Zitto: CCM inachonganisha viongozi wa CHADEMA

Nathubutu kusema,tishio namba moja la ccm ni dr slaa,mwanachadema mwingine makini sana ni jj mnyika.
 
This is the peak of hypocritical-deception.

People are scheming for mass sympathy. They are playing a game of ''give a baby some candy so as to collect the knife in his hand''.

Baada ya kukusanya visu unafijiri nini kuitatokea baadaye na je ataweza kukusanya kwa wote?
 
Halafu hili la urais si alisema mwaka huu hatalizungumzia tena?
Kweli kasuku ni kasuku tu.

"Nitalipia ada wanafunzi wote waliofaulu kwenda kidato cha kwanza katika kata ya Kagera". Hili nalo alihitaji kujitangaza hadharani? Mbona hasemi hao wanafunzi wako wangapi?

Ada yenyewe sh. 20,000/-. tu.Mbona hata mimi nalipia wanafunzi 20 kila mwaka kule kijijini kwe

Halafu hayo mambo kama walishayamaliza ndani ya chama, kwa nini anayafufua tena?

Nimeamini huyu jamaa anapenda sifa za kijinga. Au ana lake jambo.

Ha ha haaa, mbona na wewe unajitangaza katika hadhara ya JF? Kweli Nyani haoni kundule, ila elewa kuwa, pamoja na chuki zote, vijana wengi waliipenda CDM kwa sababu ya ZZK na kwa sasa kwa sababu ya Dr. W. Silaa!. Punguzeni chuki na majungu!
 
Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe aliyeweka kambi jimboni kwake amesema Ccm inatumia kakikundi kadogo ndani ya chama kuwachonganisha.

Amesema pia kuwa anaweza asigombee nafasi yoyote ndani ya chama lakini atabaki kuwa mwaminifu sana kwa chama chake.

Amesema ameweka kambi jimboni kuwadhibiti Ccm wasiwapotoshe wapiga kura wake.

Pia ameawataka viongozi wa chama jimboni mwake kutomtegemea yeye peke yake kujenga chama.

SOURCE: Tanzania Daima ingawa RFA walmelichakachua katika kulisoma.
 
Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe aliyeweka kambi jimboni kwake amesema Ccm ianutumia kakikundi kadogo ndani ya chama kuwachonganisha.

Amesema pia kuwa anaweza asigombee nafasi yoyote ndani ya chama lakini atabaki kuwa mwanifu sana kwa chama chake.

Amesema ameweka kambi jimbo kuwadhibiti Ccm wasiwapotoshe wapiga kura wake.

Pia ameawataka viongozi wa chama jimboni mwake kutomtegemea yeye peke yake kujenga chama.

SOURCE: Tanzania Daima ingawa RFA walmelichakachua katika kulisoma.

Ni wazi kwamba CCM wana maslahi katika sintofahamu zinazoendelea ndani ya CDM; Adui yako muombee njaa au sio?! Jambo la msingi ni kuhakikisha wana CDM hususani viongozi wa kutegemewa kama ZZK wasifanye jambo lolote linalowapa mwanya CCM kujipenyeza na kukoleza misuguano ndani ya CDM.

CCM ni kama mafisi walamizoga wanavizia mkono udondoke waudake wakimbie nao!! msiwape nafasi hata finyu kiasi gani; huu ni kama mchezo wa mpira; One mistake one goal; they will always try to capitalize on CDM's own mistakes.
 
Ben Saanane,

Ulikuja jukwaani ukamshutumu ZZK kuwa alikuwa kiongozi wa kundi la wasaliti wa CDM ambalo wewe mwenyewe ulikuwa mshiriki. Ukaliambia jukwaa la JF kuwa una ushahidi wa mambo yote uliyokuwa umeyasema juu shutuma ulizotoa.

