Zitto: Contracts review is a publicity stunt and creation of unnecessary uncertainty in the sector

Mkuu GKassanga, ZZK ni level nyingine kabisa!. Humu jf, tuna Vichwa maji kibao ambao uelewa wao ni finyu sana, lakini kazi yao kubwa humu ni kupiga kelele za kupinga kila jema na kuvurumisha mitusi!.

ZZK aliposhauri tuinunue mitambo ya Dowans au tuitaifishe, alionekana kituko!, leo tutailipa tuzo ya ICC na capacity charge ya $ 152,000 per day tunalipa Simbion!.

Tuliibiwa madini kwa mikataba mibovu kwa sababu ya usiri huku sisi hatujui!, sasa ni mikataba ya gesi nayo tutaibiwa tena kwa sabuhi hizo hizo, ZZK anasisitiza uwazi, mikataba iletwe bungeni, watu mnalalamika nini?!.

Huyu ZZK akiwa mgombea wa Chadema 2015, lile boriti kubwa la tuhuma za Chadema ni chama cha dini fulani zitafutika na amini nawaambieni, ZZK ni very bright and briliant boy fit for URT president 2015 kwa tiketi ya Chadema!.

Pasco.

Mkuu auditor huwa anakagua contract zenye query tu au? Kwanini kakagua 4 tu kati ya 26 je hizo nne haikuwa kiini macho tu?

Mkuu, hakuna ubaya wa kureview mikataba ambayo imeshaingiwa ukizingatia kumefanyika mabadiliko kwenye hiyo wizara. Kwanza kutazama upya mikataba huleta imani kwa wawekezaji. Hajaifuta!

Mkuu, bungeni wanakoshindwa kutafsiri sheria ama kwa makusudi kabisa wanaipotosha kwa maslahi yao binafsi, give us a break

Kwa hili mkuu nashauri wewe na Zitto wenu msubiri mpaka Professor akwame ndo mtoe sauti zenu
 
Tatizo watz tunapenda vitu simple na vya fastafasta, ambacho ndicho anachofanya muhongo na ndio maana watz wanamshangilia kwa sababu anawakilisha. Lakini kwa Watu makini this guy is a disaster in the long run!
Dont generalise.
Nani hajui kuwa katika sekta ya Madini na Nishati wizi uliokithiri ni kupitia mikataba ambayo hata Bungeni haipelekwi, kwa kuwa ni "Siri".

Wakati wa Mwalimu, kulikuwepo na wizi wa mchana wa "Capacity Charges"?

Give Prof Muhongo credit where he deserves.

Kuna jamaa hapo juu amesema simplicity is the trick!
Magumu mnayoyaelewa ninyi hayafanyi kazi au kutatulika kirahisi!
 
Tatizo watz tunapenda vitu simple na vya fastafasta, ambacho ndicho anachofanya muhongo na ndio maana watz wanamshangilia kwa sababu anawakilisha. Lakini kwa Watu makini this guy is a disaster in the long run!
Lakini mkuu wangu kama nimemsoma vizuri Waziri yeye anazungumzia kazi yake mezani na atafanya nini wakati Zitto anazungumzia sera mbovu akimlaumu waziri ambaye amezungumzia utaratibu wa utekelezaji wa kazi chini ya uongozi wake. Maadam sera ya CCM ni mbovu hauwezi kumtazama waizri ambaye anajaribu kuifanya kazi yake kwa ufasaha baada ya kukuta madudu mengi mezani kwake..Nadhani kinachotakiwa kushambuliwa ni mfumo mzima wa mikataba na tender hizi ambazo ipo ndani ya shirika maana usafi huanza nyumbani.. Tunaharakisha hiyo mikataba ili iweje ikiwa sera zenyewe zinawapa miliki na mamlaka makubwa mashirika ya nje ikiwa ni pamoja na misamaha ya kodi kubwa mwisho wa siku hatufaidiki kwa lolote, why leave a stone unturned!

Bungeni tuna wabunge wangapi kiasi kwamba CCM wata shindwa kuendeleza mikataba ile ile mibovu, pengine semeni itaongeza list ya walaji tu maana kama bajeiti za wizara, wabunge wanavuta posho za vikao na hata kupigia kura itakuwaje tukianza kuingia hadi kwa wawekezaji?. Binafsi nadhani waziri huyu anaweza kuwa na mapungufu yake lakini sio ktk hili maana anafanya yale yalowashida waliomtangulia. Hivi kosa lake haswa ni lipi ambalo sisi wananchi hatujaliona na siku zote tumepiga kelele dhidi ya mfumo na sera za CCM kuhusu uwekezaji nchini, halafu leo bado tunataka kuharakisha maendeleo yaloshindikana chini ya sera zile zile..
 
Zitto on this occassion you're wrong also analysis you have presented are off point. you will be better to focus on social issues which your good at. Review is common practise arround the world and reassuring for long term investors hence no noticeable capital falls since the annoucement. Don't play politics here accept it and come with another idea instead of trying too hard to critize prof. Now you look idiotic
 
Tatizo watz tunapenda vitu simple na vya fastafasta, ambacho ndicho anachofanya muhongo na ndio maana watz wanamshangilia kwa sababu anawakilisha. Lakini kwa Watu makini this guy is a disaster in the long run!
Nani asiyekuwa disaster Tanzania, talking about long run which long run? hata geographically we live in a disaster prone area and soon we will all be wiped out by Mother nature, so let the man do his Job!

Damn, unawezaje kumshusha kiasi hicho mtu wa level kama ya Bw. Dr Muhongo? Watu kama nyinyi ndio mtakaoiangusha CHADEMA, kumbuka Watanzania wengi shida yao sio Chama bali ni mabadiliko na mtu yoyote ambaye atayaleta mabadiliko wataenda naye, sasa nyinyi mkikalia kupinga kila kitu kwa kuwa tu kinatoka kwenye Serikali hya CCM, mtakuja kushangaa!

Tatizo watz tunapenda vitu simple na vya fastafasta, ambacho ndicho anachofanya muhongo na ndio maana watz wanamshangilia kwa sababu anawakilisha. Lakini kwa Watu makini this guy is a disaster in the long run!

Atleast I should not believe if you mean what you say......Ukiniambia atashindwa kwasababu he cant do it on his own nita buy your idea lakini kusema alicho sema in a long run kita i-cost nchi kuliko ambavyo itai-cost if things are to be left the way they are; I beg your pardon!
 
Mkuu GKassanga, ZZK ni level nyingine kabisa!. Humu jf, tuna Vichwa maji kibao ambao uelewa wao ni finyu sana, lakini kazi yao kubwa humu ni kupiga kelele za kupinga kila jema na kuvurumisha mitusi!.

ZZK aliposhauri tuinunue mitambo ya Dowans au tuitaifishe, alionekana kituko!, leo tutailipa tuzo ya ICC na capacity charge ya $ 152,000 per day tunalipa Simbion!.

Tuliibiwa madini kwa mikataba mibovu kwa sababu ya usiri huku sisi hatujui!, sasa ni mikataba ya gesi nayo tutaibiwa tena kwa sabuhi hizo hizo, ZZK anasisitiza uwazi, mikataba iletwe bungeni, watu mnalalamika nini?!.

Huyu ZZK akiwa mgombea wa Chadema 2015, lile boriti kubwa la tuhuma za Chadema ni chama cha dini fulani zitafutika na amini nawaambieni, ZZK ni very bright and briliant boy fit for URT president 2015 kwa tiketi ya Chadema!.

Pasco.

Na mkimchaguwa Zitto kuwa mgombea wa Chadema 2015, nawarudishieni kadi yenu na kuhamia chama kingine. Anawezaje kumuita waziri anayejaribu kusafisha uozo "irresponsible?" Si ni huyu huyu Zitto aliyemtetea Mhando asiondolewe TANESCO? Ana maslahi gani na mafisadi? Tumeona uoza alioufuga Mhando TANESCO. Wamejaribu kumsafisha kwa kumpaka tope Waziri na katibu wake, zoezi ambalo naona Zitto anaendelea kulikomalia.
 
