Zitto amkanya ndugu Jussa!

Nimshauri zito angepambana kumaliza kero za wananchi wa jimbo lake kwanza kwani wanahitaji zaidi ya walichonacho badala ya kuingilia ndoa za watu...mambo ya akina jusa na cuf yanamuhusu nini? this is crappp
 
[h=1]Salaam Za Mheshimiwa Zitto Kabwe(Chadema) Kwa Mbunge Wa CUF ismail Jussa Juu Ya Kuvuliwa Uanachama Mbunge Wa CUF Hamada Rashid .[/h]Posted on January 5, 2012 by admin
Reply
6245606932_eab4593195_z.jpg

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Kabwe
–
Ndugu Jussa, Kama rafiki yako mkubwa na unajua ninavyomheshimu Maalim Seif Kama kiongozi thabiti.Leo nakwambia usilolipenda. Sio sahihi katika demokrasia Kama yetu kumfukuza Mbunge Hamad Rashid au hata wanachama wengine wa chama chenu cha CUF.

Kama Maalim aliweza kumsamehe Salmin, aliweza kumsamehe Karume, aliweza kukubali kutangazwa kushindwa ilhali hata wewe unajua alishinda Urais wa Zanzibar iweje iwe muhali kumaliza tatizo hili dogo la Hamad Rashid? Hamad ana makosa lukuki. Nimefanya naye kazi Bungeni. Hamad pia ana mazuri mengi kafanya. Hamad amejitoa muhanga. Uamuzi wa Baraza Kuu la CUF kumfukuza uanachama ufikiriwe upya. That is my appeal to you as a friend and a fine politician

Zitto Kabwe(MB)
 
Nafikiri Zitto inambidi afikirie vingine.

CUF nafikiri ni chama tofauti sana na ni chama cha wananchi sio cha watu wacheche ambao wanakuwa na hisa kama Chadema.

Kufukuzwa kwa hamad Rashid sio jambo geni. Kwani walishawahi kufukuzwa watu maarufu kuliko Hamad rashid, akina Naila Jidawi, Mapalala na Msabaha n.k.

Kinachofuatwa ni haki na sio upendeleo.

Sio kama ulivyo fanyiwa wewe mizengwe uliyowekewa wewe ulipotaka kugombea uenyekiti wa taifa chadema.

Wewe madevu utatuambia nini na chama chako chenye hulka ya kujitoa muhanga?kama we mwenyewe?Kumbe unajua kuwa Zitto aligombea uenyekiti na kisha akafanyiwa zengwe,vipi leo Hamadi atangaze nia ya kugombea ukatibu wakati ukifika afukuzwe?Mara ngapi Shibuda ametofautiana na maoni ya chama lkn wamemwacha wanasubiri wakati mwafaka,nendeni tu kuswali msikitini
 
Kwakuwa CUF wametumia sh.500 milioni katika wilaya 10 za zanzibar kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2010,

Na kwakuwa CUF wametumia sh.70 milioni katika wilaya 123 za Tanzania bara na zenye eneo kubwa sana kijiografia ukilinganisha na Zanzibar.

Ni dhahiri kwamba kama cuf ni chama cha wananchi, bila shaka ni chama cha wananchi wa zanzibar.

Je unaweza kulinganisha na CHADEMA.

Je Chadema unajua walitumia kiasi gani katika mikoa ya kaskazini na lake zone ukilinganisha na sehemu za pwani kama Mtwara , Lindi, na Pwani. Na vile vile Zanzibar?

Kwa mantiki hiyo unaweza kusema Chadema ni chama cha kikanda (kaskazini na lake zone).

Vipi hapo?

 
Wewe madevu utatuambia nini na chama chako chenye hulka ya kujitoa muhanga?kama we mwenyewe?Kumbe unajua kuwa Zitto aligombea uenyekiti na kisha akafanyiwa zengwe,vipi leo Hamadi atangaze nia ya kugombea ukatibu wakati ukifika afukuzwe?Mara ngapi Shibuda ametofautiana na maoni ya chama lkn wamemwacha wanasubiri wakati mwafaka,nendeni tu kuswali msikitini

Pole sana.

Mbona siku hizi hakuna maandamano? au ndio pengo aliwazuia.

je umemsikia Kilaini akimkemea Job ndugai.

Pole sana.

 
ZITTO NI NANI??HILI JINA SIO GENI MWENYE KUMJUA TAFATHALI.NI MWANACHAMA WA CHAMA GANi??
 
Nyerere wakati anakosoa chama chake hakufanya hivyo akiwa na lengo la kugombea nafasi yeyote ndani ya chama chake, tofauti na HR, ametoa hutuma dhidi ya Katibu wake mkuu akiwa na sababu nyuma yake ya kutaka kushika nafasi ya ukatibu mkuu. Katika siasa hii ni tofauti kubwa sana.

kwani ni dhambi kwa Hamad Rashid kuutaka ukatibu mkuu??ye ametoa mapungufu ya Maalim,na kwa mapungufu ayo ndio maana anautaka ukatibu..angekuwa anataka kumpindua ilo lingekuwa suala jingine.
 
Pole sana.

Mbona siku hizi hakuna maandamano? au ndio pengo aliwazuia.

je umemsikia Kilaini akimkemea Job ndugai.

Pole sana.


kama mnafikiri mtairudisha Znz mikononi mwa sultan wa Oman,ni ndoto za mchana!
 
Kufukuzana uanachama kumefanyika kwa vyama vyote kuanzia CCM, Chadema, NCCR, na sasa CUF

Tunaikula hasara ni wananchi kwa kugharamia chaguzi kila leo, kwa maamuzi ya wachache kwenye vyama

Haya ndo matatizo ya CHAMA KUSHIKA HATAMU badala ya WANANCHI KUSHIKA HATAMU. Wananchi wanachagua mbunge, chama kinampiga chini kwa kumfukuza uanachama. Tunataka tuwe na mgombea binafsi haraka sana ili wananchi tunapofanya maamuzi yasivurugwe na wachache kwa kutukomoa kumuondolea uanachama. Tatizo tulipopigania Mgombea binafsi CCM walidhani ni hoja ya upinzani, wakamtisha Augustino Ramadhani akatoa Hukumu ya kitoto kukandamiza haki za wananchi. Sasa hivi Serikali imefilisika, haitaki kufanya chaguzi ndogo inaona gharama ni kubwa. Tendwa kageuka msemaji wa Serikali kuvibembeleza vyama visiendelee kufukuza wabunge, si ajabu ndo maana mafisadi wa ccm wanakubatiwa kuogopa chaguzi ndogo.
 
Igeni uvumilivu wa Chadema na Shibuda

Duh! CDM Ijicheki ktk suala la Shibuda; Jamaa anapinga hadi ilani ya uchaguzi ya chama na bado analelewa tu; Akifika 2015 Shibuda atataka kugombea urais au ACHAFUE HALI YA HEWA NDANI YA CDM. it wont be good for CDM
 
Hekima kwenye maslah ya watu wapi na wapi? ukigusa masilahi ya wakubwa wako katika politics za bongo lazima wakung'oe
 
Zitto,
CUF ni kama vile unavyoiona ManU, Liverpool, Blackburn,...., hivi ni vilabu vya England lakini wamiliki wake sio WAINGEREZA. CUF sio ya WATANZANIA ingawa kuna akina Lipumba, Mtatiro,..., na umefanya vizuri kumwomba Jusa na sio Lipumba. Tafakari.
Mkuu hili nalo neno!
 
Zitto Kabwe
Ndugu Jussa, Kama rafiki yako mkubwa na unajua ninavyomheshimu Maalim Seif Kama kiongozi thabiti. Leo nakwambia usilolipenda. Sio sahihi katika demokrasia Kama yetu kumfukuza Mbunge Hamad Rashid au hata wanachama wengine wa chama chenu cha CUF. Kama Maalim aliweza kumsamehe Salmin, aliweza kumsamehe Karume, aliweza kukubali kutangazwa kushindwa ilhali hata wewe unajua alishinda Urais wa Zanzibar iweje iwe muhali kumaliza tatizo hili dogo la Hamad Rashid?

Hamad ana makosa lukuki. Nimefanya naye kazi Bungeni. Hamad pia ana mazuri mengi kafanya. Hamad amejitoa muhanga. Uamuzi wa Baraza Kuu la CUF kumfukuza uanachama ufikiriwe upya.

That is my appeal to you as a friend and a fine politician.
'Hamad anamakosa lukuki, nimefanya nae.............' a good politician?!! Jitazame kwanza ww zito then coment unachotaka coz ktk hili umeonyesha umebase upande upi........
 
Back
Top Bottom