Mwenyekiti wa BAVICHA katika taarifa yake kwa ya vyombo vya habari baada ya kikao kilicho fukuza "masalia" alise wewe Ben Saanane umesamehewa kwa sababu umekiri makosa na umeomba msamaha kwa kumchafua kiongozi mwandamizi wa CDM (hakutajwa jina ila kila anaefuatilia JF anamjua ni nani, walisoma post zako). Siku ya pili ukaja ukapinga hapa JF kwa kutaja jina kuwa hujawahi wala hutawahi kumuomba msamaha ZZK kwa sabab huna kosa lolote ulimfanyia ZZK, jambo linaloonesha kimisingia ni kweli ulikuwa na ushahidia wa kutosha katika shutuma zako kwa ZZK.

Yaliyojiri juzi yamejiri na wana JF wameyasikia, kila mmoja moyoni anajiuliza hivi hili suala la ZZK na ushahidi wa Ben Saanane ulipolekwa CDM limeishia vipi? Inawezeka kukawa na ushahidi wa uhakika(kiasi cha kupingana na mwenyekiti wako wa BAVICHA juu ya wewe kuomba msamaha) wa sauti na video wa ndugu ZZK akisaliti chama halafu CDM wakamuacha hivi hivi tu?

Hebu tufanunulie au nifafanulie hili jambo limekuaje ndugu Saanane!

Je, hivi ni kweli ulipeleka ushahidi wako wa uhakika ndani ya chama?
Je, CDM kimetupilia mbali au kudharau ushahidi wako?
Je, kuna mchakato wowote unaendelea ndani ya chama kuhusu shutuma zako hizi kubwa kubwa kwa ndugu ZZK?
Je, bado uko katika msimamo ule ule kuwa ZZK ni msaliti na alikuwa kiongozi wako katika usaliti?
Je, kwa nini usiuweke ushahidi hapa JF kama ulivyo weka shutuma hasa ukizingatia kuwa chama hakija chukua hata hatua ya kumjadili mtuhumiwa ZZK?
Je, wewe kama mwana CDM unaemini katika mabadiliko ya kweli unalionaje hili suala ya ndugu ZZK kubaki ndani ya CDM ilihali wewe una ushahidi usio na mashaka kuwa anakisaliti chama?

Ben,
Ulikuja hapa JF ukayaanzisha na ukatueleza haya mambo, hebu yamalize basi. La sivyo picha inageuka, tena inageuka sana. Wewe unakuwa ndio msaliti(tena usaliti wa aina mbaya kabisa) na ZZK anachukua ushujaa na pongezi zote wana JF walizokupa hapa jukwaani.

Zitto,
Ndugu naomba nikuulize swali. Kama yote aliyosema Ben Saanane juu yako si ya kweli na amekusingizia shutuma zote, na msingi wa kusamehewa kwake BAVICHA ni kuomba msamaha kwa makosa yake yote ikiwemo kukushutumu wewe, na ndugu Saanane amepinga hapa JF kuwa hajawahi kuomba wala hatawahi kukuomba msamaha juu ya suala la kukushutumu kuwa kiongozi wa masalia, mbona huyu kijana hajachukuliwa hatua yoyote na chama? mbona vijana wenzake walio toa shutuma dhidi ya viongozi wengine wamechukuliwa hatua na chama?

Hebu tufafanulieni hili jambo, mmoja kati yenu hatakiwi aendelee kuwepo CMD, ila nyote bado mpo CDM!! Kuna jambo haliko sawa hapo.

Huu ufa tuuzibe leo, kabla hujamuangukia mtu halafu ukatulazimu tujenge ukuta.
 
kimya cha Ben ni cha busara zaidi,.tusahau ya nyuma and let's move on,amekata matawi na mzizi umebaki wenyewe tu,hauna madhara
 
kwa Zitto kilichopo CDM ni kutofautiana mtazamo kwa wengine huo ugomvi!
 
Yawezekana ikawa kweli...ila ZITTO ana matatizo binafsi ambayo CCM wana take advantage...japo siamini kama ni msaliti ndani ya chama........
Humjui ZITTO wewe?huyu dogo ameshanunuliwa muda mrefu sana,ni ndumila kuwili,kuna watu wanamtumia huyu.
 
mimi namtakia Zitto afya njema, na aendelee kukijenga chama kama anavyosema! Wanachadema tunampenda Zitto Kabwe sana labda ndo maana tunaumia sana kwa maneno tunayoyasikia!
 
