Zitto: Contracts review is a publicity stunt and creation of unnecessary uncertainty in the sector

Hivi wewe unaelewa kiingereza sawa sawa? Zitto kasema malivyuu kama hili ni bogazi tu kwani yashafanyika miaka nenda rudi bila kubadili chochote. Mwenzako Zitto anawataka wenye muono kama wake wapige kelele kubadili utaratibu mbovu uliopo na zaidi sana bunge liwe na mamlaka ya kujadili na kuidhinisha mikataba hiyo miovu. Mikataba hii iwe wazi ili hata wewe uwe na haki ya kuuona. Hivi kusema hayo ndio kukatisha tamaa kwa lugha ya kwenu eehh?? Duh kweli its a long way to fairness!!

Ni bunge lipi unaloongelea liwe na makucha ya ya kuangalia mikataba? bunge letu kwa sasa halina watu wenye uwezo kushinda wataalam wanaoandaa mikataba hiyo limejaa walala hoi, sasa sijui bunge linalokuwa refered hapa ni la njozi au ni hili hili lililopitisha sheria mbovu ya mafao na sasa wanataka kuiagalia tena kwa pesa za walalahoi baada ya watu wenye maono nje ya bunge kuwajulisha kuwa hicho walichopitisha ni janga ua zito na wanaounga mkono bunge kuangalia mikataba hawaoni uwezo wa bunge letu?
 
Kimsingi sikubaliani na majumuisho ya jumla na dhanifu kuwa review hii ya mikataba inayotayarishwa na Prof Muhongo ni populist in nature.
Pamoja na mchango huu mzuri maudhui ya mchango wenyewe ni kwamba kwa vile pro active stance ya kurekebisha kasoro za mikatba hiyo inatoka kwenye serikali ya CCM, basi zoezi lenyewe ni naught.

Kuna watu waliojijengea mioyoni mwao kuwa na mtazamo hasi kwa kila kitu kinachofanywa na serikali ya CCM, hata kama ni kwa faida ya wananchi waliowengi.

Prof zmuhongo( na ndg Maswi) wamepigwa vita sana pale Wizara ya Nishati na Madini, vita ya wazi wazi na hata kisiasa kupitia Wabunge.

Siyo siri kuwa mikataba hii mibovu imetayarishwa na wanasiasa ambao baadhi wananufaika nayo hadi leo hii.

Ndiyo maana tulio wengi tunashangaa sana kuwa at last kapatikana mtu mwenye kuthubutu kuchambua the pandora box ya uchafu wa mikataba ya kifisadi, watu kama Zitto wanakuja juu.

Kwa msimamo huu, je CDM ni just an idler katika gurudumu la masahihisho ya mikataba hiyo?
Kulaumu tu from a safe distance?

Mimi nachelea kukubaliana na misimamo isiyo na misingi.
Tungependa vile vile Mzee Mwanakijiji kupata maoni yako ya kisera juu ya mikakati potofu na kifisadi kwa suala la Meya wa Moshi na safari ya masomo Kigali.

Zaidi ya maneno matupu sitegemei zaidi toka wenzetu wa CDM.

naona na wewe ndugu yangu naona umenipita. Ninachosema ni kuwa hakuna ubaya kwa Muhongo au kiongozi yeyote wa CCM kufanya jambo ambalo litakipa chama umaarufu na serikali yake kupendwa. Assume kuwa Muhongo amefanya mambo kupata umaarufu yeye na serikali yake; kuna ubaya gani?
 
Mimi nachelea kukubaliana na misimamo isiyo na misingi.
Tungependa vile vile Mzee Mwanakijiji kupata maoni yako ya kisera juu ya mikakati potofu na kifisadi kwa suala la Meya wa Moshi na safari ya masomo Kigali.

Kuna mambo mengine kwa kweli huwa siyatolei maoni kwa sababu maoni ambayo wengine wameshayatoa yanawakilisha ya kwangu kwa kiasi kikubwa.
 
Mpaka mtu afe ndipo kiufahari uende kuhani msiba wakati ulikuwa na taarifa kuwa anaumwa na hukutaka kumpeleka hospitali.

Kwanini ZITTO KABWE anakatisha tamaa? Kwanini Asiache WAZIRI WA NISHATI na MADINI afanye kazi yake? Akishindwa aeleze...

Yaani ameishaanza kukatisha tamaa... Au there is 10% they will need 2 return????
 
Nakubaliana na wewe kabisa kwamba inawezekana kuna wanasiasa au watu wenye mamlaka ya kisiasa au hata watu waliokuwa na mamlaka ya kisiasa ambao wanafaidika mfumo wa sasa katika sekta ya Mafuta na Gesi. Hoja yangu mimi ni kwamba Mapitio yaliyotangazwa na Waziri wa Nishati alipokuwa anazindua Bodi ya TPDC hayatatoa jibu. Mikataba iwekwe wazi. Uwazi wa kila mtu kuona na sio Bodi ya TPDC tu. Uwazi ndio utakaoleta mabadiliko. Kwanini tukubali mapitio tu bila kuambiwa hiyo mikataba ina nini? After all wanaoambiwa wapitie ndio walioingia mikataba hiyo kwa upande mmoja na Waziri anasaini kwa upande mwingine.

Sekta ya Gesi na Mafuta haihitaji maneno matamu ya kuridhisha watu. The sector needs a radical approach ili kuepuka yaliyotokea kwenye sekta ya madini. Tunataka kutoka kuamini watu twende kwenye kuamini Taasisi. Tunataka kuhakikisha kuwa makosa yaliyofanywa kwenye sekta ya madini hayarudiwi tena. Sasa unaweza kuamua kukaa kimya na kusema Muhongo atafanya kwa niaba yangu au unaweza kuamua kushiriki kama raia kwa kusema 'ngoja kwanza, hivi hiyo mikataba inayoamriwa kupitiwa ipoje?"

Sidhani kama ni busara kufurahia mapitio wakati hata hatujui kinachopitiwa. Tulifanya makosa hayo huko nyuma kwenye Madini. Tunarudia tena kuamini kuwa mapitio ndio suluhisho la mikataba mibovu Tanzania. Mimi sipo tayari kurudia makosa yale. Ninapenda uwazi wa hii mikataba. Waziri aweke wazi mikataba hii maana hakuna sheria inayozuia. Vinginevyo ni siasa tu.

Zitto,
Mimi nashindwa kukuelewa wewe. Waziri amewataka wajumbe wa bodi wapitie hiyo mikataba mipya halafu wampe maoni yao kama inafaa au la. Wakati huo huo profesa mwenyewe atakuwa anafanya mapitio yake aone ni wapi atatofautiana au kukubaliana na wajumbe wa bodi. What is wrong with that? Wewe kumwita waziri ni irresponsible inaonyesha kuwa wewe ni irresponsible au uko mfukoni mwa "wawekezaji" ambao inaonekana unataka kuwapendeza zaidi ya maslahi ya nchi. Mwache waziri afanye kazi yake. Waache wajumbe wa bodi wapitie tusikie maoni yao. Kwenye madini kama nijuavyo, hakukuwa na mapitio. Mikataba ilisainiwa ikiwa ni siri kati ya yule aliyesaini kwa niaba ya serikali na mwekezaji. Hilo wengine tunalipinga. Waziri Muhongo hajasema kuwa hataiweka wazi mikataba baada ya kupitiwa na wajumbe wa bodi. Inaonekana wewe ndiye uliyeshoot from the hip.
 
Kwa nini unapenda kukuza tuhuma hizi za kukihusisha chama hiki na masuala ya kidini ?

Sitaki kuamini kuwa nawe unaweza kuwa kati ya wahandishi habari wanaotumika kuliingiza taifa katika machafuko ya kidini kupitia siasa, huku wanaotaka kuiba rasilimali zetu wakiwa tayari kuingia nchini.

Lakini mwenendo wako ukiendelea hivi sina budi kukuweka katika wahalifu wa kusababisha machafuko nchini.

Tafakari na uchukue hatua.
Mkuu MpigaKelele, kumbe ndio mimi ninayepiga kele kuzikuza tuhuma hizo?, cha msingi tuhuma hizo zipo na kila mwenye akili tima u anaujua ukweli kuwa Chadema sio chama na kidini wala kikanda ndio maana kina wabunge na madiwani maeneo mbalimbali na wa dini tofauti!. Kwa vile hizi ni tuhuma, na zipo, sio mimi nimezibuni, then ili kuuthibitishia umma kuwa sio kweli, Chadema lazima ifanye "affimative action" against them, tena wakati wakiandaa ilani yao ya uchaguzi 2015, nitawashauri kuiingiza "mahakama ya kadhi" na "kuirejesha Tanzania kwenye OIC"!.

