Zitto awashika wabunge pabaya

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,712
1,906
Ataka posho zote za vikao ziondolewe
Ataka panga pia lielekezwe serikalini
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wake, Deo Fulikunjombe.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, kwa mara nyingine ameibua hoja nzito iliyowahi kutaka kuligawa Bunge vipande vipande ya kutaka wabunge wasiwe wanalipwa posho za vikao akisema kuwa kazi wanayoifanya ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam, Zitto alisema haoni sababu mbunge kuendelea kulipwa posho nono kwa ajili ya kuhudhuria vikao kwa kuwa hiyo ni sehemu ya kazi yao ya kila siku.
Alisema anataka sheria ya Bunge inayotoa mwanya kwa wabunge kulipwa posho hizo ibadilishwe haraka ili kiasi hicho cha fedha kitumike kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania wengine wenye matatizo.
Zitto alisema ingawa suala hilo ni gumu, lakini ataliwasilisha katika mkutano wa Bunge la bajeti wakati atakapowasilisha bajeti yake kama Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi.
Alisema ana imani wabunge wenzake watakubali pendekezo hilo na kumuunga mkono kubadilisha sheria hiyo ili posho hizo zisiwe zinatolewa.
Katika Bunge lililopita aliyekuwa Mbunge wa Karatu, Dk. Willibroad Slaa (Chadema), aliwahi kutoa wazo kama hilo pamoja na kupendekeza mshahara wa wabunge upunguzwe kwa kuwa ni mkubwa, lakini wabunge wenzake walipinga hoja hiyo kwa nguvu zote.
Dk. Slaa alishindwa kupitisha hoja yake katika Bunge lililopita baada ya wenzake kukataa kumuunga mkono huku baadhi yao wakitoa kauli za kumkejeli na kumuona kama mtu aliyekuwa akitafuta umaarufu wa kisiasa.
Kiutaratibu wabunge wote hulipwa posho ya vikao ya Sh. 80,000 kwa siku, na posho ya kujikimu kwa kuwa ya nje makazi Sh. 70,000 hivyo kwa siku moja tu wabunge hulipwa wastani wa Sh. 150,000 siku za kazi, wakati mwishoni mwa wiki hulipwa Sh. 70,000, kwa maana hiyo kati ya wabunge wote waliopo ambao ni 350 kama posho hizo zitaondolewa serikali itaokoa kiasi cha Sh. milioni 52.5 kwa siku.
Mkutano wa Bunge la Bajeti unatarajiwa kuanza Juni 7, mwaka huu hadi Agosti 15, mwaka huu, kwa maana hiyo kutakuwa na siku za kazi 48 ambazo zitaigharimu serikali Sh. bilioni 2.52 kama posho ya vikao kwa wabunge.
Kiasi hicho kikiongezwa Sh. milioni 490 za posho ya kujikimu ya mwishoni mwa wiki ambazo ni sawa na siku 20, serikali itakuwa inatumia jumla Sh. bilioni 3.01 ambazo ni posho za wabunge bila mshahara.
Kiasi hicho kama hakitalipwa wabunge kinaweza kuelekezwa kutunisha bajeti ya elimu, barabara au afya, ambako kuna upungufu mkubwa wa fedha.
Mshahara wa mbunge kwa sasa ni Sh. milioni 2.5, kiasi hicho kikichanganywa na posho ya mafuta, kuendesha ofisi mapato yake ya ubunge yanafika kiasi cha Sh. milioni 7.19.
Nimeipenda hii post, hawa watu wageuke tuelekee kuzuri!!!!!!!!!!!

 
Waziri Mende alikuwa anakomalia pesa za BAE ili zitumike kununulia vitabu huku akijua posho za wabunge zinaweza kufanya kazi hiyo kama mapendekezo ya Zito yakifanyiwa kazi! Kumbe Mende mkuda hana lolote!
 
Waziri Mende alikuwa anakomalia pesa za BAE ili zitumike kununulia vitabu huku akijua posho za wabunge zinaweza kufanya kazi hiyo kama mapendekezo ya Zito yakifanyiwa kazi! Kumbe Mende mkuda hana lolote!
Hata zikigawanywa nusu tu, zitafanya kazi kubwa saana. Zito anafaa anaibua mambo ya msingi katika jamii yetu yanayo paswa kufanywa kwa resources tulizo nazo!!!!!!!!!!! Wana maghamba watakubali?????????
 
Thread hii imerudiwa sana, nenda kachangie kule ilipo. Unajaza server to humu.Mods ondoeni hii.
 
Ni muhimu kwa wabunge wetu wakaacha itikadi zao za vyama na kuingalia budget ya mwaka huu kwa manufaa ya maendeleo ya nchi yetu na wananchi wanaowaongoza. Tatizo kubwa tulilonalo sio ukosefu wa mapato yanayohitajika kwa recurrent na development expenditure, tatizo liko kwenye matumizi mabaya ya mapato yetu!! Tukiweza kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kutumia mapato yetu vizuri katika vipaumbele tulivyojiwekea tunaweza kubalance budget yetu na pia kupunguza utegemezi kwa watu wa nje kitu kinachotudhalilisha kama nchi iliyojitawala kwa muda wa miaka hamsini!! Mheshimiwa Zitto is trying to address this issue in a non partisan way lakini sasa wabunge wenzie hawalioni hivyo wanafikiri anajitafutia umaarufu kitu ambacho mimi kwa mtazamo wangu naona hakina ukweli!!
 
Haya ndiyo mambo ya msingi kwa Watanzania.Sio kwenda kusinzia tu mjengoni ukisubiri kutafuna kodi zetu(wananchi).
 
Thread hii imerudiwa sana, nenda kachangie kule ilipo. Unajaza server to humu.Mods ondoeni hii.

ama kweli we Abunuasi kama mleta thread anajaza Server na wewe hapa si umechangia umefanya nini????
Kilaza mkubwa we!
 
Back
Top Bottom