Zitto arudishiwa uongozi wa Bunge na CHADEMA, wamtambua Kikwete

Akienda NCCR na kuwa mwenyekiti hawezi gombea uraisi umri utambana jamani mbona kila siku twaliongelea ili?
 
Naona kichwa cha habari hii kinapotosha ukweli. Nionavyo mimi, kamati kuu imechukua hatua ya kuweka sawa namna mchakato mzima wa kushughulikia tatizo la Zitto unavyopashwa kuendeshwa. Inavyoelekea, hatua ya kumpigia kura ya kutokua na imani na uongozi wake, iliyokuwa imechukuliwa na wabunge ilikuwa inakiuka haki zake za msingi; kwakuwa huwezi kumuhukumu mtu bila ya kwanza kumpa fursa ya kujitetea. Sasa kamati kuu imesahihisha kasoro hiyo, sasa ngoma imebakia kwa Zitto mwenyewe kujisafisha kwa viongozi wenzake.
 
ZITTO HANA MAELEZO TIMAMU TO BACK-UP HIS ''DUMBEST MOVE OF ALL TIME IN TZ POLITICS'' AND THAT WAS GOING TO PRESS AND START B*TCH*NG 'BOUT HIS FELLOW MPs PHENOMENAL HEROIC WALK-OUT! PERIOD,
 
sumaye fisadi tuu!arejeshe kwanza mashamba anayomiliki morogoro na jeetu patel!

nadhani mtu yeyote anaweza kumiliki mashamba tz kama ana mtaji wa kuyaendeleza ukizingatia tz bado tuna ardhi kubwa sana. Lete point nyingine!... Mi nawachukia wale mafisadi walioficha hela nje ya nchi ambazo zinafaidisha wasio watanzania kuliko fisadi ambaye ame invest tz na kuwapa watu ajira.
 
nccr mageuzi wamemuahidi uenyekiti wa chama na agombee urais mwaka 2015 kama walivyofanya kwa al.mrema. Dogo bado analitafakari hili ingawa kuna nguvu kubwa ya marafiki zake wa ccm wanaotaka kumsajili kwa udi na uvumba!! Cuf nao wanamtaka kwa mgongo wa udini, wanapiga chapuo eti waislamu hawako salama wakiwa chadema!!!! Kwa kweli nchi hii imelaaniwa kama mambo yenyewe ndiyo haya!!

Huyu dogo mwisho atachanganyikiwa na sijui mtasema nani kamloga!
umesahau zitto atakuwa na miaka 39?
 
HILO LIMEKAMILIKA SASA TURUDI KWENYE VIPA UMBELE VYA CHADEMA
1. KATIBA MPYA
2. KUHAKIKISHA CDM INAONGOZA MAJIJI YA MBEYA, ARUSHA, NA MWANZA NA KUTUMIA ILANI YA CHADEMA
3. TUJENGE MAKAO MAKUU YA KISASA
4. OPRESHENI SANGARA
5. TUME HURU YA UCHAGUZI
6. TUME HURU KUCHUNGUZA UCHAKACHUAJI WA KURA ZA SLAA(PhD)
7.

Thank u Denyo kwa kuturudisha kwenye dira. Hapo ndiyo panapohitajika
 
Kaka nakuunga mkono kwa mchango wako ila napingana nawe kwa jambo moja sikubaliani na wanafiki walioko chadema na unafiki wanao ufanya juu ya swala la kabwe, kama zitto kakosea kamati ya maadili ya chadema ingemkalisha kikao imuonye lakini hili la wabunge kwenda bagamoyo kupiga porojo sikubaliani nalo hata kidogo,kwani ni zitto peke yake aliwasaliti chadema siku hiyo
 
Nimeshasema kuwa suala la kufukuzana halitaisadia CDM!! Ni mbinu inayotumiwa na watawanyaji wa CDM kuchochea mgogoro. Naamini kumfukuza zitto si suluhu ya mambo, bali ni kuibusha mgogoro ambao CDM wataendelea kuwa nao hadi 2015 wakijibu mashambulizi yatokanayo na zitto for nothing. Nashauri viongozi CDM WADHARAU PROPOGANDA za kisiasa, waonyanye juu ya mienendo yao na namna ya kutunza siri za chama (period)!! Wala si kumuona fulani mchawi, hata kidogo.
 
Kamati Kuu ya chadema imemtambua JK kama Rais halali na kuagiza wabunge kushiriki shughuli zote za kitaifa. Kamati Kuu imekataa kura ya kutokuwa na imani na Zitto mpaka asikilizwe kwanza kwa mujibu wa natural justice.

