Elections 2010 Zitto amlipua RC, DC Kigoma

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
Leonard Mubale na Richard Katunka, Kigoma

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Joseph Simbakalia na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, John Mongela kutowashinikiza wananchi wachague viongozi wa kisiasa wanaowataka.

Badala yake, Zitto ametaka viongozi hao wa serikali kuacha wananchi wenyewe wafanye maamuzi wenyewe ya kumpata kiongozi bora.

Akizungumza katika kampeni za ubunge Jimbo la Kigoma Kusini juzi, Zitto alisema wakuu hao wa serikali kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitumia madaraka yao kuwashawishi wananchi wawachague viongozi wanaowataka wao.

Katika mkutano huo, uliofanyika kwenye viwanja vya Communte Mwanga mjini, Zitto alisema tabia hiyo ni mbovu kwa kuwa inadumaza demokrasia nchini.


"Kila siku mkuu wa mkoa akiwa na gari la serikali yuko ofisi za CCM..., mbona haji na gari lake ofisi za Chadema?.
“Watuachie wilaya na mkoa wetu wala wasitugawe kwa misingi ya udini, waje wafanye kazi zao na wasituingilie,” alisema Zitto.

Huku akiwa anashangaliwa na umati uliokusanyika uwanjani hapo, Zitto alisisitiza; "hapa ni kwetu na sisi ndio wenye uchungu wa mji wetu watatuchaguliaje nani awe mbunge na nani awe diwani. Nina uwezo wa kufuata na kuwaeleza ana kwa ana ila nataka waelezwe na wapambe wao," alisema.

Katika mkutano huo, Zitto alimnadi mgombea ubunge wa Chadema Ally Khalfani Mleh na kuwaomba wakazi wa jimbo hilo, kumchagua ili awe mbunge wao.

Alisema endapo mgombea huyo wa Chadema atachaguliwa, ataongeza nguvu kwa wabunge wa upinzani bungeni.
Katika hatua nyingine, mgombea ubunge huyo, alisema endapo atachaguliwa atahakikisha anashirikiana na uongozi wa manispaa kurejesha hadhi ya manispaa hiyo.

Mleh ambaye ni mchumi kitaaluma, alisema kwa kipindi chote ambacho CCM imekuwa ikiongoza jimbo hilo, maisha ya wakazi wake hususani vijana na kina mama yamezidi kuwa magumu kila kukicha.

"Mkinichagua mikakati yangu ya awali kabisa ni kukutana na makundi ya vijana na kinamama na kujadili matatizo hayo kwa lengo la kuyapatia ufumbuzi," alisema.

Chanzo: Zitto amlipua RC, DC Kigoma
 
zitto is right, huyo mongella na simbakalia wanakosea kupendelea upande mmoja....
 
Nafsi zao zinawatesa, maana ni makada wa CCM. Tatizo lingine ni upeo wa hao viongozi wa serikali, fikra na mitizamo yao ni ya mwaka 47. Hawajui kuwa wananchi sasa hivi hawadanganyiki.

Kama CHADEMA ingekuwa inatumia rasilimali za serikali mbona CCM wangekuwa kama mbogo.

Mwisho wao umeshafika, hivyo ni lazima watapetape kama mfa maji
 
Aidha mwandishi kamnukuu Zitto vibaya au Zitto kakosea kimsingi. Kasema kweli wakimchagua mgombea wa CHADEMA watakuwa wameongeza nguvu ya upinzani bungeni? CHADEMA inagombania kuwa chama tawala wakati huu, sio kukaa upinzani. Upinzani watakaa CCM kipindi hiki.

We must believe in what we are doing.
 
Watuachie wilaya na mkoa wetu wala wasitugawe kwa misingi ya udini, waje wafanye kazi zao na wasituingilie,
Sielewi hapa kama Zitto anawakatalia wengine ubaguzi kwa misingi ya dini lakini yeye mwenyewe anautenda kwa misingi ya asili ya mtu anakotoka?

Na kauli hii inanitisha:

hapa ni kwetu na sisi ndio wenye uchungu wa mji wetu watatuchaguliaje nani awe mbunge na nani awe diwani

Ni jambo moja kuwakatalia Simbakalia na Mongella kwa misingi ya ofisi zao lakini ni jambo jingine kabisa kuwakatalia kwa misingi ya asili ya mahali wanakotoka. Asije kujijengea mazingira ya kufunguliwa kesi ya kukiuka sheria ya uchaguzi... He need to be ultra careful.
 
Sielewi hapa kama Zitto anawakatalia wengine ubaguzi kwa misingi ya dini lakini yeye mwenyewe anautenda kwa misingi ya asili ya mtu anakotoka?

Na kauli hii inanitisha:



Ni jambo moja kuwakatalia Simbakalia na Mongella kwa misingi ya ofisi zao lakini ni jambo jingine kabisa kuwakatalia kwa misingi ya asili ya mahali wanakotoka. Asije kujijengea mazingira ya kufunguliwa kesi ya kukiuka sheria ya uchaguzi... He need to be ultra careful.
Kama nakuelewa ila kama sikuelewi vile, for the second time, kama una kumbukumbu nzuri!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom