Zitto awatake radhi watanzania kwa kuwapotosha kuhusu posho za wabunge huku akijua posho ni kwa watu

Wastaarabu, posho inayosemwa hapa ni posho ya kuhudhuria kikao SIO posho ya kujikimu kwa kuwa nje ya kituo cha kazi, uwe unafuatia kwa makini mada.

was
 
Kwahio na walimu nao wal;ipwe posho kwa kwenda kuandaa maandalio na kusahihisha daftari na mitihani ya wanafunzi nyumbani? Pumbafu kabisa nadhaniwewe una hamu ya kuharibiwa siku asubuhi asubuhi, ngoja waje wenyewe sasaa

nimeipenda hii
 
Kwa hiyo hawapokei?..... mshaanza siasa zenu na nyie.

Mbunge au diwani yeyote anaechukua posho, ujue haipingi.

We wacha upuuzi.

Uliza iyo hela wanaingiziwaje co mambo unayotaka kuyaleta humu.
 
Acha uongo wewe.

Kwanza unachanganya vitu viwili hapa sitting allowance unaiita per diem, huo ni upotoshaji mkubwa sana. Labda tusaidiane, sitting allawance ni posho ya vikao na per diem ni posho ya kujikimu ambayo kiwango cha juu kwa watumishi wa umma wakiwemo wabunge ni 80,000/=. Hiyo posho ya vikao mtu analipwa kama anahudhuria kikao halafu hiyo ni kwa watu wazito na sio walimu, madaktrati au watumishi wengine kama unavyopotosha.

Kwa kawaida mtumishi akisafiri analipwa posho ya kujikimu tu ambayo inaanzia sh. 35,000 hadi 80,000 kutegemea cheo na mahali anapokwenda. kwa mfano, mtu kama anasafiri kuja Dar na mwingine anakwenda Rukwa, wa Dar analipwa zaidi kwa sababu ya gharama ya maisha Dar. Ikumbukwe kwamba fedha hizo ni kwa ajili ya chakula, malazi na matumizi mengine.

KWA HIYO TUSIPOTOSHE WATU KWAMBA KUNA 200,000 WANALIPWA WALIMU, MADAKTARI. HOJA YA ZITTO INAENDELEA KUSIMAMA KAMA UKOSOAJI WA KIONGOZI MWENYE UCHUNGU NA WATU WA CHINI

Nakuunga mkono mkuu! Mwalimu,polisi au daktari akipewa 200000 ujue ni mshahara!
 
Pole sana wewe pandikizi au Mbunge njaa, hivi kwa akili yako unadhani ugumu wa maisha kuweza kuongeza posho kwa asilimia zaidi ya miamoja uko kwa wabunge tu? Hamkukumbuka walimu, wafanyakazi wenye kima cha chini cha mshahara kuongeza kuwa laki tatu tu mmeona haifai, yaani nyinyi ni sawa na mafisi tu, mbunge au mtu yeyote atakayetetea hili ni sawa na fisi!!
 