??Kamati kuu ya CHADEMA imeunda jopo la wazee wa chama chini ya prof. Baregu kumsikiliza Zitto na matatizo yake na viongozi wengine wa chama ili kuleta suluhu ndani ya chama. Jopo hilo lina Shida Salum, Kitila Mkumbo kama Katibu, prof. Baregu na Shilungushela.

Wabunge wa CHADEMA wameagizwa kukutana na Zitto kwanza kabla ya kuchukua maamuzi yeyote kisha walete taarifa kwenye kamati kuu.
Ukiangalia hapo kwenye taarifa ya hali halisi. Utaona watu wanamjadili Zitto kama mtu mwenye makosa. Mbona hamsemi kwamba Zitto ni MSHINDI? Hamuoni kwamba kamati kuu imeiagiza CHADEMA imtambue Rais? Kwahiyo hata hao waliopiga kura na kutoka Bungeni ndio wanamakosa na wao ndio wanastahili wahojiwe. Hivi huo uamuzi wa kutoka Bungeni ni nani mwenye final say? Au ni kujiamulia tu? Kiufupi kamati kuu inakubali kuwa Zitto alikuwa sahihi na kwahiyo hataadhibiwa. Tulisema na tutaendelea kusema, CHADEMA hawakujipanga na hawakujua kuwa kuna ishu zitajitokeza baada ya uchaguzi na hatimaye ndio mvurugano huu. Tunaendelea kusema, CHADEMA watazame saana muundo wa viongozi wao na nani hasa mwenye mamlaka katika CHAMA wakati huo wakizingatia maslahi ya CHAMA na wananchi kwa ujumla.
 
Mafioso hawashindwi, watampa kidonge cha diclochacha wangwexin

Hizo haziponyeshi, kuna Kafulilaquine na Leticiadex!! kumeza tumia maji ya Uhai!

Nadhani CDM wamefanya vizuri kuacha natural justice to take its path...! BRAVO

Kumbe alionewa!!! thanks for confirming that, statement yako imebeba maana iliyojificha, kwa kifupi unaamini kabisa na huna haja ya kuuliza kuwa Zito ameonewa! congrats..... I too know that beyond reasonable doubt
 
mkuu nakuunga mkono, hao wanaougua kipindupindu waendelee kujiuguza, cdm ifocus kwenye strategic issues ili kuwin viti vingi bungeni 2015
 
Ni kweli, CDM wana kazi kubwa ya kuimarisha chama kila tawi na ikifika 2015 isimamisha mgombea kila jimbo bila kusahau katba mpya. Suala la waliosusia mgomo liishe kazi iendelee.
 
Chadema mnajikoroga kweli, hata miezi miwili bado eti cheo kimefitwa sasa mliweka cha nini au alitakiwa kupewa ndugu wa viongozi lakini ikatokea bahati mbaya kura ikamwangukia Zitto wakubwa hao roho zikawaruka na kuuma hivyo sasa wamepata nafasi wamefuta. Mpaka 2015 Tutaona mengi
 
Inatia hasira sana kuona thread zisizo na mashiko kama hizi halafu zinajadiliwa hapa JF.....Where are you great thinkers?
 
Ukiangalia hapo kwenye taarifa ya hali halisi. Utaona watu wanamjadili Zitto kama mtu mwenye makosa. Mbona hamsemi kwamba Zitto ni MSHINDI? Hamuoni kwamba kamati kuu imeiagiza CHADEMA imtambue Rais? Kwahiyo hata hao waliopiga kura na kutoka Bungeni ndio wanamakosa na wao ndio wanastahili wahojiwe. Hivi huo uamuzi wa kutoka Bungeni ni nani mwenye final say? Au ni kujiamulia tu? Kiufupi kamati kuu inakubali kuwa Zitto alikuwa sahihi na kwahiyo hataadhibiwa. Tulisema na tutaendelea kusema, CHADEMA hawakujipanga na hawakujua kuwa kuna ishu zitajitokeza baada ya uchaguzi na hatimaye ndio mvurugano huu. Tunaendelea kusema, CHADEMA watazame saana muundo wa viongozi wao na nani hasa mwenye mamlaka katika CHAMA wakati huo wakizingatia maslahi ya CHAMA na wananchi kwa ujumla.

