Zitto awatikisa Chadema .................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,463
911,172
Zitto awatikisa Chadema
Sunday, 12 December 2010 21:38

Boniface Meena
KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imeunda jopo la wazee wa chama hicho, litakalosikiliza maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, kuhusu mgogoro kati yake na viongozi wenzake ndani ya chama.Imeelezwa kuwa kamati hiyo pia imemtambua rasmi Rais Jakaya Kikwete kuwa ni kiongozi halali na imewaagiza wabunge wa chama hicho, kushiriki katika shughuli zote za kitaifa.

Jopo hilo la wazee hao wa Chadema, litaongozwa na Profesa, Mwesiga Baregu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kupitia tiketi ya Chadema, amekuwa katika mvutano na viongozi wenzake ndani ya Chadema, tangu alipopinga hatua ya wabunge wa chama hicho, kususia hotuba ya Rais Kikwete wakati wa ufunguzi wa Bunge la Kumi, uliofanyika mwezi uliopita mijini Dodoma mwaka huu.

Akizungumzia kukutana na Zitto, Profesa Baregu alisema wameamua kufanya hivyo kwa kuwa Zitto ni kiongozi wa chama na anahitaji kusikilizwa.

Alisema jopo hilo alikataloliongoza yeye, linawashirikisha pia mzee Nyangaki Shilungushela, Dk Kitila Mkumbo na Shida Salum ambaye ni mama yake Zitto.

"Tunazungumza ndani ya chama, ili kujenga maelewano na kuweka mambo sawa,"alisema Baregu.

Alipoulizwa kuhusu msimamo wa kamati kuu kumtambua Rais Kikwete, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa hakutaka kuzungumzia hilo na badala yake, alitaka lisubiriwe tamko rasmi la chama litakalotolewa kesho.

"Nani kasema hivyo, ni vizuri kwa gazeti makini kama Mwananchi mkasubiri taarifa kamili, itatolewa,"alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema ni vizuri kusubiriwa tamko hilo ambalo alisema litatolewa katika mkutano wa waandishi wa habari.

"Sipendi muandike taarifa zisizo rasmi ningependa usubiri hadi keshokutwa (kesho). Kutakuwa na 'press conference (mkutano wa waandishi wa habari)," alisema Dk Slaa ambaye katika uchaguzi mkuu uliopita, alikuwa mpinzani wa karibu wa Rais Kikwete.

Juzi, Kamati ya Wabunge wa Chadema, ilimvua Zitto wadhifa wake wa unaibu kiongozi wa upinzani bungeni, lakini chama hicho 'kikapigwa jeki' baada ya mfanyabiashara maarufu, Mustafa Sabodo kukipa Sh150 milioni kwa ajili ya kujenga chuo cha maadili ya uongozi.

Matukio hayo mawili pia yaliambatana na kuugua ghafla kwa Zitto na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Said Amur Arfi, ambao walilazwa katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam, kwa matatizo tofauti.

Katika siku hiyo Zitto, alipigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, hatua iliyofanywa na wabunge wa chama hicho katika mkutano wao uliofanyika mjini Bagamoyo, Pwani.

Wabunge hao pia walimtaka Zitto ajieleze kufuatia kitendo chake cha kupinga uamuzi wa pamoja wa kususia hotuba ya Rais Kikwete.

Uamuzi wa wabunge hao kumvua uongozi, ulikuwa ukitarajiwa na wengi baada ya Zitto kupinga hadharani kitendo cha wenzake, kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati Rais, alipoanza kuhutubia.

Hatua hiyo ilikuwa na lengo la wabunge hao kuonyesha kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais,kushinikiza kuandikwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi.

Uamuzi wa wabunge hao kususia hotuba ya Rais Kikwete, ulifikiwa baada ya mjadala mrefu uliokwisha kwa kupiga kura.

Zitto na wenzake tisa hawakuingia ndani ya ukumbi wa Bunge siku Rais, alipolihutubia. Baadaye, aliitisha mkutano na waandishi wa habari kueleza kupinga kitendo cha wenzake.

Baada ya Zitto na wenzake kutoingia kwenye ukumbi wa Bunge ili watekeleze uamuzi wa kutoka nje wakati Rais Kikwete akianza kuhutubia, Katibu Mkuu wa Chadema (Slaa), alisema waliosusia uamuzi huo, wangechukuliwa hatua na Kamati ya Wabunge wa Chadema.

Baadaye Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu, alitangaza kumwandikia barua Zitto na wabunge wengine tisa ambao hawakuingia kwenye ukumbi wa Bunge, kuwataka wajieleze kwa maelezo kuwa walichofanya ni utovu wa nidhamu.