Anachosema Zitto ni suala la major policy differences. Waziri anatekeleza kitu ambacho kinaendana na sera za chama chake au kimepata baraka za chama chake. Kama CCM na serikali yake wanaona kuwa hili wanalofanya litawapa umaarufu mbele ya wananchi - hata kama halina matokeo yoyote ya msingi kiuchumi - ni haki yao na ni sehemu ya siasa. Juzi Benki Kuu ya Marekani imeamua kuwa itakuwa inaingiza karibu dola bilioni 40 kwa mwezi kwa kununua madeni mbalimbali ili kuendelea kusisimua uchumi. Na kweli Wall Street inaonekana imeitikia vizuri kwani soko hilo limepanda juu kwa karibu siku mbili mfululizo.

Hata hivyo baadhi ya watu wanaona kuwa ni mbinu ya kumsaidia Obama na matokeo yake Marekani imekuwa downgraded na mojawapo ya mashirika yanayopima hali ya uchumi wa nchi mbalimbali. Na sababu waliyotoa ni hiyo hiyo.

Binafsi siwalaumu CCM kufanya lolote wanalofanya ili kujijengea political clout na kujijenga tena. Kwa mfano, treni ile ya Stesheni -Ubongo itakapoanza kazi jijini Dar ndani ya mwezi mmoja na kitu hivi serikali itapata umaarufu na CCM watapongezana and rightly so. Juzi wamefungua chuo kikuu cha kijeshi kule Kigamboni na kwa haki watu wametoa sifa kwa serikali na CCM ina haki ya kupata ujiko. Na kwa kadiri tunavyoenda tunashuhudia serikali ikifanya mambo mbalimbali kwa msingi wa kutengeneza rekodi ambayo watarudi nayo kwa wananchi na kuwaambia "we did it".

CDM wasipoangalia watakosa cha kukosoa. Tutaanza kuona CDM wataanza kuipongeza serikali kwa kazi nzuri na kwa kadiri wanavyokosa vya kukosoa ndivyo hivyo hivyo wao wenyewe watajikuta wanapoteza ujiko. Wakati CDM haijaanza kuonesha uongozi wake (labda inasubiri madaraka ili ifanye hivyo) CCM inaendelea na mabadiliko ya ndani, inaanza kutengeneza palipobomoka na pole pole (bila kelele sana) inatafuta sifa mbele ya wananchi.Waziri Muhongo na mawaziri wengine walioingia (ambao ni makada wa CCM) wana jukumu moja tu - kurudisha heshima na sifa ya chama mbele ya wananchi.

Sioni katika maelezo ya Zitto wao kama CDM watafanya nini au kuna mkakati gani wa kibunge (parliamentary process) wa kubadilisha yanayofanywa na CCM. Je kuna tofauti gani ya substance kati ya hiki kinachofanywa na CCM na kile ambacho CDM wangeamua kufanya au watakuja kufanya wakishika madaraka? Au labda swali zuri zaidi ni je sera ya CDM ya mafuta na gesi inasema nini kulinganisha na haya yanayofanywa na CCM?

Binafsi ningeelewa vizuri kama CDM wanaitisha mkutano wao wa policy review na kuangalia mapungufu ya sekta ya mafuta na gesi na kwanini sera zilizopo na mechanisms zilizopo hazitasaidia sana na wao wenyewe sera yao ingekuwaje. So far ukosoaji wa Zitto kwa Muhongo ni more on academic level than anything. Probably rightly so.
 
ZZK aliposhauri tuinunue mitambo ya Dowans au tuitaifishe, alionekana kituko!, leo tutailipa tuzo ya ICC na capacity charge ya $ 152,000 per day tunalipa Simbion!.

labda urudi nyuma kidogo na kukumbuka tulisema nini kuhusu Dowans na mitambo ile. Kununua mitambo haikuwa sahihi na inabakia kutokuwa sahihi. Kutaifisha lilikuwa ni jambo pekee sahihi kulifanya.
 
Mzee Mwanakijiji,

Kwa uzoefu wangu mimi Watanzania wengi sio kama wanaichukua CCM ila wanawachukia watu walioiteka CCM hivi karibuni, na ninafikiri vyama vya Upinzani bado havijaweza kuwasoma Watanzania, tatizo ni kwamba siku zote wanataka kuwaaminisha Watz kwamba adui yao ni CCM, na kupinga chochote kile kinachofanywa au kusemwa na mtu yoyote au taasisi yoyote ile yenye uhusiano na CCM bila kupima.

Kwa mfano Watz tumekuwa tukiishi na mgao wa Umeme siku zote ghafla amekuja Waziri akatuambia hakuna tena mgao wa Umeme na ile migao ilikuwa feki na kweli tunaona mgao hakuna, siku zote tumekuwa tukiibiwa rasilimali zetu kwa sababu ya mikataba mibovu leo kaja Waziri amesimamisha utoaji leseni na kuamuru Mikataba yote mibovu ipitiwe upya sasa mtu leo hii anakuja kutuambia kwamba this man is a disaster sijui in long run nani anajali mambo ta long run?

Sisi tunataka huduma mtu anasema mwezi ujao tunaanzisha usafiri wa treni na kweli usafiri unaanza na watu wanaona treni inafanya majaribio mambo kama haya ndiyo Watz tumekuwa hatuyaoni kwa muda mrefu, sasa kama Wapinzani wao wanataka kupinga tu, nawashauri wawe waangalifu na kuisoma jamii ya Watz (what makes us tick!) vinginevyo hata hayo majimbo yao waliyonayo watayapoteza, wakumbuke ni rahisi sana kwa CCM kurudisha imani tena kwa wananchi (kama wakijipanga) kuliko CHADEMA kuweza kuwashawishi wananchi!
 
Last edited by a moderator:
Ni maoni yangu kwamba kupitia mikataba ya mafuta na Gesi ni suala la kisiasa tu na hakuna lolote ambalo litafanyika maana tumeshafanya mapitio sana na hakuna utekelezaji. A radical approach is needed in all matters about our resources, not piecemeal reviews which add no value.

Pili, mikataba hii yote inasainiwa na Waziri wa Nishati na Madini, TPDC na Kampuni ya utafutaji. Sioni mantiki yeyote ile kwa Waziri kuitaka TPDC kupitia mikataba hii. Ndio maana nashauri kwamba mikataba iwekwe wazi. Hakuna mapitio bora zaidi kama kuweka wazi mikataba hii. Uwazi ni mapitio tosha.

Ni maoni yangu kwamba Waziri wa Nishati na Madini ana mapungufu makubwa sana na ndio maana anajihami sana katika maamuzi yake. Hafikirii sawa sawa na wala haoni madhara ya anachosema. Siku sio nyingi mtathibitisha ninachosema. Matamshi mengi aliyoyasema Bungeni wakati wa mjadala wa hotuba ya Bajeti yake yalikuwa ni uwongo na ameshindwa kuthitibisha na kuishia kusema "mimi niliambiwa na Katibu Mkuu".
 
Tatizo watz tunapenda vitu simple na vya fastafasta, ambacho ndicho anachofanya muhongo na ndio maana watz wanamshangilia kwa sababu anawakilisha. Lakini kwa Watu makini this guy is a disaster in the long run!

It is very difficult to understand runs concept if not studied economics. Hello, Mkumbo, the long run you are talking about does not stand alone; it starts with, and actually is a summation of many short runs that generate into meso run before turning into a long run. Muhongo is right! Zitto is a poor small populist. Astonishing indeed, very recently, the same Zitto was quoted advocating for moratorium of gas exploration licensing!

Are you aware of extractive industries policy shift the Guinea government has recently clogged? The politics of oil, gas and minerals are quite distinct from the rest of FDIs. Policy generalisation may not work with these resources. The MNCs and TNCs employ the best experts on earth; know how to work with bogus governments (Equatorial Guinea) or smart governments (Botswana). So whichever status Tanzania Government decides to assume, extractors will always come and work!
 