Watanzania watanzania wenzangu, nashauri tuache jazba katika mambo ambayo hatuna fact nayo, twende tukafanye tafiti kisha turejee, hii ni kwa sababu wengi wetu huwa tunakuwa mabingwa wa kusema tu hata kama hatuna ushahidi,ninaamini kuwa ktk hili la posho wengi wetu hatuna ushahidi wa kutosha kuwa kila mtumishi anastahili kulipwa shilingi ngapi akisafiri kikazi, aidha si kweli kwamba mbunge anapokuwa dododma hastahili kulipwa malipo ya kujikimu, hakika na kama sis ni wa kweli ni lazima tukubaliane na mchokoza mada kuwa kituo cha kazi cha mbunge ni jimboni kwake dodoma ni extended working area na kwa hiyo anapokuwa dodoma ndiyo maana hulipwa posho zinazoonekana kulalamikiwa na badhi ya watu ilhali akiwa jimboni kwake halipwi posho bali mshahara tu. Kwa hiyo tusijivishe upofu ktk hili, lkabda tuangalie uhalali wa kiasi na maisha halisi ya mtanzania, nikubalane na wale waliosema kuwa ongezeko la ukali wa maisha na gharama zake si kwa wabunge pekee ni pamoja na watanzania wengine. tuliangalie hilo na namna ya kusolve matatizo wa wa tz. Kwa ujmla tusidanganyane kuwa mbunge mwenye njaa yaani asiyelipwa vizuri kuwa naweza kufanya kazi yake vizuri,itatokea mara chache sana na tena ni wachache sana wataofanya kazi hiyo,leo tunasema kuwa wafanyakazi wanalalamika kuwa hawafanyi kazi vizuri kutokana na maslahi yao kuwa duni. Ni kwa nini tusifikirie kuwa hata wabunge wakiwa na maslahi duni watashindwa kufanya kazi zao vizuri? Haki iwe ni kwa watu wote, nia wasiwasi na watanzania wengi kuhusu suala la kufikiri sawasawa, wengi mnapelekwa na kuishi kwa hisia hamfanyi tafiti za uhakika ili kujua ukweli wa mambo na nndiyo maana unakuta mtu anaandika upuuzi hapa JF badala ya kujadili mada kwa kutoa hoja madhubuti. Hivi kweli unataka mbunge wa Hai atoke jimboni kwake na kuja dodoma au Dar au kokote kwenye kamati za bunge halafu asiwezeshwe namna ya kuishi na ategemee mshahara wake na halafu afanye kazi yake sawasawa? huku wafanyakazi wengine wakidai kuwa mishahara ni kidogo, imeelezwa na SPIKA makinda kuwa MSHAHARA wa mbunge ni sh 2,400,000/=,unakatwa kodi shilingi 700,000/= kwa mwezi bado makato mengine ambapo ameeda mbali makinda kuwa kuna mikopoya magari, mbunge anjikuta amebaki na kama shilingi 1,000,000/=, huo ndiyo mshahara wake anaobaki nao kwa mwezi, sasa apate chakula na matumizi mengine ya kibinadamu,wakati huohuo unamtaka atumie msahara huo kujigharamia akiwa dodoma,dsm, au kwingineko kwa mshahara huo, inawezekanaje. Labda mnifafanulie waungwana, Hapa cha msingi tuangalie uwiano wa posho za wabunge na hali halisi za watanzania eitha kwa kuzipunguza au serikali iache kufanyaufisadi wa kukusanya mapato yake na kuishia kwenye matumbo ya watu ili fedha hizo ziweze kutumika kuboresha maisha ya watanzania wake wote ili iwe tofauti na hivi sasa. Binafsi sikubaliani na mtu anyesema kuwa mbunge akiwa dodoma au dsm huku yeye akiwa antokea kioma,hai,mwanza,arusha,shinyanga,tabora nk kuwa asigharamiwe gharama za kuishi, sikubaliani naye kwa sababu wabunge siyo wakazi wa dodom bali dodoma ni extended working area,hivyo wawallipe fedha kujikimu kkwa kuzingatia mahitaji ya eneo husika. vilevile mji kama wa rusha Hotel nyingi ni kati sh.70,000/= hadi 500,000/=,hotel yenye usalama na hadhi ya viongozi, ukimlipa kweli sh.70,000/= unakuwa umemtendea haki kweli?
Ndiyo maana nashauri tufanye tafiti halafu ndiyo tuje tujadili hapa na kutoa mapendekezo juu ya nini serikali isiyotujali watu wake ifanye kwa maslahi yeu sote,na iache kutpuuza.ccm mnasikia....,Tuache kuwa na jazba badala yake tuzame kwenye hoja na bila kumbeza mtu kwa sababu zetu binafsi tena zisizokuwa na ukweli.
Nwasilisha na ninakaribisha changamoto kwa hoja zenye ithibati makini.

Ni lini kama wabunge mlikaa na kupigiania kuongeza mshahara wa kima cha chini cha wafanyakazi waishio Dodoma ingalao, manake huko si ndio mmeona maisha ni magumu? Iweje leo ghafla muone posho zenu ndio ni muhimu kuongezwa zaidi ya wafanyakazi wengine wote. Eti mbunge hatafanya kazi kwa umakini kwa sababu ya njaa, ni kazi gani kwani mabayo mmefanya nchi mpaka leo kazi kusinzia na kula posho za vikao tu, mikataba mibovu, rasilimali zinaibiwa, uchumi mbovu kuna kikubwa kipi mmefanya zaidi ya kuunga mkono hoja kishabiki tu!! Naona mmeamua kujiunga JF kutetea ulaji , tunawaambia ukweli mwisho wenu si mzuri!!
 
