Zitto apendekeza Dowans itaifishwe; Serikali yapinga! Mgao waendelea...

Anatarajia kujaribu tena kuipigia debe mitambo ya Dowans. Kwa kuwa mgao umeshika kasi, basi atasema: "Siliniwaambia? Sasa kiko wapi?"

Atasema mtambo wa Dowans utamaliza tatizo kwani mashine zile bado ziko pale Ubungo badala ya kuamriwa kuondolewa -- ni kubonyeza tu button -- na lo! umeme huoooooo!!!!! hakuna mgao tena!!!!!

Kavuta mzigo huyo! Halafu yake anaweweseka kupoteza kiti chake mwaka ujao. CCM (wale mafisadi watatu wanayoiongoza) wamemwahidi awapigie debe hili la Dowans, ili wapate USD 60m kutoka kwa walipa kodi, nao watahakikisha anashinda kile kiti, akiwa huko huko Chadema!

Nyie ngojeni tu, mtajionea mambo.
 
Typical wabongo too much know! kila mtu anajua na kukandia, hatuko mbali kuwafikia ndugu zetu wa kikenya. we are expectionally good in destroying what our fathers and forward thinker like Nyerere has been trying to build for years!!
 
Binafsi Zitto kisha niangusha vibaya sana yaani kaharibu kabisa harakati zake za kimapinduzi.. Nilikuwa naye na nilimwelewa sana ambiton yake, lakini kutokana na saga hili la Dowans anaonyesha wazi he is just an Opportunist..samahani mkuu Zitto lakini wewe kama mpinzani kushikilia hoja ya Dowans kama ni suluhu ya tatizo la Umeme nchini ni kujiweka ktk hali ngumu sana kisiasa..Hon. Harper (Ur role model) would never touch issue kama hii na kusimama upande dhoofu..Bora akae kimya kabisa!
 
Natumai hatasema kwamba alikuwa right alipopigia debe ununuzi wa mitambo ya kifisadi ya *~Dowans.

Kama hatasema hivyo basi hakuna tena mkutano. Kwani atasema nini zaidi? Kwamba alikosea kutetea Dowans na ndiyo maana Rashidi aliandaa mgawo au?
 
Mkuu,

Hivi huyu kijana hana washauri? Kwa nini asiwaachie serikali wakahangaika na mizengwe yao ya umeme? Naona anafanya mchezo wa kununu kesi kama nilivyosikia kuwa kuna kabila fulani linapenda sana mchezo huo. Kama ningeweza kumshauri, ningemwambia afunge mdomo wake. Damage aliyoipata kwa kauli zake kuhusu Dowans ni kubwa sana kiasi kwamba hatakiwi kuanzisha mijadala mingine isiyokuwa na tija. Anyway, sikio la kufa....!

Yah, kijana kweli hana busara.

Ila tusubiri tuone sarakasi zake, huenda kuna nguvu 'fulani' nyuma ya hii kadhia nzima na taratibu mbivu zitajitenga na mbovu.
 
Kwa kweli sijajua Tanesco na serikari at large walichukua hatua gani tangu wakati ule Idris alipotishia mgao baada ya zoezi la kushawishi ununuzi wa mitambo ya dowans kushindikana. inaonekana hakuna juhudi endelevu zilizo fanyika, kwani naamini hatua sahihi zingechukuliwa mpaka sasa tungekuwa na mitambo mingine mipya inafungwa katika hatua za mwisho mwisho. Vile vile kulikuwa na tetesi za kutumia umeme wa IPTL ambao umesimamishwa kwa miaka takribani miwili sasa, sina hakika hapo napo wamefikia wapi. kweli miafrika ndivyo tulivyo.
 
Jay,

Ungekuwa Bongo basi ungeonja machungu ya mgawo huu na ukajaribu kuunganisha 'siasa za umeme' zinazoendelea na kujua kuwa tunachezeana akili.

Hebu soma hapa:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/497-siasa-hizi-za-umeme-zitatufikisha-pabaya.html

Sidhani kama nina la kuongeza zaidi!

Invsible,

Kinachowasumbua mlioweka makazi ya kudumu dar is poor plan ya kizazi cha kifisadi. JOTO AND NO POWER lazima mkumbuke DOWANS tu. Nasikia hata Kitalu #1 kimezungukwa na magorofa. Lol
 
umeme imekuwa Tatizo sio bongo tu nchi nzima tuna suffer na hili janga la umeme
 
Mlioko Marekani mkisikia Rais wetu kaja huko mshawishini akutane na wakuu wa makampuni yanayotengeneza haya majenereta. Asitume mtu, akutane nao yeye mwenyewe.
 
Hope hatakuja na na cheap shot tactics za i told u so,hapa kuna sabotage/corruption kubwa sana,miezi tisa tangu mitambo ya Dowans imezimwa wameshindwa kununua mingine?wanafikiri watu wakipigwa mgawo watasalimu amri....sielewi JK anafanya kazi gani anafikiri kukimbiza mwenge Butiama ni muhimu kuliko umeme unaoua uchumi wa nchi!
 
Ewe sikio la kufa embu zinduka usikie hii dawa,achana na issue hizi zinakupotezea muda,serikali kuu yenyewe ndiyo inajua what game they play,so you better stay away from this,kama unaenda kujikampenia hiyo ni poa ila si vinginevyo!!
 
Mhe, Zitto Kabwe (MB) atakuwa na Press Conference kesho Oktoba 15, mida ya saa 6 adhuhuri Cortyard Hotel - Dar es Salaam.

Press Conference hii itahusiana na Mgawo wa Umeme unaoendelea. Kwa waandishi mlio Dar tunatarajia mtatufahamisha kinachoendelea. Kama kawaida, JF itatuma mwakilishi wake kutufahamisha kilichojiri.

Stay tuned

Kawaambie Zitto, ili wajifunze!
 
Sidhani kama kuna jipya

Nadhani hapa tunakuwa wabinafsi kidogo, kwetu sisi wa JF tunajua wazi Mh. Zitto ataongea nini?

Lakini tukumbuke kwamba audience anayokwenda kui-address sio JF ni wananchi wengine ambayo wanafikiwa kwa njia ya radio tu, magezeti tu, au runinga tu...

Hivyo Mh. Zitto endelea achana na wanaJF... kama nia ilikuwa kutu-address sisi wanaJF basi ungekuja kumwaga vitu vyako hapa.

Pili, Mheshimiwa Zitto ni mshindani wa CCM na Serikali iliyoko madarakani... hivyo pale ambapo ana nafasi ya kuwapiga bao la kisigino lazima atumie hiyo opportunity.

Mwisho Nakutakia kila la kheri, kwenye hili nipo nawe daima, kwenye la kuwa mwenyekiti wa chama nilikataa, na kweli ukajitoa.
 
Back
Top Bottom