... Benki Kuu ya Marekani imeamua kuwa itakuwa inaingiza karibu dola bilioni 40 kwa mwezi kwa kununua madeni mbalimbali ili kuendelea kusisimua uchumi. Na kweli Wall Street inaonekana imeitikia vizuri kwani soko hilo limepanda juu kwa karibu siku mbili mfululizo.

Hata hivyo baadhi ya watu wanaona kuwa ni mbinu ya kumsaidia Obama na matokeo yake Marekani imekuwa downgraded na mojawapo ya mashirika yanayopima hali ya uchumi wa nchi mbalimbali.
Benki Kuu ya Marekani, na Obama, na madeni ya Marekani na miitikio ya masoko ya Wallstreet yanatusaidia nini kuhusu siasa za Mbunge wa Kigoma na sera za Wizara ya madini ya Tanzania? Huwezi ukaitathmini Tanzania kutokea Ann Arbor, Michigan halafu ukawa coherent, ndio utajikuta unaongelea fiscal policy ya Marekani wakati wengine wanaongelea mikataba ya madini ya Tanzania. Nje ya mguso!
 
It is very difficult to understand runs concept if not studied economics. Hello, Mkumbo, the long run you are talking about does not stand alone; it starts with, and actually is a summation of many short runs that generate into meso run before turning into a long run. Muhongo is right! Zitto is a poor small populist. Astonishing indeed, very recently, the same Zitto was quoted advocating for moratorium of gas exploration licensing!

Are you aware of extractive industries policy shift the Guinea government has recently clogged? The politics of oil, gas and minerals are quite distinct from the rest of FDIs. Policy generalisation may not work with these resources. The MNCs and TNCs employ the best experts on earth; know how to work with bogus governments (Equatorial Guinea) or smart governments (Botswana). So whichever status Tanzania Government decides to assume, extractors will always come and work!

You look at DRC, they have been fighting for a generation now, but that hasn't stopped the big boys from bringing in more shavels! Joseph is happily playing with his toys and checking emails in Kinshasa while the digging continues!
 
.....

Huyu ZZK akiwa mgombea wa Chadema 2015, lile boriti kubwa la tuhuma za Chadema ni chama cha dini fulani zitafutika na amini nawaambieni, ZZK ni very bright and briliant boy fit for URT president 2015 kwa tiketi ya Chadema!.

Pasco.

Kwa nini unapenda kukuza tuhuma hizi za kukihusisha chama hiki na masuala ya kidini ?

Sitaki kuamini kuwa nawe unaweza kuwa kati ya wahandishi habari wanaotumika kuliingiza taifa katika machafuko ya kidini kupitia siasa, huku wanaotaka kuiba rasilimali zetu wakiwa tayari kuingia nchini.

Lakini mwenendo wako ukiendelea hivi sina budi kukuweka katika wahalifu wa kusababisha machafuko nchini.

Tafakari na uchukue hatua.
 
Benki Kuu ya Marekani, na Obama, na madeni ya Marekani na miitikio ya masoko ya Wallstreet yanatusaidia nini kuhusu siasa za Mbunge wa Kigoma na sera za Wizara ya madini ya Tanzania? Huwezi ukaitathmini Tanzania kutokea Ann Arbor, Michigan halafu ukawa coherent, ndio utajikuta unaongelea fiscal policy ya Marekani wakati wengine wanaongelea mikataba ya madini ya Tanzania. Nje ya mguso!

ndio tatizo la kufikiria kuwa Tanzania ni kakisiwa ambapo mambo yanayofanyika ndani yake hayana implication yoyote kutoka nje. NI fikra hizi zinawafanya wengine msiweze kuangalia nje ya Tanzania kujifunza. Bahati mbaya sana (labda pia ni nzuri) ulimwengu tunaoishi umefungamana sana kiasi kwamba mambo mbalimbali tunaweza kujifunza kutoka ndani na nje. Ni upeo mdogo kudhani kuwa kuangalia yanayofanywa nje ya Tanzania ili kujifunza ni kutoka nje.