Kwanza nimpongeze huyo jamaa aliyewalisha hii mada hapa JF, PILI NIWALAUMU WACHANGIAJI WACHACHE AMBAO WANAANDIKA VITU VISIVYOKUWA NA KICHWA WALA MIGUU. hii kwa sababu hapa JF ni sehemu ya fikraa zinazoishi na siyo kuandika vitu visivyokuwa na hoja zilizotafitiwa. Nadhani inaweza ikawa vema tukafanyia utafiti wa hayo aliyoyasema badala ya sisi wachangiaji kuanza kusema YALE YALEEEEEEEEEEE, wengine au unatania.., wakuu hatuwezi kufika. Sisi tutembelee ofisi za serikali husasani ofisi ya rais menejiment ya utumishi wa umma, tutapata takwimu sahihi na iwapo itakuwa ni uwongo tutajadili, tusipinge kabla hatufanya tafiti. Mwingine anaweza kusema kuwa yeye ni mtumishi wa serikali kwamba hakuna kitu kama hicho, lakini hajawahi kupata kutoka nje ya kituo chake cha kazi sasa huyo atajuaje mambo haya ya posho kwa viwango mbalimbali?Tujipe nafasi tufuatillie ili kujua ukweli. Ikibainika kuwa kama amevyotueleza jamaa inabidi tuanzishe mchakato wa kuzipunguza au kuwaogezea wafanyakazi wengine mishahara na posho ikiwa ni sambamba na kuangalia namna bora kuondoa umasikini wa wasio wafanyakazi.iwapo serikali itashindwa kusikiliza yale ambayo tunayataka itabidi turejee kuangalia nini tufanye ili ituheshimu watanzania na mawazo yetu,hii ni kwa sababu serikali ya ccm ni ya kijanjajanja,

Wastarabu
Join Date : 6th December 2011
Posts : 1
Rep Power : 0

Munengami
Join Date : 6th December 2011
Posts : 2
Rep Power : 0

Very interesting!!!!!
 
Wastarabu
Join Date : 6th December 2011
Posts : 1
Rep Power : 0

Munengami
Join Date : 6th December 2011
Posts : 2
Rep Power : 0

Very interesting!!!!!

Mijitu mijinga bwana, eti linataka kuonyesha kuwa linaungwa mkono, wakati lina ID mbili, mbuzi kabisa!!
 
Watanzania mnashangza sana, mnashindwa kuelewa kuwa posho za wabunge zimeongezeka kutokana na ukweli kuwa wao walikuwa wakilipwa kiasi kidogo sana ikilinganishwa na watumishi wengine wa serikali kuu kama vile makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi wa mashirika ya umma,halmashauri mbalimbali nchini, walimu polisi, madaktari na wengine wengi wanapoenda kufanya kazi nje ya vituo vyao vya kazi kwa mfano mwali au polisi au daktari au mtumishi yeyote yule anapotoka mwanza kwenda Dar es salaam kikazi hulipwa sitting allowance au perdiem ya shilingi 200,000 au zaidi au pungufu kulingana na cheo au hadhi yake. Kwa hiyo siyo kweli kwamba posho za wabunge ndizo kubwa tu kuliko za wengine, tusiwe watu wa kuwabagua wenzetu, bango linashikwa kwa wabunge pekee yao, mbona hatuwashikii watumishi wengine? siyo kweli kwamba walimu hawalipwi posho wakisafiri kama wabunge nje ya vituo vyao vya kazi, mwalimu au polisi au mtumishi yeyote yule anaposafiri hulipwa hizo posho kulingana na cheo chao. kwa hiyo tusilaumu wenzetuy kwa sababu wana safiri sana kikazi, tatizo kubwa ni kuwa watumishi kama walimu huwa hawapati trip sana kama wabunge lakini wangepata trip kama wabunge wasingelalamika, na ofcourse haiwezekani wafanyakazi wote wakalingana katika kila kitu,hii ni kwa sababu nature ya kazi za wafanyakazi ni tofauti. Nashauri Zitto Kabwe awe mkweli katika hili, analijua vizuri sana kuwa watumishi wote hulipwa posho wanaspokuwa nje ya vituo vyao vya kazi kama wabunge na si wabunge peke yao. Msema kweli ni mpenzi wa mungu, Katika hili zitto kawapotosha watanzania, Azungumzie na watumishi wengine, lakini inaelewka kuwa anataka kuongeza umaarufu kwa kuwarubuni watu, vilevile akaunti yake imeshiba sana, wakati fulani gazeti moja liliandika kuwa an zaidi ya shilingi milioni 500, huku akiwa na magari yenye garama kubwa sana yaani HUMMER, RANGEROVER, MA VX,NISSAN nk. yote haya kayapataje? Atueleze yametoka wapi,Ni vema akawa anaeleza ukweli badala ya kutaka umaarufu kuwa yeye ni mzalendo huku ikiwa ni kinyume chake, lakini inwezekana akawa na chanzo kingine cha mapato, lakini isije ikawa ni misaada anayoomba kwa ajili ya jimbo lake halafu anafanyia mambo yake.
Katika hili la posho tusiwaonee wabunge na wala mimi binafsi siwalaumu wale wote wanopinga ongezeko hili ila wa kulaumiwa ni zitto aliyepotosha huku akijua kuwa hata watumishi wengine hulipwa posho kama wabunge na wwengine huzidi hata wabunge. Tutafakari upya na tusipelekwe na watu wanaotaka umaarufu kwa kuwalaghai wenzao

