Zitto: Anatetea Maslahi ya Taifa zaidi kuliko ya waliompa Ubunge?

Mpita Njia,

..kuna dhana kwamba haiwezekani Mbunge akatetea maslahi ya taifa, na wakati huohuo akawa karibu na wananchi wa jimbo lake.

..CCM pia wanajaribu kuwahadaa wananchi kwamba wabunge toka vyama vya upinzani hawana uwezo wa kuhamasisha na kupeleka maendeleo majimboni mwao.

..binafsi ningependa Zitto awe kati wa wanasiasa ambao wata-prove kwamba dhana hizo mbili nilizozitaja hazina ukweli wowote.
 
..binafsi ningependa Zitto awe kati wa wanasiasa ambao wata-prove kwamba dhana hizo mbili nilizozitaja hazina ukweli wowote.
naamini kuwa Zito atafanikiwa ku-prove hivyo si wka maana ya kuwa hajihusishi na watu wa jimbo lake, la hasha. Zitto yu karibu sana na wapiga kura wake kuliko watu wanavyodhani. Wapo wanaoamini kuwa Mbunge kushinda jimboni ndio kuwa karibu na wananchi wakati kuwa karibu na wananchi ni kuwasaidia kutatua matatizo yanayowakabili, hata kama watakaa muda mrefu wasikuone kimwili... Zito is doing just that
 
naamini kuwa Zito atafanikiwa ku-prove hivyo si wka maana ya kuwa hajihusishi na watu wa jimbo lake, la hasha. Zitto yu karibu sana na wapiga kura wake kuliko watu wanavyodhani. Wapo wanaoamini kuwa Mbunge kushinda jimboni ndio kuwa karibu na wananchi wakati kuwa karibu na wananchi ni kuwasaidia kutatua matatizo yanayowakabili, hata kama watakaa muda mrefu wasikuone kimwili... Zito is doing just that

maybe Zitto (my great man) is doing but Shelukindo is not, if you want to prove waulize huko Tanga.
 
Mpita Njia,

..mimi siyo mwananchi wa Kigoma Kaskazini. pia hakuna aliyenituma niwasemee.

..ninachojaribu kusema ni kwamba Zitto can and should juggle btn kutetea masuala ya kitaifa na vilevile awe karibu na wananchi wake.

..Kigoma Kaskazini siyo sawa na jimbo la Ubungo au Temeke. Kigoma in general iko nyuma sana kimaendeleo wanahitaji wabunge waliokaribu nao na wakereketwa wa kweli wa maendeleo yao.

NB:

..habari kwamba Zitto amelitekeza jimbo lake zilianza kutolewa na waziri mkuu Pinda bungeni.

..vilevile kuna mchangiaji wa jamii forums namheshimu sana naye alidai mambo jimboni kwa Zitto siyo mazuri.
Mpita njia swala hili nilimuuliza mimi na naona anakujibu wewe. Nilijua huyu au anazungumza asichokijua kwa ushabiki wa Yanga na Simba au katumwa aseme PR hapa.
Ni vema katubu na kusema ukweli wote.
Kwa sababu hiyo naomba achangie mengine lakini kwa habari ya Zito anyamaze. Asidandie treni:Dataaibika bure.
Kwa taarifa yake Tanzania Yote shida zetu ni moja hata kama mbunge mnalala naye chumba kimoja:( Maana hakuna duka la mbunge peke yake. Hakuna barabara ya mbunge peke yake na hakuna maji ya mbunge peke yake. Hakuna umeme wa mbunge peke yake. Nk,nk,nk,nk,nk,nk.
 