This is the peak of hypocritical-deception.

People are scheming for mass sympathy. They are playing a game of ''give a baby some candy so as to collect the knife in his hand''.

Thank you God!

Chama kimeyashinda Mauti!

In Chadema we trust.
 
Ni faraja kuwa umeona ukweli na kuwatambua wabaya wa CHADEMA. Mpende adui, na ukimjua dui wako huwa hakusumbui. Ni vema umeuambia umma kuwa hakuna mgogoro CHADEMA bali ni hali ya demokrasia, maana watu walikuwa wanakuelewa vibaya. Kweli umekomaa! Bravo!!!!!!!!!!!!!
 
Ben Saanane,

Ulikuja jukwaani ukamshutumu ZZK kuwa alikuwa kiongozi wa kundi la wasaliti wa CDM ambalo wewe mwenyewe ulikuwa mshiriki. Ukaliambia jukwaa la JF kuwa una ushahidi wa mambo yote uliyokuwa umeyasema juu shutuma ulizotoa.

Mwenyekiti wa BAVICHA katika taarifa yake kwa ya vyombo vya habari baada ya kikao kilicho fukuza "masalia" alise wewe Ben Saanane umesamehewa kwa sababu umekiri makosa na umeomba msamaha kwa kumchafua kiongozi mwandamizi wa CDM (hakutajwa jina ila kila anaefuatilia JF anamjua ni nani, walisoma post zako). Siku ya pili ukaja ukapinga hapa JF kwa kutaja jina kuwa hujawahi wala hutawahi kumuomba msamaha ZZK kwa sabab huna kosa lolote ulimfanyia ZZK, jambo linaloonesha kimisingia ni kweli ulikuwa na ushahidia wa kutosha katika shutuma zako kwa ZZK.

Yaliyojiri juzi yamejiri na wana JF wameyasikia, kila mmoja moyoni anajiuliza hivi hili suala la ZZK na ushahidi wa Ben Saanane ulipolekwa CDM limeishia vipi? Inawezeka kukawa na ushahidi wa uhakika(kiasi cha kupingana na mwenyekiti wako wa BAVICHA juu ya wewe kuomba msamaha) wa sauti na video wa ndugu ZZK akisaliti chama halafu CDM wakamuacha hivi hivi tu?

Hebu tufanunulie au nifafanulie hili jambo limekuaje ndugu Saanane!

Je, hivi ni kweli ulipeleka ushahidi wako wa uhakika ndani ya chama?
Je, CDM kimetupilia mbali au kudharau ushahidi wako?
Je, kuna mchakato wowote unaendelea ndani ya chama kuhusu shutuma zako hizi kubwa kubwa kwa ndugu ZZK?
Je, bado uko katika msimamo ule ule kuwa ZZK ni msaliti na alikuwa kiongozi wako katika usaliti?
Je, kwa nini usiuweke ushahidi hapa JF kama ulivyo weka shutuma hasa ukizingatia kuwa chama hakija chukua hata hatua ya kumjadili mtuhumiwa ZZK?
Je, wewe kama mwana CDM unaemini katika mabadiliko ya kweli unalionaje hili suala ya ndugu ZZK kubaki ndani ya CDM ilihali wewe una ushahidi usio na mashaka kuwa anakisaliti chama?

Ben,
Ulikuja hapa JF ukayaanzisha na ukatueleza haya mambo, hebu yamalize basi. La sivyo picha inageuka, tena inageuka sana. Wewe unakuwa ndio msaliti(tena usaliti wa aina mbaya kabisa) na ZZK anachukua ushujaa na pongezi zote wana JF walizokupa hapa jukwaani.

Zitto,
Ndugu naomba nikuulize swali. Kama yote aliyosema Ben Saanane juu yako si ya kweli na amekusingizia shutuma zote, na msingi wa kusamehewa kwake BAVICHA ni kuomba msamaha kwa makosa yake yote ikiwemo kukushutumu wewe, na ndugu Saanane amepinga hapa JF kuwa hajawahi kuomba wala hatawahi kukuomba msamaha juu ya suala la kukushutumu kuwa kiongozi wa masalia, mbona huyu kijana hajachukuliwa hatua yoyote na chama? mbona vijana wenzake walio toa shutuma dhidi ya viongozi wengine wamechukuliwa hatua na chama?