CRAP! Jina lako haliendani na upuuzi ulioandika hapo! hebu tukumbushe weye ni mbunge wawapi vileee....
 
Masaburi mkubwa wee... Umeingia jana JF kuja kuleta utumbo wako humu!!! Aliyekuambia mwalimu, polisi au nesi analipwa "sitting allowance" ni nani?? Rudi kwake akakueleze upya! Watumishi wa umma analipwa "per diem" akiwa nje ya kituo cha kazi na hiyo si kila mtumishi.. Mwalimu kama sio kwenda kusahihisha mitihani au kusimamia upigaji kura, anaweza kaa hata miaka 10 hajatoka nje ya kituo chake hivyo anasikia tu kuwa kuna "per diem"!!
Lakini hao "wezi" wenzako wabunge wana uhakika kila June to September si chini ya siku 90 bunge la BAJETI 200,000 X 90 posho ya kuweka masaburi chini tu... bado per diem kwa siku hizo 90 X 80,000/= mafuta n.k. And still mwisho wa mwezi wanakinga not less than 7,000,000/=!! bado kuna vikao vya bunge vya Novemba, Februari na Aprili. And remember most of them wapo kwenye bodi za mashirika kadhaa na pia bado wanahudhuria vikao vya kamati mbali mbali za ubunge kote huko ni posho tu..
 
Watanzania mnashangza sana, mnashindwa kuelewa kuwa posho za wabunge zimeongezeka kutokana na ukweli kuwa wao walikuwa wakilipwa kiasi kidogo sana ikilinganishwa na watumishi wengine wa serikali kuu kama vile makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi wa mashirika ya umma, halmashauri mbalimbali nchini, walimu polisi, madaktari na wengine wengi wanapoenda kufanya kazi nje ya vituo vyao vya kazi.

Kwa mfano mwali au polisi au daktari au mtumishi yeyote yule anapotoka Mwanza kwenda Dar es salaam kikazi hulipwa sitting allowance au perdiem ya shilingi 200,000 au zaidi au pungufu kulingana na cheo au hadhi yake.

Kwa hiyo siyo kweli kwamba posho za wabunge ndizo kubwa tu kuliko za wengine, tusiwe watu wa kuwabagua wenzetu, bango linashikwa kwa wabunge pekee yao, mbona hatuwashikii watumishi wengine? siyo kweli kwamba walimu hawalipwi posho wakisafiri kama wabunge nje ya vituo vyao vya kazi, mwalimu au polisi au mtumishi yeyote yule anaposafiri hulipwa hizo posho kulingana na cheo chao.

Kwa hiyo tusilaumu wenzetuy kwa sababu wana safiri sana kikazi, tatizo kubwa ni kuwa watumishi kama walimu huwa hawapati trip sana kama wabunge lakini wangepata trip kama wabunge wasingelalamika, na ofcourse haiwezekani wafanyakazi wote wakalingana katika kila kitu,hii ni kwa sababu nature ya kazi za wafanyakazi ni tofauti.