Kwani haijulikani nani aliamua chadema kususia hotuba ya rais?
 
quote_icon.png
Originally Posted by Mtemakuni
Nadhani CDM wamefanya vizuri kuacha natural justice to take its path...! BRAVO

Kumbe alionewa!!! thanks for confirming that, statement yako imebeba maana iliyojificha, kwa kifupi unaamini kabisa na huna haja ya kuuliza kuwa Zito ameonewa! congrats..... I too know that beyond reasonable doubt
Yaani kwa Mtemakuni kuandika hivyo tayari ume draw conclution kuwa Zitto kaonewa, ina maana chochote atakachosema Mtemakuni utaamini ni kweli, je akisema kesho ni mwisho wa dunia utaamini, Waberoya don't be obsessive usiwe kama abunuasi.
 
Akienda NCCR na kuwa mwenyekiti hawezi gombea uraisi umri utambana jamani mbona kila siku twaliongelea ili?

wakichakachua umri kama masauni?? sijui malisa??? hawashindwi kitu kama wenje na bashe wenyewe sio raia kipi kinachowashinda kufanya???
 
Nyie hamjui Zitto kiundani!!! Zitto ni mtu anayeamini kuwa makini kuliko wabunge wengine vijana akiamioni mtaji alionao mkononi wa uwajibikaji aliochapa kazi kipindi (bunge) kilichopita. Lakini amesahau kipindi alichonacho ni kifupi kuelekea mwisho wake wa kisiasa, kwa sababu maamuzi ya kizuzu yoyote atayoyafanya yatakuwa na athari kubwa sana. Mfano akihamia CCM inawezekana jamii ikamuona msaliti na akapoteza mvuto kisiasa kama alivyo na CCM kupitia makachero wao wakaona hauziki kivile hivyo wakaamua kumtosa tofauti na anavyofikiri yeye. Hapo utakuwa mwanzo wa kufa kisiasa kwa Zitto. Akibaki CDM domo lake halifungi hivyo CDM wanaweza kumuona kama huyu jamaa ni shetani aliyevaa kanzu hivyo kila ambacho atasema kitaonekena kama hakina maana hata kama kina maana, maana atakuwa amepoteza imani kwa wanaCDM bila ya yeye kujua au huku akijua.
Ushauri wa bure Zitto achana na UNAFIKI fanya siasa ya kweli kama ulivyokuwa kabla kujaenda kwenye kamati ya madini mzee. Kila siku wewe ipo siku watu watakuchoka na wataamua kukutosa hata kama maamuzi hayo yatakuwa na gharama. Mwisho uhusiano wako na WCCM hususani JK na wengine wengi watu hawauelewi ni kwa tija ipi? Mwisho dudub liumalo usilipe kidole ikasema litakula kidogo jua mkono wote utaondoka.
 
Zitto nakuona humu, haya yote yanayotokea huna haja ya kumlaumu mtu wa kumlaumu ni wewe mwenyewe.

Umekuwa modal wangu kwa muda mrefu sana lakini kadri siku zinavyokwenda umekuwa ukini discourage kwa kiasi fulani. Maji yameshamwagika tunaweza kusaidiana kuyazoa lakini tuelewe hayatakuwa masafi kama yalivyokuwa, sikulaumu kwa kitendo chako cha kutofautiana mawazo tatizo ni kutoka nje na kutangaza siri za vikao tena kwenye media. Najua ulifanya hivyo ili kuonesha hisia zako lakini hukufikiria hisia za wengine na hisia za chama chako.

Elewa kuwa chama ni mkusanyiko wa watu wenye mawazo na maoni tofauti lakini wakiwa wafuasi wa itikadi moja, kikishaitwa chama mawazo yanawekwa kwenye pool moja yanatakiwa yawe standardized (Normal distribution) asitokee mtu akawa nje ya distribution inayotakiwa, sasa wewe ulitaka uende nje ya normal distribution, ninaposema normal distribution si kuwa lazima wote muwe na mawazo sawa.

Ushauri wangu tulia angalia ulipo anzia na ulipojikwaa chukua mazuri acha mabaya, popote utakapokwenda utayakuta haya tena yanaweza yakawa mabaya zaidi, hata ukiamua kuanzisha chama chako huwezi kukwepa haya ninayoyasema vinginevyo kitakuwa kinaendeshwa ki dikteta.



There are currently 82 users browsing this thread. (23 members and 59 guests)
Luteni Gurtu baraka boki Mzee wa Rula Nyamgluu Anfaal RockSpider Kanigini Zitto Butola PayGod Madcheda Libaba
Mkombozi Lonestriker RealMan Kinyamana MWANALUGALI bullet magee tzjamani kilemi Iteitei Lya Kitee
 
Back
Top Bottom