Hebu tufafanulieni hili jambo, mmoja kati yenu hatakiwi aendelee kuwepo CMD, ila nyote bado mpo CDM!! Kuna jambo haliko sawa hapo.

Huu ufa tuuzibe leo, kabla hujamuangukia mtu halafu ukatulazimu tujenge ukuta.

Unaharaka ya wapi ndugu?

Unadhani Chadema huwa kinakurupuka tu kufanya maamuzi ya siasa zake makini zenye mafaa kwa taifa?

CCM hawana jipya tena! Tumewakamata juu na chini!
 
Mkuu naona kama alisingiziwa kwa kuwa kama hakusingiziwa na alikuwa kinara wa masalia kwa nini wasimjadili na kumfuta? Iweje wafuasi wafutwe wakati kinara na mfadhili wao bado anaendelea kuwepo chamani? Naona kama Zitto alikuwa anasingiziwa tu na hao akina Mr 8 O'clock kwani waliothibitishwa na Chama kuwa wasaliti wamepata haki yao.

Niliwahi kuzungumza na kafulila wakati fulani akanieleza matatizo mengi sana ya chadema na hizi timua timua zake na ugawaji wa wanachama ndani ya chadema toka ule wa marehemu chacha wangwe ambapo wao kina kafulila,zitto,halima mdee,marehemu rejia na wengine alikiri walikua wanatumiwa na mbowe kumshughulikia marehemu "rasta" a.k.a. chacha ambae mbowe alimuona tishio kwake na kundi lake kutokana na misimamo isiyoyumba,akaenda mbali kwa kunieleza hata ilipofika zamu ya zitto kushughulikiwa kutoka na kutofautiana na mbowe kuhusu nafasi ya uenyekiti pia kuna watu akiwamo mbunge wa ubungo wa sasa,mbunge wa kawe wa sasa na wengine walitumiwa na mwenyekiti kwa kutumia mbinu zilezile walizokua wakizitumia kwa chacha,lakini zitto akiwa ujerumani siku moja alimpigia simu kafulila na kumuambia kwamba anaonelea aliondoe jina lake kwenye kugombea nafasi ya uenyekiti,kafulila alimuasa sana kwamba akifanya hivyo basi kwa jinsi anavyomjua mbowe wao wote kina kafulila waliokua mstari wa mbele kumuunga mkono yeye zitto ndio watakaotolewa kafara kwa kuwa hawana muscles za kutosha kama yeye!
 
Ni faraja kuwa umeona ukweli na kuwatambua wabaya wa CDM. Mpende adui, na ukimjua dui wako huwa hakusumbui. Ni vema umeuambia umma kuwa hakuna mgogoro CDM bali ni hali ya demokrasia, maana watu walikuwa wanakuelewa vibaya. Kweli umekomaa! Bravo!!!!!!!!!!!!!
Hii nadhani ungemtumia PM tu au ungemfuata kule facebook.
 
Unaharaka ya wapi ndugu?

Unadhani Chadema huwa kinakurupuka tu kufanya maamuzi ya siasa zake makini zenye mafaa kwa taifa?

CCM hawana jipya tena! Tumewakamata juu na chini!

Hapa wewe ndio umekurupuka,maana huyo bwana ana maswali ya ,msingi sana,kati ya ben na zitto kuna mmoja nimtu hatari sana kuendelea kuachwa akitamba ndani ya chadema,acha watupatie ufafanuzi zaidi nani ni mtu hatari kati yao na kwanini zitto anaonekana kama ni untouchable ndani ya cdm,aliwaponza kina kafulila yeye akaendelea kupeta leo hawa kina shonza sijui yeye bado yumo ,kuna nini hapa,je zitto ni mkubwa kuliko chadema au?
 
Back
Top Bottom