Zitto 'amgeuzia kibao' CAG

Swash Bizo

Senior Member
Jan 29, 2011
141
93
WAZIRI Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe ametaka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ichunguzwe kwa uzembe wa kushindwa kukagua hesabu za ruzuku za vyama vya siasa kwa muda wa miaka mitatu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kabwe alisema CAG ameshindwa kukagua ruzuku ya Sh83 bilioni iliyotolewa kwa vyama vya siasa nchini tangu mwaka 2005 hadi 2010.

Alisema ingawa kuna tatizo katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, CAG hawezi kumtupia mzigo huo pekee yake kwani naye anahusika.

"Nikiwa Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, ninamwomba CAG afanye audit (ukaguzi) kwa vyama vyote vya siasa kwa miaka mitatu iliyopita sasa na siyo baada ya miezi sita," alisema Kabwe na kuongeza:

"Ruzuku ya vyama vya siasa ni eneo ambalo huwa haliangaliwi kabisa na fedha nyingi ya walipa kodi inakwenda katika vyama. Kuanzia mwaka 2005 mpaka 2010 jumla ya Sh 83 bilioni zimetolewa kama ruzuku kwa vyama vya siasa," alisema Kabwe na kuongeza:

"Fedha zote hizi kwa miaka yote hii, hazikuwa zinakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG)."

Kwa mujibu wa Kabwe, ubadhirifu unaoweza kujitokeza kwenye fedha za ruzuku zinazotolewa kwa vyama vya siasa, unatokana pamoja na mambo mengine na CAG kushindwa kukagua ruzuku hizo tangu vyama vianze kuipata mwaka 1996.

"Ndiyo maana kumekuwa na ubadhirifu mwingi wa fedha za ruzuku kwenye vyama takriban vyote hapa nchini," alisema Zitto.

Alisema mwaka 2008, alipeleka pendekezo la mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa katika Bunge la Novemba kutaka vyama vikaguliwe na CAG.

Alisema pendekezo lake lilisomeka: "Vyama vyote vitakaguliwa na CAG na itakuwa ni jukumu la vyama vya siasa kupeleka taarifa zao kwa CAG kwa mujibu wa sheria."

"Hivyo tangu mwaka 2008 vyama vinatakiwa vikaguliwe na CAG kwa mahesabu yao lakini mpaka sasa hakuna chama ambacho kimeshakaguliwa," alisema Zitto na kuongeza:

"CAG mwaka huu amelalama tu kwenye taarifa yake kuwa vyama havikupeleka taarifa zao kwa Msajili. Ametoa miezi sita ili wasahihishe makosa? miezi sita ili watafute nyaraka za kugushi ili kuyaweka mahesabu sawa?" alihoji.

Kabwe alisema kauli ya CAG kwamba hahusiki kuvikagua vyama vya siasa ni kukwepa majukumu kwani sheria ya sasa inamtaka afanye hivyo kwa kuteua wawakilishi.

"Hakuna sababu kwa CAG kutoa miezi sita kwa vyama, bali vyama sasa viheshimu Public Audit Act,(Sheria ya Ukaguzi wa Fedha za Umma), Public Finance Act (Sheria ya Fedha za Umma) and (na) Political Parties Act (Sheria ya Vyama vya Siasa)"

Kwa mujibu wa Kabwe, CAG anapaswa kudai mahesabu kutoka kwa vyama na wala si kusema kuwa hahusiki na watu binasi. "Vyama siyo ‘individuals', vyama ni taasisi," alisema.

"Kwa sheria mpya, wakaguzi wa vyama wanapaswa kuteuliwa na CAG na siyo vyama kwenda kuokota wakaguzi na kuweka hesabu zao kama ambavyo imezoeleka," alisema.

Zitto alisema vyama vya siasa ndivyo vinavyounda Serikali, hivyo iwapo haviheshimu fedha za walipa kodi, Serikali wanazounda haziwezi kuheshimu fedha za walipa kodi.

"Ruzuku iliyotolewa kwa vyama mwaka 2010 ilikuwa ni mara tatu ya Bajeti ya Wizara ya Afrika Mashariki au ni zaidi ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara. CAG ni lazima afanye kazi yake," alisema na kuongeza:

"Msajili wa Vyama naye achunguzwe, ofisi yake inafanya kazi kwa mujibu wa sheria, kwa nini hakuwa na taarifa za vyama vya siasa wakati yeye ndiye mwenye jukumu la kusimamia vyama."

"Iwapo anashindwa kusimamia ruzuku kukaguliwa atawezaje kusimamia matumizi ya fedha kwenye uchaguzi wakati uchaguzi uligubikwa na matumizi ya fedha nyingi za kifisadi," alidai Zitto.

Ripoti ya CAG iliyoishia Juni 30 mwaka 2010, imeeleza kuwa vyama sita vyenye wawakilishi bungeni vimeshindwa kuonyesha taarifa za matumizi ya ruzuku ya Sh17.14 bilioni.

Vyama hivyo ni CCM, CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi, TLP na UDP. Katika hesabu za kawaida kuhusu fedha hizo, chama hicho tawala kimepata mgawo wa Sh12 bilioni kutokana na asilimia 70 ya mgawo.

CUF kinachopata asilimia 20 ya ruzuku kimepata mgawo wa Sh3.43 bilioni, Chadema chenye asilimia nane Sh1.37 bilioni na vyama vitatu vinavyoshikilia asilimia mbili Sh343 milioni.

Akijibu Madai hayo, Utouh alisema: "Sijakwepa majukumu. Fedha zinatoka serikalini, zinakwenda kwa Msajili wa Vyama."

"Yeye (Msajili), ndiye mwenye kazi ya kuvigawia vyama fedha hiyo na sheria inataka baada ya matumizi, vyama vinapaswa kutengeneza hesabu zake na kuziwakilisha kwa Msajili. Siyo kazi yangu kuvitengenezea mahesabu vyama vya siasa."

Kuhusu madai ya Zitto kwamba utaratibu huo wa Msajili kukagua vyama uko kwenye sheria ya zamani ambayo Zitto alidai kwamba alishatoa mapendekeza bungeni na kufanyiwa marekebisho, yanayomtaka CAG kuteua wakaguzi wa hesabu za vyama vya siasa, Utouh alisema:

"Mwulize yeye (Zitto) chama chake kilishanipelekea mahesabu ili niyakague kama anajua hivyo ndivyo inavyotakiwa? Tupo hapa kufanya kazi. Hatupo kukwepa majukumu. Mwulize kama hivyo ndivyo sheria inavyotaka Chadema ilishawahi kuniletea mahesabu yake?"
 
Ni hoja ya msingi kwa political parties kuwasilisha mahesabu yao ya pesa za ruzuku wa CAG. Ubadhilifu mwingi unaihusisha viongozi walioko serikalini na wale waliopo bungeni, labda ndiyo maana hoja ya Zitto haikupita. Nini kifanyike basi? Endelea kupiga kelele mwishowe utasikilizwa. Mataifa mengi duniani hasa yale yanayoendelea ambapo vyama vya siasa vinatafuta ruzuku serikalini, lazima mahesabu yao yawasilishwe kwa CAG kila mwaka wa fedha na CAG lazima aiweke ripoti yake hadharani na wabadhirifu wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria. Tanzania tufuate mfumo huu. Hizi ni fedha za walipa kodi walalahoi... Mimi nakupongeza Zitto kwa hoja hii.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Zitto anataka Mbowe achafuke kwani inawezekana bado analipwa deni lake la nyuma kwa kukifadhiri chama.Maamuzi ya kumlipa Slaa 12m per month na mahitaji mengine aliyokuwa akipata akiwa bungeni hayakupitishwa katika vikao halali vya chama.Zitto alishtuka tu Slaa baada ya kujadiliana na Mbowe anakula hizo.

CAG hakuweza kukagua hizo hesabu,Chadema yenye muelewa Zitto Kabwe mbona hakushauri chama kiandae na kuita mkaguzi ata kama ni kutoka Private firm kukagua.Hapa Zitto anataka kuwashika wenzake pabaya kwani anajua baada ya hesabu hizi kukaguliwa atazipata kupitia POAC na hapo ndo patachimbika maake Slaa anasema ka kuku (ruzuku) kenyewe kadogo ndo maana hakafiki majimboni.
 
Kashtukia nini huyu kijana tena?

Mmh i can smell some kind of bomb behind this statement...........think its gonna blow out soon
 
Zitto anataka Mbowe achafuke kwani inawezekana bado analipwa deni lake la nyuma kwa kukifadhiri chama.Maamuzi ya kumlipa Slaa 12m per month na mahitaji mengine aliyokuwa akipata akiwa bungeni hayakupitishwa katika vikao halali vya chama.Zitto alishtuka tu Slaa baada ya kujadiliana na Mbowe anakula hizo.

CAG hakuweza kukagua hizo hesabu,Chadema yenye muelewa Zitto Kabwe mbona hakushauri chama kiandae na kuita mkaguzi ata kama ni kutoka Private firm kukagua.Hapa Zitto anataka kuwashika wenzake pabaya kwani anajua baada ya hesabu hizi kukaguliwa atazipata kupitia POAC na hapo ndo patachimbika maake Slaa anasema ka kuku (ruzuku) kenyewe kadogo ndo maana hakafiki majimboni.

watu wanavyotafuta ulaji hawawezi zungumzia ruzuku, maana wanafahamu ni bomu kali.
 
kwanini mzungumzaji anakazania 12m za mshahara wa slaa kama vile ni kitu cha ajabu. Acha ku demonstate u public sector wako, wewe unaona katibu mkuu wa cdm kulipwa hivyo ni makosa, wa CCM analipwa ngapi? ama nikuulize wewe unalipwa ngapi kwani? wewe kama kwenye kibarua chako ulitaka kulipwa chochote tu ama according to scale yao imekula kwako, wenzako kwenye private sector hayo ni malipo ya kawaida sana, ama kweli u backward unazidi pale unapokosa naasi ya kusoma
 
Vyama vya siasa vijitegemee vyenyewe sisi walipa kodi tumeshachoka kubeba mzigo huu mkubwa, 83 billioni ingewekezwa kwenye afya labda migomo ya madaktari pale Muhimbili ingepungua.
 
kwanini mzungumzaji anakazania 12m za mshahara wa slaa kama vile ni kitu cha ajabu. Acha ku demonstate u public sector wako, wewe unaona katibu mkuu wa cdm kulipwa hivyo ni makosa, wa CCM analipwa ngapi? ama nikuulize wewe unalipwa ngapi kwani? wewe kama kwenye kibarua chako ulitaka kulipwa chochote tu ama according to scale yao imekula kwako, wenzako kwenye private sector hayo ni malipo ya kawaida sana, ama kweli u backward unazidi pale unapokosa naasi ya kusoma

Tunataka vyama vyote vipeleke mahesabu kwa CAG.
Ungekuwa na kumbukumbu nzuri nafikiri ungekubaliana nami SLAA ni mnafiki, hasa ukitilia maanani ile kauli yake eti wabunge wapunguziwe mishahara, wakati ule aliisema kwasababu alijua wabunge hawataikubali. Sasa leo kwenye chama anachokijenga mbona hajakataa ile namba aliyokuwa anaikataa bungeni?
 
Vyama vya siasa vijitegemee vyenyewe sisi walipa kodi tumeshachoka kubeba mzigo huu mkubwa, 83 billioni ingewekezwa kwenye afya labda migomo ya madaktari pale Muhimbili ingepungua.

Nakubaliana na wewe, ruzuku ifutwe ni ujambanzi tu kama ujambazi mwingine.
 
Back
Top Bottom