Zitto amjia juu Waziri Mkuu: Aandika barua kuhoji matumizi ya "Stimulus Package"

je makampuni yaliyopewa pesa hizi hayana uhusiano na rostam, lowasa na chenge? tunaomba orodha yake hapa. ni matayarisho ya uchaguzi mkuu 2015? au zilishatumika uchaguzi wa 2010?
wanasiaisa waone huruma kwa maskini wa nchi hii. walaaniwe mafisadi
 
Waziri mkuu kadanganya bunge tena kwa mara nyingine. Kanuni za bunge zinasema achukuliwe hatua gani? .
 
Welcome back Zitto, baada ya magamba kuvuka ccm naona umerudi nyumbani. I fully support you katika kudai maelezo na ikiwezekana uwajibikaji. Usiridhike na maelezo hewa au ya hovyo hovyo, we need to know walitumiaje pesa zetu. Kama ilikuwa ni EPA nyingine this time we will fire them
 
Kama mimi niliyeko nje ya system ninajua kuwa taarifa ya CAG iko hewani wakati mkuu wa shughuli za bunge hajui, huyu kweli ni mwongo wa kimataifa.
Au atakuwa ***** kiutendaji
 
Inasikitisha sana kuwa na viongozi mabogasi wasiojali chochote. Watanzania sijui nini kitatufanya tufanye maamuzi ya pamoja kuking'oa hiki chama. Mimi nadhani watanzania walioko vijijini ndio wengi na wanachoamini hayo maisha wanayoishi ndio Mungu aliyowaandikia waishi, hawajui kuwa Mungu ameipa Tanzania kila aina ya utajiri, MAFUTA, MADINI YA KILA AINA, MAZIWA, MITO NA BAHARI, WANYAMA WA KUPENDEZA, NA ARDHI YENYE RUTUBA.

Kwa kweli inauma sana tunavyofanywa wajinga.

WANA JF TULIANZISHE. MIDDLE CLASS IKIAMUA KUFANYA MABADILIKO INAWEZA KUPAMBNA KWA NGUVU ZAO ZOTE.
 
Bravo Zitto, naomba isiishie hapo kama kuna utaratibu wowote wa kuwawajibisha hao wahusika tafadhalini hakikisheni wamewajibishwa. Na kama waziri mkuu atakuwa amelidanganya bunge tuwaombe wataalam wa vifungu vya sheria vichukue mkondo wake. na kama kiongozi mkuu alitakiwa awe amesoma hiyo taarifa ya mkaguzi wa mahesabu lakini kwa uzembe akawa hajausoma , awajibishwe pia.:disapointed:
 
Namshukuru mungu kwa kumrudisha jembe wetu kundini faida ya kuwa na zitto nkubwa kiasi chakutopimika nakupongeza sana jembe ila tizama usije kuteleza tena maana nilisikia jana wabunge wa ccm wakidai wanakuheshim sana na ukae pembeni uache wenje aonewe lakini nashukuru kwa moyo wako wakupigania wanyonge kaza but umma unakutegemea
 
CDM wanatakiwa kumshtaki kwa UMMA huyu mzee maana sasa uongo wake umezidi kiwango haiwezekani yeye kila wakati anasema uongo.Hawezi kuwafanya watanzania mataahira, haiwezekani PM asione ripoti ya ukaguzi wa hesabu za serikali.ina maana kazi yake ni nini, anakula kodi zetu bure huyu babu.
KWELI KAKA HAKA KAZEE KANA MATATIZO,YEYE KUTOKUISOMA RIPOTI YA MKAGUZI NI SAWA NA MAMA KUMSAHAU MWANAYE ANAYEMNYONYESHA,HUYU ATAKUWA MAMA MZEMBE KULIKO WOTE!! Kajiuzulu!!
 
Sielewi inakuwaje Mkuu wa nchi aagize taarifa ipatiwe PM na Waziri wa fedha from that date then PM aseme hana taarifa na hajaisoma? Yuko pale kutekeleza matakwa ya nani? Huyu kweli ni wa kuaminiwa kwamba atasimamia na kutekeleza maagizo ya mkuu wake na wananchi? Hakika nimeshindwa kuelewa uelewa wa PM na jibu lake kwa bunge na Mh Ztto! Inabidi awajibishwe huyu!
 
Fanyeni mpango nasi tunaotumia simu tuweze isome kwani tunaona mnachangia lakini hatujui(hakisomeki kwa kutumia simu) kilichoandikwa.
 
Hii sio siasa, ni kipimo cha utendaji kazi wa serikali yoyote itakayokaa madarakani kwa nia ya kutumikia wananchi walipa kodi halali.
 
Stimulus Tanzania?, every year, every day is recession for Tanzania, sasa hii stimulus imefanya kazi gani hasa?, na ni kina nani walipatiwa?, Kama 2005 ilikuwa EPA ikawafanya gamba liwe gumu na kuamua kulivua, basi 2010 itakuwa hii kitu, very soon gamba litarudia hali yake ya awali.

CCM hawawezi kudanganya watanzania matumizi ya 1.7tr kama stimulus wakati, hakuna physical evidence from this. Labla watuambie ilikuwa ni bail out na hata hivyo wawataje ni makampuni gani waliokuwa bailed out na je wameanza kupata faida?, wanarudisha pesa yetu?. Hawa jamaa lazima watueleze na kama watalifumbia macho hili basi very soon, wataitana Dodoma kujivua gamba upya.
 
Stimulus Tanzania?, every year, every day is recession for Tanzania, sasa hii stimulus imefanya kazi gani hasa?, na ni kina nani walipatiwa?, Kama 2005 ilikuwa EPA ikawafanya gamba liwe gumu na kuamua kulivua, basi 2010 itakuwa hii kitu, very soon gamba litarudia hali yake ya awali.

CCM hawawezi kudanganya watanzania matumizi ya 1.7tr kama stimulus wakati, hakuna physical evidence from this. Labla watuambie ilikuwa ni bail out na hata hivyo wawataje ni makampuni gani waliokuwa bailed out na je wameanza kupata faida?, wanarudisha pesa yetu?. Hawa jamaa lazima watueleze na kama watalifumbia macho hili basi very soon, wataitana Dodoma kujivua gamba upya.

Moja ya makampuni kupata ni OLAM....ati walinunua pamba kwa wakulima halafu soko la dunia likaanguka hivyo serikali ikawa-rescue
 
Bravo Zitto, hii inaonesha jinsi ulivyo makini katika kujenga hoja. Hili nalo sijui watajivua gamba? Tusubiri!
 
Kuna topic moja niliisoma humu zamani iliyataja makampuni yote na kiasi walichopewa, mengi yalikuwa makampuni ya kununua pamba., najaribu kutafuta nikiipata nitairudisha hapa tena
 
mbona email ya barua ni mbowe2008@gmail.com ?


123.JPG (barua zote za kiofisi ziandikwe kwa kiongozi wa upinzani)
 
Halafu wanadai wamejivua gamba! Bado wana magamba mengi tu ya kuyavua.
 
Back
Top Bottom