Nina uhakika wa asilimia moja kutokana na mwitikio wako hapo juu nilichokuwa najaribu kukitolea mfano kwa kutumia Obama na Federal Reserve kitakuwa kimekupita kabisa pembeni.
 
Mzee Mwanakijiji,

Kimsingi sikubaliani na majumuisho ya jumla na dhanifu kuwa review hii ya mikataba inayotayarishwa na Prof Muhongo ni populist in nature.
Pamoja na mchango huu mzuri maudhui ya mchango wenyewe ni kwamba kwa vile pro active stance ya kurekebisha kasoro za mikatba hiyo inatoka kwenye serikali ya CCM, basi zoezi lenyewe ni naught.

Kuna watu waliojijengea mioyoni mwao kuwa na mtazamo hasi kwa kila kitu kinachofanywa na serikali ya CCM, hata kama ni kwa faida ya wananchi waliowengi.

Prof zmuhongo( na ndg Maswi) wamepigwa vita sana pale Wizara ya Nishati na Madini, vita ya wazi wazi na hata kisiasa kupitia Wabunge.

Siyo siri kuwa mikataba hii mibovu imetayarishwa na wanasiasa ambao baadhi wananufaika nayo hadi leo hii.

Ndiyo maana tulio wengi tunashangaa sana kuwa at last kapatikana mtu mwenye kuthubutu kuchambua the pandora box ya uchafu wa mikataba ya kifisadi, watu kama Zitto wanakuja juu.

Kwa msimamo huu, je CDM ni just an idler katika gurudumu la masahihisho ya mikataba hiyo?
Kulaumu tu from a safe distance?

Mimi nachelea kukubaliana na misimamo isiyo na misingi.
Tungependa vile vile Mzee Mwanakijiji kupata maoni yako ya kisera juu ya mikakati potofu na kifisadi kwa suala la Meya wa Moshi na safari ya masomo Kigali.

Zaidi ya maneno matupu sitegemei zaidi toka wenzetu wa CDM.
 
Last edited by a moderator:
Zitto said:
Ni maoni yangu kwamba kupitia mikataba ya mafuta na Gesi ni suala la kisiasa tu na hakuna lolote ambalo litafanyika maana tumeshafanya mapitio sana na hakuna utekelezaji.Matamshi mengi aliyoyasema Bungeni wakati wa mjadala wa hotuba ya Bajeti yake yalikuwa ni uwongo na ameshindwa kuthitibisha na kuishia kusema "mimi niliambiwa na Katibu Mkuu".

Kama majibu haya ya Zitto kusema ni siasa,basi naamini na yeye ameyasema kwa kutumia siasa.
Zitto said:
Ni maoni yangu kwamba Waziri wa Nishati na Madini ana mapungufu makubwa sana na ndio maana anajihami sana katika maamuzi yake. Hafikirii sawa sawa na wala haoni madhara ya anachosema

na kauli zake dhidi ya Muhongo zina dalili ya chuki maybe kwasababu alisema kuwa kapokea rushwa na kupelekea uchunguzi ufanyike?
Kijakazi said:
Kwa mfano Watz tumekuwa tukiishi na mgao wa Umeme siku zote ghafla amekuja Waziri akatuambia hakuna tena mgao wa Umeme na ile migao ilikuwa feki na kweli tunaona mgao hakuna
Kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu,karibia yote aliyoyasema Prof Muhongo yameonekana kuwa ya ukweli(mfano mpango wa Tanesco,ambapo mgawao sasa haupo),tunasubiri tu hizo tuhuma za rushwa uchunguzi wake ukamilike na kusiwe na hizo siasa dhidi ya Muhongo.
Zitto said:
Wiki iliyopita niliandika mawazo yangu haya kuhusu sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania. Bahati mbaya sana haikuwekwa hapa kwenye mjadala. Ni vema kuiweka maana masuala haya yanafanana.
Halafu ndugu Zitto anasema anshangaa kwanini hiyo article yake haikuletwa humu,anasema hivyo na wakati yeye ni member,haya bwana mkubwa.
Zitto said:
Sioni mantiki yeyote ile kwa Waziri kuitaka TPDC kupitia mikataba hii. Ndio maana nashauri kwamba mikataba iwekwe wazi. Hakuna mapitio bora zaidi kama kuweka wazi mikataba hii. Uwazi ni mapitio tosha.

Kuiweka wazi binafsi naamini haitasadia kwasababu bunge wengi ni wa ccm,na ikiwekwa wazi kitakachofanyika sana sana ni kwa wabunge baadhi ya wapinzani kuhongwa kama vilivyokuwa zile issue za Barrick na mambo bado yakabarikiwa na bunge la ccm wakishirikiana na baadhi ya mamluki wa upinzani.

Pasco said:
Mkuu GKassanga, ZZK ni level nyingine kabisa!. Humu jf, tuna Vichwa maji kibao ambao uelewa wao ni finyu sana, lakini kazi yao kubwa humu ni kupiga kelele za kupinga kila jema na kuvurumisha mitusi!.

Endapo mjadala huu utaendelea kwa muda,basi na mimi nitakuja kuchangia baada ya kuwasoma wote Zitto na Muhongo,nashindwa kufanya hivyo sasahivi kwasababu Zitto amesema yale ya Muhongo ni siasa,wakati wengi wetu hatujaona hivyo.Hilo limenifanya niamini kuwa yeye ndo ameleta siasa,kama kuna watu watajadiliana hapa si kwa kuwajadili Zitto na Muhongo,wala kuwatukana wana JF kwa hasira na kuwaita vichwa maji as if Muhongo ndo mwana JF!Tusijadili kitu kingine bali hoja zao,hapo nitarudi na kuweka mchango wangu zaidi(hoja kwa hoja),na hilo ni baada ya kuwasoma wote vyema,na kuanalyze articles zao.

Mjadala mwema.
 
masopakyindi,

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba inawezekana kuna wanasiasa au watu wenye mamlaka ya kisiasa au hata watu waliokuwa na mamlaka ya kisiasa ambao wanafaidika mfumo wa sasa katika sekta ya Mafuta na Gesi. Hoja yangu mimi ni kwamba Mapitio yaliyotangazwa na Waziri wa Nishati alipokuwa anazindua Bodi ya TPDC hayatatoa jibu. Mikataba iwekwe wazi. Uwazi wa kila mtu kuona na sio Bodi ya TPDC tu. Uwazi ndio utakaoleta mabadiliko. Kwanini tukubali mapitio tu bila kuambiwa hiyo mikataba ina nini? After all wanaoambiwa wapitie ndio walioingia mikataba hiyo kwa upande mmoja na Waziri anasaini kwa upande mwingine.

Sekta ya Gesi na Mafuta haihitaji maneno matamu ya kuridhisha watu. The sector needs a radical approach ili kuepuka yaliyotokea kwenye sekta ya madini. Tunataka kutoka kuamini watu twende kwenye kuamini Taasisi. Tunataka kuhakikisha kuwa makosa yaliyofanywa kwenye sekta ya madini hayarudiwi tena. Sasa unaweza kuamua kukaa kimya na kusema Muhongo atafanya kwa niaba yangu au unaweza kuamua kushiriki kama raia kwa kusema 'ngoja kwanza, hivi hiyo mikataba inayoamriwa kupitiwa ipoje?"

Sidhani kama ni busara kufurahia mapitio wakati hata hatujui kinachopitiwa. Tulifanya makosa hayo huko nyuma kwenye Madini. Tunarudia tena kuamini kuwa mapitio ndio suluhisho la mikataba mibovu Tanzania. Mimi sipo tayari kurudia makosa yale. Ninapenda uwazi wa hii mikataba. Waziri aweke wazi mikataba hii maana hakuna sheria inayozuia. Vinginevyo ni siasa tu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom