Ninalaani kwa nguvu zote ukatili na vitisho kwa Dr. Ulimboka na madaktari wote. Mwito wangu kwao ni kuwa wana azma na nia nzuri kuboresha huduma za afya na maslahi ya taaluma zao na katu wasirudi nyuma. Pia wampe mwenzao sapoti kubwa hasa wakati huu mgumu.

Pole Dr, Ulimboka, poleni familia yake na madaktari kwa ujumla

Wanahaarakati na
 
Haiingii akilini kwa binaadam yeyote mwenye fikra japo kidogo, eti Serikali wakuchukuwe, wakupige, wakutupe Mabwepande halafu waje haki za binaadam kukuota.
 
Watu wengi wanyonge wana namba za LHRC maana hupewa msaada wa kisheria...ndivyo LRHC walivyopata habari
Kama waliomuokota wanamjua Ulimboka, walijua wakiripoti Polisi ndio wamempoteza.
Jeshi la Polisi lijiulize kwa nini Wananchi hawakuwaamini wao wakaamini LHRC
Hilo ndio swali kubwa...sio lako
 
Hata SUMAYE na ufisadi wake alishawahi kusema kuwa, Mtu aneyetumia kalamu kuwachafua wenzake, akipata madaraka atatumia mtutu kuwanyamazisha wanaompinga. Ndio JK huyo, hana tofauti na Mseveni au Idd Amin.
 
Ni kawaida ya serikal ya ccm, hata km wamehusika wataleta propoganda. Hili suala la kuua watu hata mh mbowe aliliongelea juz mbungeni. Ccm na serkal yake ndio walivyo. Achen jaman huo mtindo.
 
Serikali hii hii, haiwezi kutoa tamko lolote itaendelea na uchunguzi hadi watu hasira zenu ziwatoke na watamlazimisha ulimboka kukanusha yote, NGOJA TUSUBIRI.

Eh mungu mpe uponyaji kijana.
Si vyema alivyofanyiwa.
 
serikali ya kihuni huwa ina mbinu za kihuni katika kutatua matatizo..naanza kuamnin kwa nini Nyerere alikuwa hataka JK awe rais...

Mbona ni afadhali wakati wa JK amepigwa na amepatikana, wakati wa Nyerere usinge muona kabisa na angetoweka kwenye historia ya ulimwengu, wewe hata historia hujui kumbe. Nyamaza kama hujui kitu.
 
Back
Top Bottom