Zitto atikisa Bagamoyo leo

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Naibu Katibu Mkuu wa CDM Zitto Kabwe jioni hii anatarajiwa kutikisa mji wa Bagamoyo katika kampeni za kumnadi mgombea udiwani wa CDM katika kata ya Magomeni.

Mgombea udiwani huyo wa CDM anaungwa mkono na wananchi na kuna uwezekano mkubwa wa kushinda katika uchaguzi utakaofanyika jumapili wiki hii.

Wakati Zitto yuko Bagamoyo viongozi wakuu wa chama hicho wamejichimbia maeneo mbalimbali nchini kuhakikisha CDM inapata ushindi mkubwa katika kata 29 zitakazofanya uchaguzi.Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kwa wiki nzima yuko mikoa ya kusini huku Katibu mkuu wake Dr Wilbroad Slaa amejichimbia Kanda ya ziwa kwa wiki mbili sasa.

Mjumbe wa Kamati Kuu Godbless Lema akisaidiwa na Kamanda Henry Kilewo yuko Kanda ya Kaskazini huku Mkurugenzi wa Mafunzo na operesheni Benson Kigaila akipambana Kanda ya Kati.

Makamanda wengine walioko mstari wa mbele wa mapambano ni Alphonce Mawaazo na Ally Bananga wakipigania Kata za Mkoa wa Morogoro.
 
Hivi ndivyo inavyotakiwa. Zitto ni lazima ajikite katika ujenzi wa chama na si vinginevyo. Long live CHADEMA.
 
Molemo Leo anamsifu ZZK maajabu!
Anyway,hizi ndo siasa tunazotaka sio za majungu na fitna! Kila la kheri ZZK na Viongozi wengine(hata na wale ambao hawana majina) katika kuhakikisha ushindi kwa chama.
 
Molemo Leo anamsifu ZZK maajabu!
Anyway,hizi ndo siasa tunazotaka sio za majungu na fitna! Kila la kheri ZZK na Viongozi wengine(hata na wale ambao hawana majina) katika kuhakikisha ushindi kwa chama.

Mkuu wangu ulinisoma vibaya sana.Ukweli siku zote lazima usemwe peupe.Kila anayefanya jambo jema kuiweka CDM juu lazima asifiwe.Ukiona anayepinga kila kitu huyo ni mchawi na hafai katika safari ya ukombozi.Pamoja sana Kamanda.
 
Yeah kikubwa zitto jenga chama urais unakuja wenyewe usiukimbilie
nakuunga mkono hoja yako,chama cha kwake wananchi wa kwake haraka ya nini,mbona slaa hatukutarajia kama angegombea ? Dogo zzk punguza hasira mambo mazuri hayana haraka...
 
Back
Top Bottom