Kama kutetea haki na usawa ni uhalifu, usisubiri mpaka nikiendelea, nakushauri unikiingize kabisa kwenye hiyo list ya wahalifu na ikibidi uniripoti kabisa ili vyombo husika vifanya "prevention" kabla ya hayo machafuko!.

Ila pia, tatilo lako Mkuu Mpiga kelele, nimeshalijua!, na sio lako tuu bali ni la wengi, kwa vile kwa urais wa 2015, wewe tayari unaye mgombea wako kichwani wa tiketi ya Chadema, hivyo akitajwa mwingine yoyote ambaye sio, inakuwa nongwa!, na haswa huyo anayetajwa kama sio wa imani yako, unaona kama vile ni dhambi!.
P.
 
Ahsante sana Mkuu FJM

Tunaweza kuwa na mbunge mmoja mmoja lakini bunge kama taasisi hatuna. Tuna rubber stamp ya kulinda maslahi ya watu wachache. Nakubaliana na mdau mmoja aliyesema tatizo si kuweka mambo wazi. Kwani nani asiyejua EPA au Rada? Nini kimefanyika?

Tanzania tumefika mahali viongozi hawaoni aibu hata chembe kuiba mchana kweupe! Mwaka jana Tanzania ilipoingia mkataba na China kujenga bomba la gas, hawa wazungu wa Songosongo walileta kelele sana. Hawakutaka kabisa bomba jingine obviously kulinda maslahi yao. Sasa wanaanza kutishia watu kuwa hawati kuwekeza kwenye nchi ambayo mikataba inabilika? Huko kwao mbona mambo yanabadilika?

Australia walibalisha mikataba ya madini na sasa makampuni yanalipa kodi kubwa sana. Mbona hayo makampuni hayakuhama?Tabia ya kuwabembeleza wawekezaji hata kwa rasilimali ambazo hawawezi kupata sehemu nyingine kirahisi ndio inatufanya tuonekane kama wanasesere. Mchana hawa wazungu watakutisha ukibalisha mikataba wataondoka, jioni wakwenda George & Dragon kucheka jinsi watanzania walivyo mazezeta!
 
Last edited by a moderator:
Bora nawe umeliona hili. Halafu watu wakipinga hoja zake anaanza kushusha kejeli.

Kwa nini unapenda kukuza tuhuma hizi za kukihusisha chama hiki na masuala ya kidini ?
Sitaki kuamini kuwa nawe unaweza kuwa kati ya wahandishi habari wanaotumika kuliingiza taifa katika machafuko ya kidini kupitia siasa, huku wanaotaka kuiba rasilimali zetu wakiwa tayari kuingia nchini.

Lakini mwenendo wako ukiendelea hivi sina budi kukuweka katika wahalifu wa kusababisha machafuko nchini.

Tafakari na uchukue hatua.

Mkuu GKassanga, ZZK ni level nyingine kabisa!. Humu jf, tuna Vichwa maji kibao ambao uelewa wao ni finyu sana, lakini kazi yao kubwa humu ni kupiga kelele za kupinga kila jema

Pasco.
 
Oil gas contracts extremely biased in favour of rich oil companies that we really have nothing to loose if they close shop. At any rate oil bride has lots of suitors knocking at the doors. Exit west, karibu East.
 
Nakubaliana na wewe kabisa kwamba inawezekana kuna wanasiasa au watu wenye mamlaka ya kisiasa au hata watu waliokuwa na mamlaka ya kisiasa ambao wanafaidika mfumo wa sasa katika sekta ya Mafuta na Gesi. Hoja yangu mimi ni kwamba Mapitio yaliyotangazwa na Waziri wa Nishati alipokuwa anazindua Bodi ya TPDC hayatatoa jibu. Mikataba iwekwe wazi. Uwazi wa kila mtu kuona na sio Bodi ya TPDC tu. Uwazi ndio utakaoleta mabadiliko. Kwanini tukubali mapitio tu bila kuambiwa hiyo mikataba ina nini? After all wanaoambiwa wapitie ndio walioingia mikataba hiyo kwa upande mmoja na Waziri anasaini kwa upande mwingine.

Sekta ya Gesi na Mafuta haihitaji maneno matamu ya kuridhisha watu. The sector needs a radical approach ili kuepuka yaliyotokea kwenye sekta ya madini. Tunataka kutoka kuamini watu twende kwenye kuamini Taasisi. Tunataka kuhakikisha kuwa makosa yaliyofanywa kwenye sekta ya madini hayarudiwi tena. Sasa unaweza kuamua kukaa kimya na kusema Muhongo atafanya kwa niaba yangu au unaweza kuamua kushiriki kama raia kwa kusema 'ngoja kwanza, hivi hiyo mikataba inayoamriwa kupitiwa ipoje?"

Sidhani kama ni busara kufurahia mapitio wakati hata hatujui kinachopitiwa. Tulifanya makosa hayo huko nyuma kwenye Madini. Tunarudia tena kuamini kuwa mapitio ndio suluhisho la mikataba mibovu Tanzania. Mimi sipo tayari kurudia makosa yale. Ninapenda uwazi wa hii mikataba. Waziri aweke wazi mikataba hii maana hakuna sheria inayozuia. Vinginevyo ni siasa tu.
Mkuu Zitto, pamoja na nia yako nzuri, naamini wewe kwa capacity yako na position yako, umeshawahi kuiona hii mikataba, mikataba yote hii inacho kipengele cha usiri "expressly" not "impliedly"!, hilo unalijua, hivyo kusema hakuna sheria inayozuia nayo ni siasa kwa sababu unaelewa fika, mikataba hiyo haiwezi kuweka wazi unless imeamua kuivunja!.

Kitu ambacho wewe au nyinyi wabunge mnachoweza kufanya ni
  1. Kilitua bunge kuihoji serikali, kile kipengele cha "usiri" kwenye mikataba ya rasilimali za taifa, kinakuwepo kwa madhumini gani?.
  2. Mpitishe azimio la bunge kuwa mikataba yote inayohusu rasilimali za taifa, ipitishwe bungeni kuwa ratified na bunge, kama ilivyo mikataba ya kimataifa!.
  3. Mkataba ukishasainiwa unakuwa binding, ndio maana Barrick wakagomea kubadili mikataba yao iendane na sheria mpya, na ni kweli Prof. Muhongo hawezi kufanya lolote kwa mikataba iliyokwisha ingiwa, ila review itasaidia kubaini mapungufu hivyo kutofanya makosa kwenye mikataba ya future.
  4. Nyinyi kama wabunge, fanyeni 'Study Tour" to lern kwenye nchi za Afrika zanya mikataba bora kama Botswana na Namibia na sio kung'ang'ania "Shopping Tour" za ulaya tuu ili kurudi na yale ma jumbo suitcases tuu!.
  5. Concentration iwekwe kwenye kuwajengea uwezo Watanzania to learn how the game is played ili watu wetu wazalendo, waingie ndani ya game to play tofauti na ilivyo sasa Watanzania are only spectectors of the show ya "oil & gas", tena tusikubali kabisa wazawa kutumika kama chambo kama wanavyofanya Barick, kuwana post kubwa za kiutendaji for face value, huku waki wa bypass on the real game which is played deep underground!.

Bado niko na wewe kuhakikisha umri kwenye katiba mpya unapunguzwa, jina unalipekeka, mengineyo ni matokeo tuu!.

Pasco.
 
labda urudi nyuma kidogo na kukumbuka tulisema nini kuhusu Dowans na mitambo ile. Kununua mitambo haikuwa sahihi na inabakia kutokuwa sahihi. Kutaifisha lilikuwa ni jambo pekee sahihi kulifanya.
Bali Usahihi ni kuilipa Dowans Fidia kupitia uamuzi wa mahakama inayozidi mara dufu ya bei iliyohitajika kuinunua mitambo kabla ya kesi.Kuinunua ndiyo ilikuwa sahihi kuitaifisha ilikuwa ni janga jingine kubwa la Taifa labda kama ingefanyika wakati bado ni richmond.Kwa kuitafisha sinema ingekuwa kama ilipofikia Leo hii kwani wangekimbilia mahakamani na mngepigwa bakora tu kwani tayari tulishajiweka kitanzi ndani ya kitu kilichoitwa mkataba!
 
Mkuu GKassanga, ZZK ni level nyingine kabisa!. Humu jf, tuna Vichwa maji kibao ambao uelewa wao ni finyu sana, lakini kazi yao kubwa humu ni kupiga kelele za kupinga kila jema na kuvurumisha mitusi!.

ZZK aliposhauri tuinunue mitambo ya Dowans au tuitaifishe, alionekana kituko!, leo tutailipa tuzo ya ICC na capacity charge ya $ 152,000 per day tunalipa Simbion!.

Tuliibiwa madini kwa mikataba mibovu kwa sababu ya usiri huku sisi hatujui!, sasa ni mikataba ya gesi nayo tutaibiwa tena kwa sabuhi hizo hizo, ZZK anasisitiza uwazi, mikataba iletwe bungeni, watu mnalalamika nini?!.

Huyu ZZK akiwa mgombea wa Chadema 2015, lile boriti kubwa la tuhuma za Chadema ni chama cha dini fulani zitafutika na amini nawaambieni, ZZK ni very bright and briliant boy fit for URT president 2015 kwa tiketi ya Chadema!.

Pasco.

Its either ZZK or EL.......I hear you!!.....
 
Bali Usahihi ni kuilipa Dowans Fidia kupitia uamuzi wa mahakama inayozidi mara dufu ya bei iliyohitajika kuinunua mitambo kabla ya kesi.Kuinunua ndiyo ilikuwa sahihi kuitaifisha ilikuwa ni janga jingine kubwa la Taifa labda kama ingefanyika wakati bado ni richmond.Kwa kuitafisha sinema ingekuwa kama ilipofikia Leo hii kwani wangekimbilia mahakamani na mngepigwa bakora tu kwani tayari tulishajiweka kitanzi ndani ya kitu kilichoitwa mkataba!
Mkuu Kazi Ndio Kipimo cha Utu,
Mara baada ya Richmond kushindwa kazi na ku uhuisha huo mkataba kwa Dowans, tulipaswa tukatae, ili mkataba uvunjike kwa failure of performance, hivyo Richmond ange wind off na kunegotiate na sisi safe exist, akafungasha virago vyake na kusepa, kwa sababu mashine tulisharigharimia kwa kuzikodisha kwa bei kubwa kuliko hata kununua mpya!.

Trick ya kuuvunja mkata mbovu ni kumsokomeza kwenye kona, yule aliyeshindwa kutimiza wajibu wake na sio kumbeleza kama tulivyofanya!. Mkataba angevunja yeye na mitambo ingekuwa yetu!.
 
Zitto, Jasusi, Pasco,

.. naunga mkono hoja ya Zitto kwamba tunapaswa kusimamisha kwa muda utoaji leseni za utafutaji gesi na mafuta.

..tatizo ni kwamba Prof.Muhongo hakubaliani na ushauri huo, na amenukuliwa akimrushia kijembe Zitto Kabwe kwamba hana utaalamu na mambo anayoyazungumzia.

..ningependa kusikia kwanini Waziri hakubaliana na ushauri wa Zitto, ukizingatia kwamba waziri mwenyewe anakiri kwamba mikataba ya gesi iliyopo sasa hivi ina mibovu.
 
Last edited by a moderator:
Bali Usahihi ni kuilipa Dowans Fidia kupitia uamuzi wa mahakama inayozidi mara dufu ya bei iliyohitajika kuinunua mitambo kabla ya kesi.Kuinunua ndiyo ilikuwa sahihi kuitaifisha ilikuwa ni janga jingine kubwa la Taifa labda kama ingefanyika wakati bado ni richmond.Kwa kuitafisha sinema ingekuwa kama ilipofikia Leo hii kwani wangekimbilia mahakamani na mngepigwa bakora tu kwani tayari tulishajiweka kitanzi ndani ya kitu kilichoitwa mkataba!

Hapana.. kuinunua na hata sasa kulipa ni kosa kubwa kwa sababu ni morally wrong. Dowans haikutakiwa kabisa kuwa na mkataba wa Tanesco na Richmond. It is as simple as that. Ubaya wa yote haya ni kuwa haikuwahi kuhojiwa hata mara moja na Bunge au na watu wengine ilikuwaje Dowans wachukue mkataba wa Richmond na Tanesco, at least not on the ground ambayo niliandikia huko nyuma. Kumbuka kuwa kesi hii haikuwa inahoji suala la Dowans kuchukua mkataba wa Richmond kitu ambacho mimi nilikisemea nyuma.