Zitto hata viti maalum tutakupa mzee wetu kijana achana na hawa jamaa wa kigoma kama wanakuzenguwa. SISIEMU imewakaa sana damuni ndo maana wanapewa mwekezaji wa TRL mhindi. Sijawahi ona. Zitto warudishie Jimbo lao na tutakupa kiti maalumu
 
Kwa kawaida si hulka yangu kushiriki kwenye mijadala ya kashfa kama washika dau wengine walivyofanya kwenye post inayohusu mdau Mwakalinga,lkn huwa nafanya uhakiki kabla sijaleta kitu hapa na nilichosema kuhusu harakati za mwenzetu na kugombea ubunge Kyela ni kweli tupu!

Labda ambacho sikueleweka ni kutumia tamathali za semi niliposema "Mwakalinga aingia Kyela" ukweli ilikuwa hajafika Kyela phyisical lkn "kiroho" tayari huyu jamaa alikuwa Kyela muda mrefu!

Jasusi,kuanzia tarehe 1 hadi 5 mwezi August mwaka 2009,uwepo hapa ambako nitakuletea habari moja kwa moja toka ama kiwanja cha Mwakangale-Kyela mjini,au kutoka kule kijijini Katumba ambako labda rasmi mbio za kuwania ubunge Kyela zitakapotangazwa kuwa ndiyo zinaanza!

Mkuu Heshima mbele sana,

- Kwa taarifa yako ni kwamba muda mchache uliopita ndio kwanza finally, George amefika Kyela kwa gari akitokea Dar, ambako alikuwepo jana baada ya kumaliza matembezi yake ya likizo kwenye mbuga za wanyama, Arusha na nyumba za makumbusho Zanzibar.

- Amekwenda Kyela, yaani nyumbani pamoja na mengine ni kusalimia familia yake na kupumzika kidogo kwa angalau wiki moja, kabla hajaondoka kuelekea Dar na mwishowe UK, anaikoishi na kufanya kazi na familia yake, yaani mke na watoto wake.

- Tunajaribu kuwa on top of this ishu kuepusha majungu tu, nothing of a big deal kuwepo kwake Kyela na likizo yake nzima kwa ujumla. Ya kugombea ubunge ni mpaka yeye mwenyewe atakaposema wazi kama kweli anayo hiyo nia, kitu ambacho sio kuvunja sheria ya Jamhuri kama tunavyotaka kuaminishwa na baadhi ya wenzetu hapa, kama ambavyo pia sio a crime kuwepo huko Kyela kiroho as you reported before, au?

Respect.

Kamanda FMeS!
 
Mchukia Fisadi said:

Mpita njia swala hili nilimuuliza mimi na naona anakujibu wewe. Nilijua huyu au anazungumza asichokijua kwa ushabiki wa Yanga na Simba au katumwa aseme PR hapa.
Ni vema katubu na kusema ukweli wote.

Kwa sababu hiyo naomba achangie mengine lakini kwa habari ya Zito anyamaze. Asidandie treni:Dataaibika bure.
Kwa taarifa yake Tanzania Yote shida zetu ni moja hata kama mbunge mnalala naye chumba kimoja:( Maana hakuna duka la mbunge peke yake. Hakuna barabara ya mbunge peke yake na hakuna maji ya mbunge peke yake. Hakuna umeme wa mbunge peke yake. Nk,nk,nk,nk,nk,nk.



Mchukia Fisadi,

..unachozungumza ni nadharia zaidi kuliko reality on the ground.

..halafu unaongea kwa hasira hasira sana. punguza jazba.

..Mpita Njia amenielewa na tunasonga mbele.
 
Wakulu heshima mbele sana,

- Naomba kusema hivi, Zitto ni mwanasiasa kijana sana, ambaye msimamo wake kisiasa kwa taifa letu, lilifikia kutufanya wananchi wengi kumuweka kwenye level ya juu mno na hata kumfungia nafasi ya kughafirika kiuongozi knowing kwamba ni kijana sana na siasa za taifa, amekuwa akisema maneno mengi mazuri kulingana na masilahi yetu wananchi na kwa muda mrefu sana, mpaka pale alipokubali kuwemo kwenye kamati ya rais ya madini na pale aliposema Dowans ni safi wengi tukashindwa kumuelewa na tumeishia kumuhukumu sana unfairly kwa kukosa hard facts against his words and actions as a leader,