Wakati taarifa hizo za kuvuliwa uongozi wa Zitto zikibainika, mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini alilkuwa ametoka katika Hospitali ya Aga Khan, alikokuwa amelazwa kwa ugonjwa wa tumbo.

Jana gazeti la Mwananchi lilichapisha habari zilizomkariri Zitto, akidai kuwa ugonjwa huo ulitokana na kula chakula chenye sumu.

Taarifa zilisema Zitto alilazwa katika wodi namba 57 iliyoko katika ghorofa ya tatu na alikuwa amechukuliwa vipimo vyote ili kutihibitisha kiini cha ugonjwa wake.

Hata hivyo madaktari katika hospitali hiyo, walisema hawakuona tatizo na kwamba wanasubiri kipimo kikubwa.

Akizungumza na gazeti hili akiwa hospitalini, Zitto aliwataka Watanzania kutokuwa na hofu na kuugua kwake kwa kuwa ni ugonjwa wa kawaida na kuwasihi wamuombee apone haraka.

"Watanzania wasiwe na wasiwasi na kuugua kwangu. Hii ni kawaida tu, madaktari wananipa matibabu niombeeni nipone haraka," alisema Zitto.

Kuhusu hatua ya chama hicho kumvua madaraka, Zitto , alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu hajapata taarifa rasmi kutoka chama chake mbali na kusoma kupitia katika vyombo vya habari.

Alisema hata hivyo, hakuwahi kuomba kupewa wadhifa huo na kwamba ikiwa watu waliomwona anafaa kufanya kazi na kumpa wadhifa huo, wakiamua kumnyang’anya siyo tatizo kubwa kwake.

“Kwa sasa nadhani suala la afya yangu ndiyo muhimu zaidi. Ngoja kwanza nitoke hapa na afya yangu iimarike na kama kutakuwa kuna sababu ya mimi kuzungumza, nitazungumza,” alisema Zitto:

“Lakini ikumbukwe kuwa mimi sikuwahi kuomba wadhifa huu, kwa hiyo kama watu walionipa wameamua kunibadilishia, mimi sidhani kama kuna tatizo.”

Alipoulizwa kuhusu madai ya Zitto kuvuliwa wadhifa ndani ya Bunge, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe,alisema chama kitatoa taarifa baadaye.
 
"Lakini ikumbukwe kuwa mimi sikuwahi kuomba wadhifa huu, kwa hiyo kama watu walionipa wameamua kunibadilishia, mimi sidhani kama kuna tatizo."

Kama ni kweli Zitto aliyazungumza haya sasa iwaje idaiwe ................aitikisa Chadema................................something is missing in this reportage.............
 
Hili lichama limeanza kuwa na mambo ya kipuuzi...nod maana sipendi kupiga Kura kwa ajili ya maujinga Kama haya
 
Heading yako haijakaa vizuri, chama kukaa na kujadili viongozi na wanachama wake siyo jambo la ajabu, na kama ni kweli wamemvua uongozi na yeye anasema amekubali kwa kuwa ndiyo waliyompa hayo madaraka sa inakuwaje awatikise Chadema.

hata hao jamaa wa CCM kuna wakati wanakaa na kujadili viongozi na wanachama wao mbona hamsemi wanaitikisa CCM. hujawahi kusikia kamati ya Mwinyi, Msekwa na Kinana kuwajadili kina Lowasa, Sita na wengine?

Kawaida Kamati na uongozi wa juu popote pale unauwezo wa kumwajibisha kiongozi au mwanachama wowote, tushashuhudia ANC ya Afrika kusini ikimuamuru Tabo Mbeki ajiuzulu uraisi wa nchi.

Zito siyo chadema na Chadema siyo Zito hata akiondoka leo hii Chadema itaendelea kuwepo tu na 2015 Chadema inachukuwa nchi na kuleta mapinduzi mapya na halisi ambayo yataleta tija mpaka kwa mwanachi mmojammoja
 
Heading yako haijakaa vizuri, chama kukaa na kujadili viongozi na wanachama wake siyo jambo la ajabu, na kama ni kweli wamemvua uongozi na yeye anasema amekubali kwa kuwa ndiyo waliyompa hayo madaraka sa inakuwaje awatikise Chadema.

yaelekea hujanielewa.....hiyo heading hata mimi ninaikosoa.........ni ya Mwananchi...........
 
Zito siyo chadema na Chadema siyo Zito hata akiondoka leo hii Chadema itaendelea kuwepo tu na 2015 Chadema inachukuwa nchi na kuleta mapinduzi mapya na halisi ambayo yataleta tija mpaka kwa mwanachi mmojammoja

Kwenye hili tupo sote.......................
 
Back
Top Bottom