Malafyale
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 13,813
- 11,126
Kuna madai kwa wananchi wa jimbo la Kigoma Kaskazini hawana imani na Mbunge wao, Kabwe Zitto hivyo huenda atalazimika kufanya kazi ya ziada ili abaki kwenye nafasi hiyo.
Inadaiwa kuwa, wapiga kura jimboni humo hawana imani na Zitto kwa kuwa tangu achaguliwe mwaka 2005 hajawasaidia.
Wapiga kura hao wametoa maelezo hayo walipozungumza waandishi wa habari kutoka chama cha waandishi wa Habari mkoa Kigoma waliokuwa wakifanya ziara ya mafunzo kwa vitendo katika vijiji mbalimbali vya jimbo hilo wakati wa mafunzo yao ya uandishi wa Habari za vijijini yaliyofadhiliwa na baraza la Habari Tanzania (MCT).
Wamesema,tangu Zitto achaguliwe mwaka 2005 kuwawakilisha bungeni,hawajawahi kumuona hata mara moja wakimaanisha kwamba, hajawahi kuwatembelea kusikiliza shida zinazowakabili, na pia hakwenda kutoa shukurani kwa kumchagua kuwa Mbunge wao.
Mkazi wa kijiji cha Bitale, Muyera Yahya amewaeleza waandishi wa habari kijijini hapo kuwa Zitto anapaswa kwenda na hoja nzito kuwashawishi wananchi wa kijiji hicho kumchagua tena kuwa Mbunge.
Yahya amesema, Zitto badala ya kwenda kufahamu matatizo yanayowakabili na kuhamasisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi, amekuwa akizungumzia hoja za Buzwagi ambazo hazina umuhimu wowote kwao.
Mkazi wa kijiji cha Chankabwimba, Kayla Mussa, amedai kuwa,hata katika ziara za viongozi wa kitaifa wa serikali Mbunge huyo hashiriki, viongozi hao wamekuwa wakiambatana na wabunge wengine akiwemo Mbunge wa jimbo la Kigoma mjini Peter Serukamba.
Hivi Karibuni Waziri Mkuu alifanya ziara mkoani Kigoma maalum kwa ajili ya kuweka mawe ya msingi ya ujenzi wa barabara za Mwandiga Manyovu na Kigoma Kidahwe kiwango cha lami, na katika ziara hiyo takribani wabunge wote mkoani Kigoma walihudhuria isipokuwa Zitto na Manju Msambya.
Sehemu kubwa ya Barabara hizo zinapita katika jimbo la Kigoma Kaskazini na kwa muda mrefu mbunge huyo alikuwa akisema kuwa yeye ndiye aliyepigia debe hadi serikali kutafuta fedha kwa ajili ya miradi hiyo.
Wakati akiwa katika ziara hiyo,Waziri Mkuu alishangaa kutomuona mbunge wa jimbo la Kigoma kaskazini ,Zitto kwa kuwa miradi hiyo ipo jimboni kwake, wabunge wengine wa mkoani humo walihudhuria.
Waziri Mkuu alisema, kama ni bungeni hata yeye alikuwa huko na wabunge wengine alioambatana nao walitoka bungeni Dodoma hivyo alishangaa kwa nini Zitto hakuwapo na akahoji kama suala hilo halimuhusu.
Hivi karibuni, Pinda alimweleza Zitto bungeni kuwa, kama anataka kuendelea kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini itabidi afanye kazi ya ziada.