Nashauri Zitto Kabwe awe mkweli katika hili, analijua vizuri sana kuwa watumishi wote hulipwa posho wanaspokuwa nje ya vituo vyao vya kazi kama wabunge na si wabunge peke yao. Msema kweli ni mpenzi wa mungu, Katika hili zitto kawapotosha watanzania, Azungumzie na watumishi wengine, lakini inaelewka kuwa anataka kuongeza umaarufu kwa kuwarubuni watu, vilevile akaunti yake imeshiba sana, wakati fulani gazeti moja liliandika kuwa ana zaidi ya shilingi milioni 500, huku akiwa na magari yenye garama kubwa sana yaani HUMMER, RANGEROVER, MA VX, NISSAN nk. yote haya kayapataje?

Atueleze yametoka wapi, Ni vema akawa anaeleza ukweli badala ya kutaka umaarufu kuwa yeye ni mzalendo huku ikiwa ni kinyume chake, lakini inwezekana akawa na chanzo kingine cha mapato, lakini isije ikawa ni misaada anayoomba kwa ajili ya jimbo lake halafu anafanyia mambo yake.

Katika hili la posho tusiwaonee wabunge na wala mimi binafsi siwalaumu wale wote wanopinga ongezeko hili ila wa kulaumiwa ni zitto aliyepotosha huku akijua kuwa hata watumishi wengine hulipwa posho kama wabunge na wwengine huzidi hata wabunge. Tutafakari upya na tusipelekwe na watu wanaotaka umaarufu kwa kuwalaghai wenzao

Tatizo siyo zito ndugu, wala tatizo si upotoshaji wake. Tatizo ni kwanini wabunge tu? Kwa nini gharama za maisha zimepanda kwao tu na si kwa watumishi wote? Pia ningependa kukuuliza ni mwalimu yupi na polisi yopi anayelipwa posho ya maaa anapokuwa nje ya kito chake cha kazi? Huku ana gari, ana allowance ya mafuta na mengineyo mengi, na huku akipata nshahara zaidi ya milioni kila mwezi?
Wameshindwa kutupa kima cha chini cha laki tatu na kumi na tano. Mbunge ana kazi gani ngumu ya maana ya kumzidi daktari, mwalimu, polisi naporofessional nyigine? Mbunge ana mazingira gani magumu ya kufanyia kazi km hao uloowayaja hapo juu.
Mshahara wa mtumishi wa kawaida tena wa mwezi unaongezwa kwa tsh alfu kumi, ishirin tena kwa malalaniko na kusema serikali haina pesa. Leo mbunge anaongezewa laki na thelathini bila kwere. pesa zinatoka wapi.
Napat auchungu nashindwa kuendelea kuongea. Ningekuwa na uwezo ningewapiga bastola woote wabunge nikianza na spika wao. Eee Mungu tenda miujiza kwa TANZANIA
 
Whatever the posho. Iwe ya kujikimu, iwe ya nje ya kituo cha kazi au iwe ya kuhongea. IT IS TOO MUCH and ENOUGH IS ENOUGH!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Watanzania mnashangza sana, mnashindwa kuelewa kuwa posho za wabunge zimeongezeka kutokana na ukweli kuwa wao walikuwa wakilipwa kiasi kidogo sana ikilinganishwa na watumishi wengine wa serikali kuu kama vile makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi wa mashirika ya umma, halmashauri mbalimbali nchini, walimu polisi, madaktari na wengine wengi wanapoenda kufanya kazi nje ya vituo vyao vya kazi.

Kwa mfano mwali au polisi au daktari au mtumishi yeyote yule anapotoka Mwanza kwenda Dar es salaam kikazi hulipwa sitting allowance au perdiem ya shilingi 200,000 au zaidi au pungufu kulingana na cheo au hadhi yake.

Kwa hiyo siyo kweli kwamba posho za wabunge ndizo kubwa tu kuliko za wengine, tusiwe watu wa kuwabagua wenzetu, bango linashikwa kwa wabunge pekee yao, mbona hatuwashikii watumishi wengine? siyo kweli kwamba walimu hawalipwi posho wakisafiri kama wabunge nje ya vituo vyao vya kazi, mwalimu au polisi au mtumishi yeyote yule anaposafiri hulipwa hizo posho kulingana na cheo chao.