- Ninaamini kwamba kama kuna some political missstep, alizifanya either innocently as a human being na kushindwa kuisoma political situation ya the times, au Zitto simply ni arrogant. I mean kwamba after all Mwakyembe´s report on Richmonduli isingekua rahisi politically kutu'convince wananchi kuwepo kwa anything positive au beneficial kwa taifa coming out of anything associated with Rostam, au Lowassa as of Dowans, na the fact kwamba our sitting president hajaonyesha seriousness ya ku'solve kero zinazotusumbua wananchi zaidi tu ya kutuhadaa all the times kwamba anazijua na kuzijua tu, yalikuwa ni makosa makubwa sana politically kwa Zitto kukubali kujiunga na kamati ya rais pamoja na support yake kwa Dowans, the timing was wrong on his part,

- Ingawa CCM knew what they were doing yaani they were neutralizing him kisiasa na itworked, Zitto should have know better kwamba haiwezekani one day CCM wakakufukuza bungeni kwa sababu ya ishu ya madini, ukafanya maandamano yaliyo li-freeze taifa kule Jangwani halafu the following week hao hao CCM wakakuita kwenye kamati ya madini tena kwa nia njema, that was a political naivette´ on Zitto decision kukubali wito huo, it was simply wrong na ndipo alipoanza kuwashitua wananchi wengi kama he was for real kama alivyokuwa amejijenga mwanzoni, siasa kama sheria ni historia Zitto alipaswa kusoma alama za nyakati kwamba last time Kolimba alifanyiwa kama yeye, alipopingana nao walimpa kazi lakini ghafla akafariki labda hapa Zitto ana bahati hiyo tu kwamba ni mzima mpaka leo pamoja na kukubali kwake kama Kolimba.

- Naomba kwa nia njema kumwambia Mheshimiwa Zitto, ambaye ninamheshimu sana as a leader kwamba ajaribu sana kuirudisha the lost trust na sisi wananchi wengi ambao tulikuwa tunamuaminia sana huko nyuma, bado ni kijana na siku zote kuna room ya kukosea na kurudi kwenye mstari, otherwise ninamtakia kazi njema na uongozi wa taifa letu na bado imani ipo ingawa imejeruhiwa, kwa sababu no matter what siwezi kumlinganisha na the Serukambas.

Respect.

Kamanda FmES!
 
Mpita Njia,


NB:

..habari kwamba Zitto amelitekeza jimbo lake zilianza kutolewa na waziri mkuu Pinda bungeni.

..vilevile kuna mchangiaji wa jamii forums namheshimu sana naye alidai mambo jimboni kwa Zitto siyo mazuri.
kwani ulitegemea pinda aseme vinginevyo

eti mambo ya buzwagi, kwani hawajui kwamba mapato ya nchi yanakusanywa pamoja alafu ndiyo yanagawiwa, ingekuwa si hivyo headquaters za makampuni kibao zipo dar na kodi ingewanufaisha wa dar tuu
 
Wana JF,

Naomba nimtetee Malafyale si kwa sababu ni chief (Omutwale) mwenzangu bali kwa sababu nipo hapa chunguni nikioanisha habari za magazetini juu ya Zitto na jimbo lake dhidi ya uhalisia.

Niko hapa Kigoma kwa siku kadhaa. Kuna kila ishara kwamba Zitto ametegwa na akategeka kwa mara nyingine tena na kuonekana si kitu wala chochote kama mtetezi wa wanyonge/wapiga kura. Ni hivi wakati wa ulipaji fidia kupisha ujenzi wa hii barabara ambayo Pinda amekuja kuizindua, nyumba ya Zitto iliyo Manyovu haikuwemo kabisa na wala barabara ilikuwa haiigusi nyumba ya Zitto. Ila kwa sababu za kisiasa wakaamua na nyumba ya Zitto ipitiwe na aingizwe kwenye orodha ya watakaofidiwa. Labda Zitto alifikiri hapa alikuwa anatendewa haki hata kabla ya kuiomba au kuidai, lakini ukweli wa mambo sivyo! Zitto alikuwa anachonganishwa na wapigakura. Zitto amelipwa hela stahili kwa nyumba yake. Malipo yake yako juu maradufu zaidi ya nyumba (naviita vibanda) vya majirani na wapigakura wake. Elimu ndogo ni tatizo, wananchi wanashindwa kuona tofauti kati ya thamani ya nyumba kama ya Zitto na zile zao za udongo na makuti. Na hapa ndipo wazee wa ku-take advantage tayari wamepata point ya nyongeza kumsulubu Zitto kwa wapigakura. Na hii point nakuhakikishia kwa hakika tayari imembomoa Zitto kwa kiasi kikubwa maeneo ambako barabara inapita na kumefanyika hamishahamisha/bomobomoa.

Enewehi, maadamu Zitto ni Mbunge wa kitaifa na kwa sasa kuna kila dalili kuwa amekubali kugombea tena basi na aitekeleze ile Plan B (Jimbo ndani ya Jiji Kuu)
 
Kigoma kama wameshamchoka- basi agombee mji wowote mkubwa (Dar, Ar n.k)..atapata ili aweze kuangalia matatizo ya kitaifa kwa uhuru zaidi!
 
Mkuu Heshima mbele sana,

- Kwa taarifa yako ni kwamba muda mchache uliopita ndio kwanza finally, George amefika Kyela kwa gari akitokea Dar, ambako alikuwepo jana baada ya kumaliza matembezi yake ya likizo kwenye mbuga za wanyama, Arusha na nyumba za makumbusho Zanzibar.

- Amekwenda Kyela, yaani nyumbani pamoja na mengine ni kusalimia familia yake na kupumzika kidogo kwa angalau wiki moja, kabla hajaondoka kuelekea Dar na mwishowe UK, anaikoishi na kufanya kazi na familia yake, yaani mke na watoto wake.

- Tunajaribu kuwa on top of this ishu kuepusha majungu tu, nothing of a big deal kuwepo kwake Kyela na likizo yake nzima kwa ujumla. Ya kugombea ubunge ni mpaka yeye mwenyewe atakaposema wazi kama kweli anayo hiyo nia, kitu ambacho sio kuvunja sheria ya Jamhuri kama tunavyotaka kuaminishwa na baadhi ya wenzetu hapa, kama ambavyo pia sio a crime kuwepo huko Kyela kiroho as you reported before, au?

Respect.

Kamanda FMeS!

Heshima yako mkuu FMeS!

Kwa bahati nzuri mimi binafsi ninatokea Kyela makazi yangu ya kudumu yapo Kyela,tena kama haitoshi natokea kijiji cha Katumba-songwe nyumbani kwa George Mwakalinga na dakika si zaidi ya 15 kwa usafiri wa Baiskeli kuelekea kijiji cha Ngonga-Mwangupili nyumbani kwa Dr Mwakyembe!Kwa kifupi nawajua sana wapambanaji hawa.

Mwakalinga atagombea ubunge Kyela na hili nina uhakika wa asilimia zaidi ya 100,na Mwakalinga ni more than smarter hasa kwa umakini wake wa kuchagua timu yake ya kampeni ambayo itakuwa imesheheni wasomi,makada na watu wa kawaida lkn wazawa waliopo ndani na nje ya tz!

Ilikuwa atangaze nia yae ya kugombea si kabla ya tarehe 5 august,lkn bado hatujajua kama utangazaji huu utafanyika Kyela mjini au ktk moja ya viwanja vya shule kule Katumba au mahali pengine popote,na tutawajulisha lini shughul hii itafanyika!na hata kama kahairisha kutangaza kwa sababu ya Upepo wa kisiasa napo tutawafahamisha!

Lkn kumtoa Dr Mwakyembe ndani ya kura za maoni si kazi haba kwani mbunge huyu kwenye baadhi ya kata anachukuliwa kama 'mungu mtu'na yeyete anayepanga hata kumbishia kitu huchukuliwa kama mhaini!,kwa hiyo mpiganaji Mwakalinga anatakiwa afanye kazi ya ziada!

Yetu macho na mimi kama mpiga kura hai wilayani Kyela nitamsubiri yeyote kati yao atakayepitishwa na CCM tupambane nao kwenye sanduku la kura;kati yao hamna mwenye hati miliki ya ubunge wa jimbo la Kyela!
 
Malafyale uliandika:
icon1.gif
Mwakalinga Awasili Kyela Kumuangusha Dr Mwakyembe
George Mwakalinga mwana Kyela aliyekuwa anaishi na kufanya kazi kama mtaalaum wa kompyuta nchini UK amewasili Kyela majuzi na tayari ametangaza kuwania ubunge wa wilaya ya Kyela ndani ya CCM!

Mwakalinga ametoka kuongea na wana Kyela sasa hivi kwenye hotel ya kisasa ya Sativa na watu waliokuwepo hapo wanasema hapana shaka Mwakalinga kaletwa Kyela na vigogo ndani ya CCM na serikalini na dhahiri anaungwa mkono na mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mzee Mwakalinga na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Japhet Mwakasumi!

Mwakalinga,ambae pia ana vitege uchumi vingi sana wilayani Kyela zikiwemo hotel kubwa za kisasa tayari yupo Kyela,na kaanza kuzunguka kwa kasi vijijini kujinadi kwa wana CCM na kuna kila ukweli kuwa viongozi wa CCM wilayani na mkoani wamebariki kuanza huku kwake kampeni kabla ya muda wake.

Maelezo yako yanaonyesha wazi kabisa kuwa Mwakalinga alikuwa Kyela. Sasa hata kuhutubia na kuzunguka vijijini ALIZUNGUKA KIROHO?

Ndiyo maana MNAMUOGOPA namna hiyo maana jamaa anatumia hadi ROHO kuja kuhutubia na kuzunguka vijiji vya Kyela. Sasa akija yeye mwenyewe kuhutubia na kuzunguka, mtu chali.

Mkuu, nilifikiri walau huwa una elements za aibu.
Kwa kuona hilo tu, naanza kuona mkuu utakuwa mtu hatari sana kusikilizwa na kufuatwa, kwani waweza fanya jambo bila aibu wala huruma kwa mtendwa.

Nawahurumia hao WAZUNGU wa watu unaopeleka Tanzania.

Mkuu, umeshakuwa kama saa mbovu. Najua kuna siku utasema kweli. Ila sintajihangaisha sana kufahamu hiyo siku. Heri niamini kuwa, wee ni saa mbovu.
Ndimi Sikonge, mshiriki mwenzio wa KIROHO, Moravian Church.
 
mtoa habari ni mnafiki na kada wa CCM.u got the wrong place to lie dude.go find somewhereelse.wanaJF wote ni wasomi and they know wots goin on..so dont just copy and paste some nonsense issues that we dont need to hear unless u have some solid proof....
 
Politikisi za Tanzania ndivyo zilivyo. Tutaendelea hivyo hivyo hadi tukishaanza kuchinjana kama Rwanda ndipo tutajua kuwa utaifa ni wa muhimu zaidi na kuanza kujijenga tena. Nampa hongera dada yetu Irene Uwoya aliyeamua kuhamia Rwanda kwa vile alijua wazi kuwa radi haipigi mara mbili.
 
Kuna madai kwa wananchi wa jimbo la Kigoma Kaskazini hawana imani na Mbunge wao, Kabwe Zitto hivyo huenda atalazimika kufanya kazi ya ziada ili abaki kwenye nafasi hiyo.

Inadaiwa kuwa, wapiga kura jimboni humo hawana imani na Zitto kwa kuwa tangu achaguliwe mwaka 2005 hajawasaidia.

Wapiga kura hao wametoa maelezo hayo walipozungumza waandishi wa habari kutoka chama cha waandishi wa Habari mkoa Kigoma waliokuwa wakifanya ziara ya mafunzo kwa vitendo katika vijiji mbalimbali vya jimbo hilo wakati wa mafunzo yao ya uandishi wa Habari za vijijini yaliyofadhiliwa na baraza la Habari Tanzania (MCT).

Wamesema,tangu Zitto achaguliwe mwaka 2005 kuwawakilisha bungeni,hawajawahi kumuona hata mara moja wakimaanisha kwamba, hajawahi kuwatembelea kusikiliza shida zinazowakabili, na pia hakwenda kutoa shukurani kwa kumchagua kuwa Mbunge wao.

Mkazi wa kijiji cha Bitale, Muyera Yahya amewaeleza waandishi wa habari kijijini hapo kuwa Zitto anapaswa kwenda na hoja nzito kuwashawishi wananchi wa kijiji hicho kumchagua tena kuwa Mbunge.

Yahya amesema, Zitto badala ya kwenda kufahamu matatizo yanayowakabili na kuhamasisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi, amekuwa akizungumzia hoja za Buzwagi ambazo hazina umuhimu wowote kwao.

Mkazi wa kijiji cha Chankabwimba, Kayla Mussa, amedai kuwa,hata katika ziara za viongozi wa kitaifa wa serikali Mbunge huyo hashiriki, viongozi hao wamekuwa wakiambatana na wabunge wengine akiwemo Mbunge wa jimbo la Kigoma mjini Peter Serukamba.

Hivi Karibuni Waziri Mkuu alifanya ziara mkoani Kigoma maalum kwa ajili ya kuweka mawe ya msingi ya ujenzi wa barabara za Mwandiga – Manyovu na Kigoma – Kidahwe kiwango cha lami, na katika ziara hiyo takribani wabunge wote mkoani Kigoma walihudhuria isipokuwa Zitto na Manju Msambya.

Sehemu kubwa ya Barabara hizo zinapita katika jimbo la Kigoma Kaskazini na kwa muda mrefu mbunge huyo alikuwa akisema kuwa yeye ndiye aliyepigia debe hadi serikali kutafuta fedha kwa ajili ya miradi hiyo.

Wakati akiwa katika ziara hiyo,Waziri Mkuu alishangaa kutomuona mbunge wa jimbo la Kigoma kaskazini ,Zitto kwa kuwa miradi hiyo ipo jimboni kwake, wabunge wengine wa mkoani humo walihudhuria.

Waziri Mkuu alisema, kama ni bungeni hata yeye alikuwa huko na wabunge wengine alioambatana nao walitoka bungeni Dodoma hivyo alishangaa kwa nini Zitto hakuwapo na akahoji kama suala hilo halimuhusu.

Hivi karibuni, Pinda alimweleza Zitto bungeni kuwa, kama anataka kuendelea kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini itabidi afanye kazi ya ziada.

sijaelewa hiyo sehemu niliyopigia mstari.Kuna kura ya maoni iliyoendeshwa kuhakiki hilo?by the way Habari Leo is not a source i can trust when it came to issues za wabunge wasio wa sisiemu..ndaga fijo malaflaye
 
Hao jamaa wa kigoma tuwasamehe tu bure. Hawajui kuwa akitetea maslai ya taifa ni moja kwa moja pia jimboni kwao wataguswa? Nimemkumbuka Mzee Mwanakijiji na ile makala yake ya seti, kwamba hatuangalii seti kubwa inayoutuunganisha, tumebase kwenye viji-seti vidogo vidogo ambavyo si msingi wenyewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom