BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,006
• Zitto ataka wabunge wa zamani waombe radhi
Na Said Mwishehe, Mwanza
Majira
NAIBU Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Zitto Kabwe, amewataka wabunge wa mwaka 1995 hadi 2000 kuwaomba radhi Watanzania, kwa madai kuwawalipitisha sheria mbovu ya madini na kulisababisha Taifa hasara ya dola milioni 883 za Marekani ambazo ni sawa na sh. trilioni moja za Tanzania kwa sasa.
Bw. Zitto alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Mwanza eneo la Ilemela, ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa ziara ya Operesheni Sangara inayoendeshwa na chama hicho ambayo imeandaliwa kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Alidai kuwa wabunge waliokuwa bungeni katika kipindi hicho, ndio wanaopaswa kulaumiwa kwa kupitisha muswada wa sheria ya madini, ambayo inatoa mwanya kwa kampuni za madini nchini, kukwepa kulipa kodi kwa visingizio mbalimbali na kulikosesha Taifa mabilioni ya fedha Kwa kipindi kirefu sasa na bila sababu za msingi.
Aliwaambia wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo, kuwa mwaka 1997, Bunge lilipitisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Sheria mbalimbali za Fedha, ambayo ndiyo iliyoweka msingi wa sheria za kodi za madini bila kujali maslahi ya nchi na matokeo yake kutokea kwa hasara kubwa.
Bw. Zitto alisema katika sheria hiyo, kuna kipengele cha asilimia 15
kinachosema kuwa baada ya kampuni ya uchimbaji madini kutoa gharama zake za uzalishaji, inaruhusiwa kuongeza asilimia nyingine 15 ya gharama hizo.
Alisisitiza kuwa kutokana na sheria hiyo, tangu mwaka 1997 hadi mwaka jana, kipindi cha miaka 10, Serikali imeingia hasara ya dola milioni 883.
"Endapo fedha hizo zingekusanya zingesaidia mambo mbalimbali ya
maendeleo" alisisitiza Bw. Zitto na kuongeza: "Wabunge ndio wanapaswa kulaumiwa, lakini pia wawaombe radhi Watanzania kwa kusababisha hasara na kuzipa faida kampuni za madini," alisema.
Kutokana na hali hiyo, aliyewahi kuwa mbunge wa Kisesa kuanzia mwaka 1995 hadi 2000 kupitia UDP, Bw. Erasto Tumbo, ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA aliwaomba radhi Watanzania hadharani kwa kuwa miongoni mwa wabunge waliopitisha sheria hiyo.