Kwa hiyo tusilaumu wenzetuy kwa sababu wana safiri sana kikazi, tatizo kubwa ni kuwa watumishi kama walimu huwa hawapati trip sana kama wabunge lakini wangepata trip kama wabunge wasingelalamika, na ofcourse haiwezekani wafanyakazi wote wakalingana katika kila kitu,hii ni kwa sababu nature ya kazi za wafanyakazi ni tofauti.

Nashauri Zitto Kabwe awe mkweli katika hili, analijua vizuri sana kuwa watumishi wote hulipwa posho wanaspokuwa nje ya vituo vyao vya kazi kama wabunge na si wabunge peke yao. Msema kweli ni mpenzi wa mungu, Katika hili zitto kawapotosha watanzania, Azungumzie na watumishi wengine, lakini inaelewka kuwa anataka kuongeza umaarufu kwa kuwarubuni watu, vilevile akaunti yake imeshiba sana, wakati fulani gazeti moja liliandika kuwa ana zaidi ya shilingi milioni 500, huku akiwa na magari yenye garama kubwa sana yaani HUMMER, RANGEROVER, MA VX, NISSAN nk. yote haya kayapataje?

Atueleze yametoka wapi, Ni vema akawa anaeleza ukweli badala ya kutaka umaarufu kuwa yeye ni mzalendo huku ikiwa ni kinyume chake, lakini inwezekana akawa na chanzo kingine cha mapato, lakini isije ikawa ni misaada anayoomba kwa ajili ya jimbo lake halafu anafanyia mambo yake.

Katika hili la posho tusiwaonee wabunge na wala mimi binafsi siwalaumu wale wote wanopinga ongezeko hili ila wa kulaumiwa ni zitto aliyepotosha huku akijua kuwa hata watumishi wengine hulipwa posho kama wabunge na wwengine huzidi hata wabunge. Tutafakari upya na tusipelekwe na watu wanaotaka umaarufu kwa kuwalaghai wenzao
Dogo acha kuuza sumu jukwaani, weka source maana umejifanya wewe mwenyewe ni Zitto na kumhukumu. Zitto hawezi kufukz Moshi kama huo.

Whatever the posho. Iwe ya kujikimu, iwe ya nje ya kituo cha kazi au iwe ya kuhongea. IT IS TOO MUCH and ENOUGH IS ENOUGH!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Hilo hapana ndugu,

Huwezi kukata posho zote maana zingine lengo lake ni kumwezesha mtumishi kutimiza wajibu wake ambao kwa huo aliajiriwa kutumikia watanzania. Kwa mfano, mtu akisafiri nje ya kituo chake cha kazi analipiwa nauli ya kufika kule anakoenda na pia kupewa posho ya kujikimu (yaani kumwezesha kuishi awapo kule maana kumbuka hapo yuko mbali na nyumbani). Ndiyo maana inalipwa kulingana na cheo na mahali anakokwenda mtu. Kwa sasa posho hiyo inaanzia 35,000 - 80,000 kwa siku, ili kumwezesha mtumishi huyu kulala, kula na dharura yoyote inayoweza kujitokeza maana huyu mtu yuko mbali na kwake.

Labda nikuulize wewe, kwa mfano mfanyabiashara akimtuma mtu ili aende Mwanza kusimamia upakiaji wa mizigo yake na kazi ikapangwa kufanyika kwa siku mbili, je itakuwa sawa kumwambia atumie mshahara wake awapo Mwanza wakati kituo chake cha kazi ni Mbeya? Naomba hili suala la posho tuliangalie kwa makini, na siku zote wapinzani wa posho, tunapinga zile zisizo na tija, kama sitting allowance, responsibility allowance (posho ya wajibu/majukumu) wakati aliajiriwa kutimiza wajibu huohuo ambao kwa huo analipwa posho na nyingine za hovyo. Na kumbuka posho nyingi zisizo na tija wanalipwa maofisa wakuu/vigogo ambao mishahara ni mikubwa mno tayari
 
Back
Top Bottom