Dowans haikurithi mkataba wa Richmond kihalali. Sasa kwenda kununua tena mashine zile kutoka kwa Dowans wakati tayari tulishalipia wakati zikiwa na Richmond ingekuwa ni ujinga wa hali ya juu. Hata hivi sasa wakilipia kama wanavyofanya tutakuwa tumelipa karibu shilingi bilioni 300 kwa majenereta ya bilioni 60! Kutaifisha siyo jambo geni na linafanyika mahali popote duniani kwa maslahi ya umma pale ambapo mashirika au taasisi zinakuwa zimefanya makosa dhidi ya umma - kitu ambacho naamini Dowans walikifanya. Wala lisingekuwa janga. Ikumbukwe tulikuwa hatutaifishi kitu kisicho chetu; tulikuwa tunataificha kitu ambacho kilichukuliwa pasi ya uhalali na kukirudisha mikononi mwa watu halali.
 
Mkuu Kazi Ndio Kipimo cha Utu,
Mara baada ya Richmond kushindwa kazi na ku uhuisha huo mkataba kwa Dowans, tulipaswa tukatae, ili mkataba uvunjike kwa failure of performance, hivyo Richmond ange wind off na kunegotiate na sisi safe exist, akafungasha virago vyake na kusepa, kwa sababu mashine tulisharigharimia kwa kuzikodisha kwa bei kubwa kuliko hata kununua mpya!.

Trick ya kuuvunja mkata mbovu ni kumsokomeza kwenye kona, yule aliyeshindwa kutimiza wajibu wake na sio kumbeleza kama tulivyofanya!. Mkataba angevunja yeye na mitambo ingekuwa yetu!.

uko karibu kiasi; mkataba ulitakiwa kuvunjwa na Tanesco kwa sababu Richmond aliurithisha kwa Dowans bila kuitaarifu Tanesco kama mkataba ulivyotakiwa. It was as simple as that.
 
Zitto,
Mimi nashindwa kukuelewa wewe. Waziri amewataka wajumbe wa bodi wapitie hiyo mikataba mipya halafu wampe maoni yao kama inafaa au la. Wakati huo huo profesa mwenyewe atakuwa anafanya mapitio yake aone ni wapi atatofautiana au kukubaliana na wajumbe wa bodi. What is wrong with that? Wewe kumwita waziri ni irresponsible inaonyesha kuwa wewe ni irresponsible au uko mfukoni mwa "wawekezaji" ambao inaonekana unataka kuwapendeza zaidi ya maslahi ya nchi. Mwache waziri afanye kazi yake. Waache wajumbe wa bodi wapitie tusikie maoni yao. Kwenye madini kama nijuavyo, hakukuwa na mapitio. Mikataba ilisainiwa ikiwa ni siri kati ya yule aliyesaini kwa niaba ya serikali na mwekezaji. Hilo wengine tunalipinga. Waziri Muhongo hajasema kuwa hataiweka wazi mikataba baada ya kupitiwa na wajumbe wa bodi. Inaonekana wewe ndiye uliyeshoot from the hip.
Jasusi,I love you bro!coz msimamo wako ni dhabiti na haujawahi kuyumba!you're the man!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kazi Ndio Kipimo cha Utu,
Mara baada ya Richmond kushindwa kazi na ku uhuisha huo mkataba kwa Dowans, tulipaswa tukatae, ili mkataba uvunjike kwa failure of performance, hivyo Richmond ange wind off na kunegotiate na sisi safe exist, akafungasha virago vyake na kusepa, kwa sababu mashine tulisharigharimia kwa kuzikodisha kwa bei kubwa kuliko hata kununua mpya!.

Trick ya kuuvunja mkata mbovu ni kumsokomeza kwenye kona, yule aliyeshindwa kutimiza wajibu wake na sio kumbeleza kama tulivyofanya!. Mkataba angevunja yeye na mitambo ingekuwa yetu!.
Pasco,

..tatizo ni kwamba Richmond ilikuwa kampuni ya wakubwa walioko serikalini.

..mimi naamini kabisa kuna watu wamefanya makusudi/hujuma ili serikali ishindwe ktk kesi ile.

..mawazo na ushauri wa Zitto yanaweza kuwa na mantiki ukizingatia ukweli huo hapo juu.

..tatizo ni kwamba Zitto hakuwa na ujasiri wa kusema kwamba anatoa ushauri ule kwasababu Richmond/Dowans ni mali ya wakubwa, na kwamba option ya kununua mitambo ya Richmond/Dowans ilikuwa ni kukubali nusu shari kuliko shari kamili.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom