Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Zitto, natanguliza pole kwa yatakayofuata kwenye thread hii.

Unaanguliza pole kwa ripoti ya gazeti la Uhuru! Angalia source kwanza ya habari hiyo kabla ya kutanguliza pole; mimi natoa pole kwa CCM maana kama wanakuzali sifa za Zitto basi ujue wamelewa mchana kweupe.
 
Tumeshindwa kufikiri hata kwa upeo wa elimu ya shule zetu za sekondari za Kata na kugundua kuwa walioleta habari hii ya kipuuzi ni Gazeti la CCM-linaloitwa Uhuru?

Sasa kama tumeshindwa kugundua kuhusu upupu wa chanzo hiki cha habari utakuja kung'amua nini kingine kisichofaa ktk maisha yako wewe mwenzangu MTZ uliyewekwa pembeni kwenye kuufaidi uchumi wa nchi hii?Kweli CCM siku hizi ni wahuni kabisa!

Uhuru muajirini mhariri Mkumbwa azidi kuwaombea kura za huruma kwa wanainchi mnaowatelekeza kwa miaka 5 na kuja kuwakaumbuka hadi kukaa nao kwenye mavumbi wakati wa kampeni!
 
23 September 2010
Na waandishi wetu

kabwee_fr.jpg

WAKATI kampeni zikipamba moto, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, amekiri serikali ya CCM imejenga uchumi imara. Amepongeza utendaji kazi wa serikali za CCM na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi.

Zitto anayewania ubunge Kigoma Kaskazini, alisema hayo juzi jioni katika Uwanja wa Mashujaa, alipomnadi mgombea ubunge wa Mtwara Mjini, kwa tiketi ya chama hicho, Jetha Othuman. Akizungumzia mafanikio ya serikali ya CCM, Zitto alimmwagia sifa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, akisema amefanya mambo makubwa katika uongozi wake na kama kuna makosa ni ya kibinadamu.

“Hakuna anayeweza kila kitu kama yapo yaliyomshinda huo ni ubinadamu,” alisema Zitto na kuongeza kuwa, uchumi imara uliwezesha kushuka kwa mfumko wa bei. Aliwaponda watu wanadai serikali ya CCM inabagua wapinzani, akisema imekuwa ikitekeleza Ilani kwa kufikisha maendeleo hata kwenye maeneo yanayoshikiliwa na wapinzani.

“Wanaosema serikali ya CCM inabagua katika kugawana keki ya taifa hao ni waongo, imefikisha maendeleo hata kwa wapinzani,” alisema huku akitoa mfano wa maendeleo yaliyofanyika katika majimbo ya Karatu, Kigoma na Sumbawanga. Alisema Kigoma ni ngome ya upinzani, lakini imepiga hatua kubwa katika maendeleo, akitaja miradi mikubwa iliyotekelezwa ya barabara, maji na umeme.

Source: UHURU

Mmmmmmmmhh!!
Makubwaaaa hayooo!!!!
 
Zitto anasema palipo na ukweli

JEYKEYWAUKWELI;

Habari ambayo chanzo chake ni Gazeti la Uhuru chini ya Muongozo wa kiuandishi wa matakwa ya viongozi wa CCM HAIWEZI kuwa legitimate kwa wa TZ wasio na mapenzi ya chama hicho,maana habari zao huwa wanaipendelea CCM!

Kama Zitto angesema maneno hayo basi ndiyo ingekuwa imepamba kurasa ya magazeti yote ya jana/leo tofauti na sasa ambao ni Uhuru ya CCM tu wameripoti(Kama kweli)!

Kwa ufupi habari yako Jeykey hainunuliki,haina ukweli wowote,ni ya kisiasa na kwa hivyo basi na nimeitupilia mbali!
 
Hawa ndio watu wanaoomba kura za wa tz ili wapewe ridhaa ya uongozi!! Matusi na dharau kwao ni kitu cha kawaida hawa si ndio watakuja kutuacha kwenye mataa hawa! Tusiwape kura kabisa na tutahakikisha hata vile viti vyao vichache vya ubunge tunawanyanganya safari hii !!
 
aNGUKO LA SLAA LINAKUJA ZITTO MTU MAKINI SAANA KAONA MAFANIKIO YA JK
Hapa chini ulisema hivi
mPAKA SASA HIVI ZITTO ANATANGATANGA BAADA YA kuona kule kigoma atashidwa vibaya na mgombea wa CCM
Mbona umeweza kusoma? pole saana ndo ZITTO WENU ANAPOTEA HIVYO

Mkuu mbona unajichanganya hivyo! Unaposema mtu "anatangatanga" au "anapotea" hauwezi kusema huyo mtu ni makini.Post moja unaposema ni makini posts nyingine unasema sio makini inaonyesha jinsi gani hichi kiroba kilivyo kulemea.Jaribu kwenda pole pole labda unaweza kueleweka.
 
Mimi sijaona baya alilofanya Mheshimiwa Zitto.

"To get along with your opponents is not double faced, it is called GROWING UP!" (edited quote)
:playball:
 
Tusisahau kuwa uhuru ni chombo cha propaganda cha CCM, hainingii akilini Zito kuisifu CCM, uhuru wamechukua sentensi moja tu wakaitengeneza wanavyotaka wao, uhuru pamejaa wataalamu waliobobea kwa uwongo wengi wao wamesoma Urusi. Tuleteeni habari hiyo kutoka vyombo huru vya habari
 
zito alikuwa mtwara kwa mkapa na kuvuta hisia za waliokuwa wakimsikiliza asingeweza kumshambulia mkapa, hili la keki ya taifa aliwaondoa hofu kuwa eti wakichagua upinzani hawatapata maendeleo au mgao kutoka serikali ya ccm, akawapa mfano wa karatu ambako kuna upinzania lakini wapo mbele kuliko mtwara.

kuonyesha udhaifu wa kikwete ni lazima angezungumzia ukomavu wa mkapa

mmesahau pareto theory? you canot talk of youself being better bila kumpaka matope mwingine
 
True freedom must be expressed through the human ability to think critically, to analyze and to make informed decisions about oneself, his society and the world - Sidanganyiki2010
 
Aliyekuwa mbunge machachali Mh Zitto kabwe alielekea kupozteza tunu yake kwa taifa
mwaka 2006-7 kila mwannchi alimjua zitto lakini sasa hivi zitto kapotea kwnye vuchwa vya wananchi,

Je zitto ndo anapotea kama mrema ?
 
Aliyekuwa mbunge machachali Mh Zitto kabwe alielekea kupozteza tunu yake kwa taifa
mwaka 2006-7 kila mwannchi alimjua zitto lakini sasa hivi zitto kapotea kwnye vuchwa vya wananchi,

Je zittu ndo anapotea kama mrema ?

hakuna mtu anayeitwa zittu kwenye siasa za Tanzania
 
Aliyekuwa mbunge machachali Mh Zitto kabwe alielekea kupozteza tunu yake kwa taifa
mwaka 2006-7 kila mwannchi alimjua zitto lakini sasa hivi zitto kapotea kwnye vuchwa vya wananchi,

Je zittu ndo anapotea kama mrema ?
Hebu kaa pembeni kama huna vitu vya maana vya kujadili. Huu ni uzushi na uzandiki.
 
Na wakitaka kuona jinsi gani chadema inaanguka wacheze na zitto

lile ndio jiwe pekee ambalo linaifanya chadema in'gare
 
Aliyekuwa mbunge machachali Mh Zitto kabwe alielekea kupozteza tunu yake kwa taifa
mwaka 2006-7 kila mwannchi alimjua zitto lakini sasa hivi zitto kapotea kwnye vuchwa vya wananchi,

Je zitto ndo anapotea kama mrema ?

Dua la Kuku
 
Na wakitaka kuona jinsi gani chadema inaanguka wacheze na zitto

lile ndio jiwe pekee ambalo linaifanya chadema in'gare

Sio kweli kuna vijana wanaompiku Zitto si tu kwa kujenga hoja na kuzitetea bungeni bali wanampiku hata kielimu mmoja wao ni Halima Mdee!! Sasa wameingia wengine wengi tu mjengino!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom